Tuesday, January 12, 2016
5.Samia Suluhu Hassani.
 Mwana mama aliyegawanya miaka  55 katika familia, elimu na siasa. Akiwa anazaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1960, Bi Samia anapata bahati  ya mtende.Kuwa makamu Wa rais na mwanamke wa kwanza kushika wazifa huo. Baada ya miaka 54 ya uhuru wa Tanzania .Hata hivyo nafasi kama hiyo pamoja na vyeo vikubwa anavyovipata mwaka 2015 sio jambo geni kwa Samia. Kwani baada ya kufanya kazi na N.g.os, Shirika la Chakula duniani na ubunge , marais wawili kwa awamu tofauti waliwahi kumteua mara tatu  mwanaharakati huyo kuwa waziri. Mwaka 2000  Rais wa Zanzibar,Amani Karume alimteua Suluhu kuwa waziri wa Leba, jinsia na watoto ikifuatiwa na mwaka 2005 waziri wa utalii. Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete pia alimteua awe waziri wa mambo ya muungano. Ukiwa unataka kujua nini kipo nyuma ya pazia, Bi Suluhu hasiti kwa hilo, anatoa siri kwa maneno yasiozidi manne (4),kwamba amefika hapo kutokana na’’ ueledi na umakini katika kila jambo analolifanya’’.Ni kweli asemacho kwa sababu katikati ya miaka ya 80 (1986)Samia Hasani Suluhu alihitimu elimu ya mambo ya utawala chuoni Mzumbe. Mwishoni mwa hiyo miaka ya 80 (1989) Aliongeza elimu yake katika moja ya chuo huko Pakistan na mwanzoni mwa miaka ya 90(1991)Bi Suluhu alihitimu elimu nyingine ya uongozi Hyderabad, India, na mapema mwaka 1994 alihitimu elimu ya mambo ya uchumi  huko Uingereza katika chuo cha Manchester na katika mwaka Wa neema, 2015, Samia alipata ujuzi mpya wa uchumi na maendeleo ya jamii katika chuo cha kimarekani kinachoitwa Southern New Hampshire. Lakini pamoja na yote hayo Bi Samia ni mke, na mama Wa watoto wanne. Tena anayelea na kupenda familia yake vizuri.Kwa historia hii bi Samia ni miongoni mwa wanawake maarufu na wenye ushawishi nchini.Kama  Asha Rose Migiro, Janeth Magufuli, Anna Mwighwira, Salima Kikwete nikitaja kwa uchache .

4.Mbwana Ally Samatta.
 Wazungu wana msemo usemao "umri ni namba" . Kwa maana idadi ya Miaka tuliyonayo sio kikwazo cha kutokuwa watu tunaojikusudia kuwa. Hakika unaweza fanya chochote katika umri wowote. Haya ndio maelezo yanayomvisha kilemba  bwana Samata. Mchezaji aliyezliwa 1992 na mwaka 2015 kugeuka dhahabu  pale alipo pewa tuzo ya ufungaji bora wa ligi za mabingwa afrika. Ikifuatiwa na kuwania tuzo ya mchezaji bora Wa afrika anayecheza ligi za ndani. Ni mswahili wa kwanza kuleta mchango kwa timu akiiwezesha  timu yake kutwaa kombe la mabingwa wa afrika 2015 . Pengine unajiuliza Samata ni nani?. Huyu ni mtanzania mwenye umri wa miaka 23 anayechezea timu ya mpira Wa miguu nchini Kongo inayoitwaTP Mazembe . Mnamo mwaka 2011 Samata aliuzwa kwa dau nono la dola za kimarekani mil 100(shilingi  mil 150 za kipind kile )na  Simba Sport Club.Huku yeye akipewa sh. Mil 50. Mpk mwaka wa neema, 2015, Mbwana Samatta tayari anamiliki pesa, mali, majumba matano na magari ya kifahali  manee;Range Rover yenye thamani ya mil 80 na Chrysler crossfire ya mil 50. Tukisahau habari ya utajiri , Samata anamudu vyema nafasi ya ushambuliaji akiwa uwanjani . Kwa mwaka 2015 tu ameifungia tp mazembe goli saba, kitu kilichomfanya awindwe na ligi za ulaya kw tiketi ya timu za ubelgiji .Kwa nafasi hiyo Samata ataingia kwenye orodha ya watanzania wachache waliowahi kuchezea ligi za nje ya bara la Afrika.Tukikumbuka kuwa wachezaji wengine waliofikia hiyo hatua ni pamoja na Haruna Moshi "Bobani", Athuman Machupa waliokuwa Sweden, Renatus .Njohole, Uswizi, Mwinyi Kazimoto, Qatar .Henry Joseph, Norway na Danny Mrwanda aliyekuwa Vietnam.Tunakutakia mafanikio mema Samata.

 3..Amri Athuman 'King majuto'.
 
Kama sio kipofu utakubali mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwa gwiji wa vimbwanga nchini, mzee king majuto. Kwani tumeshuhudia siku moja baada ya kuachia filamu mpya ya Shikamoo Mzee . Tenda za pesa zilimfuata mzee wa watu. Akifanya matangazo ya bidhaa tofauti tofauti zaid ya muigizaji mwingine.  Hivyo kutawala sura za magazeti, vipindi vya TV na redio . Ni miaka miwili imepita (2013-2015) tangu Majuto atangazwe kama muigizaji aliyelipwa vizuri na kampun ya steps production. Akipokea kiasi cha sh. Mil 20 kwa mwezi, kwenye mahojiano aliofanya na kipindi cha Amplifya kinachorushwa na Miradi Ayo.  Habari inayoashiria kuwa, huenda na mwaka 2015, Majuto akawa mbele kwa kupiga mpunga mnono. Kwa sababu muigizaji huyo wa comedy kanyakua tuzo ya mchekeshaji bora Wa mwaka , pale viwanja vya Nyerere Dar es salaam.Akiwabwaga akina Jangala,  Salma Jabu"Nisha" ambao  ni wachekeshaji wazuri nchini. Ni zaidi ya miaka 50  tangu Majuto aanze kufanya kazi za uchekeshaji . Anasema "Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 tokanimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu"Miongoni mwa filamu zilizomuweka sokoni ni Daladala, Mtu mzima ovyo, Naenda kwa Mwanangu, Back from New York na Shikamoo Mzee. Mbali na yote mvunja mbavu huyu ni baba Wa familia ya watoto tisa na  amefanikiwa kujenga nyumba tatu, kuanzisha shamba kubwa la kilimo .kusomesha wanae, kwenda Makka na kununua magari matano. Kwa maendeleo haya ,mzee ni changamoto kubwa kwa wachekeshaji wanao chipukia na wale wakongwe kama Onyango, Mzee Jangala, Senga , Pembe, Brother K, Nisha na wengine. 

0 comments:

Popular Posts