Friday, March 20, 2015

Binafsi nimezoe miradi ya familia ni maduka ya bidhaa kama simu, nguo, mifugo, daladala, n.k. Ambayo huanza na kasi ,baadae kudorora na baadhi ya miradi kupotea kabisa.Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya  miradi mitatu ya familia ni mradi mmoja tu hudumu.Na kwa huo mradi unaodumu hakika uongozi  ni sindano kubwa katika kufuma timu ya usimamizi wake.Wakati biashara hii inayomilikiwa kiasi kikubwa na wanafamilia inategemea sana menegementi bora. Mataifa ya Izrael , Canada ambayo uchumi wake umestawishwa kwa zaidi ya asilimia 65 na miradi ya familia.Wanatambua siri nyingine za kufanikiwa kwa biashara zao. Moja, ni mgawanyo wa majaukumu baina ya wanafamilia. Baba, mama ,kaka  na dada anahusika na jukumu moja moja kati ya uhasibu, matangazo, utafiti, soko na maboresho. Korea na India ambao pia ni majabari wa miradi ya familia. Wanatambua fika kuwa,ukuu wao katika hizo biashara ni matokeo mazuri ya kuweka mipango ya kudumu ambayo hufuatwa na kila kizazi kinachorisishwa mradi. Palestine taifa lenye miradi mingi ya famillia kama kitovu cha uchumi wake, pia wanang’oa mizizi ya maendeleo yao. Wakibainisha kuwa kutoweka hisia za ndani katika hizi biashara ni nyota njema inayoangaza mafanikio ya miradi ya familia.Katika suala la hisia mtama zaidi unamwagwa  kuwa,sio kila ndugu ajiriwe au kupata huduma ya bure, ila vigezo na masharti vizingatiwe. Na Italy ambao ni watengenezaji suti wazuri wameachia mikono ya familia inue haya mavazi ya thamani  katika kila  jicho la ulimwengu. Zaidi ya asilimia 90  ya miradi ya kifamilia nchini humo huepuka matumizi mabaya ya faida inayozalishwa na mradi , jambo linalozuia mparaganyiko na kusambaratika kwa biashara zao.Ikumbukwe tu kuwa miradi hii ni ya aina nyingi kama vidonge.Kuna miradi mikubwa kuna miradi midogo.Barafu,karanga,na nyanya za magengeni ni miradi ya familia yenye sura ndogo.Makampuni ya gari,simu,vitabu , ni  miradi ya familia yenye sura kubwa.Unafahamu biashara kubwa za kifamilia ambazo zitakuacha mdomo wazi ?,Basi usichoke, tazama namba moja hadi kumi hapa chini.
1.Toyota

2.Ford Motor

3.Tata group

4.Volkswagen

5.Samsung

6.LG

7.Motorola

8.Siemens

9.Kodak

10.World Wrestling Entertainment(WWE)



Popular Posts