Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label teknolojia. Show all posts
Showing posts with label teknolojia. Show all posts
Wednesday, December 21, 2016
Toka ulimwengu ugeuke kijiji.Habari husambaa haraka
kuliko moto wa petrol.Hauhitaji nguvu
kufuatilia mitindo,teknolojia,siasa na michezo. Siku izi kila mmoja ni
model,IT,photographer ,kiongozi,na mchambuzi.Kwa sababu taarifa zinapatikana kila mahali.Kuanzia facebook
,Whats apps.Instagram na kwingineko.Ukaribu wa dunia na mitandao ya kijamii ni chachu ya uelevu..Utitiri wa vyanzo vya habari kupitia simu za mikononi laptop na tablets zilizounganishwa na internet ni shina la wasomi na kundi la waelevu tulionao.Kuendena na kasi ya mabadiliko yanayotokea ughaibuni kote inategemea unamiliki kifaa gani? Ukinunua tecno,huwawei,Samsung,iphone au ipad yenye 3G hakika wewe umeukata.Kwani internet ni mama wa habari ,aliyezaa mitandao ya kijamii .Inayokupatia kile unachotaka .Familia hii inakuwa kila siku kwa maana kunazaliwa
mitandao mipya na followers wapya. Je unajua list ya social networks bora 2016?.
1.Facebook2.Youtube
3.Reddit
4.Tweeter

5.Pinterest
6.Instagram
7.Tumblr
8.Linked In

9.Yahoo Answers
10.Yelp
Tuesday, July 7, 2015
Mabadiliko
ni kama maji huweza kuchukua umbo la sura yeyote. Na huweza kufuata uelekeo
mmoja au zaidi. Ukitazama sura ya teknolojia
iliopo leo utabaini hii sio taswira iliokuepo jana, yaani miaka 20 iliyopita. Mageuzi
haya yanatokea huku wagunduzi kuntu wakiwa ni miongoni mwa watu adimu katika hiki
kipindi. Richa ya kukosekana kwa wagunduzi nguri wakiwemo; Isack Newton, Pythogrus,
Edson Thomas, kati ya miaka 1995 hadi 2015 . Kuna upepo wa mabadiliko
unaoletwa na waboreshaji wanaofuata misingi ya hao wagunduzi kuntu. Wagunduzi
dhahiri, wangunduzi halisi , wagunduzi waliovuma miaka yote. Ndani ya hiki kipindi cha miongo miwili ( miaka
20 ). Kuna wabunifu wanaochipukia na kumiminika
kama utitiri. Hawa ndio shina
linaloshikilia urahisi wa maisha na urahisi wa mawasiliano katika dunia ya leo.
Hali inayopelekea mambo yaliokuwa hayawezekani miaka 20 iliyopita kufanikiwa. Na
hapa ni baadhi ya hayo mambo
1.IMO,SKYPE
Kitendo cha kuonana ana kwa ana baina ya watu wawili walio katika sehemu tofauti za mchi , ilikuwa ni kitendawili katika niaka ya 90. Ahsanteh kwa teknolojia ya imo na skype kwa kuleta nyuso na sauti za watu karibu. Wapendanao waliokuwa wametenganishwa na umbali, masomo, kazi na majukumu ,sasa wanafursa ya kusalimiana na kutazamana kwa ukaribu kama pua na mdomo.
2.WHATSAPP
Ilikuwa ni
rahisi kwa mganga wa kienyeji wakati
ule. Kuendesha majadiliano na watu anaowaona yeye tu , kama hiyo haitoshi
aliweza kusema kitakachojiri duniani
kabla ya mimi na wewe kutambua lolote.Baada ya simu kuingia kila mtu kapatiwa
uwezo huo. Tena kama ina whats app ndio mtajadiliana hadithi zote kuanzia; siasa
, katiba, tamaduni , uongozi, ajira, michezo, burudani ,utabiri wa hali ya
hewa,kubet n.k .Vyanzo vya hizi habari kwa mwaka 2015 sio tena ‘mafundi’ au waganga
wa kienyeji pekee bali ni rafiki zako,wanafunzi
wenzako,wafanyakazi na jamaa uliohifadhi namba zao katika simu ya kiganjani
mwako. Kwa kutumiana jumbe za sauti,picha na video Whats app hukupa maarifa pamoja na taarifa za hayo matukio mbalimbali
3.YOUTUBE
1995,Televisheni ilikuwa ni kila kitu juu ya
masuala ya video. Kuona ‘kichupa’ au video mpya ya msanii unayempenda ilikupasa
utege jicho kwa luninga. Ukikosa tukio kubwa katika taarifa ya habari ulitakiwa
kuwa mvumilivu hadi taarifa irudiwe, vinginevyo ungoje kipindi maalumu au mwisho wa wiki. Hali sio
hiyo tena miaka ya kuanzia 2005, na Shukrani za kipekee ziendee youtube kwa kutupa uhondo wa video tulizokosa,
tuzitakazo katika muda wowote, mahali popote na kwa mtu yeyote. matukio makubwayaliokupita au uliyoyakosa
katika tv utayapa hapa.
4.SHAZAM
Unakumbuka
enzi hizo ukisikia mziki mzuri redioni, unatamani mtangazaji ataje jina la huo
wimbo?. Ama unapita mahala kuna mdundo wa nyibo za ughaibuni,zinakugusa moyoni lakini
hujui msanii wala jina la wimbo? Hii shida sasa imefika mwisho.Mwaka 2015 Kazi
imerahisishwa sana . Ni vyepesi zaidi ya
kumsukuma mlevi. Kwa kutumia shazam unaelekeza tu simu au komputa karibu na
mdundo wa nyimbo, na ndani ya sekunde
umeshapata jina la msanii na nyimbo
.
5.GOOGLE
EARTH
Zamani
ilikuwa ni ngumu kufika pointi moja bila
kuwa na mwenyeji, bila kuuliza ama kupanda chombo cha usafiri. 2015 unaweza
kutembea dunia nzima bila kukwea pipa, kuchukuwa treni, kupita na meli wala
kupanda basi. Ikiwa una google earth na mji una ramani mtandaoni , utaelekezwa njia za kupita kwa mguu, kwa gari hadi sehemu
za kuvinjari, hotel, supermarket, beach na
kona za afya ; hospitali, zahanati, na
maduka ya madawa baridi. Google hawatoi tu ramani bali pia vituo mhimu
unavyotaka kujua
.
6.FACEBOOK
Karibu kila
mmoja ana damu ya uandishi. kubali!, kataa!. Kwa maana anafurahi kushirikisha
jamii dhidi ya mafanikio ,mipango, ndoto,
huku akitia moyo marafiki na kuomba
msaada wa maombi kwa ndugu hata pongezi kuto kwa jamaa . Mmoja yupo huru kutoa
mawazo na hisia zake mbele ya wengine. Hii sehemu ya maisha ya mtu mmoja dhidi
ya wengine hufanyika kwa maandishi yanayoambatanishwa na picha nzuri ya
mhusika. Kama ishara ya kujuza jamii nini kinachoendelea upande wake. Endapo hujui
ninachojaribu kuelezea hapa, nakusihi
jiunge na facebook, ukashuhudie jinsi uhuru wa kujieleza ‘freedom of expression’
inavyotendewa haki. Ikiwa una kumbukumbu nzuri, pengine umebahatika kuishi na
wezee katika miaka ya 90. Utaona bibi na
babu zetu hawakufaidi dhana nzima ya uhuru wa mawasiliano.Ukilinganisha na
FACEBOOK
7.TWITTER
Nakumbuka
nilisoma kitabu kimoja zamani kidogo, ambacho kilielezea namna wafalme
walivyokuwa wakituma jumbe ulimenguni.Kitendo kilifanya na mtu mwenye mbio sana
aliagizwa kupeleka nyaraka katika himaya nyingine , na hiyo himaya iliteua mjumbe wao mwenye kasi sana mpaka
falme ya tatu .Ambayo pia ilieneza habari katika falme ya nne. Mtindo uliendelea mpaka falme ya sita ,saba hadi ya mwisho.Na baada ya miaka habari ilienea
ulimenguni kote. Stori ya hiki kitabu chenye maisha ya zamani, kinafunua muongozo
wa teknolojia ya twitter . Kitu ambacho twitter hufanya japo ni ni ndani ya sekunde,au
dakika tu. Ni kueneza habari kwa haraka, Hivyo miomgoni mwa matumizi mengi ya
tweeter, dunia nzima hujua nini
kimejiri. Kwa kuendeleza habari husika iwe ni Alshabab, Sunami, mapinduzi, ongezeko
la joto n.k .Ndani ya masaa taarifa
itakuwa imefika uchina, Marekani, uingereza, Brazil, Australia na Tanzania .
Dunia nzima hupelekewa taarifa kwa kufanya swala endeleve linaloitwa ‘retweete’
8.INSTAGRAM
Wakati sote
tunaamini bank ni nyumba ya pesa, ghala ni nyumba ya mazao na msitu ni sehemu
ya miti. Basi instagram ni nyumba au
sehemu ya picha. Zamani kuona picha ya msanii, mtu maarufu au kiongozi mkubwa
ilikuwa nadra, mpaka utafte gazeti au kutembelea maneo ya kazi zao. Ahsanteh
Instagram kutuletea pozi, dizaini, mbwembwe na matukio mengi ya watu hawa
katika mfumo wa picha.
9.EBAY, AMAZON,
KUPATANA
Unakumbuka
wakati unauza bidhaa na hakuna mteja? .Unataka kununua mali hakuna hakuna muuzaji?.
Ilikuwa ni zama ya miaka ya 90. Kuanzia mwaka 2015 Ebay, Amazoni, Kupatana.com (
Tanzania ) inatoa uhuru wa kuuza na
kununua bidhaa yoyote mtandaoni. Hapa utapata nyumba, mavazi, usafiri, vitabu, mashamba n.k
10.HULKSHARE,
SOUND CLOUD
Sauti ina
thamani yake na ili hii haiba idhihirike haina budi kukusanywa pamoja katika
mfumo flani. Miaka ya 90, miziki ilitunzwa
vyema katika santuri, kanda , cd na baadae miaka ya 2000 , zikaingia flash. Lakini
ukisahau mbinu hizi . Hulkshare na sound clound ni mapinduzi makubwa miongoni
mwa mengi katika kutunza, kusikiliza na kupakuwa au ku ’download’ sauti, nyimbo,
midundo, mziki unayoipenda.
Tuesday, December 2, 2014
Mwezi novemba mwaka 2014 nilifika mkoa fulani hapa Tanzania kwa ajili ya mahafali . Na kwa kuwa matumizi ya simu za kisasa''smartphone'' ni makubwa kwa kila mmoja ili nibidi ninunue simu ya dizaini hiyo ilahisishe mambao yangu. Hii ilikuwa ni simu ya tecno H6 iliyoweza kupiga picha za ubora mzuri kama zile za kamera ya kawaida. Ila mungu si Athumani asubuhi ya keshokutwa, siku mbili baadae, niliamkia mazoezini kama ada yangu . Nikikimbia kando ya bahari ya hindi kwa muda wa nusu saa hali iliopelekea kuchoka sana kwani ni muda sijafanya joging. Hata jioni nikiwa katika mgahawa mmoja ,najivinjari kwa smartphone mkono wa kushoto na maji mkono wa kulia nikinywa taratibu kwa fundo la kizembe bado nilihisi uchovu wa mwili na akili uliotokana na zoezi la asubuhi. Baadae kidogo niliondoka eneo hilo la chuo kulipokuwa na mgahawa nakuelekea nje. Nikiwa nje nilitaka kuwajuza marafiki zangu kuwa nipo tayari mkoani hapo, ndio ghafla nashishituka sina simu mfukoni wala mkononi. Japo akili ilikuwa imechoka , niliweza kumbuka kuwa , kabla ya kulipia maji kwa muhudumu niliacha simu mezani na sikuichukua wakati naondokka eneo hilo. Nikafanya jitihada za kumdadisi mhudumu hakuweza kufahamu lolote. Nikauliza watu waliokuwa karibu yangu wakitazama mechi ya West Brom na Arsenal Betting iliyochezwa siku hiyo ya jumamosi tarehe 29 novemba , nao pia walikana kuiona smartphone yangu mpya iliyokuwa na siku tatu tu toka ninunue. Hatimaye nimeuliza mtandaoni na majibu yao yameshauri matumizi ya programm zifuatazo.
1. LOOKOUT. Hii ni moja ya programm inayomwezesha mmliki wa simu aina ya android kubaini mienendo ya simu iliyopotea. Huku ikitoa taarifa mahala simu ilipo , Pia hii programu inapiga picha za siri bila mwizi au aliyechukua kutambua na kutuma moja kwa moja kwa anuani yako uliojisajilia katika hiyo programm.Ina uwezo wa kufunga ama kufuta habari binafsi zilizondani ya simu na endappo upo karibu na mtu mwenye simu yako programm inakuwezesha kuruhusu simu itoe alarm na kumkamata mwizi.
2. LOOKOUT PLAN B. Tofauti ya programm hii na ya kwanza ni kuwa Lookout plan B hutumika na baadhi ya simu tu zinazotumia mifumo ya android. Na wakati programm zote katika hii list zinahitaji kuwekwa katika simu kabla haijaibiwa, Lookout plan b inaweza kuingizwa katika kifaa kilichopotea ama kuibiwa hata baada ya mwizi kutokomea Ni kwa njia ya mtandao Lookout Plan B huweza kufikia simu iliyopokonywa.
3. PREY. Kama zilivyo programm nyingine hii pia inapatikana Google play , yaani katika simu zitumiazo android . Au kwa urahisi sana zinajulikana kwa jina la '' simu za tachi' '(touch). Prey ni programm ambayo inauwezo wa kuonyesha mitandoo yote inayotumiwa na simu yako iliyopotea. Lakini hata kama kulikuwa na picha za muhimu hii ni prograam iayoweza kuzihifadhi katika account au anuani yako ya google.Zaid Prey huweza kutumika hata kutafta laptop na tablets zilizopotea.
4. FIND MY PHONE. Hii programm inatofautiana na nyingine kwa kuwa inawafaa watumiaji wa Iphone na vifaa vingine vinavyotengenezwa na kampuni ya Mac.Ambao ni wazalishaji wa ipod, ipad na simu zaIphone. Habari nyeti za mtu alizoacha katika simu hupelekwa na progrmm hii hadi uwanja wa icloud. ambako mmliki wa simu hufika kwa kufanya usajili mdogo. Hapa utajua simu yako iko wapi, nani anaitumia kwa kutazama picha zilizopigwa kwa usiri wakati mwizi akiitumia.

5. ANDROID DEVICE MANAGER, Ni aina nzuri ya programm katika kurudisha simu kwa kuwa ina sifa kama programm nyingine ikiwemo ile ya kuwafaa watumiaji wa android, Pia ina mambo muhimu ya kuzingatia kama ; kupata simu iliyopotea .kwanza. inatakiwa iwe imeunganishwa na mtandao, pili, iunganishwe na na programm hii kabla haijaibiwa, tatu, simu itaonekana baada ya kuwa karibu na minara ya simu, huduma za wireless, bloothooth na mifumo mingine yenye kutuma mawasiliano katika satellite za google , nne, kuifikia simu iliyopotea unatakiwa kutumia simu tofauti, computer au kifaa kingine. Mwisho hii programm kama hizo zilizotajwa juu hupata simu ikiwa imewashwa na sio kuzimwa
.Kumbuka ni vyema kutoa taarifaya upotevu wa mali yako katika uongozi wa serikali kama polisi au ofisi ya kijiji kabla ya kufanya ufuatiliaji kwa kutumia programm hizi.
Thursday, January 23, 2014
Bila shaka umewahi kufika dukani kutazama kompyuta ukashindwa uchague ipi?. Pengine umewahi kuchagua mashine kadhaa na ukashindwa ununue ipi? . Na hata baada ya kununua kifaa hiki umekutwa na hisia za kutaka kuuza?. Kama haitoshi , baada ya kuuza umebaki njia panda kwa maswali mengi, utachukua tena kompyuta ya sifa gani?.Usiumize kichwa .Haya maswali na mengine mengi ni jambo la kawaida hasa kwa watumiaji wengi wa kompyuta, huu ni wakati wa changamoto kama ilivyo katika kuchagua bidhaa ya aina yeyote ile . Linapokuja swala la sifa zipi ni bora na zipi sio bora, unapohitaji kuchukua, kuchagua , kupendekeza ama kununua kompyuta . Mtumiaji anapaswa kuwa na mwanga halikadharika elimu kiasi ,kuhusu tabia na uimara wa hiki chombo cha umeme . Hivyo kabla ya uamuzi wa kuchukua, kuchagua ,kupendekeza ama kununua kompyuta husika, inakupasa uwe na ujuzi na uelewa wa kutosha juu ya hiki chombo. Katika kukujuza zaidi juu ya sifa, tabia na uimara wa kifaa hiki cha digitali, Kitabukwanza inakuletea mambo 10 muhimu ya kuzingatia unapohitaji kompyuta .
1.Unapaswa kujua jina la kompyuta
2.Unapaswa kubainisha aina ya matumizi (elimu/mchanganyiko/mengineyo)
3.Unataka mashine ya ukubwa wa kiasi gani(Local disk)
4.Unahitaji kompyuta yenye kuchakata kwa uwezo gani(Processor)
5.Uwezo wa kompyuta kurejea kumbukumbu ulizo tia ndani(RAM)
6.Ukubwa wa kioo(screen resolution) ni muhimu kwa watazamaji wa filamu''movies''
7.Unataka aina gani ya mfumo wa kuendeshea kompyuta (window xp,vista,7,8,mac)
8.Inaandika/inachoma mfumo gani wa santuri(cd/vcd/dvd writer)
9.kamera(web cam)ni muhimu kwa mitandao ya kijamii,skype,facebook n.k
10.Ukubwa/umbo(size)
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...














.gif)
















