Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Tuesday, January 12, 2016
5.Samia Suluhu Hassani.
Mwana mama aliyegawanya miaka 55 katika familia, elimu na siasa. Akiwa
anazaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1960, Bi Samia anapata bahati ya mtende.Kuwa makamu Wa rais na mwanamke wa
kwanza kushika wazifa huo. Baada ya miaka 54 ya uhuru wa Tanzania .Hata hivyo
nafasi kama hiyo pamoja na vyeo vikubwa anavyovipata mwaka 2015 sio jambo geni
kwa Samia. Kwani baada ya kufanya kazi na N.g.os, Shirika la Chakula duniani na
ubunge , marais wawili kwa awamu tofauti waliwahi kumteua mara tatu mwanaharakati huyo kuwa waziri. Mwaka
2000 Rais wa Zanzibar,Amani Karume
alimteua Suluhu kuwa waziri wa Leba, jinsia na watoto ikifuatiwa na mwaka 2005
waziri wa utalii. Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete pia alimteua
awe waziri wa mambo ya muungano. Ukiwa unataka kujua nini kipo nyuma ya pazia,
Bi Suluhu hasiti kwa hilo, anatoa siri kwa maneno yasiozidi manne (4),kwamba
amefika hapo kutokana na’’ ueledi na umakini katika kila jambo analolifanya’’.Ni
kweli asemacho kwa sababu katikati ya miaka ya 80 (1986)Samia Hasani Suluhu
alihitimu elimu ya mambo ya utawala chuoni Mzumbe. Mwishoni mwa hiyo miaka ya
80 (1989) Aliongeza elimu yake katika moja ya chuo huko Pakistan na mwanzoni
mwa miaka ya 90(1991)Bi Suluhu alihitimu elimu nyingine ya uongozi Hyderabad,
India, na mapema mwaka 1994 alihitimu elimu ya mambo ya uchumi huko Uingereza katika chuo cha Manchester na
katika mwaka Wa neema, 2015, Samia alipata ujuzi mpya wa uchumi na maendeleo ya
jamii katika chuo cha kimarekani kinachoitwa Southern New Hampshire. Lakini
pamoja na yote hayo Bi Samia ni mke, na mama Wa watoto wanne. Tena anayelea na
kupenda familia yake vizuri.Kwa historia hii bi Samia ni miongoni mwa wanawake
maarufu na wenye ushawishi nchini.Kama Asha Rose Migiro, Janeth Magufuli, Anna
Mwighwira, Salima Kikwete nikitaja kwa uchache .
4.Mbwana Ally Samatta.
Wazungu wana msemo usemao "umri
ni namba" . Kwa maana idadi ya Miaka tuliyonayo sio kikwazo cha kutokuwa
watu tunaojikusudia kuwa. Hakika unaweza fanya chochote katika umri wowote.
Haya ndio maelezo yanayomvisha kilemba
bwana Samata. Mchezaji aliyezliwa 1992 na mwaka 2015 kugeuka
dhahabu pale alipo pewa tuzo ya ufungaji
bora wa ligi za mabingwa afrika. Ikifuatiwa na kuwania tuzo ya mchezaji bora Wa
afrika anayecheza ligi za ndani. Ni mswahili wa kwanza kuleta mchango kwa timu
akiiwezesha timu yake kutwaa kombe la
mabingwa wa afrika 2015 . Pengine unajiuliza Samata ni nani?. Huyu ni mtanzania
mwenye umri wa miaka 23 anayechezea timu ya mpira Wa miguu nchini Kongo
inayoitwaTP Mazembe . Mnamo mwaka 2011 Samata aliuzwa kwa dau nono la dola za
kimarekani mil 100(shilingi mil 150 za
kipind kile )na Simba Sport Club.Huku yeye
akipewa sh. Mil 50. Mpk mwaka wa neema, 2015, Mbwana Samatta tayari anamiliki
pesa, mali, majumba matano na magari ya kifahali manee;Range Rover yenye thamani ya mil 80 na
Chrysler crossfire ya mil 50. Tukisahau habari ya utajiri , Samata anamudu vyema
nafasi ya ushambuliaji akiwa uwanjani . Kwa mwaka 2015 tu ameifungia tp mazembe
goli saba, kitu kilichomfanya awindwe na ligi za ulaya kw tiketi ya timu za
ubelgiji .Kwa nafasi hiyo Samata ataingia kwenye orodha ya watanzania wachache waliowahi
kuchezea ligi za nje ya bara la Afrika.Tukikumbuka kuwa wachezaji wengine
waliofikia hiyo hatua ni pamoja na Haruna Moshi "Bobani", Athuman
Machupa waliokuwa Sweden, Renatus .Njohole, Uswizi, Mwinyi Kazimoto, Qatar .Henry Joseph,
Norway na Danny Mrwanda aliyekuwa Vietnam.Tunakutakia mafanikio mema Samata.
3..Amri Athuman 'King
majuto'.
Kama sio kipofu utakubali mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwa gwiji wa
vimbwanga nchini, mzee king majuto. Kwani tumeshuhudia siku moja baada ya
kuachia filamu mpya ya Shikamoo Mzee . Tenda za pesa zilimfuata mzee wa watu.
Akifanya matangazo ya bidhaa tofauti tofauti zaid ya muigizaji mwingine. Hivyo kutawala sura za magazeti, vipindi vya
TV na redio . Ni miaka miwili imepita (2013-2015) tangu Majuto atangazwe kama
muigizaji aliyelipwa vizuri na kampun ya steps production. Akipokea kiasi cha
sh. Mil 20 kwa mwezi, kwenye mahojiano aliofanya na kipindi cha Amplifya
kinachorushwa na Miradi Ayo. Habari
inayoashiria kuwa, huenda na mwaka 2015, Majuto akawa mbele kwa kupiga mpunga
mnono. Kwa sababu muigizaji huyo wa comedy kanyakua tuzo ya mchekeshaji bora Wa
mwaka , pale viwanja vya Nyerere Dar es salaam.Akiwabwaga akina Jangala, Salma Jabu"Nisha" ambao ni wachekeshaji wazuri nchini. Ni zaidi ya
miaka 50 tangu Majuto aanze kufanya kazi
za uchekeshaji . Anasema "Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 tokanimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu"Miongoni mwa filamu zilizomuweka sokoni ni Daladala, Mtu
mzima ovyo, Naenda kwa Mwanangu, Back from New York na Shikamoo Mzee. Mbali na
yote mvunja mbavu huyu ni baba Wa familia ya watoto tisa na amefanikiwa kujenga nyumba tatu, kuanzisha
shamba kubwa la kilimo .kusomesha wanae, kwenda Makka na kununua magari matano.
Kwa maendeleo haya ,mzee ni changamoto kubwa kwa wachekeshaji wanao chipukia na
wale wakongwe kama Onyango, Mzee Jangala, Senga , Pembe, Brother K, Nisha na
wengine.
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...
0 comments:
Post a Comment