Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label ndoto. Show all posts
Showing posts with label ndoto. Show all posts
Tuesday, June 7, 2016
Bahati ni ndoa ya vitu viwili: maandalizi na fursa.Fursa ni msingi wajambo moja,nafasi .Nafasi ni mahusiano ya mambo matatu;nia uwezo na utekelezaji..Palikuepo na mtu mmoja alie amini katika bahati,fursa,nafasi, na utekelezaji .Huyo mmoja alikuwa kiongozi.Uongozi wake ulijaa utani.Hata moja ya kauli yake pendwa akiwa na raia wake ilikuwa ni hii.''Ndugu wana nchi msidharau vitu vidodo,vitu vidogo vinaumiza,kama mnabisha jaribuni kukalia sindano'' .Halaiki ilikufa kwa mbavu baada ya huu utani.Ukitaka kuamini vitu vidogo ni muhimu vinaendesha dunia,na ukivithamini utafurahia ,hautaumia ungana nami kwenye hizi stori zifuatazo
Hakuwahi kujiona kama mpiga ngumi,au bingwa wa makonde kimataifa.Mpaka pale alikumbwa na mkasa mdogo sana.Mohamedi Ali akiwa kijana mdogo miaka kama kumi na kitu ivi.Aliibiwa baiskel anayoipenda .Na akaripoti kwa askari kuwa akimpata mwizi atampiga.Askari alimwambia atamwajibishaje mwizi yule wakati hana uwezo wa kupigana.Basi ikabidi askari amfundishe Mohamedi Ali kuchapa masungwi.Baada ya kuiva hakumtafta mwizi ila akaingia kwenye mashindano ya ngumi
.
2.MOHAMMED DEWIJ
Safari yake ki siasa ilianza baada ya kuona tukio dogo mkoani mwake Singida.Anasimulia''Nimetoka(Singida mjini) km 6 nakutana na mzee mmoja,kulikuwa kuna maji ya njano chini ,alikuwa na ndoo na sinia,amechuchumaa akiteka maji nakutia ndani ya chombo.Nikamsalimia mzee Shikamoo,unafanya nini hayo maji,akasema haya maji ndio tunakunywa sisi.Sikumwamini hadi pale nimefika kwake na kuona watoto wakinywa maji yale yale ,mzee akanisihi MO,kwa nini usigombee ubunge?''Sauti ikamgusa Bwana MO.MO akagombea ubunge.MO akachimba visima .Wananchi wa Singida wakanufaika kwa huduma ya maji.

3.JUX
Licha ya kupenda kun'gaa na mziki ,Juma jux hakuwahi kufikiri kama ni mwimbaji.Jux alikuwa anafanya hip hop kama vijana wengi wa mtaani. Nini kilimbadilisha? Baada ya Jux kumsindikiza msanii mkubwa studio.anatokewa na jambo dogo linaloleta hamu ya uimbaji..Na hapa jux mwenyewe anasimulia .''Tulienda studio na Cyril,Cyril alitakiwa kufanya collabo na Makamua .Makamua alikuwa msanii mkubwa.Basi(Cyril) akampigia Makamua,Makamua akadai atakuja, tulichoma sana mahindi pale(tulikaa sana).Kuanzia kama saa moja mpaka saa tano tano.Maneke( producer wa muziki) akawa kaweka ile Beat.Ile beat imewekwa mie nikawa kama naimba tu unajua mzuka wa studio.Maneke akasikia naimba,akasema ebu imba tena,nikaimba.Akanambia mbona unaweza kuimba kwa nini unachana(kurap).Saa izo naogopa kinoma naogopa ile mic sana,sio nilikuwa naogopa kuimba,nilikuwa naogopa kusikiliza nyimbo yangu mwenyewe kwenye redio,nilikuwa naona aibu sana.Akasema(Maneke) unaweza kuimba jaribu.Nakumbuka ndo mara ya kwanza naingia booth kurekodi''
Saturday, May 28, 2016
Ndoto sio tu kile kitu unachokiona uwapo usingizini bali pia ni kile unachotamani kukiona uwapo macho na kinakunyima usingizi.Ni mara nyingi miongoni mwetu tumekuwa na ndoto kadhaa.Kupunguza mwili,kupata kazi,kununua kiwanja,kuoa,kusomesha,kufanya biashara na mengineyo.Tuwazapo ndoto za aina hii dhahiri tunafungua vichwa kuwa vielevu,tunavisaidia kuwa komavu,tunaviwajibisha kuwa na busara halikadhalika hatuviepushi kuwa imara .Na njia kuu ya kutimiza ndoto yako ni pamoja na kufanikisha za wengine.Huku ukichukua masomo mhimu kutoka katika usumbufu na urahisi mmoja aliopitia.Ikiwa hapo juu tumeona ndoto ni kama mizizi inayoshikilia shina na matawi ya maisha yetu kwa maana zinagusa afya,ajira,makazi,familia,na uchumi, ni vigumu sana kutenganisha binadamu na ndoto,ndoto na binadam.Swali la msingi ni nini kifanyike ili ''kugarantee'' ndoto zetu? .Yapo mambo mengi ya kufanya ila hapa nakushauri kwa haya mawili matatu ya kuufanya ili ndoto itimie na kudumu milele.
1.ANZA HAPO ULIPO
Namna ndogo ya kukaribisha ndoto kubwa ni pamoja na kuanza kuona kila jambo gumu ni jepesi, kila linaloshindikana linawezekana.Na namna tulivyo leo ni matunda ya maamuzi tuliofanya jana.Inawezekana tunasubiri sana,hatuamini mazingira yanayotuzunguka,au watu tunaoishinao.Lakini ukweli ni kuwa maisha ni popote.Dangote ni bilionea mwenye heshima duniani anayetokea Afrika sehemu iliyowahi kuitwa ni bara la giza.Facebook ni mtandao mkubwa wa kijamii ulimwenguni lakini uliogunduliwa huko mabwenini.
2.TUMIA ULICHONACHO.

Muumbaji wetu ni wa ajabu sana ,wakati wa kuumba binadamu hakumnyima cha kufanya.Kama huna mikono una macho,kama huna macho una miguu kama huna miguu una mikono,kama huna mikono una mdomo na kama huna kinywa basi una akili.Akimaanisha Usipocheza kikapu kama Jordan utakuwa Goal keeper kama Kaseja.Usipokuwa na Sauti ya kuimba kama Steve Wonder utakuwa mzungumzaji mzuri kama Nyerere.Na usipokuwa ''genius'' kama Einstein utakuwa msomi kama profesa Lipumba.Usipokua mwandishi kama Shakespear utakuwa mtunzi kama Shaban Robert.Tumia ulichonacho na ndoto yako itimie..
3.FANYA UNACHOWEZA.
''Kwani wao weweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?''Ni swali alilouliza Juma Nature msanii mwenye ushawishi katika mziki wa kizazi kipya .Kinachopelekeaa mwingine kuweza ni mjumuiko wa makosa na masahihisho wanayofanya.Hutenda kiasi kidogo leo,kiasi kingine kesho na kingine tena kesho kutwa.Jumla ya utendaji huu kwa wiki,mwezi,mwaka ni mkubwa kiasi cha kutisha mtu mwingine .Na kila hatua mpya inakuwa bora kuliko iliyopita.
4.USIVUNJE SHERIA.
''Ukivunja sheria utapigwa tu'' Mizengo Pinda,waziri mkuu mstaafu aliwahi kusema.Hivyo akati tukitegemea neema kuu ndani na nje ya ndoto zetu hatuna budi kuheshimu kanuni na taratibu .Hasa zile zinazoongoza nchi,zinazolinda mtu na kutetea uhuru wa kila mmoja.katika umiliki wa rasilimali.Sitegemei utimize ndoto kwa njia ya wizi,dhuruma,ukabaji,unyang'anyi na njia nyingine zisizo halali.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...