Showing posts with label kipaji. Show all posts
Showing posts with label kipaji. Show all posts
Tuesday, June 7, 2016
Bahati ni ndoa ya vitu viwili: maandalizi  na fursa.Fursa ni msingi wajambo moja,nafasi .Nafasi ni mahusiano ya mambo matatu;nia uwezo na utekelezaji..Palikuepo na mtu mmoja alie amini katika bahati,fursa,nafasi, na utekelezaji .Huyo  mmoja alikuwa kiongozi.Uongozi wake ulijaa utani.Hata moja ya kauli yake pendwa akiwa na raia wake ilikuwa ni hii.''Ndugu wana nchi msidharau vitu vidodo,vitu vidogo vinaumiza,kama mnabisha jaribuni kukalia sindano'' .Halaiki ilikufa kwa mbavu baada ya huu utani.Ukitaka kuamini vitu vidogo ni muhimu vinaendesha dunia,na ukivithamini utafurahia ,hautaumia ungana nami kwenye hizi stori zifuatazo

1.MUHAMMAD ALI
Hakuwahi kujiona kama mpiga ngumi,au bingwa wa makonde kimataifa.Mpaka pale alikumbwa na mkasa mdogo sana.Mohamedi Ali akiwa kijana mdogo miaka kama kumi na kitu ivi.Aliibiwa baiskel anayoipenda .Na akaripoti kwa askari kuwa akimpata mwizi atampiga.Askari alimwambia atamwajibishaje mwizi yule wakati hana uwezo wa kupigana.Basi ikabidi askari amfundishe Mohamedi Ali kuchapa masungwi.Baada ya kuiva hakumtafta mwizi ila akaingia kwenye mashindano ya ngumi 

.
2.MOHAMMED DEWIJ
Safari yake ki siasa ilianza baada ya kuona tukio dogo mkoani mwake Singida.Anasimulia''Nimetoka(Singida mjini) km 6 nakutana na mzee mmoja,kulikuwa kuna maji ya njano chini ,alikuwa na ndoo na sinia,amechuchumaa akiteka maji nakutia ndani ya chombo.Nikamsalimia mzee Shikamoo,unafanya nini hayo maji,akasema haya maji ndio tunakunywa sisi.Sikumwamini hadi pale nimefika  kwake na kuona watoto wakinywa maji yale yale ,mzee akanisihi MO,kwa nini usigombee ubunge?''Sauti ikamgusa Bwana MO.MO akagombea ubunge.MO  akachimba  visima .Wananchi wa Singida  wakanufaika kwa huduma ya maji.

3.JUX
Licha ya kupenda kun'gaa  na  mziki ,Juma jux hakuwahi kufikiri kama ni mwimbaji.Jux alikuwa anafanya hip hop kama vijana wengi wa mtaani. Nini kilimbadilisha? Baada ya Jux kumsindikiza msanii mkubwa studio.anatokewa na jambo dogo linaloleta hamu ya uimbaji..Na hapa  jux mwenyewe anasimulia .''Tulienda studio na Cyril,Cyril alitakiwa kufanya collabo na Makamua .Makamua alikuwa msanii mkubwa.Basi(Cyril) akampigia Makamua,Makamua akadai atakuja, tulichoma sana mahindi pale(tulikaa sana).Kuanzia kama saa moja mpaka saa tano tano.Maneke( producer wa muziki) akawa kaweka ile Beat.Ile beat imewekwa mie nikawa kama naimba tu unajua mzuka wa studio.Maneke akasikia naimba,akasema ebu imba tena,nikaimba.Akanambia mbona unaweza kuimba kwa nini unachana(kurap).Saa izo naogopa kinoma naogopa ile mic sana,sio nilikuwa naogopa kuimba,nilikuwa naogopa kusikiliza nyimbo  yangu mwenyewe kwenye redio,nilikuwa naona aibu sana.Akasema(Maneke) unaweza kuimba jaribu.Nakumbuka ndo mara ya kwanza naingia booth kurekodi''
Saturday, May 28, 2016
Ndoto sio tu kile kitu unachokiona uwapo usingizini bali pia ni kile unachotamani kukiona uwapo macho na kinakunyima usingizi.Ni mara nyingi miongoni mwetu tumekuwa na ndoto kadhaa.Kupunguza mwili,kupata kazi,kununua kiwanja,kuoa,kusomesha,kufanya biashara na mengineyo.Tuwazapo ndoto za aina hii  dhahiri  tunafungua vichwa kuwa vielevu,tunavisaidia kuwa komavu,tunaviwajibisha kuwa na busara halikadhalika hatuviepushi kuwa imara .Na njia kuu ya kutimiza ndoto yako ni pamoja na kufanikisha za wengine.Huku ukichukua masomo mhimu kutoka katika usumbufu na urahisi mmoja aliopitia.Ikiwa hapo juu tumeona ndoto ni kama mizizi inayoshikilia shina na matawi ya maisha yetu kwa maana zinagusa afya,ajira,makazi,familia,na uchumi, ni vigumu sana kutenganisha binadamu na ndoto,ndoto na binadam.Swali la msingi ni nini kifanyike ili ''kugarantee'' ndoto zetu? .Yapo mambo mengi ya kufanya ila hapa nakushauri kwa haya mawili matatu ya kuufanya ili ndoto itimie na kudumu milele.

1.ANZA HAPO ULIPO
Namna ndogo ya kukaribisha ndoto kubwa ni pamoja na kuanza kuona kila jambo gumu ni jepesi, kila linaloshindikana  linawezekana.Na namna tulivyo leo ni matunda ya maamuzi tuliofanya jana.Inawezekana tunasubiri sana,hatuamini mazingira yanayotuzunguka,au watu tunaoishinao.Lakini ukweli ni kuwa maisha ni popote.Dangote ni bilionea mwenye heshima duniani anayetokea Afrika sehemu iliyowahi kuitwa ni bara la giza.Facebook ni mtandao mkubwa  wa kijamii ulimwenguni lakini uliogunduliwa huko mabwenini. 

2.TUMIA ULICHONACHO.
Muumbaji wetu ni wa ajabu sana ,wakati wa kuumba binadamu hakumnyima cha kufanya.Kama huna mikono una macho,kama huna macho una miguu kama huna miguu una mikono,kama huna mikono una mdomo na kama huna kinywa basi una akili.Akimaanisha Usipocheza kikapu kama Jordan utakuwa Goal keeper kama Kaseja.Usipokuwa na Sauti ya kuimba kama Steve Wonder utakuwa mzungumzaji mzuri kama Nyerere.Na usipokuwa  ''genius'' kama Einstein utakuwa msomi kama profesa Lipumba.Usipokua mwandishi kama Shakespear utakuwa mtunzi kama Shaban Robert.Tumia ulichonacho na ndoto yako itimie.. 
3.FANYA UNACHOWEZA.
''Kwani wao weweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini?''Ni swali alilouliza Juma Nature msanii mwenye ushawishi katika mziki wa kizazi kipya .Kinachopelekeaa mwingine kuweza ni mjumuiko wa makosa na masahihisho wanayofanya.Hutenda kiasi kidogo leo,kiasi kingine kesho na kingine tena kesho kutwa.Jumla ya utendaji huu kwa wiki,mwezi,mwaka ni mkubwa kiasi cha kutisha mtu mwingine .Na kila hatua mpya inakuwa  bora kuliko iliyopita.  

4.USIVUNJE SHERIA.
''Ukivunja sheria utapigwa tu'' Mizengo Pinda,waziri mkuu mstaafu aliwahi kusema.Hivyo akati tukitegemea neema kuu ndani na nje ya ndoto zetu hatuna budi kuheshimu kanuni na taratibu .Hasa zile zinazoongoza nchi,zinazolinda mtu na kutetea uhuru wa kila mmoja.katika umiliki  wa rasilimali.Sitegemei utimize ndoto kwa njia ya wizi,dhuruma,ukabaji,unyang'anyi na njia nyingine zisizo halali.
Monday, June 23, 2014

Kwa rika ni kijana , kijana wa futi 5, mtazamo ni  chanya, chanya inayo aksi elimu  ya juu, idadi ni wa pili kati ya watoto watano wa familia ya mh Abraham.L.Chaula.Ni mwajibikaji, ni mwanamapinduzi na   mwanaharakati asimamapo kati ya ndugu, jamaa na rafiki zake  . Utendaji ni mwana fasihi anayefanya sanaa inayoshabiana na vitu vitatu muhimu ambavyo ni, maisha, mazingira halikadhalika tamaduni inayomzunguka.  Kwake uthubutu ni kujituma, kujaribu na kufikia malengo. Kitu ambacho ni cha thamani na kinahitaji  juhudi zaidi  . Huyu siye mwingine  isipokuwa ni Izacka chaula(Chella), ambaye ni mmoja ya watu waliobahatika kuliona jua takribani miongo miwili na nusu iliyopita. Kwa maana ya kutimiza  miaka    24 sasa toka azaliwe mwaka 1990 , huko  wilayani Njombe (hivi sasa ni mkoa) ndani ya mji wa Iringa. Akiwa huko mwanzoni mwa miaka ya 2000, ana umri usiozidi  miaka 10 , kipaji chake  kama  vipaji vingine kinastawishwa na kuchavushwa na baba yake mdogo anayeitwa Zakayo L Mwalongo (Mtoza Mc)  ,ambaye ukaribu wake na Chella  unajenga kundi linaloitwa MICHANO LUKUKI, kama ngao ya ujuzi  katika uandishi wa tungo maridhawa. Hatimaye mtoto huyu  wa pili kati ya watoto watano anagundulika na karama ya kupenyeza mawazo pevu, endelevu na shawishi  kwa uwezo wake katika uandishi wa beti na mizani mahiri ,jambo ambalo linamfanya awe mjuzi wa matatizo , changamoto na matukio  mbalimbali ya jamii na jumuiya anayoishi. Baadae sifa ya uandishi wa  mashahiri yenye kuonya, kukanya na kufungua mboni na ngome za masikio mengi, inajenga taswira pevu , komavu , pale anapokuwa   shule ya msingi Kibena  mkoani Njombe. Hapo shuleni marafiki wanaelewa na kutambua harakati na Sanaa anayoifanya Chella . Ndipo sasa  anatilia maanani tunu yake aliobarikiwa kuwa nayo na kuboresha zaidi hicho kipaji , anapoingia  sekondari ya Mpechi na Philip Mangula   na kupata  nafasi ya kushiriki shindano linaloitwa Philip Mangula Star Search (PMSS).Tukio linaloandaliwa na uongozi wa shule, mahususi   kutafuta vipaji vya wanafunzi shuleni hapo. Mnamo mwaka 2008 akiwa kidato cha nne shuleni Mangula , Izacka Chaula maarufu sasa kama Chella anakuwa mshindi namba moja  zidi ya washiriki wengine wapatao 30, walioshindana katika tukio hilo la kumtafta bingwa mmoja.  Safari ya matumaini, iliyojaa utashi na wingi wa ueledi inapata mafanikio, pale mshindi huyu    anapobahatika kujiunga na elimu ya kidato cha sita, Kwiro Boys high school, huko wilayani Mahenge Ulanga, mkoani Morogoro. Ni ndani ya mji huo usio na bahari, hisia za kutaka kurejea studio zinamshamiri  mwanafunzi huyu  . Hivyo anashawishika  kuandaa tungo ya nyimbo yake ya kwanza anayoipa jina la “Rudi mkoa”. Kibao kinachoelezea tabia ya vijana wengi kulowea katika miji mikubwa kama Dar es salaam huku wakisahua kurudi mikoani mwao.Ila utunzi na Sanaa hii haibadiri dira na imani yake katika elimu, kwani yeye huamini  kuwa, elimu ndio taa inayoweza kufukuza giza la ujinga na kurejesha nuru ya maarifa. Mwaka 2011 mwanaharakati huyu anafaulu kidato cha sita, hivyo  anajiunga na masomo ya juu katika chuo cha SAUT Mtwara (STEMMUCO ). Akiwa chuoni hapo anapata fursa ya kuwa mmoja kati ya  wanachuo wanaounda kundi  linalojihusisha na maswala ya muziki na sanaa,kundi hilo linajulikana kama Stemmuco All Stars  .Vitu vitatu anavyovipenda chella ndani ya kundi ni umoja na ushirikiano wa wanazuoni,vipaji vikubwa walivyonanvyo wasomi wenzake na michango mizuri itokanayo na mitazamo chanya. Mbali na shughuli za kikundi , thamani na mchango  wa wanakikundi ,Chella amekutanisha mawazo yake na watu wengine  wenye tunu ya kuandaa mashahiri yenye shabaha katika  kuelimisha na kufunza. Hawa mahodari wa fasihi andishi ni pamoja na Mtoza mc, Domokaya, BeckaTittle, Jebby Mubarak, Joseph Haule’’ prof jay’’, P-the MC, Juma Kassim Kiroboto ‘‘juma nature’’ Juma Jazz , Nicolazo n.k.Wanaomsaidia Kutoa kwa ufasaha kila aina ya uwezo na kitu alichanacho msomi na mtanzania huyu. Anafanikiwa kuandika mashairi mazuri na hatimaye kutia sauti yake inayoibua chachu , mapinduzi, na mabadiliko ya sanaa yake.Hali hii ni kielelezo tosha  jinsi mwanaharakati, mwanamapinduzi na mwajibikaji huyu  anavyopigana kwa hali na mali  hata kuingia mikoa zaidi ya mitano ,mitaa zaidi ya tisa,katika studio zaidi ya 10 ,akifanya kazi na waandaji wa midundo(music producer) wasiopungua 7 na kushirikiana na wasanii wanaonzia 10 hadi 20.Chella amefanikiwa kuingia baadhi ya miji kama  Dodoma, Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Njombe Mbeya, Ruvuma na Mtwara . Akifikia mitaa mbalimbali  ya mikoa hiyo kama Railway, Masaki, Kinondoni, Kigogo, Mbezi, na kuingia studio za Tongwe Rec, Mkubwa na Wanawe, Koma studio, Robbies Rec , Kp Rec, Shine Rec, Natal Rec, Baridi Touch, E-Lab,Kimya Rec , Mama Land Rec, George Rec,Goka rec,AB Rec  na nyingine  nyingi, chini ya waandaji mahiri wa muziki  nchini wakiwemo akina Geof Master(manuva), Kona Beats,Main, Jero,Pezo,Tonny(Efficiency man), Necka Beats, Jose Braiz Beats,Kagusa Andrew. Uchaguzi wa  wadau hawa wa   muziki , umezingatia  vitu vikuu viwili ambavyo ni, uchipukizi na ukongwe wao katika tasinia ya mziki, unaochangia   kazi kuwa  na uzuri. Upekee na ubunifu tofauti wa kazi zao. Mantiki inayopelekea kuonekana kwa vionjo vya kiasili na radha iliyojificha ndani ya sanaa na kazi za mwana hip hop na msomi huyu. Baadhi ya kazi ambazo Chella kafanya ni pamoja na Rudi mkoa (Dar imekupa kiburi), tatizo nini (ft Geof Master), nitafika ft becka Title, mimi na Yule ft Juma jazz, ningezaliwa Dar, naongea na wallet, Bado napambana,jiulize , usiniache , Azimio la kijiji n.k, . Kazi hizi na ushirikiano  alioufanya  msanii huyu na wajuzi wengine toka nje na ndani ya tasnia ya muziki imesaidia katika kumjengea mtazamo  wa ziada  Ukiachilia kando kimkoa, kikanda na kitaifa Chela ana mtazamo na ndoto za kufikia ngazi ya kimataifa kwa kufanya kazi bora zaidi kama zile za kina Marshall Bruce Mathers ''eminem''na wana hip hop  wengine wanaofanya vizuri duniani kote. 
                                                      






















Monday, January 7, 2013
Katika viungo muhimu binadamu alivyobarikiwa kuwa navyo moja wapo ni mikono. Mikono  huweza kumfanya mtu mmoja awe maarufu au kubaki kawaida,matumizi chanya ya mikono hujenga,hukuza na kuleta kipaji kikubwa.Hata sasa sura ya mikono utaiona yenye thamani machoni pako kama  thamani ya dhahabu,almasi na pengine hata zaidi  lulu.Zifuatazo ni picha za vipaji kumi(10) vitokanavyo na mikono
1.Mchezo wa kikapu


2.uchoraji



3.uandishi

4.uandaaji mziki

5.ufundi radio



6.kupika


7.kutafsiri vitendo

8.kudaka
 
9.ujenzi

10.kuchapa(typing)

  

Popular Posts