Tuesday, January 17, 2017
Waswahili husema ‘siku hazilingani’ ni kweli. Leo ukifurahi, kesho utaduwaa. Na richa ya juhudi kubwa inayopimwa na jasho zito , majanga hayaishi kutuandama. Wakati mwingine chozi la uchungu linapita  . Jicho linazibwa  usione  fursa hata moja mbele yako. Na ghafra ukishtuka umeshajikwaa kwenye kisiki cha umaskini. Hapo utajiuliza maisha yana maana kweli?Na hakutakuwa na jibu.Maana matatizo yanakuwasha  kuliko upupu.Shida zinashamili kama magugu.Sikio halisikii habari njema tena.Ukifungulia redio  ikutie moyo ,majonzi ndo kwanza yanakithiri.  Matangazo  ni ya nafasi za shule zaidi ya nafasi za ajira, ni ya vyuo zaidi ya mahala pa kazi. Katika juhudi za kuepuka huo mfadhaiko unageuza jicho mpaka kulia kwako ambako kuna ‘tv’.Ni kipindi cha habari , bila kuamini mboni zako unajionea viongozi wakitumbuliwa Ili hali mifumo ikiachwa.Hasa elimu. Kabla hujaongeza sauti ya luninga , simu yako inayokaribia kukata ‘charge’sababu ya shida za umeme ,inaita.Ni ndugu analalamika maisha magumu pesa hakuna..Mkopeshe japo "jero" . Bila mafanikio ya kumweleza jinsi ulivyopigika,simu yake inakata hana voucher.Kufumba na kufumbua,,umeme umekata na simu inazima kumbe hata bila ya voucher kuisha bado mawasiliano yangekata tu.Ukiwa kwenye joto kali baada ya umeme kukata unabakia kutazama sura yako kwenye  televisheni iliyozima. Punde mwenyekiti wa wapangaji anakumbusha ni zamu yako kulipa LUKU,mzunguko ushakufikia. Ungali bado katika hali hii ya sintofahamu baada ya simu kumaliza moto, redio kupoteza matumaini  tv kuzima na sasa kulipa LUKU.Anakuja baba mwenye nyumba kudai chake. Utatamani kusikia maneno ya wasanii hawa.
1.’’Acha kulia ni shida za dunia ebu tulia’’Jose chamillioni
2.’’Haya yote ni maisha ipo siku yatakwisha leo mmoja anangaika mambo yamebadilika’’P funk
3. ’’Kama unapata moja kwa nini usipate na mia,hiyo inawezekana kwa wote waliona nia’’Prof jay
4.’’usikubali wakakushinda,Kwani wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini’’Juma nature
5. ’’Wakati wako ndio leo kutimiza malengo yako nakusihi anza sasa jishughurishe utapata’’Ben Paul.
6.’’Na ugumu wote wa maisha shida zote za  kutaabisha usikate tama usivunije moyo’’Kara Jeremiah

0 comments:

Popular Posts