Wednesday, December 21, 2016
Toka ulimwengu ugeuke kijiji.Habari husambaa haraka kuliko  moto wa petrol.Hauhitaji nguvu kufuatilia mitindo,teknolojia,siasa na michezo. Siku izi kila mmoja ni model,IT,photographer ,kiongozi,na mchambuzi.Kwa sababu taarifa  zinapatikana kila mahali.Kuanzia facebook ,Whats apps.Instagram na kwingineko.Ukaribu wa dunia na mitandao ya kijamii ni chachu ya uelevu..Utitiri wa vyanzo vya habari kupitia simu za mikononi  laptop na tablets zilizounganishwa na internet ni shina la  wasomi na kundi  la waelevu  tulionao.Kuendena na kasi ya mabadiliko yanayotokea ughaibuni kote inategemea unamiliki kifaa gani? Ukinunua tecno,huwawei,Samsung,iphone au ipad yenye 3G hakika wewe umeukata.Kwani internet ni mama wa habari ,aliyezaa mitandao ya kijamii .Inayokupatia kile unachotaka .Familia hii inakuwa kila siku kwa maana kunazaliwa mitandao mipya na followers wapya. Je unajua list ya social networks bora 2016?.
1.Facebook
Image result for facebook

2.Youtube
Image result for youtube

3.Reddit
Image result for reddit

4.Tweeter
Image result for twitter

5.Pinterest
Image result for pinterest

6.Instagram













7.Tumblr
Image result for tumblr logo
8.Linked In
Image result for linkedin

9.Yahoo Answers
Image result for yahoo answers
10.Yelp
Image result for yelp
Monday, December 12, 2016
Haya ni mazungumzo ya babu wa kisasa  na mjukuu .Mjukuu aliuliza swali kwa babu.''Babu kuishi ni nini?'' Babu akamjibu ''Kuishi ni  safari  baina ya  pande kuu mbili, upande wa kuzaliwa na upande wa kifo''.Mjukuu kwa mshangao akauliza tena''kuzaliwa na kifo?.Babu kwa hali ya utulivu akajibu,ndio mjukuu wangu.Kila mmoja imemlazimu kuzaliwa na kufa.Kuja na kuondoka.Mjukuu akadakia''kwa hiyo babu,nani anajua nitakufa lini?''Babu akasogeza kiti vyema na kumueleza mjukuu.'' Tofauti na mungu ni wachache wanaoweza kusema utakufa lini.Nao ni watabiri au watu waliopewa nguvu ya kuona hatima ya maisha yako''.''Kwani wewe huwezi?'' Mjukuu akang'ang'aniza huku akimukazia macho babu yake.Babu kwa kutambua tabia ya ung'ang'anizi wa mjukuu,alianza kwa kusema.''Chozi ni kimiminika cha matukio mawili.furaha na huzuni.Mtu analia machozi, huzuni ikimshika. Anaomboleza  kwa sababu uwepo wako ulimpa mengi ya kujifunza .Mfululizo wa uhai wako ni somo linalojiandika kila siku vichwani mwa watu….Wachache watasahau habari ya kifo chako ndani ya muda mfupi.Lakini wengi watasherekea na wewe muda wa uhai wako. Ukizaliwa wanadamu wanasherekea. Mama ,kaka na ''washikaji''  watakuenzi wakiweka siku maalumu kwa ajili yako , ‘’birthday’’. Kila mwaka ifikapo tarehe ya siku uliozaliwa ‘maswaiba’ watakuambia ‘’Happy birthday’’ ’’Happy born day’’ na maneno mengi ya lugha maridhawa.Ili wakonge mtima wako na chozi la furaha likutoke.Kana kwamba hiyo haitoshi.Wataenda mbali zaidi  wakiandika’’Uishi miaka buku( 1000.). Kuna jambo hawatalitambua ,nalo ni mwisho wa maisha yako. Nawe mjukuu wangu  utakufa baada tu ya kupita duara nne za kuishi.

DUARA LA KWANZA UTAKUWA NA  NGUVU UNA MUDA UNA IDEA HUNA PESA.
Wewe kama inge ukiingia duniani utakuwa na nguvu mikononi  na miguuni.Kwa nguvu ulizonazo. Itakuja siku utazunguka huku na huko.Muda  mwingi ukijaribu sehemu kubwa ya  mawazo yako.Ufanye nini uache nini.Mambo mengi yanakusibu.Karibu yote yanawezekana.Ila mchawi atakuwa mtaji.Tatizo litakuwa ni pesa. Kwa mazingira yako hiki kitakuwa kipindi  kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 29
Image result for no money

DUARA LA PILI UTAKUWA NA NGUVU  UNA PESA UNA IDEA HUNA MUDA
Kama vile simba jike, nguvu zako zitakuwa maradufu mwilini. Ukifanya shughuri ngumu kushinda hapo mwanzo.Kwa kila kazi ujira utaingia. Akaunti ya idea itasoma vizuri, utakuwa na utulivu kwenye jambo moja. Kwani muda wa majaribio ulishapita.Itafika kipindi utaitwa aidha Boss, mwalimu, dokta, mfanyabiashara n,k.Uwapo njiani kuelekea ofisini au kurudi nyumbani. Utaelewa maana halisi ya bango lililonyuma ya lori, daladala, hiace, bus au boda boda linalosomeka’’Tatizo ni muda’’Kwa sababu kipindi hiki utakuwa na wingi wa majukumu.Muda wako utakakuwa mfinyu.Utafanya kazi, zaidi ya kupumzika.Hapo utakuwa una umri wa miaka 30-39
Image result for no time
.
DUARA LA TATU UTAKUWA NA KIKOMO CHA NGUVU UNA MUDA UNA PESA HUNA IDEA.
Kuna nyakati zinakuja nguvu ya mwili itafika kikomo.Haitaongezeka kabisa.Utastafishwa kazi au utafikiria kustaafu mwenyewe.Utendaji wako utakuwa ule wa ‘’one step at a time’’Kazi nyingi hazitafanyinyika mara moja.Hakuna namna, utakabidhi vijana. Wenye nguvu zaidi yako.Muda mwingi utazunguka huku na kule.Kuanzia Milima mirefu ( Kilimanjaro, Evaristi) mbuga za wanyama (Serengeti ,Amazoni ) ,   majangwani  (Dubai,Cairo) hadi fukwe za bahari (Mombasa, Brazil).Wakati unakula jasho na meema ya ulimwengu.Fedha itakuwa inaongezeka kila kukicha.Na utabaini kuwa una kosa kitu.Nacho  ni kimoja tu.idea. una wingi wa pesa ,una  uchache wa idea.Utaanzisha mashindano ya kutafuta idea.Watu kadhaa wataulizwa ''kwa kiwango cha pesa flani unaweza kufanya nini?''.Hapa mjukuu utakuwa una umri kati ya miaka 40-70.

Image result for no idea

DUARA LA NNE UTAKUWA NA IDEA UNA PESA UNA MUDA HUNA NGUVU.

Baada ya mashindano na  matembezi ya huku na kule na kumuona huyu na yule..Jua litazama.Utakuwa ni mchovu.Kwani kichwa kitakuwa na mengi.Utapumzika na kisha kuchuuja idea ulizopata.Utaitwa mshauri wakampuni mwenye busara.   Atoae mawazo madogo, yanayotengeneza faida kubwa ya pesa.Watumishi wako wataamini wewe si wa kawaida  .Kwa namna unavyotatua shida ngumu na kuleta maslahi  kirahisi. .Jina lako litabebwa na heshima uliojenga.Nafasi yako italeta marafiki wapya.Makanisa, Misikiti ,Shule ,Vyama na taasisi nyingi zitakupenda. Hautosita kuzisaidia pale unapoweza.Wajukuu na watu watakupenda. Shida ni moja  tu,nguvu..Nguvu itapungua kila mwaka, utakuwa taratibu sana.Hautokuwa mtu wa safari za mara kwa mara.Siku za usoni utashindwa kufanya vidogo ulivyoweza mwanzoni. Hutofunga tai, viatu, vishikizo wala kuvaa mkanda..Hautoweza kujinywesha maji wala kujilisha chakula.Ukiona hizi dalili mjukuu wangu zinakupata,tambua mwisho wa uhai wako umefika.Hapa utakuwa na umri wa miaka 71 na kuendelea

Image result for tired black old man
Monday, July 18, 2016

Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani  ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo  na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo  ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa  lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini  mara saba katika  kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?.  Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya  hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.

1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain

2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki


3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr

4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''

5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya tatizo na utatuzi
6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.
7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea  kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo safi zaidi ya ulivyokuwa hapo  mwanzo
8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo utalisogelea.

9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.

Sunday, July 10, 2016
Mambo!. Kila kukicha  kinazaliwa kipaji kipya Tanzania.Na kila ,mwaka kunazaliwa studio mpya mtaani.Tangu sanaa ya mziki igeuke ajira.Vijana wa kibongo wameikimbilia fursa.Hakuna anayetaka kubakia shabiki kama mimi au wewe.Vijana wanataka kuwa wasanii na maproduza. Wanatamani kulingana au kumzidi Diamond na Alikiba,Nahreel na Lamar.Ni kitu kizuri kuwa na mtazamo wa mafanikio.Lakini ni kitu kibaya kutoweka daraja thabiti la kufikia hiyo ndoto au hayo mafanikio..Sitaki uchoke ndg ila nakumbusha tu kuwa,huwezi  kuitwa msanii au kufanya sanaa  ,Kama hauna mbinu na  akili ya ziada. Bilashaka unatambua kuwa hata mvuvi hawezi kuvua samaki iwe sangara au pweza, bila ujuzi. Mfano Mvua sangara anaamini hawezi kupata sangara kwa kutumia chakula asichokipenda sangara .Halikadhalika mvuvi wa  pweza anatambua hatoweza kumpata pweza bila kuiingia kwenye maji yanayopendwa  na pweza. Wembe ni ule ule mmoja hata kwa wewe unaetaka kufanya mziki hapa nchini, bila kujali ni Hiphop, taarabu, kwaito zuku, bolingo, segere, singeli, baikoko n.k. Huwezi kujizolea wafuasi bila kujua wanachopendelea .Bila kujua tabia ya mziki.Na kuonekana mjuzi kama yule mvuvi anayejua samaki anahitaji nini ,inachukua mbinu na akili ya ziada kama nilivyotangulia kusema,Gharama na nguvu pia .Kati ya mbinu nyingi ambazo unazijua,umezisikia .Kuna  chache nakukumbushia  ambazo kwa namna moja ama nyingine naamini zitakusogeza mahala katika jitihada na harakari za kuwa msanii nyota wa mziki Tanzania.


 1.Uandishi .Joh Makin anasema''Uandishi wa nyimbo ni feeling na feeling ni kama mtu anavyopata mtoto yaani kuna uumbaji''Lady Jay Dee anaelezea zaidi kwa kusema''mara nyingi nyimbo mimi ninazoandika huwa ni vitu vya ukweli ambavyo aidha ni kwangu au kwa jamii''
.

2.Collabo(kushirikiana). Msanii Alikiba anasema''Unaweza kufanya nyimbo na mastaa isiwe nzuri,Staa kwa staa.Unaweza kufanya na underground(chipukizi) na ikawa nzuri.Sometimes feeling zina kuwa tofauti tunaamka  tofauti''

3,Manager: A.Y anaelezea kuwa''Kuna vigezo vya kunimeneji mimi cha kwanza ufanye kazi atleast mara tatu ya mimi ninavyofanya kazi, kingine ni lazima huyo manager aje na networking(mtandao)wake''.Na kuhusu wasanii chipukizi anaongezea'' mtu hana single au anayo moja hajapata nafasi ya kutengeneza atleat hit song(nyimbo nzuri pendwa) nne kujipima na wasanii wengine,hapo hapo anataka manager,huwezi kuwa na manager wakati hujaijua biashara yako hata kwa kiasi fulani''


4.Promo(utanbulisho na matangazo ya wimbo):Ommy Dimpozi anashauri''Kwenye huu mziki kuna aina ya promo inaweza kufanya mziki usikae sana,inakuwa kama unavumisha kitu vuu kweli kina kuja na ule upepo alafu  ukipotea upepo na nyimbo inapotea na watu wanataka tena nyimbo mpya.Kwa hiyo kuna zile aina za promo za vurugu zinaweza sababisha nyimbo zisikae''

5.Kujiamini.Jaji maarufu wa kipindi cha kusaka vipaji vipya,Bongo star search bwana master Jay anasema''.Msanii anatakiwa kuwa mtu ambaye anajiamini kupita kiasi,hutaki kuwekeza hela yako kwa mtu ambaye ana kipaji lakini hajiamini.Mtu mwenye kipaji nusu na kujiamini mia anaweza kufanya vizuri kuliko mwenye kipaji mia na kujiamini nusu''
,
6.Fanya research(tafiti) Profesa jay anasema''Ukitaka kufanya mziki mzuri lazima ufanye mziki wa watu,sio ufanye mziki wangu(mtu binafsi),so lazima ufanye research watu wanahitaji nini na kwa muda gani,lazima uangalie jamii yako inayokuzunguka,ambayo unataka kuiimbia ipo katika situation(hali) gani ,kama wanataka bata(anasa,furaha) waimbie nyimbo za bata,kama wapo kwenye stuation ngumu waimbie nyimbo za kuwapa moyo''

7.Mafanikio: Mambo makubwa yote  wanayomiliki wanamziki hayatokani na mziki pekee.Mwana Fa anasema''Nilichogundua ni kwamba wasanii wote matajiri,hawafanyanyi mziki pekee hawawi matajiri kwa sababu yamziki.Mifano yote hai tunayo''



8.Hitimisho;Msanii Chemical anasema''Sanaa ni kuchukua kile ulichonacho ukijumlisha na vya watu wengine vingi''

Saturday, June 25, 2016
Wakati wengine wakisema ujuzi ni aina ya  kazi au shughuri yenye kufanyika vizuri baada ya  elimu au mafunzo maalumu.Wahenga wanasema  ujuzi hauzeeki.Kwa maana  ni  uwezo unaopatikana kwa mtu hasa akiwa amepita hatua ya  kupokea  maelekezo, na kufanya matendo mengi.Dhana ya ujuzi imekuwa ya kikazi au ki uwezo kulingana na mfumo  anaoaksi mtu..Ukiwa ni  mtumishi wa ofisi rasmi ujuzi wako itakuwa ni utoaji wa huduma inayokubalika hapo kazini kwako.Na endapo umejiajiri au kuajiriwa sekta zisizo rasmi ,ujuzi ni ule uwezo wa kutoa matokeo mazuri ya  chochote  chema unachofanya.Kwa muda mwingi njozi kubwa na fikira pana zimekuwa kama  baba na mama wa ujuzi  katika mazingira yetu.Kujua zaidi kuhusu hilo fuatilia haya maneno 10

1.Kama mmea ustawivyo kwa mbolea na sio jua kali ndivyo Ujuzi umtajirishavyo mtu na sio maneno matupu

2.Ni vyema kila mmoja akawa na kila ujuzi na asiutumie,kuliko kutokuwa na huo ujuzi na ukataka uutumie


3.Kuna sheria za kufuata ili ubahatike,na kila jambo haliundi bahati,kwa waelevu wanatambua ujuzi ni njia mathubuti ya kuwa mtu mwenye bahati


4.Kumpatia mwanao ujuzi ni bora kuliko kumpatia vipande elfumoja vya madini ya dhahabu

5.Elimu huja kwa kujifunza ila ujuzi huja kwa uzoefu.


6.Elimu pekee sio ujuzi, bali ikizidishwa mara elfukumi ndio itakuwa ujuzi

7.Marudio ni mama wa ujuzi

8.Ujuzi ni mshikamano wa  uzoefu,akili na upenzi wa jambo vikiwa pamoja

9.Ujuzi na kujiamini ni jeshi lisilopigwa wala kushindwa


10.Kama huna ujuzi  ipo siku  inakuja kipaji chako kitakwama,kwani ujuzi  ni dhana ya matendo,bidii na shauku ya kutaka uwe bora kila kukicha,

Popular Posts