Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts
Thursday, September 11, 2014
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na ajira hawakuweza kutafta mvuto kwa namna inayohusisha gharama kubwa.Hawakuweza kuingia gym, hawakuwrza kumudu vifaa maluum vya bei mbaya. Hali iliyopelea mmoja kati yao kutafta mwalimu wa mazoezi ya mwili kwa njia ya mkopo. Na mwingine kujisimamia katika mazoezi ya aina hiyo bila mwalimu kabisa. Neema alipata msaada mkubwa toka kwa huyu mwalimu wa mazoezi. Ibrahim halikadhalika alifanikiwa kutokana na bidii aliyojiwekea katika mazoezi. Wawili hawa katu hawakukata tamaa ya mazoezi hata siku moja kwa kuwa walipenda michezo kuliko kitu kingine.Walipenda kuwa wanamitindo kuliko kazi nyingine. Walivutiwa na uzuri kuliko sifa nyingine. Baada ya miezi mitatu kupita huku zoezi ni kama dini na kitu cha muhimu kwao, mmoja wa vijana hawa anatokea kuwa kisura aliyevutia sana na mwingine ni mtanashati aliyependeza sana. Huku siri yao kubwa kufika hapo walipo ndani ya muda kidogo, ikitokana na juhudi katika mazoezi yafuatayo..
1,KURUKA KAMBA. Ni zoezi rahisi lisilochukua gharama kubwa.Zoezi hili linafanyika sehemu nyingi kwa sababu vifaa vyake ni rahisi kubeba na hupatikana kwa uepesi.Kwa kuwa linahusisha mikono,miguu,mgongo na viungo vingine vya mwili,huongeza stamina,nguvu na kukaza misuri ya mrukaji. Ni moja ya zoezi zuri katika kupunguza uzito wa mwili.
2.KUKIMBIA.Ni zoezi linalofanyika uwanjani,barabarani,mbugani na sehemu nyingi za uwazi mkubwa.Zoezi hili hupendeza pasipokuwa na jua kali hasa majira ya asubuhi na majira ya jioni..Ni moja ya zoezi zuri kwa mapafu na moyo.Kwani viungo hivi hurejesha msukumo wa damu na hewa kuwa vyema,kiasi cha mkimbiaji kupata nguvu na pumzi ya kutosha katika mwili wake.
3.PUSH UP. Ni zoezi rahisi, linalochukua gharama ndogo sana na gharama hii ni muda pekee . Mbali na muda, push up hazihitaji uwanja mpana zaidi ya chunba chako. Kwa kupiga push up ndani ya nyumba itakusaidia kukaza mwili sehemu ya juu. Ukianza na kupanuka kifua, ikifuatiwa na kuimarisha mabega, mikono mgongo na tumbo. Ni zoezi zuri kwa ukakamavu
4.KUOGELEA . Ni mchezo ambao huvutia watu wengi, watoto kwa wakubwa wenye kipato na wasionacho. Lakini wakati karibu kila mmoja anafurahai mchezo huo, kuna faida nyingi mwili hupata Kwanza ni mara mbili ya zoezi la kukimbia, na huimarisha misuli ya mwili kutokana na ukinzani wa maji. Pili huondoa mfadhaiko na msongo wa mawazo, tatu ni zoezi linalohusisha
miguu, mikono, mabega na viungo vya mwili karibu vyote na baadae mwili hujengeka na kukaa fiti.
5.KUENDESHA BAISKEL. Kwa kuendesha tu usafiri wa baiskel ni sehemu ya zoezi muhimu sana kwa afya . Miguu inapokazana kupita mpando na ama tambarare. Mwili unashitua misuli inayosukuma nguvu zaidi . Zoezi hili linasaidia ubongo kwa kuwa makini na kunakiri chochote kinachoendelea. Unapofikia hatua ya kutoa jasho wakati wa zoezi hili , inasaidia kupunguza taka mwili na mafuta yasiotakiwa mwilini. Hatimaye mwendeshaji mwenye uzito mkubwa atakuwa anapunguza uzito endapo tu ataendesha baiskel mara kwa mara.
Thursday, February 20, 2014
Mazoezi ni lulu katika mwili ni nuru katika akili ni siri katika ushindi .Hapa ni baadhi ya mazozi yakifanyika ufukweni na timu ya wacheza kikapu , STEMMUCO , ilipokuwa mkoani Lindi
1.2
3
4
5
6
7
8
9
10
12
13
14
Sunday, October 27, 2013
Kuna vitu vingi binadamu ni vigumu kuviepuka. Moja ya vitu hivi ni kitendo cha kusinzia, kulala au vingenevyo utavyopenda kuita. Usingizi unamahusiano ya karibu sana na maisha yetu ya kila siku. Furaha, wasiwasi na aina nyingine za hisia huathiriwa kwa kiasi kikubwa na usingizi. Mbali na kuathiri, usingizi hutawala hali nzima ya kila siku. Kwa kutekeleza vyema , kawaida au vibaya katika majukumu. Majukumu haya ni pamoja na kusoma, kutibu, kufundisha n.k. Sababu ipelekeayo aina fulani ya utekelezaji leo, ni matokeo ya muda na masaa ya usingizi mtu aliopata kusinzia jana . Baadhi ya tafiti na chunguzi za kisayansi zinaonyesha binadamu kwa wastani hupaswa kulala kwa masaa yasiopungua manane(8). Mafanikio haya ya kisayansi katika tafiti na uchunguzi hayakutinananga hapo tu, bali yalijikita ndani zaidi na kupata mwanya wa kutoa faida kadhaa zitokanazo na usingizi. Na hivyo zifuatazo ni faida tisa zitokanazo na usingizi.
1.Kujenga kinga ya mwili
2.Huboresha kumbukumbu
3.Huwezesha kutafakari vyema
4.Kuharakisha umetaboli''metabolism''
5.Huleta hali nzuri''good mood''
6.Hupunguza mfadhaiko''stress''
7.Hupelekea kujifunza vyema
8.Huchochea umakini''concentration''
9. Hupunguza uzito wa mwili
Saturday, September 21, 2013
Baada ya kuona sababu kuu nne(4)za usahaurifu katika kujisomea.Hapa tutatazama njia mbadala za kuepuka tatizo la usahaurifu.Lakini mbali na kuzungumzia njia hizi mbadala.Inampasa msomaji kujenga kumbukumbu wakati wa kusoma. Kwa kuachana na sababu zipelekeazo usahaurifu,na kuanza kusoma vitu vichache,kuweka umakini wa kutosha,kuelewa anachosoma na kuwa katika hali njema ya afya.Na hizi zifuatazo ni njia mbadala sita(6) za kuepuka usahaurifu.
1.Zingatia mlo bora kwa afya
2.Fanya mazoezi ya mwili
3.Pata masaa takribani 8 usinziapo
4.Weka kanuni binafsi zitakazo kukumbusha
5.kazia kumbukumbu kwa kufundisha wenzako
6. Zingatia,tunza na tumia vyema muda
Monday, September 16, 2013
Usahaurifu katika usomaji ni hali ya ubongo kushindwa kurejea,kukumbuka au kuwaza baadhi ya vitu vilivyosomwa muda uliopita.Hivi vitu ni pamoja na maada mbalimbali(topics), masomo na majibu ya maswali kadhaa ambayo huwa ni muhimu katika kusoma. Bila kuzingatia mtu alisoma kwa muda gani,mfupi au mrefu ,masaa mengi au machache,usahaurifu umekuwa kikwazo kwa watu wengi sana hasa wanafunzi,hata kupelekea kutofanya vyema katika mitihani na masomo yao kwa ujumla.Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuna sababu nyingi zipelekeazo mtu mmoja kusahau.Katika kurasa hii tutangalia sababu hizi katika makundi makuu manee(4).
1.Usomaji wa vitu vingi bila mpangilio na ratiba maalum
2.Kutoweka umakini wa kutosha katika kile kinachosomwa
3. Mwanafunzi kutoelewa anachokisoma
4. Hali ya kiafya kama mawazo,msongo ,magonjwa n.k
Monday, January 7, 2013
Katika viungo muhimu binadamu alivyobarikiwa kuwa navyo moja wapo ni mikono. Mikono huweza kumfanya mtu mmoja awe maarufu au kubaki kawaida,matumizi chanya ya mikono hujenga,hukuza na kuleta kipaji kikubwa.Hata sasa sura ya mikono utaiona yenye thamani machoni pako kama thamani ya dhahabu,almasi na pengine hata zaidi lulu.Zifuatazo ni picha za vipaji kumi(10) vitokanavyo na mikono
1.Mchezo wa kikapu2.uchoraji
3.uandishi
4.uandaaji mziki
5.ufundi radio
6.kupika
7.kutafsiri vitendo
8.kudaka
9.ujenzi
10.kuchapa(typing)
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...


































