Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Wednesday, January 27, 2016
2.Millard Afrael Ayo.
Mwandishi wa habari , aliowahi kupewa tuzo ya mtangazaji bora wa
kiume anayependwa(2014), mwaka mmoja mbele, 2015, taaluma ya habari inamfanya atabasamu
kwa kufanikisha ufunguzi wa Kituo
binafsi cha redio alichokiita TZA.Ndani ya mwaka huo tabasamu inaendelea kushamiri
baada ya Millard Ayo. Com Kutunukiwa tuzo ya Website/blog inayopendwa Tanzania.
Katika tuzo za watu zilizofanyika Hyatt Legency, Dar es salaam. Ushindi huo
unakuja kwa kuziacha tovuti nyingine
kama; issamichuzi.blogspot.com, jamii forum. Com, dj chokamusic. Com. 2015 pia ilistawisha
mbegu za tabasamu jingine pale huyu mtu wa nguvu anayesihi watu wakae karibu na
speaker za redio, kuanzisha
Application(Millard Ayo app) inayopatikana Google play na play store.App
Inayosaidia wapenzi wa Habari anazotoa wasipitwe na chochote kile. Lakini tujiulize, Millard Afrael Ayo ni mtu
wa namna gani?...Huyu ni miongoni mwa Watanzania wabunifu, anaejua kutumia muda, wazo, pesa, na watu kwa dhamira ya kutimiza ndoto zake. Ndani ya
muda wa miaka 11 (toka 2004 alipoanza kazi ya utangazaji had 2015 mwaka wa
neema) Millard katoka ngazi ya ufukara mpaka Ile ya maisha bora. Wakati miaka
11 sio muda kidogo kwa hayo mabadiliko makubwa aliofanya. Huo muda umezaa
mawazo na mipango yakinifu ikiwemo; kufanya kazi na vituo bora vya matangazo
Tanzania (redio one /itv, clouds fm ) .Muda umezaa fikra za kuboresha
production, show na matangazo ya hewani yatakayofanyika chini ya Radio
yake.TZA. Mpango ambao ni moja ya malengo
matano ya siri, anayosema" muda ukiwa tayari nitaweka wazi
" Kuhusu pesa je?, Ujue sio rahisi
kila mtu kutunza sh. mia na hatimae siku moja utimize kiasi cha million moja.
Uwezo wa namna hii unapatikana ndani ya kingo za nafsi chache zilizokusudia
kweli . Millard Ayo anasemaje "kwa malimbikizo ya mshahara
amepata nguvu ya kununua vifaa vyote vya TZA. "kununua camera na mic za
kisasa zinazotumika na Millard Ayo TV. Matumizi ambayo sio tu yanaimarisha
anachokipenda (kazi) bali pia humsogeza karibu na watu. Mpaka mwaka 2015
Millard Ayo ni kipenzi cha watu. Anayeshika namba Tatu (3)Kwa kuwa mtanzania
maarufu aliyefikisha idadi ya followers
million moja na zaidi huko mitandaoni(instagram)
. Huku namba moja ikishikwa na Mwanamuziki Abdul Nasib maarufu "Diamond
Plutnumz" Namba mbili inakamatwa na aliyekuwa mwandani wake Diamond na
miss Tanzania 2007, Wema Abraham Sepetu. Watu ni kiungo kikuu cha mafanikio ya
Millard. Bila pongezi, maoni, chuki, upendo na ushirikiano wao, zile ndoto,
fedha, muda, na bidii pekee visingemfikisha hapo alipo leo. Kila lakheri
millard
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...
0 comments:
Post a Comment