Tuesday, May 20, 2014
Mashindano yanayohusisha vyuo vingi vya hapa Mtwara, maarufu kama pro life, yalifikia kilele hapo jana jumapili ya tarehe 18 april,2014.Huku mshindi wa mpira wa pete akiwa ni mwenyeji wa mashindano hayo,chuo cha Sauti Mtwara(stemmuco),akifatiwa na mshindi wa mpira wa kikapu ambaye ni Bandari .Hatimaye kinara katika mchezo wa mpira wa miguu ama kandanda uliokuwa na vuta nikuvute  nyingi, hadi kufikia matuta, mshindi aliibuka tena timu ya Bandari.Hii ni sehemu ya matukio mbalimbali yaliyojili uwanjani hapo Nangwanda.





























Monday, May 12, 2014
Kila kukicha bendera ya Afrika inazidi kupepea.Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa kimataifa , 2013. Kati ya mabara saba duniani, Africa ni sehemu ya pili kwa kuwa na wakazi wengi ulimwenguni wanaofikia idadi ya watu billioni moja . Kwa namba hiyo eneo hili lenye jumla kubwa ya waafrika linakuwa nyuma ya   Asia,  bara lenye wanaume na wanawake wengi  wanaokadiriwa kufikia bilioni nne . Afrika tofauti na mabara mengine  ni mahali panapotoa fursa ya wanadamu kuishi kwa upendo , kuishi kwa mshikamano na kusaidiana kama ndugu wa familia moja. Ukaribu unaojengwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya utu . Tabia hii nzuri ni zao la  utamaduni usiohoji maswali kama wewe ni nani, unatoka wapi, unamiliki nini n.k. Wanasema ukitaka kuona shina la ukarimu, mizizi ya uungwana chonde chonde usisite kukanyaga ardhi ya Afrika. Ukitaka kuona ngozi ya kipekee iliyobeba mvuto na mwonekano asilia kama ''chocolate'' hima hima rejea barani Afrika.Pia ukipatwa na shauku ya wanyama wazuri,  madini ya kipekee, misitu na mbuga kubwa zenyekustaajabisha moyo na macho kamwe usisite kufika Afrika. Kwa kuwa ni mahali sahihi kwa hadhina hiyo. Kama haitoshi, sura nchi ya eneo hili lenye  watu wenye nguvu nyingi , linazungukwa na bahari takribani nne, ikiwemo ile ya Hindi, Atlantik,  Meditreniani na bahari Nyekundu ''Red sea''. Toka usawa wa bahari Afrika imemejaariwa miinuko mikubwa, milima mirefu hata kufikia zaidi ya mita 58OO . Mfano mwepesi kabisa  ni mlima maarufu ulimwenguni, kilimanjaro. Kando na vilima, mipando na aina nyingine za miinuko yenye kupendezesha macho sana. Bara hili lenye   kabila nyingi za  asili ya kibantu  lina mabonde, miteremko na nyufa ambazo ni njia na nyumba ya maziwa , mito na chemchemi. Sehemu hizi za maji zina majina makubwa  yavumayo Ulaya, Amerika, Australia na kwingineko ulimwenguni .Ukiachilia mbali ziwa Tanganyika na mto  Naija kuna ziwa Victoria na  mto nile  kama vivutuo maarufu  . Lakini ikumbukwe  ni ndani ya mabonde ya bara la Afrika tu  ambapo historia inasema,  fuvu la binadamu wa kwanza duniani lilivumbuliwa. Baadae teknolojia  ikathibitisha masalia ya mafuvu hayo na ya viumbe hai  wengine walioishi miaka mingi barani hapa,  imechangia wingi wa nishati ya  gesi na mafuta katika ardhi ya Afrika. Nishati hii inaweza kuzalisha umeme mkubwa sana.Gesi ya Mtwara ,Tanzania na Oil ya Naija Dellta, Naijeria ni mfano kidogo tu wa nishati hiyo iliyojificha mabondeni humo. Mwisho ni vyema kujifahamisha kuwa kama binadamu anavyopitia vipindi kadhaa hadi kukua. Halikadhalika  ardhi hii ya watu weusi imepiti vipindi vikuu takribani sita. Vikiwemo vile vya ; ukuaji wa miji  ''state formation'' ,  kukutana na wageni ''the early contcact'' , biashara ya utumwa,  biashara harali  '' legitimate trade'' ,  ukoloni,    uhuru  na hatimaye ukoloni mambo leo '' neo colonialism''









Mbuga ya Serengeti ni miongoni mwa vivutio vikubwa barani
Afrika na hapa ni wakati wa mawio

Dhahabu

Almasi

Madini ya Tanzanite




Twiga wa Afrika
msitu wa Kongo


mto Nile






Wageni toka mabara mengine wakikaribishwa Afrika ,hapo juu ni msanii Shaggy
umoja na ushirikiano ni jadi isiyofichika barani Afrika
Visura wenye rangi ya chocolate ni chimbuko la Afrika






Popular Posts