Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Monday, January 4, 2016
Nikiwa
mwanza mwaka 2004 nilikuwa mwanafunzi aliyependa somo la historia. Moja ya mada
niliyopenda ni colonialism. Mada ilinifunza , miongoni mwa athari walioleta
wakoloni ni kurudisha nyuma maendeleo ya
Tanzania. Huku maeneo ya kusini mwa nchi yakitajwa kuwa duni zaidi ya kwingine. Nikasoma pia Mtwara na
lindi ni mfano wa maeneo hayo. Lakini cha ajabu mwaka 2011 nikiwa mwaka wa
kwanza katika chuo kimoja cha hapa mtwara niliona mambo ni tofauti .Mtwara ya kipindi hiki inapiga hatua kuliko
picha niliojengewa na ile mada. Kuna ulinzi wa mali na usalama wa afya. Kuna
shule, vyuo na taasisi za elimu. Kuna viwanja vya michezo, vikundi vya sanaa na
mahala pa burudani.Kuna viwanja vya ndege,bandari na stand za bus. Kufikia
mwaka 2014, niliona Viwanda vya cement, vyombo vya habari, na rasli mali za
mafuta na gesi, huku fukwe za mtwara
mjini zikiwa na hotel nzuri na maandhari safi. Nakumbuka katika kufurahia mazingira haya nilikuwa napiga zoezi kila
alfajiri. Kisa kilichopelekea nipoteze simu.Pale uchovu uliponifanya nisahau hicho
chombo cha mawasiliano juu ya canteen ya chuo. Mungu ni mkubwa simu
ilipatikana siku kumi baadae.(Niliipata
vipi hiyo ni stori ya siku nyingine) na mwishoni mwa mwaka 2015 nikirudi chuoni kwa ajili ya kumsapoti mdogo wangu aliehitimu
chuo .Nilipata bahati kutembelea fukwe
tofauti tofauti. Msanga mkuu, Veta, makonde, bandari ya zamani . Ambapo
sikusita kuogelea baharini , wakati
nafanya hivyo mwenzangu ambaye ni mgeni hapa aliniuliza, ’’ni mambo gani ya
kuzingatia katika fukwe za mtwara?’’ Nikiwa majini nilianza kwa kumwambia . ’’Yapo
mengi ya kuzingatia ila nitaanza na haya’
’
’
1.URUMBA (wadudu).
Ukiwa unaogelea kuwa makini na wadudu walio na miiba iliyowazunguka mwili
mzima. Wakiwa katika rangi nyeusi na sura ya duara mara nyingi wadudu hawa
hujisogeza karibu na miamba . Na kwa kuwa miiba yake ni nchi moja na zaidi na
upana wa sindano ya mkono , ukimkanyaga mmoja mwiba unavunjikia mwilini mwako. Idadi
ya miiba iliyokuingia inasababisha
mwasho mkali, maumivu na baadae homa. Wenyeji wa pwani wanashauri
ukipatwa na tatizo hili(urumba) , mapema chukua
mafuta ya taa tia mahala miiba imeikuingia. Baada ya siku mbili mpaka
tatu utapona
.
2.ASKARI. Uwapo
katika fukwe za shangani, kama makonde na veta askari wa dolia ni wengi. Hivi
vikosi haviruhusu raia abaki maeneo haya muda wote. Ikifika saa 12 :30 jioni , watu
hufukuzwa. Saa 1 giza likiwa kubwa askari polisi hukamata watu . Raia hufikishwa
kituoni. Wakipewa adhabu ya kutotii sheria za fukwe.
3.MV
MAFANIKIO. Ni feli inayobeba magari ,mizigo na watu wanaotoka na kuelekea msanga mkuu.Baada
ya fukwe za veta na makonde kuwa na mashabiki wengi. Fukwe za kivuko cha Msanga
mkuu ndio imekuwa habari ya mjini miongoni mwa watu. Hakuna namna ya kuenjoy
pwani hii kama hujui utaratibu wa Mv mafanikio. Huanza asubu sana kukamilisha
safari yake. Muda wa mwisho ni jioni saa
12. Kabla ya kuondoka hupiga honii. Ukifika chomboni mkononi uwe na ticket . Kuna
nauli ya mtu, gari na mizigo mikubwa. Mpaka mwaka 2014 disemba nauli ya mtu
mzima ilikuwa ni sh. 300.
4.KUPWAA NA
KUJAA. Raha ya fukwe ipo machoni mwa mtazamaji. Hivyo ni msingi kutambua wewe
unapenda msimu wa bahari ikiwa ina maji au ikiwa haina. Kuna nyakati bahari hupwaa,
hapa ni muda maji yapo mbali sana na fukwe. Ukitazama utaona maadhari kama ya
jangwa, miamba vigumu kupata maji ya shingo wala ugoko. Na wakati imejaa huwa
ni wiki nzuri kwa waogeleaji. Ukitokea
pwani utaona fukwe zinatenganishwa na mawimbi ya amaji. Ukiyafuata yatakuanzia kweye
ugoko ,kiuno , shingo mpaka mwili mzima utabebwa .
5.SIKU KUU. Ni
siku njema kwa mambo mengi zikiwemo fukwe. Wakati wa chrismas, mwaka mpya, Idd n.k Fukwe za mtwara hufurika watu
zaidi ya mchanga. Siku kuu wanavyuo, watoto wa mjini, raia wa kawaida kutoka
kona zote za mtwara hujumuika hapa. Hizi siku mhimu huambatana na matukio mhimu
kama upigaji picha , biashara za vyakula na vinywaji. Huku mziki , nyama choma
na burudani zikiwa pale fukwe ya
makonde.
6.USAFIRI. Ni
mhimu kujua utatokaje eneo moja hadi jingine. Kama ilivyo lazima kujua
utafikaje ufukweni endapo upo nyumbani. sio vigumu , kama wewe unaishi mtwara
au ni mgeni nabado haumiliki chombo cha usafiri. Kwanza kuna usafiri wa aina
nne. Taxi,Bajaj,Bodaboda na baiskel. Pili kila usafiri una gharama yake. Wakati
taxi au gari za kukodi zikiongoza kwa gharama, bajaji na boda boda(pikipiki)
huwa ni nafuu ikitegemea na idadi yenu. Ukiwa ni mtu wa mzoezi baiskel zipo
unachotakiwa ni kukodi na kueleza unachukua kwa masaa mangapi. Mwisho kabisa
kwa wewe unaeishi mbali na hizi fukwe ni mhimu kutambua kuwa usafiri
unapatikana.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...
0 comments:
Post a Comment