Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts
Thursday, September 11, 2014
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na ajira hawakuweza kutafta mvuto kwa namna inayohusisha gharama kubwa.Hawakuweza kuingia gym, hawakuwrza kumudu vifaa maluum vya bei mbaya. Hali iliyopelea mmoja kati yao kutafta mwalimu wa mazoezi ya mwili kwa njia ya mkopo. Na mwingine kujisimamia katika mazoezi ya aina hiyo bila mwalimu kabisa. Neema alipata msaada mkubwa toka kwa huyu mwalimu wa mazoezi. Ibrahim halikadhalika alifanikiwa kutokana na bidii aliyojiwekea katika mazoezi. Wawili hawa katu hawakukata tamaa ya mazoezi hata siku moja kwa kuwa walipenda michezo kuliko kitu kingine.Walipenda kuwa wanamitindo kuliko kazi nyingine. Walivutiwa na uzuri kuliko sifa nyingine. Baada ya miezi mitatu kupita huku zoezi ni kama dini na kitu cha muhimu kwao, mmoja wa vijana hawa anatokea kuwa kisura aliyevutia sana na mwingine ni mtanashati aliyependeza sana. Huku siri yao kubwa kufika hapo walipo ndani ya muda kidogo, ikitokana na juhudi katika mazoezi yafuatayo..
1,KURUKA KAMBA. Ni zoezi rahisi lisilochukua gharama kubwa.Zoezi hili linafanyika sehemu nyingi kwa sababu vifaa vyake ni rahisi kubeba na hupatikana kwa uepesi.Kwa kuwa linahusisha mikono,miguu,mgongo na viungo vingine vya mwili,huongeza stamina,nguvu na kukaza misuri ya mrukaji. Ni moja ya zoezi zuri katika kupunguza uzito wa mwili.
2.KUKIMBIA.Ni zoezi linalofanyika uwanjani,barabarani,mbugani na sehemu nyingi za uwazi mkubwa.Zoezi hili hupendeza pasipokuwa na jua kali hasa majira ya asubuhi na majira ya jioni..Ni moja ya zoezi zuri kwa mapafu na moyo.Kwani viungo hivi hurejesha msukumo wa damu na hewa kuwa vyema,kiasi cha mkimbiaji kupata nguvu na pumzi ya kutosha katika mwili wake.
3.PUSH UP. Ni zoezi rahisi, linalochukua gharama ndogo sana na gharama hii ni muda pekee . Mbali na muda, push up hazihitaji uwanja mpana zaidi ya chunba chako. Kwa kupiga push up ndani ya nyumba itakusaidia kukaza mwili sehemu ya juu. Ukianza na kupanuka kifua, ikifuatiwa na kuimarisha mabega, mikono mgongo na tumbo. Ni zoezi zuri kwa ukakamavu
4.KUOGELEA . Ni mchezo ambao huvutia watu wengi, watoto kwa wakubwa wenye kipato na wasionacho. Lakini wakati karibu kila mmoja anafurahai mchezo huo, kuna faida nyingi mwili hupata Kwanza ni mara mbili ya zoezi la kukimbia, na huimarisha misuli ya mwili kutokana na ukinzani wa maji. Pili huondoa mfadhaiko na msongo wa mawazo, tatu ni zoezi linalohusisha
miguu, mikono, mabega na viungo vya mwili karibu vyote na baadae mwili hujengeka na kukaa fiti.
5.KUENDESHA BAISKEL. Kwa kuendesha tu usafiri wa baiskel ni sehemu ya zoezi muhimu sana kwa afya . Miguu inapokazana kupita mpando na ama tambarare. Mwili unashitua misuli inayosukuma nguvu zaidi . Zoezi hili linasaidia ubongo kwa kuwa makini na kunakiri chochote kinachoendelea. Unapofikia hatua ya kutoa jasho wakati wa zoezi hili , inasaidia kupunguza taka mwili na mafuta yasiotakiwa mwilini. Hatimaye mwendeshaji mwenye uzito mkubwa atakuwa anapunguza uzito endapo tu ataendesha baiskel mara kwa mara.
Tuesday, July 15, 2014
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo na mashabiki wengi wa kandanda.Mashindano hayo hayakuisha yakigusa hisia za wadau wake tu, bali hata wasio sehemu ya michezo hiyo ,walivutiwa.Vituo kadhaa vya redio hapa nchini vimeripoti matukio mengi yalioambatana na kombe la dunia.Ikiwemo kuongezeka kwa kipato na ajira za misimu na za kudumu hasa katika televisheni,TV cable,Ving'amuzi na mabanda ya kuonyesha mpira.Sifa hizo za kombe la dunia ni njema kwa upande mmoja ,na mwiba kwa sehemu ya pili.Huu upande ni pale michuano hiyo ilipopelekea kuhatarisha ndoa za watu, kuiba muda mwingi wa wanafunzi, kuvunja ratiba za kazi hasa kwa watumishi wa usiku.Ikumbukwe kuwa kila baada ya miaka minne kombe la dunia huandaliwa, na huenda pande za faida na hasara zikatatokea tena . Lakini mbali na yote ni mhimu mtu mmoja mmoja akajipangia utaratibu wa kuburudika na tukio hili la kihisoria huku asiwe muathirika mkubwa wa changamoto zake. Na kitu cha mwisho ni swali,je umewahi kutambua mchango wa majina haya ;Ricky Martin,Shakira , KnaanPitbull, Jenifer Lopez,Claudia Leitte, ? Haya ni majina ya nyota na wanamuziki walioshika ngao ya burudani kwa nyimbo zao moto moto katika makombe yaliopata kutokea.Nyimbo hizo zilizotenda haki ya burudani ni kama La Copa de la Vida (The Cup of Life 1998),"Hips Don't Lie (Bamboo mix 2006),''Waka waka(its time for Africa 2010)'', Waving flag 2010,"We Are One (Ole Ola 2014)","La La La (Brasil 2014)" .Miongoni mwa vibao hivyo, leo ni viashiria na nembo za vipindi katika vituo vya redio na televisheni nyingi hapa nchini. Kutambua mchango zaidi wa hayo majina tazama nyimbo zifuatazo.
2.
3.
4
5.
6.
7.
8.
9.
Monday, June 16, 2014
Kwa muda sasa radio, magazeti, tv , na mitandao imekuwa ni milango mikubwa inayofungua njia kwa tasinia ya michezo kupenyeza hadi kufikia wasikilizaji na watazamaji wengi .Hali inayosababishwa na upepo wa michezo unaovumishwa na wadau wa sekta hiyo. Wachezaji, wawekezaji na wadau wengine wa kandanda, kikapu, gofu, tenesi , mpira wa pete n.k, kwa asilimia zaidi ya 70 wameweza kufanya michezo ikawa moja ya kivutio kikubwa cha wageni halikadharika wenyeji katika nchi mbalimbali .Huku Siri ya kuwa kivutio cha aina hiyo ikibakia kuwa ni miundombinu bora na ya kisasa.Kwa kutazama kandanda, ambao ni mchezo unaoongoza kwa kupendwa na mashabiki wengi duniani, muundo wa viwanja vyake lazima ukufurahishe.Hasa ukiangalia michuano mikubwa ya mpira wa miguu kama vile kombe la dunia ,ligi kuu za mabara na mashindano mengi maarufu ya mchezo huo . Hivyo kitabu kwanza Blogspot ikapata muda wa kuandaa picha zinazoelezea hali halisi ya viwanja kadhaa nchini Tanzania. Huku swali la kujiuliza likiwa ni, je iwapo tutakuwa waandaji wa kombe la dunia, viwanja vyetu vinaweza kukidhi hadhi na viwango vinavyohitajika?.Tazama picha za viwanja vitano vya Tanzania
| Kiwanja cha ccm kirumba,mwanza kwa juu |
.
![]() |
| Uwanja wa kirumba kwa pembeni |
| ndani ya uwanja wa kirumba |
| Kiwanja cha Maji maji Songea kwa juu |
| Maji maji Songea |
![]() |
| uwanja wa maji maji kwa pembeni |
| Ndani ya uwanja wamajimaji, songea |
| Ndani ya uwanja wa maji maji songea |
| Uwanja wa Nangwanda Mtwara kwa juu |
| Uwanja wa Nyamagana, Mwanza |
| Uwanja mpya Dar es salaam kwa juu |
| Uwanja mpya na wa zamani ,Dar es salaam kwa juu |
![]() |
| uwanja mpya kwa pembeni |
![]() |
| uwanja mpya kwa pembeni |
![]() |
| Ndani ya uwanja mpya wa Dar es salaam |
Tuesday, May 20, 2014
Mashindano yanayohusisha vyuo vingi vya hapa Mtwara, maarufu kama pro life, yalifikia kilele hapo jana jumapili ya tarehe 18 april,2014.Huku mshindi wa mpira wa pete akiwa ni mwenyeji wa mashindano hayo,chuo cha Sauti Mtwara(stemmuco),akifatiwa na mshindi wa mpira wa kikapu ambaye ni Bandari .Hatimaye kinara katika mchezo wa mpira wa miguu ama kandanda uliokuwa na vuta nikuvute nyingi, hadi kufikia matuta, mshindi aliibuka tena timu ya Bandari.Hii ni sehemu ya matukio mbalimbali yaliyojili uwanjani hapo Nangwanda.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...









