Monday, February 24, 2014

Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na sura mpya ya ufaulu, masomo, mbangilio wa alama, mpangilio wa madaraja,  uwiano wa wasichana na wavulana, uwiano wa shule binafsi na shule za serikali . Katika ufaulu kiwango cha panda kwa asilimia 15.17 toka asilimia 43.08 mwaka 2012 hadi asilimia 58.25 mwaka 2013. Upande wa masomo , watahiniwa wafaulu zaidi somo la Kiswahili kwa asilimia 67.77 na wafanya vibaya katika hesabu, Basic Mathematics , ikiwa ni kwa asilimia 17.78 tu. Mpangilio wa alama umeangalia A= 1 , B+= 2, B= 3, C= 4 , D= 5 ,E= 6 na F.Matokeo ya mwaka 2013 yamekuwa na pointi (alama) nyingi tofauti na miaka mingine, ukiachilia mbali  daraja la kwanza lenye pointi (9 - 17), daraja la pili lina   pointi (18 - 24), daraja la tatu  pointi (25 - 31), daraja la nne likiwa na pointi (32 - 46)  na mwisho daraja la sifuri linalofunga madaraja yote kwa pointi (47-nakuendelea).Kwa miaka iliyopita madaraja yalikuwa  kama ifuatavyo; i (9 - 17), ii (18 - 21), iii (22- 25), iv (26 - 33) na zero (34 - nakuendelea).  Katika matokeo haya  wavulana  wanaongoza wasichana ikiwa ni kwa uwiano wa asilimia  59. 58  kwa  asilimia 56. 73 . Na Shule binafsi zikitoa wahitimu wengi waliofaulu sana zidi ya shule za serikali zinazotoa wachache. Nafasi za juu zinakamatwa na shule za binafsi huku zaidi ya shule 10 za serikali zikikamata nafasi ya mwisho. Na hizi ni shule 10 bora  matokea kidato cha nne 2013    

1. St.Francis Girls (Mbeya) st




2. Marian Boys (Pwani)
 


3. Feza Girls (Dar-es-salaam)


4. Precious Blood (Arusha)


5. Canossa (Dar-es-salaam)


6. Marian Girls (Pwani)
 





7. Anwarite Girls (Kilimanjaro)


8. Abbey (Mtwara)


9. Rosmini (Tanga)


10. DonBosco Seminary (Iringa)


0 comments:

Popular Posts