Monday, January 4, 2016

Nikiwa mwanza mwaka 2004 nilikuwa mwanafunzi aliyependa somo la historia. Moja ya mada niliyopenda ni colonialism. Mada ilinifunza , miongoni mwa athari walioleta wakoloni ni kurudisha nyuma maendeleo ya  Tanzania. Huku maeneo ya kusini mwa nchi yakitajwa kuwa duni  zaidi ya kwingine. Nikasoma pia Mtwara na lindi ni mfano wa maeneo hayo. Lakini cha ajabu mwaka 2011 nikiwa mwaka wa kwanza katika chuo kimoja cha hapa mtwara niliona mambo ni tofauti  .Mtwara ya kipindi hiki inapiga hatua kuliko picha niliojengewa na ile mada. Kuna ulinzi wa mali na usalama wa afya. Kuna shule, vyuo na taasisi za elimu. Kuna viwanja vya michezo, vikundi vya sanaa na mahala pa burudani.Kuna viwanja vya ndege,bandari na stand za bus. Kufikia mwaka 2014, niliona Viwanda vya cement, vyombo vya habari, na rasli mali za mafuta na gesi,  huku fukwe za mtwara mjini zikiwa na hotel nzuri na maandhari safi. Nakumbuka katika kufurahia  mazingira haya nilikuwa napiga zoezi kila alfajiri. Kisa kilichopelekea nipoteze simu.Pale uchovu uliponifanya nisahau hicho chombo cha mawasiliano juu ya canteen ya chuo. Mungu ni mkubwa simu ilipatikana  siku kumi baadae.(Niliipata vipi hiyo ni stori ya siku nyingine) na mwishoni mwa mwaka 2015 nikirudi chuoni  kwa ajili ya kumsapoti mdogo wangu aliehitimu chuo .Nilipata bahati  kutembelea fukwe tofauti tofauti. Msanga mkuu, Veta, makonde, bandari ya zamani . Ambapo sikusita kuogelea baharini ,  wakati nafanya hivyo mwenzangu ambaye ni mgeni hapa aliniuliza, ’’ni mambo gani ya kuzingatia katika fukwe za mtwara?’’ Nikiwa majini nilianza kwa kumwambia . ’’Yapo mengi ya kuzingatia ila nitaanza na haya’
1.URUMBA (wadudu). Ukiwa unaogelea kuwa makini na wadudu walio na miiba iliyowazunguka mwili mzima. Wakiwa katika rangi nyeusi na sura ya duara mara nyingi wadudu hawa hujisogeza karibu na miamba . Na kwa kuwa miiba yake ni nchi moja na zaidi na upana wa sindano ya mkono , ukimkanyaga mmoja mwiba unavunjikia mwilini mwako. Idadi ya miiba iliyokuingia inasababisha  mwasho mkali, maumivu na baadae homa. Wenyeji wa pwani wanashauri ukipatwa na tatizo hili(urumba) , mapema chukua  mafuta ya taa tia mahala miiba imeikuingia. Baada ya siku mbili mpaka tatu utapona
.

2.ASKARI. Uwapo katika fukwe za shangani, kama makonde na veta askari wa dolia ni wengi. Hivi vikosi haviruhusu raia abaki maeneo haya muda wote. Ikifika saa 12 :30 jioni , watu hufukuzwa.  Saa 1 giza likiwa kubwa  askari polisi hukamata watu . Raia hufikishwa kituoni. Wakipewa adhabu ya kutotii sheria za fukwe.

3.MV MAFANIKIO. Ni feli inayobeba magari ,mizigo na  watu wanaotoka na kuelekea msanga mkuu.Baada ya fukwe za veta na makonde kuwa na mashabiki wengi. Fukwe za kivuko cha Msanga mkuu ndio imekuwa habari ya mjini miongoni mwa watu. Hakuna namna ya kuenjoy pwani hii kama hujui utaratibu wa Mv mafanikio. Huanza asubu sana kukamilisha safari yake. Muda wa mwisho ni jioni  saa 12. Kabla ya kuondoka hupiga honii. Ukifika chomboni mkononi uwe na ticket . Kuna nauli ya mtu, gari na mizigo mikubwa. Mpaka mwaka 2014 disemba nauli ya mtu mzima ilikuwa ni sh. 300.
4.KUPWAA NA KUJAA. Raha ya fukwe ipo machoni mwa mtazamaji. Hivyo ni msingi kutambua wewe unapenda msimu wa bahari ikiwa ina maji  au ikiwa haina. Kuna nyakati bahari hupwaa, hapa ni muda maji yapo mbali sana na fukwe. Ukitazama utaona maadhari kama ya jangwa, miamba vigumu kupata maji ya shingo wala ugoko. Na wakati imejaa huwa ni wiki  nzuri kwa waogeleaji. Ukitokea pwani utaona fukwe zinatenganishwa na mawimbi ya amaji. Ukiyafuata yatakuanzia kweye ugoko ,kiuno , shingo mpaka mwili mzima utabebwa .
5.SIKU KUU. Ni siku njema kwa mambo mengi zikiwemo fukwe. Wakati wa chrismas, mwaka  mpya, Idd n.k Fukwe za mtwara hufurika watu zaidi ya mchanga. Siku kuu wanavyuo, watoto wa mjini, raia wa kawaida kutoka kona zote za mtwara hujumuika hapa. Hizi siku mhimu huambatana na matukio mhimu kama upigaji picha , biashara za vyakula na vinywaji. Huku mziki , nyama choma na burudani  zikiwa pale fukwe ya makonde.
6.USAFIRI. Ni mhimu kujua utatokaje eneo moja hadi jingine. Kama ilivyo lazima kujua utafikaje ufukweni endapo upo nyumbani. sio vigumu , kama wewe unaishi mtwara au ni mgeni nabado haumiliki chombo cha usafiri. Kwanza kuna usafiri wa aina nne. Taxi,Bajaj,Bodaboda na baiskel. Pili kila usafiri una gharama yake. Wakati taxi au gari za kukodi zikiongoza kwa gharama, bajaji na boda boda(pikipiki) huwa ni nafuu ikitegemea na idadi yenu. Ukiwa ni mtu wa mzoezi baiskel zipo unachotakiwa ni kukodi na kueleza unachukua kwa masaa mangapi. Mwisho kabisa kwa wewe unaeishi mbali na hizi fukwe ni mhimu kutambua kuwa usafiri unapatikana.



0 comments:

Popular Posts