Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label picha. Show all posts
Showing posts with label picha. Show all posts
Monday, June 23, 2014
Kwa rika ni kijana , kijana wa futi 5, mtazamo ni chanya, chanya inayo aksi elimu ya juu, idadi ni wa pili kati ya watoto watano
wa familia ya mh Abraham.L.Chaula.Ni mwajibikaji, ni mwanamapinduzi na mwanaharakati asimamapo kati ya ndugu, jamaa na
rafiki zake . Utendaji ni mwana fasihi
anayefanya sanaa inayoshabiana na vitu vitatu muhimu ambavyo ni, maisha, mazingira halikadhalika tamaduni
inayomzunguka. Kwake uthubutu ni
kujituma, kujaribu na kufikia malengo. Kitu ambacho ni cha thamani na kinahitaji
juhudi zaidi . Huyu siye mwingine isipokuwa ni Izacka chaula(Chella), ambaye ni
mmoja ya watu waliobahatika kuliona jua takribani miongo miwili na nusu
iliyopita. Kwa maana ya kutimiza miaka 24 sasa toka azaliwe mwaka 1990 , huko wilayani Njombe (hivi sasa ni mkoa) ndani ya
mji wa Iringa. Akiwa huko mwanzoni mwa miaka ya 2000, ana umri usiozidi miaka 10 , kipaji chake kama vipaji vingine kinastawishwa na kuchavushwa na
baba yake mdogo anayeitwa Zakayo L Mwalongo (Mtoza Mc) ,ambaye ukaribu wake na Chella unajenga kundi linaloitwa MICHANO LUKUKI, kama ngao ya ujuzi
katika uandishi wa tungo maridhawa. Hatimaye mtoto huyu wa pili kati ya watoto watano anagundulika na
karama ya kupenyeza mawazo pevu, endelevu na shawishi kwa uwezo wake katika uandishi wa beti na mizani
mahiri ,jambo ambalo linamfanya awe mjuzi wa matatizo , changamoto na matukio mbalimbali ya jamii na jumuiya anayoishi. Baadae
sifa ya uandishi wa mashahiri yenye
kuonya, kukanya na kufungua mboni na ngome za masikio mengi, inajenga taswira
pevu , komavu , pale anapokuwa shule ya msingi Kibena mkoani Njombe. Hapo
shuleni marafiki wanaelewa na kutambua harakati na Sanaa anayoifanya Chella . Ndipo
sasa anatilia maanani tunu yake aliobarikiwa kuwa nayo na kuboresha
zaidi hicho kipaji , anapoingia sekondari
ya Mpechi na Philip Mangula na kupata nafasi ya kushiriki shindano linaloitwa Philip
Mangula Star Search (PMSS).Tukio linaloandaliwa na uongozi wa shule, mahususi
kutafuta vipaji vya wanafunzi shuleni hapo. Mnamo mwaka 2008
akiwa kidato cha nne shuleni Mangula , Izacka Chaula maarufu sasa kama Chella
anakuwa mshindi namba moja zidi ya washiriki
wengine wapatao 30, walioshindana katika tukio hilo la kumtafta bingwa mmoja. Safari ya matumaini, iliyojaa utashi na wingi
wa ueledi inapata mafanikio, pale mshindi huyu anapobahatika kujiunga na elimu ya kidato cha
sita, Kwiro Boys high school, huko wilayani Mahenge Ulanga, mkoani Morogoro. Ni ndani ya mji huo usio na bahari, hisia
za kutaka kurejea studio zinamshamiri mwanafunzi
huyu . Hivyo anashawishika kuandaa tungo ya nyimbo yake ya kwanza
anayoipa jina la “Rudi mkoa”. Kibao kinachoelezea tabia ya vijana wengi kulowea katika miji mikubwa kama Dar es salaam huku wakisahua kurudi mikoani mwao.Ila utunzi na Sanaa hii haibadiri dira na imani yake katika elimu, kwani yeye huamini kuwa, elimu ndio taa inayoweza kufukuza giza la ujinga na
kurejesha nuru ya maarifa. Mwaka 2011 mwanaharakati huyu anafaulu kidato cha
sita, hivyo anajiunga na masomo ya juu katika chuo cha SAUT Mtwara (STEMMUCO ). Akiwa chuoni hapo anapata fursa ya kuwa mmoja kati ya wanachuo wanaounda kundi linalojihusisha na maswala ya muziki na
sanaa,kundi hilo linajulikana kama Stemmuco All Stars .Vitu vitatu anavyovipenda chella ndani ya kundi ni umoja na ushirikiano wa wanazuoni,vipaji vikubwa walivyonanvyo wasomi wenzake na michango mizuri itokanayo na mitazamo chanya. Mbali na shughuli za kikundi , thamani na
mchango wa wanakikundi ,Chella amekutanisha
mawazo yake na watu wengine wenye tunu
ya kuandaa mashahiri yenye shabaha katika kuelimisha na kufunza. Hawa mahodari wa fasihi
andishi ni pamoja na Mtoza mc, Domokaya, BeckaTittle, Jebby Mubarak, Joseph Haule’’ prof
jay’’, P-the MC, Juma Kassim Kiroboto ‘‘juma nature’’ Juma Jazz , Nicolazo n.k.Wanaomsaidia
Kutoa kwa ufasaha kila aina ya uwezo na kitu alichanacho msomi na mtanzania huyu. Anafanikiwa
kuandika mashairi mazuri na hatimaye kutia sauti yake inayoibua chachu ,
mapinduzi, na mabadiliko ya sanaa yake.Hali hii ni kielelezo tosha jinsi mwanaharakati, mwanamapinduzi na
mwajibikaji huyu anavyopigana kwa hali
na mali hata kuingia mikoa zaidi ya
mitano ,mitaa zaidi ya tisa,katika studio zaidi ya 10 ,akifanya kazi na
waandaji wa midundo(music producer) wasiopungua 7 na kushirikiana na wasanii
wanaonzia 10 hadi 20.Chella amefanikiwa kuingia baadhi ya miji kama Dodoma, Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Njombe Mbeya, Ruvuma
na Mtwara . Akifikia mitaa mbalimbali ya
mikoa hiyo kama Railway, Masaki, Kinondoni, Kigogo, Mbezi, na kuingia studio za Tongwe
Rec, Mkubwa na Wanawe, Koma studio, Robbies Rec , Kp Rec, Shine Rec, Natal
Rec, Baridi Touch, E-Lab,Kimya Rec , Mama Land Rec, George Rec,Goka rec,AB Rec na nyingine
nyingi, chini ya waandaji mahiri wa muziki nchini wakiwemo akina Geof Master(manuva), Kona Beats,Main,
Jero,Pezo,Tonny(Efficiency man), Necka Beats, Jose Braiz Beats,Kagusa Andrew. Uchaguzi wa wadau hawa wa
muziki , umezingatia vitu vikuu viwili ambavyo ni, uchipukizi na
ukongwe wao katika tasinia ya mziki, unaochangia kazi kuwa
na uzuri. Upekee na ubunifu tofauti wa kazi zao. Mantiki
inayopelekea kuonekana kwa vionjo vya kiasili na radha iliyojificha ndani ya sanaa na kazi za mwana
hip hop na msomi huyu. Baadhi ya kazi ambazo Chella kafanya ni pamoja na Rudi
mkoa (Dar imekupa kiburi), tatizo nini (ft Geof Master), nitafika ft becka Title, mimi
na Yule ft Juma jazz, ningezaliwa Dar, naongea na wallet, Bado napambana,jiulize
, usiniache , Azimio la kijiji n.k, . Kazi hizi na ushirikiano alioufanya
msanii huyu na wajuzi wengine toka nje na ndani ya tasnia ya muziki
imesaidia katika kumjengea mtazamo wa
ziada Ukiachilia kando kimkoa, kikanda na
kitaifa Chela ana mtazamo na ndoto za kufikia ngazi ya kimataifa kwa kufanya
kazi bora zaidi kama zile za kina Marshall Bruce Mathers ''eminem''na wana hip hop wengine wanaofanya vizuri duniani kote.
Monday, May 12, 2014
Kila kukicha bendera ya Afrika inazidi kupepea.Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa kimataifa , 2013. Kati ya mabara saba duniani, Africa ni sehemu ya pili kwa kuwa na wakazi wengi ulimwenguni wanaofikia idadi ya watu billioni moja . Kwa namba hiyo eneo hili lenye jumla kubwa ya waafrika linakuwa nyuma ya Asia, bara lenye wanaume na wanawake wengi wanaokadiriwa kufikia bilioni nne . Afrika tofauti na mabara mengine ni mahali panapotoa fursa ya wanadamu kuishi kwa upendo , kuishi kwa mshikamano na kusaidiana kama ndugu wa familia moja. Ukaribu unaojengwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya utu . Tabia hii nzuri ni zao la utamaduni usiohoji maswali kama wewe ni nani, unatoka wapi, unamiliki nini n.k. Wanasema ukitaka kuona shina la ukarimu, mizizi ya uungwana chonde chonde usisite kukanyaga ardhi ya Afrika. Ukitaka kuona ngozi ya kipekee iliyobeba mvuto na mwonekano asilia kama ''chocolate'' hima hima rejea barani Afrika.Pia ukipatwa na shauku ya wanyama wazuri, madini ya kipekee, misitu na mbuga kubwa zenyekustaajabisha moyo na macho kamwe usisite kufika Afrika. Kwa kuwa ni mahali sahihi kwa hadhina hiyo. Kama haitoshi, sura nchi ya eneo hili lenye watu wenye nguvu nyingi , linazungukwa na bahari takribani nne, ikiwemo ile ya Hindi, Atlantik, Meditreniani na bahari Nyekundu ''Red sea''. Toka usawa wa bahari Afrika imemejaariwa miinuko mikubwa, milima mirefu hata kufikia zaidi ya mita 58OO . Mfano mwepesi kabisa ni mlima maarufu ulimwenguni, kilimanjaro. Kando na vilima, mipando na aina nyingine za miinuko yenye kupendezesha macho sana. Bara hili lenye kabila nyingi za asili ya kibantu lina mabonde, miteremko na nyufa ambazo ni njia na nyumba ya maziwa , mito na chemchemi. Sehemu hizi za maji zina majina makubwa yavumayo Ulaya, Amerika, Australia na kwingineko ulimwenguni .Ukiachilia mbali ziwa Tanganyika na mto Naija kuna ziwa Victoria na mto nile kama vivutuo maarufu . Lakini ikumbukwe ni ndani ya mabonde ya bara la Afrika tu ambapo historia inasema, fuvu la binadamu wa kwanza duniani lilivumbuliwa. Baadae teknolojia ikathibitisha masalia ya mafuvu hayo na ya viumbe hai wengine walioishi miaka mingi barani hapa, imechangia wingi wa nishati ya gesi na mafuta katika ardhi ya Afrika. Nishati hii inaweza kuzalisha umeme mkubwa sana.Gesi ya Mtwara ,Tanzania na Oil ya Naija Dellta, Naijeria ni mfano kidogo tu wa nishati hiyo iliyojificha mabondeni humo. Mwisho ni vyema kujifahamisha kuwa kama binadamu anavyopitia vipindi kadhaa hadi kukua. Halikadhalika ardhi hii ya watu weusi imepiti vipindi vikuu takribani sita. Vikiwemo vile vya ; ukuaji wa miji ''state formation'' , kukutana na wageni ''the early contcact'' , biashara ya utumwa, biashara harali '' legitimate trade'' , ukoloni, uhuru na hatimaye ukoloni mambo leo '' neo colonialism''
![]() |
| Mbuga ya Serengeti ni miongoni mwa vivutio vikubwa barani Afrika na hapa ni wakati wa mawio |
![]() |
| Dhahabu |
![]() |
| Almasi |
![]() |
| Madini ya Tanzanite |
![]() |
| Twiga wa Afrika |
![]() |
| msitu wa Kongo |
![]() |
| mto Nile |
![]() |
| Wageni toka mabara mengine wakikaribishwa Afrika ,hapo juu ni msanii Shaggy |
![]() |
| umoja na ushirikiano ni jadi isiyofichika barani Afrika |
![]() |
| Visura wenye rangi ya chocolate ni chimbuko la Afrika |
Thursday, February 20, 2014
Mazoezi ni lulu katika mwili ni nuru katika akili ni siri katika ushindi .Hapa ni baadhi ya mazozi yakifanyika ufukweni na timu ya wacheza kikapu , STEMMUCO , ilipokuwa mkoani Lindi
1.2
3
4
5
6
7
8
9
10
12
13
14
Wednesday, November 6, 2013
Ni jumamosi, wiki ya tatu ya mwezi oktoba,mashindano makubwa yanayoshirikisha michezo na burudani mbalimbali katika chuo kishiriki cha SAUTI,Stella Maris Mtwara, yakiarudi kwa kishindo kikuu. Haya mashindano ni maarufu sana kama BIG SCORE. Huku mwaka huu, 2013 yakichukua sura nyingine kabisa. Mashabiki, wachezaji na viongozi hawarudi nyuma pia kufanya kila liwezekanalo katika kuboresha sura hii mpya. Msimu huu washiriki wanaongezeka. Wakitoka ngazi tofauti za elimu kama ngazi ya cheti,stashahada na shahada. Mbali na wimbi la ushiriki, michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na mpira wa mikono unatiwa hamasa na radha kwa ingizo jipya la wachezaji hodari na mashabiki machachari. BIG SCORE kama mashindano mengine, inaundwa na uongozi wenye malengo mengi. Moja ya malengo hayo ni kukuza na kuendeleza mahusiano mema baina ya washiriki. Kwa maana ya wanafunzi, , viongozi, watawala, wafanyakazi na watu wengine ambao ni sehemu ya jamii ya hiki chuo,Stella Maris Mtwara.Hapa chini ni baadhi tu ya matukio yaliopata kujiri katika uzinduzi wa mashindano haya ya wanataaluma.
1
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...
























