Saturday, February 27, 2016
Siku zote maisha ya mwanadamu yanaaongozwa na miiko au kanuni. Ni miiko hiyohiyo ambayo ilianza toka zamani lakini ambayo lengo lake kubwa lilikuwa ni kutuelekeza mambo yapi tufanye na mambo yapi tusiyafanye katika maisha ili tufanikiwe. Wale waliofuta miiko hiyo ni kweli walifanikiwa, na wale walioikiuka walishindwa katika maisha yao kwa naman fulani.

Kwa bahati mbaya au nzuri miiko au kanuni hizo zinafanya kazi katika maisha yetu mpaka sasa. Wengi huwa hawajui katika hili, lakini upo umuhimu mkubwa sana wa kuijua na kuifuata hiyo miiko au kanuni na kuamua kuachana na mambo ambayo yanawezayakawa kizuizi kwetu cha mafanikio. Katika makala hii tutaangalia mambo ambayo ni lazima tuyaache ili tufanikiwe.

Yafuatayo Ni Mambo Unayotakiwa Kuyaacha katika Maisha Yako.
1. Acha kuruhusu makosa madogo madogo, hatimaye yakawa makosa makubwa na yakakuzuia kufanikiwa .

2. Acha kukimbia changamoto zinazokukabili, pambana nazo mpaka ufanikiwe na kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako.

3. Acha kusahau kule ulikotokea. Yapo mambo ya kujifunza kutokana na kule tulikotoka.

4. Acha siku zote kujijengea tabia ya kulalamika. Kama utaebndelea kufanya hivyo utashindwa katika mambo yako mengi sana .

5. Acha kamini kuwa utashindwa kwa kile unachokifanya. Kila mara na kila wakati amini wewe ni mshindi wa maisha yako.

6. Acha kuruhusu pesa ikakutawala. Matokeo yake itawale pesa na hiyo itakusaidia kufikia uhuru wa kipesa.

7. Acha Kurusu hofu ikakutawala maisha yako. Kwa kadri utakavyozidi kuwa na hofu ndivyo ambavyo maisha yako yatazidi kuwa mgumu. Hiyo yote ni kwa sababu utashindwa kufanya mambo yako kwa sababu ya hofu ulizonazo.

8. Acha kuanzisha biashara, huku ukiwa unategemea bahati ndiyo ufanikie. Ondoa mawazo ya bahati na fanya biashara yako kwa kujimini, utafanikiwa.

9. Acha kujijengea tabia ya kufurahia, hasa ple mambo yaw engine yaopkuwa mabaya. Badala yake wape moyo na kuwafariji.

10. Acha kuogopa kusonga mbele, hata kama kuna wakati unahisi kama vile unakwama. Wewe endelea kukazana na kusonga mbele na mwisho wa siku utafanikiwa.....

Makala kwa msaada wa mwungwanablogspot.com

0 comments:

Popular Posts