Saturday, February 15, 2014
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza  maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia. Kusoma  ni mchakato wa kutambua na kubaini  alama, unaopelekea mtu kujenga maana. Maana hupatikana katika mpangilio  wa alama husika.Alama hizi ni kuanzia irabu , konsonanti hadi silabi. Ambazo kwa pamoja huunda neno,   kirai, kishazi na hatimaye sentensi .Sentensi pia hujenga aya , na hizi aya  zikiungana  huunda kitu kinaitwa  habari . Wakati unagundua jinsi  mfumo mzima ujengao habari unaundwa na vipengele vidogo vidogo zaidi ya kimoja .Kusoma na kuelewa habari pia kunaundwa na mbinu kadhaa. Kutoa mwangwa zaidi juu ya huu muundo wa usomaji katika  makala, kitabu au chanzo chochote cha maarifa. Tazama hizi mbinu   nne  za usomaji .
1. Kusoma kwa kina neno baada ya neno katika habari (Usomaji dhati)'Intensive reading'

2.Kusoma habari kubwa ukipitia upesi maeneo baadhi tu, na sio kila neno (usomaji wa haraka   zaidi )'scanning reading'

3.Kusoma   ili kupata maana ya habari kwa ujumla  (usomaji kawaida)'extensive reading'

4.Kusoma kwa kulenga dhana na wazo muhimu tu katika habari,na kuacha maeneo mengine.
(usomaji haraka)'skimming reading'
 

4 comments:

  1. Somo hili niliuwa nikilitafuta sana ila leo nimelipata.. asante

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa huu ujumbe. Nimesaidika

    ReplyDelete
  3. Maelezo faafu heko ya maana ya kusoma na aina zake

    ReplyDelete
  4. Maelezo faafu ya maana ya kusoma na aina za kusoma, heko.

    ReplyDelete

Popular Posts