Showing posts with label maneno. Show all posts
Showing posts with label maneno. Show all posts
Monday, July 18, 2016

Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani  ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo  na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo  ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa  lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini  mara saba katika  kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?.  Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya  hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.

1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain

2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki


3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr

4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''

5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya tatizo na utatuzi
6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.
7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea  kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo safi zaidi ya ulivyokuwa hapo  mwanzo
8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo utalisogelea.

9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.

Saturday, June 25, 2016
Wakati wengine wakisema ujuzi ni aina ya  kazi au shughuri yenye kufanyika vizuri baada ya  elimu au mafunzo maalumu.Wahenga wanasema  ujuzi hauzeeki.Kwa maana  ni  uwezo unaopatikana kwa mtu hasa akiwa amepita hatua ya  kupokea  maelekezo, na kufanya matendo mengi.Dhana ya ujuzi imekuwa ya kikazi au ki uwezo kulingana na mfumo  anaoaksi mtu..Ukiwa ni  mtumishi wa ofisi rasmi ujuzi wako itakuwa ni utoaji wa huduma inayokubalika hapo kazini kwako.Na endapo umejiajiri au kuajiriwa sekta zisizo rasmi ,ujuzi ni ule uwezo wa kutoa matokeo mazuri ya  chochote  chema unachofanya.Kwa muda mwingi njozi kubwa na fikira pana zimekuwa kama  baba na mama wa ujuzi  katika mazingira yetu.Kujua zaidi kuhusu hilo fuatilia haya maneno 10

1.Kama mmea ustawivyo kwa mbolea na sio jua kali ndivyo Ujuzi umtajirishavyo mtu na sio maneno matupu

2.Ni vyema kila mmoja akawa na kila ujuzi na asiutumie,kuliko kutokuwa na huo ujuzi na ukataka uutumie


3.Kuna sheria za kufuata ili ubahatike,na kila jambo haliundi bahati,kwa waelevu wanatambua ujuzi ni njia mathubuti ya kuwa mtu mwenye bahati


4.Kumpatia mwanao ujuzi ni bora kuliko kumpatia vipande elfumoja vya madini ya dhahabu

5.Elimu huja kwa kujifunza ila ujuzi huja kwa uzoefu.


6.Elimu pekee sio ujuzi, bali ikizidishwa mara elfukumi ndio itakuwa ujuzi

7.Marudio ni mama wa ujuzi

8.Ujuzi ni mshikamano wa  uzoefu,akili na upenzi wa jambo vikiwa pamoja

9.Ujuzi na kujiamini ni jeshi lisilopigwa wala kushindwa


10.Kama huna ujuzi  ipo siku  inakuja kipaji chako kitakwama,kwani ujuzi  ni dhana ya matendo,bidii na shauku ya kutaka uwe bora kila kukicha,

Thursday, April 16, 2015
Katika moja ya kipindi  cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa kwanza ni ‘utajiri’ na msamiati wa pili  ni ‘tajiri’. Mmoja alisisitiza ''utajiri ni kuwa na chakula kingi,nguo nyingi na nyumba nyingi'' Wapili alikanusha usemi wa mtu wa kwanza na kaka wa tatu akadakia kwa mbwembwe zote akisema''tajiri au utajiri ni kuwa na kile unachotaka''. Mimi kama mtazamaji nilivutiwa  sana na hayo mazungumzo kiasi cha kuweza kutofautisha hiyo nomino (tajiri) na kivumishi (utajiri) kwa upana. Na kabla msomaji hujafika mbali  naomba kwanza tuelewane katika haya mambo mawili; utajiri na tajiri. Nikisema utajiri namaanisha ni kiasi ama hali ya kuwa na uhuru wa fedha unaoambatana na kumiliki mali na raslimali kwa kiwango  ambacho ni tofauti na watu wengi wanaokuzunguka. Na tajiri ni yule mtu ambaye kafikia hiyo hali ya kumiliki  ukwasi (pesa,mali,raslimali) zaidi , kufuatia mipango, jitihada, malengo na bidii katika uwekezaji alioanza  muda mrefu . Huu mchakato wa muda mrefu unaeleza wazi  kuwa, miongoni mwa matajiri wengi   mafanikio  sio lelemama bali ni jasho itokanayo na kudhibiti  matumizi zidi ya mapato. Kitendo kinachowapelekea  mabilionea  wengi wabakiwe na akiba ambayo hutumika mara mbili. Kwanza katika kununua ‘asset’ na pili kulinda biashara zao.Matumizi ya fedha ya ziada katika kununua assets kama  viwanja, mashamba, nyumba za kupangisha hutoa faida nyingine . Hivyo kunakuwa na utajiri mpya unaoletwa na hizo ‘assets’  .  Mchezo ambao ni mwendelezo kama  vile kuku awezavyo kutotoa mayai na mayai yakaleta kuku wengi zaidi.Na tumizi la pili ni jinsi akiba inavoweza kulinda hazina ya mtu mwenye pesa, kwani  akiba inayotokana na miradi ya tajiri huifadhiwa kwa minajili ya kuokoa jahazi pale tu mambo yanapokwenda mrama.Endapo ikitokea ujasiliamali wa  bilionea  unakumbwa na dhoruba ya madeni na hasara, hadi kuyumbisha mradi. Akiba ya tajiri huyo huja kama nanga inayoweza kulinda mradi wake zidi ya dhoruba (madeni, hasara). Na hivyo kuendelea salama akiwa kifua mbele daima. Mpaka hatua hii bado hatujaona siri kubwa za matajiri, ungependa kuzijua ??,Basi msikilize Bill Gate, Michael Jordan, Steve Jobs, Oprah Winfrey na wengine  wakidadavua siri nane za matajiri.

1. ''Kuzaliwa masikini sio kosa lako,kufa masikini ni kosa''Anatoa siri hiyo  Bill Gate ambaye aliacha chuo na kuonekana hafai hadi pale  alipopigana na kujipatia mafanikio  ya utajiri mkubwa ulioletwa na jitihada ya kuanzisha kampuni yake maarufu duniani kama Microsoft.


2.''Nakubali kuna kushindwa , kila mmoja hushwindwa  ila sikubali  kutojaribu tena' Ni siri ya pili anayotoa Michael Jordan, ambaye amewahi kukataliwa na timu yake ya shule ikisemekana hakuwa na kiwango cha kuridhisha katika mchezo wa kikapu simanzi iliyomfanya kumwaga kilio cha uchungu kama mtoto mchanga . Na leo hii baada ya kutoghairi na'kujaribu tena ' Jordan anaitwa mchezaji bora duniani wa ‘basket’ na mwanamichezo tajiri ulimwenguni.


3.''Kila mmoja ni balozi wa maisha yake , hakuna mwingine atawakilisha au kuishi kwa ajili yako''Ni siri ya tatu anayosema  Oprah Winfey aliyewahi kutimuliwa  kazi katika kituo kimoja cha television kwa madai kuwa hakufiti katika hiyo tasinia ya habari. Jambo lililomfanya ajisimamie na kuwa  vyote ‘balozi’na ‘mtendaji’ wa maisha yake akanzisha kipindi  cha televisheni (oprah show) ambacho kilijichukulia umaarufu mkubwa hata kumfanya afungue kituo binafsi cha tv, Oprah tv network. Uwekezaji uliofungua daraja la ujasiliamali na Oprah kuwa miongoni mwa wanawake matajiri duniani.


4.''Maranyingine unapofanya ubunifu ni rahisi kutenda makosa, ni vyema kuyabaini  mapema (makosa) na kusahihisha'' Hii ni siri ya nne iliyobeba mafanikio ya Steve Jobs, muasisi aliyewahi kusimamishwa kwenye kampuni aliyoianzisha mwenyewe kwa madai ya kutofanya vizuri katika kampuni. Kitendo kilichomfanya aionyeshe dunia yeye ni nani hasa pale linapokuja swala la ubunifu wa  teknolojia'innovation'. Kwani hasira za bwana Steve zimesababisha Ipod na iphone kuheshimika sokoni na yeye kurudi kwenye kampuni yake ya Apple kama kinara wa ubunifi aliyeingia kwenye chati ya matajiri wakubwa duniani.


5''Usiogope kufa,ogopa kutojaribu'' Ni maneno ya bwana Shawn Corey Carter maarufu kama Jay Z. Ambaye alitemwa na kampuni kadhaa zinazojihusisha na usambazaji wa ‘albam’.Kisa kilichomchochea mwanamziku huyo wa miondoko ya kufoka foka kuuza na kusambaza kazi zake mwenyewe . Huku akiwa ni mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja (mama). Jay z hakusita kujaribu .kwa kuuza nakala za kazi yake ndani ya gari dogo, na kwa miguu hadi akajulikana na kupata kianzio. Hatua iliyomfanya awe na njozi njema ya kutengeneza Recording Rebel, mavazi  na uwekezaji kibao hadi kuwa miongoni mwa wasanii tajiri duniani 

.
6.''Siri yangu kuwa  na  biashara iliyofanikiwa ni matokeo ya kujituma kwa   bidii'' Anasema Aliko Dangote ambaye alitoka nyumbani na kwenda kuchapa kazi kwa mjomba wake , mtu muhimu  aliyemsaidia Dangote kupata mtaji na kufanya biashara  za sukari, cement ,.Akawa sio tu muuzaji bali mzalishaji wa hizo bidhaa. Baraka hiyo ni jambo lililofungua njia ya mwafrika huyu kuitwa tajiri wa kwanza Nigeria, Tajiri mkubwa Afrika na tajiri wa kwanza duniani kwa watu  weusi. (kwa muujibu wa gazeti la uchumi, Forbes 2014)


7.''Nafasi ya kuishi ni moja lakini hiyo moja ukiitumia vizuri inatosha'' Ni siri ya saba inayosemwa na kundi la the Beatles ambalo linaundwa na waingereza wanne waliofukuzwa studio kwa kile kinachosemakana' wana sauti mbaya na wasingekuwa na manufaa yeyote katika soko la muziki'. Maneno hayo yaliwafanya The beatles watafute studio zaidi na kupiga kazi kama vichaa hadi kuvunja rekodi ya mauzo hapo Uingereza na Marekani. Baadae  album yao ikaitwa ya kwanza na bora duniani . Hivyo ikawa ni fursa ya kupata pesa na kuwekeza . Nafasi iliyopelekea kupata heshima ya ulimwengu kama kundi bora la muda wote katika miondoko ya ‘rock’ na watu waliokamata fedha chafu zaidi miongoni mwa makundi ya miaka ya 1960.



8.''Mafanikio ni asilimia 1 inayotokana na asilimia 99 ya  kushindwa'' ni siri ya mwisho inayoletwa kwenu  na bwn Soichiro Honda ambaye ni enjinia wa kijapani aliepigwa chini na kampuni ya Toyota baada ya kutomzania kama injinia bora.Soichiro hakuwa na  vigezo ikiwemo elimu ya juu.Na hili hakukubali liwe ndio tatizo, kwani kama wenzake tuliowaona,Soichiro Honda aliendelea kutengeneza mashine za magari na pikipiki huku hatua hiyo ikitafsiriwa na baadhi ya watu kama ni ukanjanja na kushindwa.Mazingira yaliomjengea kiu ya kutaka kufanikiwa haraka.Kabla ya kupata tuzo kutoka ujerumani na kuwa raisi wa kampuni yake mwenyewe inayojulikana kama  Honda Motor Company.Inayofanya vizuri dunia nzima  ,kwa kuzarishi sio tu  piki piki bali pia jenereta,magari,mashine za kufyeka nyasi n,k.

Tuesday, March 4, 2014
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo tayari kusikiliza sauti mhimu  toka moyoni mwako.Miongoni mwa sauti hizi ni pamoja na ile nia  ya kutafuta ukweli wa jambo,  kutafta maamuzi sahihi na  kupata mawazo endelevu , na yakinifu. Endapo mmoja ana kiu katika kuona matunda  ya sauti hizi, huyu mtu ni wazi kuwa ana chemichemi za hekima ndani yake. Kama ilivyo kwa ufahamu, hekima halikadharika hupatikana kwa mtu yeyote aliye na nia kama zilizotajwa hapo juu. Huyu mtu wa hekima na busara hutoka katika tabaka la aina yeyote.Kuanzia kwa wazee, vijana, wanaume, wanawake, mabwana, watumwa, tajiri, masikini, wasomi hadi wasiosoma .Matabaka haya ya watu katika jamii hayahukumu mgawanyo wa hekima na busara ndani ya vichwa vya wanajamii.Hugawanya tu mitazamo yao. Kutokana na hali hii tunapata misemo, maneno, nahau na methati juu ya maisha, kazi, dini , tamaduni na vitu chungumzima vinavyosukuma gurudumu la jitihada katika maendeleo ndani na nje ya jamii zetu . Misemo, maneno na aina nyingi za fasihi simulizi mara nyingi zimekuwa haziathiriwi na vipindi, nyakati hata muda. Ni kwa kuwa fikira pevu,chanya na yakinifu zilitumika kuchimbua mizizi ya hekima iliyokuwa imejificha chini sana. Na hizi fikira ni matokeo ya ugumu na urahisi wa mapambano ya kila siku zidi ya maisha , yanaoibua uzoefu wa kukabiliana na changamoto za mara kwa mara au zile zinazofanana. Hapa ni maneno na misemo ya maisha toka kwa watu kumi mashuhuri duniani.
1.''Maisha ni kile kinachokutatiza wakati unapangilia mikakati yako ''John Lennon(mwanamziki)

2.''Maisha ni asilimia 10 ya kile kinachonipata  na asilimia 90 ni kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali'' Charles Swindolls(mchungaji)

3.''Muda wako unakikomo, kamwe usipote kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu mwingine''Steve Job(mhasisi wa Kampuni ya  Apple )


4.''Maisha  huchanua na kusinyaa kutokana  na ujarisi wa mtu husika''Anais Nin(mwandishi wa kihispania)


5.''Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotaraji''Henry David Thoreau(mwandishi wa kimarekani)


6.''Maisha hayapimwi kwa idadi ya pumzi tuivutayo ,hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu''Maya Angelou(mshairi)


7.''Changamoto hupendezesha maisha,na kukabiliana nazo ndio  maana  halisi ya maisha''Joshua J Marine(mtoa nukuu)

8.''Mtu hata badili maisha yake kama hakuanza na kubadiri fikira zake''William James(mwanasaikolojia)

9.''Kwa kutazama tu ulichonacho maishani ,kila siku utahisi unazaidi,ila kwa kutazama unachokosa maishani  kamwe hutokuwa na zaidi''Oprah Winfrey(muongozaji wa maonyesho ya televisheni)


10.''Maisha ni kile ukitendacho,ipo hivyo.itakuwa hivyo''Grandma moses(msanii wa vitu asili katika umri mkubwa)

Saturday, July 27, 2013
Ni miongoni mwa  maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha  ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanadamu bila kubagua kama  ni mwalimu au mwanafunzi,amesoma ama hakusoma .Tutangalia aina mbili za elimu.Elimu rasmi na elimu isiyorasmi( formal and non-formal education).Hapa kuna tumaini jema katika kufahamu ukweli na pengine maana juu ya maisha.Kwani kuna misemo na maana nyingi sana za maisha katika aina hizi mbili za elimu .  Kama ilivyo katika misamiati mingine mingi , msamiati wa maisha umeibuka gumzo hata kupelekea wanafalsafa ,wasanii  na waelimishaji  wengi kujaribu kuongelea  maisha.Mawazo yao katika maana ya maisha ,inatofautiana sana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.Tofauti kubwa ni katika mtazamo, uwezo wa kutafakari na kufikiri .Kutoka Tanzania tutangalia misemo na maana mbalimbali za maisha zitokanazo na wasanii watano(5)sambamba na sanaa zao za muziki.

1. "Maisha ni kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka"Fid q



2."Maisha ni kama gwaride kuna mwisho na wa kwanza ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza"Stamina

3.''Maisha siyo  komborela ukasubiri kubutua jipange jitume ipo siku utafunua"Nay wa Mitego


4."Maisha ni kutenda na siyo majaribio"Mrisho Mpoto


5."Amini wewe ndiye steringi na maisha ndio sinema"Prof jay

Thursday, November 22, 2012
Ukitazama dhana ya elimu kwa kimantiki,lazima utapata wigo mpana wenye maana au tafsiri zaidi ya moja.Kutofautina huku kwa maana ni matakeo ya upeo wa mtu mmoja hadi mwingine.Na hizi ni  nukuu saba(7)zilizopata kunenwa juu ya elimu
1."elimu ni nguvu"Francis Bacon
 2."elimu ni mwanga"margaret fuller
3."elimu ni bahari haina mwisho"Mufti Menk

 4."elimu ni kile kibakiacho baada ya kujifunza"Albert Einstein

5."elimu  ni mstakabari  kwa ajili ya kujitegemea"Mwl.Nyerere


6."elimu kama ni ghali basi jaribu ujinga"  Derek Bok
 7."elimu ni msingi wa maisha"christine Gregoire
 

Popular Posts