Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Tuesday, July 7, 2015
Mabadiliko
ni kama maji huweza kuchukua umbo la sura yeyote. Na huweza kufuata uelekeo
mmoja au zaidi. Ukitazama sura ya teknolojia
iliopo leo utabaini hii sio taswira iliokuepo jana, yaani miaka 20 iliyopita. Mageuzi
haya yanatokea huku wagunduzi kuntu wakiwa ni miongoni mwa watu adimu katika hiki
kipindi. Richa ya kukosekana kwa wagunduzi nguri wakiwemo; Isack Newton, Pythogrus,
Edson Thomas, kati ya miaka 1995 hadi 2015 . Kuna upepo wa mabadiliko
unaoletwa na waboreshaji wanaofuata misingi ya hao wagunduzi kuntu. Wagunduzi
dhahiri, wangunduzi halisi , wagunduzi waliovuma miaka yote. Ndani ya hiki kipindi cha miongo miwili ( miaka
20 ). Kuna wabunifu wanaochipukia na kumiminika
kama utitiri. Hawa ndio shina
linaloshikilia urahisi wa maisha na urahisi wa mawasiliano katika dunia ya leo.
Hali inayopelekea mambo yaliokuwa hayawezekani miaka 20 iliyopita kufanikiwa. Na
hapa ni baadhi ya hayo mambo
1.IMO,SKYPE


Kitendo cha kuonana ana kwa ana baina ya watu wawili walio katika sehemu tofauti za mchi , ilikuwa ni kitendawili katika niaka ya 90. Ahsanteh kwa teknolojia ya imo na skype kwa kuleta nyuso na sauti za watu karibu. Wapendanao waliokuwa wametenganishwa na umbali, masomo, kazi na majukumu ,sasa wanafursa ya kusalimiana na kutazamana kwa ukaribu kama pua na mdomo.
2.WHATSAPP
Ilikuwa ni
rahisi kwa mganga wa kienyeji wakati
ule. Kuendesha majadiliano na watu anaowaona yeye tu , kama hiyo haitoshi
aliweza kusema kitakachojiri duniani
kabla ya mimi na wewe kutambua lolote.Baada ya simu kuingia kila mtu kapatiwa
uwezo huo. Tena kama ina whats app ndio mtajadiliana hadithi zote kuanzia; siasa
, katiba, tamaduni , uongozi, ajira, michezo, burudani ,utabiri wa hali ya
hewa,kubet n.k .Vyanzo vya hizi habari kwa mwaka 2015 sio tena ‘mafundi’ au waganga
wa kienyeji pekee bali ni rafiki zako,wanafunzi
wenzako,wafanyakazi na jamaa uliohifadhi namba zao katika simu ya kiganjani
mwako. Kwa kutumiana jumbe za sauti,picha na video Whats app hukupa maarifa pamoja na taarifa za hayo matukio mbalimbali
3.YOUTUBE
1995,Televisheni ilikuwa ni kila kitu juu ya
masuala ya video. Kuona ‘kichupa’ au video mpya ya msanii unayempenda ilikupasa
utege jicho kwa luninga. Ukikosa tukio kubwa katika taarifa ya habari ulitakiwa
kuwa mvumilivu hadi taarifa irudiwe, vinginevyo ungoje kipindi maalumu au mwisho wa wiki. Hali sio
hiyo tena miaka ya kuanzia 2005, na Shukrani za kipekee ziendee youtube kwa kutupa uhondo wa video tulizokosa,
tuzitakazo katika muda wowote, mahali popote na kwa mtu yeyote. matukio makubwayaliokupita au uliyoyakosa
katika tv utayapa hapa.
4.SHAZAM
Unakumbuka
enzi hizo ukisikia mziki mzuri redioni, unatamani mtangazaji ataje jina la huo
wimbo?. Ama unapita mahala kuna mdundo wa nyibo za ughaibuni,zinakugusa moyoni lakini
hujui msanii wala jina la wimbo? Hii shida sasa imefika mwisho.Mwaka 2015 Kazi
imerahisishwa sana . Ni vyepesi zaidi ya
kumsukuma mlevi. Kwa kutumia shazam unaelekeza tu simu au komputa karibu na
mdundo wa nyimbo, na ndani ya sekunde
umeshapata jina la msanii na nyimbo
.
5.GOOGLE
EARTH
Zamani
ilikuwa ni ngumu kufika pointi moja bila
kuwa na mwenyeji, bila kuuliza ama kupanda chombo cha usafiri. 2015 unaweza
kutembea dunia nzima bila kukwea pipa, kuchukuwa treni, kupita na meli wala
kupanda basi. Ikiwa una google earth na mji una ramani mtandaoni , utaelekezwa njia za kupita kwa mguu, kwa gari hadi sehemu
za kuvinjari, hotel, supermarket, beach na
kona za afya ; hospitali, zahanati, na
maduka ya madawa baridi. Google hawatoi tu ramani bali pia vituo mhimu
unavyotaka kujua
.
6.FACEBOOK
Karibu kila
mmoja ana damu ya uandishi. kubali!, kataa!. Kwa maana anafurahi kushirikisha
jamii dhidi ya mafanikio ,mipango, ndoto,
huku akitia moyo marafiki na kuomba
msaada wa maombi kwa ndugu hata pongezi kuto kwa jamaa . Mmoja yupo huru kutoa
mawazo na hisia zake mbele ya wengine. Hii sehemu ya maisha ya mtu mmoja dhidi
ya wengine hufanyika kwa maandishi yanayoambatanishwa na picha nzuri ya
mhusika. Kama ishara ya kujuza jamii nini kinachoendelea upande wake. Endapo hujui
ninachojaribu kuelezea hapa, nakusihi
jiunge na facebook, ukashuhudie jinsi uhuru wa kujieleza ‘freedom of expression’
inavyotendewa haki. Ikiwa una kumbukumbu nzuri, pengine umebahatika kuishi na
wezee katika miaka ya 90. Utaona bibi na
babu zetu hawakufaidi dhana nzima ya uhuru wa mawasiliano.Ukilinganisha na
FACEBOOK
7.TWITTER

Nakumbuka
nilisoma kitabu kimoja zamani kidogo, ambacho kilielezea namna wafalme
walivyokuwa wakituma jumbe ulimenguni.Kitendo kilifanya na mtu mwenye mbio sana
aliagizwa kupeleka nyaraka katika himaya nyingine , na hiyo himaya iliteua mjumbe wao mwenye kasi sana mpaka
falme ya tatu .Ambayo pia ilieneza habari katika falme ya nne. Mtindo uliendelea mpaka falme ya sita ,saba hadi ya mwisho.Na baada ya miaka habari ilienea
ulimenguni kote. Stori ya hiki kitabu chenye maisha ya zamani, kinafunua muongozo
wa teknolojia ya twitter . Kitu ambacho twitter hufanya japo ni ni ndani ya sekunde,au
dakika tu. Ni kueneza habari kwa haraka, Hivyo miomgoni mwa matumizi mengi ya
tweeter, dunia nzima hujua nini
kimejiri. Kwa kuendeleza habari husika iwe ni Alshabab, Sunami, mapinduzi, ongezeko
la joto n.k .Ndani ya masaa taarifa
itakuwa imefika uchina, Marekani, uingereza, Brazil, Australia na Tanzania .
Dunia nzima hupelekewa taarifa kwa kufanya swala endeleve linaloitwa ‘retweete’
8.INSTAGRAM
Wakati sote
tunaamini bank ni nyumba ya pesa, ghala ni nyumba ya mazao na msitu ni sehemu
ya miti. Basi instagram ni nyumba au
sehemu ya picha. Zamani kuona picha ya msanii, mtu maarufu au kiongozi mkubwa
ilikuwa nadra, mpaka utafte gazeti au kutembelea maneo ya kazi zao. Ahsanteh
Instagram kutuletea pozi, dizaini, mbwembwe na matukio mengi ya watu hawa
katika mfumo wa picha.
9.EBAY, AMAZON,
KUPATANA


Unakumbuka
wakati unauza bidhaa na hakuna mteja? .Unataka kununua mali hakuna hakuna muuzaji?.
Ilikuwa ni zama ya miaka ya 90. Kuanzia mwaka 2015 Ebay, Amazoni, Kupatana.com (
Tanzania ) inatoa uhuru wa kuuza na
kununua bidhaa yoyote mtandaoni. Hapa utapata nyumba, mavazi, usafiri, vitabu, mashamba n.k
10.HULKSHARE,
SOUND CLOUD


Sauti ina
thamani yake na ili hii haiba idhihirike haina budi kukusanywa pamoja katika
mfumo flani. Miaka ya 90, miziki ilitunzwa
vyema katika santuri, kanda , cd na baadae miaka ya 2000 , zikaingia flash. Lakini
ukisahau mbinu hizi . Hulkshare na sound clound ni mapinduzi makubwa miongoni
mwa mengi katika kutunza, kusikiliza na kupakuwa au ku ’download’ sauti, nyimbo,
midundo, mziki unayoipenda.
Monday, June 15, 2015
A.Y au Ambwene Yessaya ni mwanamziki mkongwe anayetetemesha bongo fleva likija swala la mafanikio.Msanii huyu kajiwekea mizizi mirefu hadi nje ya mipaka ya Tanzania.Akianzia na kundi la East Coast Army ,A.Y anapata umarufu kwa uwezo wake wa kurap vizuri,na baadae anajitegemea huku akifanyakazi na wasanii wakubwa kama Sean Kingstone,Romeo,n,k. Na hapa anakuuliza ''Ni kitu gani huwafanya watu wawe na
mafanikio?'' kisha anasema ''Leo namalizia kukupa siri 10 ambazo ukizizingatia utabadilika na
kuwa mtu ambaye kila mmoja atakuwa akikuangalia kama mfano.''Ambwene Yessaya(2015).
1. siri ya kwanza:UNAVYOFIKIRIA NDIO
KILA KITU
Siku zote kuwa na mawazo
chanya. Fikiria mafanikio na sio kushindwa. Kuwa makini na mazingira hasi. Siri
hii inafaa kuwa ya muhimu zaidi kwenye orodha ya mambo ntakayokuambia.Imani kuwa unaweza kuyafikia malengo
yako inapaswa kuwa imara. Pindi unapojiambia mwenyewe kuwa ‘siwezi..’, basi
hautaweza. Mambo chanya huwatokea watu chanya.
2. siri ya pili:KUWA MSTAHIMILIVE NA
JITUME
Mafanikio ni kama marathon
na sio mbio fupi. Kamwe usikate tamaa. Ukimuuliza kila mtu aliyefanikiwa leo au
ukisoma historia za watu wenye uwezo mkubwa kifedha na maisha kwa jumla,
utagundua kuwa walijituma sana hadi kufika hapo
walipo.
Hakuna njia ya mkato katika kufikia
kilele cha mafanikio. Lakini kama unafanya kitu ambacho unakipenda – basi sioni
hata kama unaweza kukiita ni kazi!
3. siri ya tatu: KUWA TOFAUTI
Kama utafanya kitu kile
kile kama wengine wanavyofanya, ni ngumu sana kuwa na mafanikio. Ni muhimu sana
kupata kitu tofauti na kukomaa nacho.Hivi ndivyo itakuwa rahisi
watu kukuona na wewe kupata unachotaka. Iwe ni fedha, uhusiano wenye maana, mtu
tofauti huvutia wote.
4. siri ya nne: ANZA SASA
Watu wengi hushindwa
kuufikia uwezo wao wa juu kabisa kwasababu huwa hawaanzi kufanya kitu. Siku
zote wamekuwa ni watu wa kujiandaa, kujipanga na kusubiri muda mzuri wa kuanza.Kama ningeendelea kusubiri
hadi leo pengine nisingekuwa na mafanikio haya niliyonayo. Kama nisingechukua
hatua za kusafiri na kwenda Kenya, Uganda na kwingineko, nisingekuwa msanii
ninayejulikana kama hivi sasa.Kama nisingekuwa mjasiri na
kuamua mwenyewe kubadilisha video zangu na kuzigharamikia, naamini nisingewapa
moyo wasanii wenzangu wanaowekeza sasa kwenye kazi zao. Kujiongeza ni neno
sahihi hapa! Kama unataka kujenga
nyumba, ni ngumu kupata kwa mfano shilingi milioni 50 za hapo hapo ili uanze.
Anza kwa hicho ulichonacho mkononi na utashangaa kuwa una nyumba tayari! Si
unaujua ule usemi kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha?
Je
unasubiri kitu fulani kabla ya kuanza? Ni kitu gani kibaya sana kinaweza
kutokea kama ukianza sasa? Kama wewe ni mtu ambaye umekuwa ukisubiri muda
muafaka ufike, acha kusoma post hii na anza kufanya kile umekuwa ukitaka
kufanya. Post hii itaendelea kuwepo hapa hapa ukirejea tena. Ha ha ha ha!
Tukutane kwenye siri ya tano!
5. siri ya tano:ISHI KWA
KILE ULICHONACHO/UNACHOINGIZA
Watu wenye uwezo huepuka
sana kutumia hovyo fedha zao. Lakini cha ajabu, miongoni mwa wengi wenye kipato
cha chini huishi maisha yaliyo juu ya uwezo wao. Hutumia zaidi kuliko kile
wanachoingiza na hivyo kujikuta na madeni mengi. Kama wewe ni mtu wa aina hii,
punguza sasa ili kujiwekea akiba kwaajili yako na familia yako.
6. siri ya sita:KUJIWEKEA TABIA NJEMA ZA KILA
SIKU
Tabia njema ni msingi wa
kutengeneza utajiri. Tofauti kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao
hawajafanikiwa ipo kwenye tabia zao za kila siku. Watu waliofanikiwa wana tabia
njema ama ili kueleweka zaidi niyaite mazoea mengi mazuri kuliko yale mabaya.
Kama unaelewa kuwa tabia
zako mbaya zinakukwamisha kuwa tajiri, utambuzi huo utakuwa ni hatua ya kwanza
katika kuboresha mienendo yako.
Kwenye kitabu chake
kiitwacho ‘Rich Habits - The Daily Success Habits of Wealthy Individuals’, Tom
Corley anakupa ushauri wa kuchukua karatasi na kuorodhesha tabia zako mbaya
kwenye column moja na kisha zibadilishe kila moja kwenye column nyingi kwaajili
ya tabia njema. Mfano ni kama huu:
Tabia mbaya
Ninaangalia mno TV
Sikumbuki majina ya watu
Ninajizuia mwenyewe hadi kuwa na saa moja tu ya kuangalia TV
Ninaandika majina ya watu na kuyakumbuka
Watu wengi waliofanikiwa huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Ninajizuia mwenyewe hadi kuwa na saa moja tu ya kuangalia TV
Ninaandika majina ya watu na kuyakumbuka
Watu wengi waliofanikiwa huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Tabia njema
Kisha kwa siku 30, fuata
maelekezo ya kwenye orodha ya tabia zako njema. Utashangaa namna
utakavyofanikiwa.
7. siri ya saba:USIOGOPE
KUOMBA MSAADA
Watu waliofanikiwa hawana
kasumba ya kufa na tai shingoni kama mjerumani. Walipokumbana na vikwazo
walitafuta msaada wa hali na mali kwa wale waliokuwa na nafasi kuwazidi.
Kila mmoja na ule uthubutu
wa kufanya mambo yake mwenyewe, ni nzuri katika upande mmoja lakini pia mbaya
katika upande mwingine.
Kama kuna mtu unamfahamu ni
mjuzi kwenye sekta fulani na unahisi anaweza kukusaidia katika mradi wako sio
mbaya ukimshirikisha katika ushauri.
8. siri ya nane:NI MARUFUKU
KUKATA TAMAA
Safari ya kuyafikia
mafanikio sio rahisi hata kidogo. Kama unataka kuwa na maisha mazuri kwa njia
halali, ni lazima utakutana na vikwazo vingi ambavyo kama hutokuwa jasiri, ni
rahisi sana kuanguka.Usikate tamaa pale mambo
yanapokuwa magumu. Watu waliofanikiwa huvumilia. Hubadilisha njia. Hujaribu
kitu kipya. Husonga mbele. Wanaweza kubadilisha muelekeo lakini huendelea
mbele.
9. siri ya tisa:TAFUTA
USHAURI KWA WATU WALIOFANIKIWA
Watu wengi waliofanikiwa
huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia
kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika
nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama
ukienda mwenyewe.Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana
afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe
baadhi ya siri zake.
10.siri ya kumi:JIWEKEE AKIBA
Wahenga walisema akiba
haiozi na haba na haba hujaza kibaba. Watu wengi hudhani kuwa ili uweze kuweka
akiba ni lazima uwe na kipato cha juu. Nakubali kabisa kuwa wakati mwingine
watu hujikuta tukishindwa kutunza chochote kwasababu majukumu ni mengi kuzidi kipato
chetu, lakini hebu chukua mfano huu:
Wakati ulipokuwa ukiingiza
50,000 kwa wiki, kwanini uliweza kuishi kwa hicho unachokipata na maisha
yalienda? Kisha ulipokuja kupata 100,000 kwa wiki maisha yalibadilika kwa muda
lakini baadaye ukaja kuona tena kuwa hiyo nayo haitoshi! Fundisho hapo ni kuwa
binadamu hatuwezi kuridhika kwa kile tunachokipata na kwamba tunaishi kwa kile
kinachopatikana.
Kwahiyo kama unaingiza
50,000 kwa wiki, ukifanikiwa tu kuweka 5,000 kwa wiki, kwa mwaka mzima utakuwa
umeweka akiba ya 260,000! Lakini pia utaweza kujibana na kuishi kwa 45,000
iliyobakia.
Wengi wenu hapa mnapata
zaidi ya hapa hivyo kama mkiwa na desturi ya kujiwekea akiba, hutaamini kiasi
cha fedha ambacho utakuwa umefikisha baada ya mwaka mmoja au miaka mitano kwa malengo
marefu zaidi. Anza sasa kujiwekea akiba.
Watu wengi waliofanikiwa
huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia
kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika
nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama
ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya
njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa
tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Je! Siri hizi 10 nilizokupa
zimekufundisha au kukuwekea kitu kichwani?
Ni kwa muda sasa katika jamii nyingi kumwona kijana kavaa headphone akisikiliza mziki. Swali tunalojiuliza. Ni je hawa vijana wanavutiwa na asali ipi katika hiyo burudani? Tena sio jambo la kushangaza kusikia mdundo mkubwa ndani ya vyumba vya wanachuo na makazi ya vijana hasa wale walio wapya katika ajira.Wakati mikito ya muziki haitenganishwi na masikio ya vijana wengi.Siku hizi kuna magari,kumbi za starehe,ambazo ni mahususi kwa kuweka wadau wa mziki pamoja.Kama wewe ni mpezi wa fukwe lazima utakua unazijua hiace na gari binafsi ambazo huja na mziki 'mnene'.Na kama umeingia night club au kupita mahala penye disco ni rahisi sana kubaini kundi la masharobalo wakiegeza mfano wa wasanii wa magharibi wanaofanya miondoko ya kufoka foka. Remmy Ongala kutoka Afrika aliwahi kuuliza mziki ni nini?Kujua zaidi mziki ni nini na kwa sababu gani vijana wanapenda sana mziki soma tafiti hapa chini.
1.Kufanya kazi wakati kuna mziki inapelekea hali chanya na kuongeza uzarishaji
2.Mdundo na mkito hufanya akili ijiamini na kuwa na nguvu
3.Kusikiliza mziki mara kwa mara ni tiba ya ubongo dhidi ya uvimbe wa hilo eneo(brain tumor)
5.Sauti kubwa kwa baadhi ya wapenda mziki huwapa furaha
6.Maneno na mapigo katika baadhi ya miziki hupunguza msongo wa mawazo
7.Mziki hukomaza hisia changa na ni dawa ya kujiamini
9.kiafya inasemekana mziki huchangia kuzalishwa kwa chembe hai , kinga ya mwili na hupunguza matatizo ya moyo
Sunday, June 14, 2015
Wahenga
husema ukitaka kuruka juu sharti uagane na nyonga na mgaa gaa na upwa hali wali
mkavu.Ivi ni nani anayeamini mwalimu anaweza kufika mbali awe raisi au kiongozi
wa nchi? Wakati ukweli unasadiki kuwa, nafasi
hizo za juu huheshimika kwa sababu ni kitovu cha mamlaka makubwa na hukaliwa na
wachache .Kuna asilimia kubwa ya
viongozi katika ikulu chimbuko lao
linatokana na kazi ya kufundisha watu darasani.Kitendo kinachowapa msingi wa kusimama mbele ya halaiki
wakizungumza na kuongoza .Haya matunda
ya ualimu ni kiiza machoni pa watu
wanaobeza taaluma hiyo kila kukicha.Kwa madai kuwa ’ualimu
ni kitanzi cha ajira ‘ na(walimu) hawaishiwi vitimbwi dhidi ya serikali .Ukizingatia
katika moja ya sherehe za wafanyakazi hapa nchini, waalimu wamewahi kutuma ujumbe kwa raisi uliovuta
umakini wa mamilioni ya watanzania.Ujumbe ulibeba maneno mawili tu , yaliosomeka ’’shemeji unatuchaje’’lakini
‘message’ ilikuwa ‘sent and delivered’.hahahaha lazima ucheke.Ukiweka kando mzaha huo na ubezaji, bilashaka tutakubaliana kuwa viongozi na waalimu wana mambo kadhaa yanayoendana,moja ikiwa ni watu wanaofanya kazi karibu na jamii , lakini pia wana fursa
inayowaka kama mwenge wa taifa
unaosubiliwa kwa hamu ulete maendeleo ya nchi.Basi sikuchoshi tena na wafuatao
ni maraisi waliofikia hicho cheo ilihali wanajua
dustor,chaki na rula zinakazi gani ubaoni
1.Baraka
Obama.
2.Yoweri
Museveni.
3.Robert
Gabriel Mugabe
4.bill
Clinton
5.Kwame
Nkrumah
6.John
Evans Atta Mills
7.kenneth
Kaunda
8.Benito
Mussolin
9.julius
Nyerere
Thursday, April 16, 2015
Katika moja
ya kipindi cha luninga niliona mabishano
baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati
wa kwanza ni ‘utajiri’ na msamiati wa pili ni ‘tajiri’. Mmoja alisisitiza ''utajiri ni
kuwa na chakula kingi,nguo nyingi na nyumba nyingi'' Wapili alikanusha usemi wa
mtu wa kwanza na kaka wa tatu akadakia kwa mbwembwe zote akisema''tajiri au
utajiri ni kuwa na kile unachotaka''. Mimi kama mtazamaji nilivutiwa sana na hayo mazungumzo kiasi cha kuweza
kutofautisha hiyo nomino (tajiri) na kivumishi (utajiri) kwa upana. Na kabla
msomaji hujafika mbali naomba kwanza
tuelewane katika haya mambo mawili; utajiri na tajiri. Nikisema utajiri namaanisha
ni kiasi ama hali ya kuwa na uhuru wa fedha unaoambatana na kumiliki mali na raslimali
kwa kiwango ambacho ni tofauti na watu
wengi wanaokuzunguka. Na tajiri ni yule mtu ambaye kafikia hiyo hali ya
kumiliki ukwasi (pesa,mali,raslimali) zaidi , kufuatia mipango, jitihada, malengo
na bidii katika uwekezaji alioanza muda
mrefu . Huu mchakato wa muda mrefu unaeleza wazi kuwa, miongoni mwa matajiri wengi mafanikio sio lelemama bali ni jasho itokanayo na
kudhibiti matumizi zidi ya
mapato. Kitendo kinachowapelekea mabilionea wengi wabakiwe na akiba ambayo hutumika mara
mbili. Kwanza katika kununua ‘asset’ na pili kulinda biashara zao.Matumizi ya fedha ya ziada katika kununua assets kama viwanja, mashamba, nyumba za kupangisha hutoa
faida nyingine . Hivyo kunakuwa na utajiri mpya unaoletwa na hizo ‘assets’ . Mchezo ambao ni mwendelezo kama vile kuku awezavyo kutotoa
mayai na mayai yakaleta kuku wengi zaidi.Na tumizi la pili ni jinsi akiba inavoweza kulinda
hazina ya mtu mwenye pesa, kwani akiba inayotokana
na miradi ya tajiri huifadhiwa kwa minajili ya kuokoa jahazi pale tu mambo yanapokwenda
mrama.Endapo ikitokea ujasiliamali wa bilionea unakumbwa na dhoruba ya madeni na hasara, hadi kuyumbisha mradi. Akiba ya tajiri
huyo huja kama nanga inayoweza kulinda mradi wake zidi ya dhoruba (madeni, hasara). Na
hivyo kuendelea salama akiwa kifua mbele daima. Mpaka hatua hii bado hatujaona
siri kubwa za matajiri, ungependa kuzijua ??,Basi msikilize Bill Gate, Michael Jordan, Steve Jobs, Oprah Winfrey na wengine wakidadavua siri nane za matajiri.
1. ''Kuzaliwa
masikini sio kosa lako,kufa masikini ni kosa''Anatoa siri hiyo Bill Gate ambaye aliacha chuo na kuonekana
hafai hadi pale alipopigana na kujipatia
mafanikio ya utajiri mkubwa ulioletwa na
jitihada ya kuanzisha kampuni yake maarufu duniani kama Microsoft.
2.''Nakubali
kuna kushindwa , kila mmoja hushwindwa ila sikubali
kutojaribu tena' Ni siri ya pili anayotoa Michael Jordan, ambaye amewahi
kukataliwa na timu yake ya shule ikisemekana hakuwa na kiwango cha kuridhisha
katika mchezo wa kikapu simanzi iliyomfanya kumwaga kilio cha uchungu kama mtoto
mchanga . Na leo hii baada ya kutoghairi na'kujaribu tena ' Jordan anaitwa
mchezaji bora duniani wa ‘basket’ na mwanamichezo tajiri ulimwenguni.
3.''Kila
mmoja ni balozi wa maisha yake , hakuna mwingine atawakilisha au kuishi kwa
ajili yako''Ni siri ya tatu anayosema Oprah Winfey aliyewahi kutimuliwa kazi katika kituo kimoja cha television kwa
madai kuwa hakufiti katika hiyo tasinia ya habari. Jambo lililomfanya ajisimamie
na kuwa vyote ‘balozi’na ‘mtendaji’ wa
maisha yake akanzisha kipindi cha
televisheni (oprah show) ambacho kilijichukulia umaarufu mkubwa hata kumfanya
afungue kituo binafsi cha tv, Oprah tv network. Uwekezaji uliofungua daraja la
ujasiliamali na Oprah kuwa miongoni mwa wanawake matajiri duniani.
4.''Maranyingine
unapofanya ubunifu ni rahisi kutenda makosa, ni vyema kuyabaini mapema (makosa) na kusahihisha'' Hii ni siri ya
nne iliyobeba mafanikio ya Steve Jobs, muasisi aliyewahi kusimamishwa kwenye
kampuni aliyoianzisha mwenyewe kwa madai ya kutofanya vizuri katika kampuni. Kitendo kilichomfanya aionyeshe dunia yeye ni nani hasa
pale linapokuja swala la ubunifu wa teknolojia'innovation'. Kwani
hasira za bwana Steve zimesababisha Ipod na iphone kuheshimika sokoni na yeye
kurudi kwenye kampuni yake ya Apple kama kinara wa ubunifi aliyeingia kwenye
chati ya matajiri wakubwa duniani.
5''Usiogope
kufa,ogopa kutojaribu'' Ni maneno ya bwana Shawn Corey Carter maarufu kama Jay Z. Ambaye alitemwa na kampuni kadhaa zinazojihusisha na usambazaji wa ‘albam’.Kisa kilichomchochea mwanamziku huyo wa miondoko ya kufoka foka kuuza na kusambaza kazi
zake mwenyewe . Huku akiwa ni mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja (mama). Jay z
hakusita kujaribu .kwa kuuza nakala za kazi yake ndani ya gari dogo, na kwa miguu hadi akajulikana
na kupata kianzio. Hatua iliyomfanya awe na njozi njema ya kutengeneza Recording Rebel, mavazi na
uwekezaji kibao hadi kuwa miongoni mwa wasanii tajiri duniani
.
6.''Siri
yangu kuwa na biashara iliyofanikiwa ni matokeo ya kujituma kwa bidii'' Anasema Aliko Dangote ambaye alitoka
nyumbani na kwenda kuchapa kazi kwa mjomba wake , mtu muhimu aliyemsaidia Dangote kupata mtaji na
kufanya biashara za sukari, cement ,.Akawa sio tu muuzaji bali
mzalishaji wa hizo bidhaa. Baraka hiyo ni jambo lililofungua njia ya mwafrika huyu kuitwa
tajiri wa kwanza Nigeria, Tajiri mkubwa Afrika na tajiri wa kwanza duniani kwa
watu weusi. (kwa muujibu wa gazeti la
uchumi, Forbes 2014)
7.''Nafasi
ya kuishi ni moja lakini hiyo moja ukiitumia vizuri inatosha'' Ni siri ya saba
inayosemwa na kundi la the Beatles ambalo linaundwa na waingereza wanne waliofukuzwa
studio kwa kile kinachosemakana' wana sauti mbaya na wasingekuwa na manufaa
yeyote katika soko la muziki'. Maneno hayo yaliwafanya The beatles watafute studio
zaidi na kupiga kazi kama vichaa hadi kuvunja rekodi ya mauzo hapo Uingereza na
Marekani. Baadae album yao ikaitwa ya
kwanza na bora duniani . Hivyo ikawa ni fursa ya kupata pesa na kuwekeza . Nafasi iliyopelekea kupata heshima ya ulimwengu kama kundi bora la muda wote katika
miondoko ya ‘rock’ na watu waliokamata fedha chafu zaidi miongoni mwa makundi ya
miaka ya 1960.
8.''Mafanikio
ni asilimia 1 inayotokana na asilimia 99 ya kushindwa'' ni siri
ya mwisho inayoletwa kwenu na bwn Soichiro
Honda ambaye ni enjinia wa kijapani aliepigwa chini na kampuni ya Toyota baada ya kutomzania kama injinia bora.Soichiro hakuwa na vigezo
ikiwemo elimu ya juu.Na hili hakukubali liwe ndio tatizo, kwani kama wenzake
tuliowaona,Soichiro Honda aliendelea kutengeneza mashine za magari na pikipiki huku hatua hiyo
ikitafsiriwa na baadhi ya watu kama ni ukanjanja na kushindwa.Mazingira
yaliomjengea kiu ya kutaka kufanikiwa haraka.Kabla ya kupata tuzo kutoka
ujerumani na kuwa raisi wa kampuni yake mwenyewe inayojulikana kama Honda Motor Company.Inayofanya vizuri dunia
nzima ,kwa kuzarishi sio tu piki piki bali pia jenereta,magari,mashine
za kufyeka nyasi n,k.
Friday, March 20, 2015
Binafsi
nimezoe miradi ya familia ni maduka ya bidhaa kama simu, nguo, mifugo, daladala, n.k. Ambayo huanza
na kasi ,baadae kudorora na baadhi ya miradi kupotea kabisa.Tafiti zinaonyesha kuwa kati
ya miradi mitatu ya familia ni mradi mmoja
tu hudumu.Na kwa huo mradi unaodumu hakika uongozi ni sindano kubwa katika kufuma timu ya
usimamizi wake.Wakati biashara hii inayomilikiwa kiasi kikubwa na wanafamilia
inategemea sana menegementi bora. Mataifa ya Izrael , Canada ambayo uchumi wake
umestawishwa kwa zaidi ya asilimia 65 na miradi ya familia.Wanatambua siri
nyingine za kufanikiwa kwa biashara zao. Moja, ni mgawanyo wa majaukumu baina ya
wanafamilia. Baba, mama ,kaka na dada anahusika na jukumu moja moja kati ya
uhasibu, matangazo, utafiti, soko na maboresho. Korea na India ambao pia ni
majabari wa miradi ya familia. Wanatambua fika kuwa,ukuu wao katika hizo biashara
ni matokeo mazuri ya kuweka mipango ya kudumu ambayo hufuatwa na kila kizazi
kinachorisishwa mradi. Palestine taifa lenye miradi mingi ya famillia kama
kitovu cha uchumi wake, pia wanang’oa mizizi ya maendeleo yao. Wakibainisha kuwa
kutoweka hisia za ndani katika hizi biashara ni nyota njema inayoangaza mafanikio
ya miradi ya familia.Katika suala la hisia mtama zaidi unamwagwa
kuwa,sio kila ndugu ajiriwe au kupata huduma ya bure, ila vigezo na
masharti vizingatiwe. Na Italy ambao ni watengenezaji suti wazuri wameachia
mikono ya familia inue haya mavazi ya thamani katika kila jicho la ulimwengu. Zaidi
ya asilimia 90 ya miradi ya kifamilia
nchini humo huepuka matumizi mabaya ya faida inayozalishwa na mradi , jambo
linalozuia mparaganyiko na kusambaratika kwa biashara zao.Ikumbukwe tu kuwa
miradi hii ni ya aina nyingi kama vidonge.Kuna miradi mikubwa kuna miradi midogo.Barafu,karanga,na
nyanya za magengeni ni miradi ya familia yenye sura ndogo.Makampuni ya
gari,simu,vitabu , ni miradi ya familia yenye sura
kubwa.Unafahamu biashara kubwa za kifamilia ambazo zitakuacha mdomo wazi ?,Basi
usichoke, tazama namba moja hadi kumi hapa chini.
1.Toyota
2.Ford Motor
3.Tata group
4.Volkswagen
5.Samsung
6.LG
7.Motorola
8.Siemens
9.Kodak
10.World
Wrestling Entertainment(WWE)
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...












































Dar+Es+Salaam