Showing posts with label wasanii. Show all posts
Showing posts with label wasanii. Show all posts
Monday, December 8, 2014
Kwa muda mwingi wasanii wamekuwa wazungumzaji wakuu , wakisema visa na mikasa ya kila siku.Sauti zao hujadili makosa ya jamii, mafanikio ya jamii n.k. Wakati wakiongelea  makosa ambayo huambatanishwa na shughuri za kibinadamu zisizofanikiwa au kutekelezwa kwa kiwango stahiki. Pia wasanii huangaza mafanikio ya watu katika jamii kwa kutazama  jitihada za mwanaume au mwanamke zilizotoa matunda katika utaftaji wa maisha bora.Msaani mmoja anapofanikisha kuongea juu ya kushindwa na kufaulu kwa kugusia shida na raha lazima kazi yake ipendwe na jamii.Vile vile msanii anapoweza kutia moyo watu au  mtu aliyepoteza matumaini ya kuishi halikadhalika kazi yake hupendwa.  Na pale huyu msanii akifumbua fumbo  gumu kwa wananchi, mchango wake daima hausahauliki mapema. Katika jopo la la watu ambao ni kioo cha jamii ,hatuwezi kuwasahau wanamuziki. Kwa kuwa ni miongoni mwa wasanii muhimu katika jamii, ambao hugeuka waalimu na kutoa maarifa ya mambo yatukabiliyo kila mara. Hivyo nakusihi ufuatilie kile wasnii wa Afrika mashariki wanachosema   kuhusu maisha.

1.''maisha ni kama safari ni safari hakuna ajuaye kesho itakuaje''Jaquar


2.''Maisha ni sawa na kupiga mbizi,leo juu kesho chini,usinicheke kukosa.''Twanga pepeta.

3''Maisha ya mtaani ninanayo yaona sio sawa na ya shule niliyoyasoma''FID Q,na witness



4.'' Maisha ni fumbo fumbua,maisha ni bahati ,ifumbate  maisha ni mapigano,pigana'' Mwijuma Muumin

5.''Maisha ni kitendawili kigumu sana leo umepata kesho umekosa'' kimobitel

6.''maisha ni tendo lifanikishe,maisha ni huzuni ishinde,maisha ni mtihani faulu'' Mwijuma Muumin

7 .''Maisha ni safari nitafika msafiri kwa imani ya kuamnika sitofichwa kama siri''One the Incredible

8. ''maisha ni karata unaweza ukalamba dume,ukalamba garasha, ukalamba mzungu wa nne''Geez Mabovu



Tuesday, July 15, 2014
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku  ilikonga mioyo ya wanamichezo na mashabiki wengi wa kandanda.Mashindano hayo hayakuisha yakigusa hisia za wadau wake tu, bali hata wasio sehemu ya michezo hiyo ,walivutiwa.Vituo kadhaa vya redio hapa nchini vimeripoti matukio mengi yalioambatana na kombe la dunia.Ikiwemo kuongezeka kwa kipato na ajira za misimu na za kudumu hasa katika televisheni,TV cable,Ving'amuzi na mabanda ya kuonyesha mpira.Sifa hizo za kombe la dunia ni njema kwa upande mmoja ,na mwiba  kwa sehemu ya pili.Huu upande  ni pale michuano hiyo ilipopelekea  kuhatarisha ndoa za watu, kuiba muda mwingi wa wanafunzi, kuvunja ratiba za kazi hasa kwa watumishi wa  usiku.Ikumbukwe kuwa kila baada ya miaka minne kombe la dunia huandaliwa, na huenda pande za faida na hasara zikatatokea tena  . Lakini mbali na yote ni mhimu mtu mmoja mmoja akajipangia utaratibu wa kuburudika na tukio hili la kihisoria huku asiwe muathirika mkubwa wa changamoto  zake. Na kitu cha mwisho ni swali,je umewahi kutambua mchango wa majina haya ;Ricky Martin,Shakira , KnaanPitbull, Jenifer Lopez,Claudia Leitte, ? Haya  ni majina ya nyota na wanamuziki walioshika ngao ya burudani kwa nyimbo zao moto moto  katika makombe yaliopata kutokea.Nyimbo hizo zilizotenda haki ya burudani ni kama La Copa de la Vida (The Cup of Life 1998),"Hips Don't Lie (Bamboo mix 2006),''Waka waka(its time for Africa 2010)'', Waving flag 2010,"We Are One (Ole Ola 2014)","La La La (Brasil 2014)"  .Miongoni mwa vibao hivyo, leo ni  viashiria  na  nembo   za vipindi   katika vituo vya redio na televisheni nyingi hapa nchini. Kutambua mchango zaidi wa hayo majina tazama nyimbo  zifuatazo. 

2.

3.

4

5.

6.

7.

8.

9.


Monday, June 23, 2014

Kwa rika ni kijana , kijana wa futi 5, mtazamo ni  chanya, chanya inayo aksi elimu  ya juu, idadi ni wa pili kati ya watoto watano wa familia ya mh Abraham.L.Chaula.Ni mwajibikaji, ni mwanamapinduzi na   mwanaharakati asimamapo kati ya ndugu, jamaa na rafiki zake  . Utendaji ni mwana fasihi anayefanya sanaa inayoshabiana na vitu vitatu muhimu ambavyo ni, maisha, mazingira halikadhalika tamaduni inayomzunguka.  Kwake uthubutu ni kujituma, kujaribu na kufikia malengo. Kitu ambacho ni cha thamani na kinahitaji  juhudi zaidi  . Huyu siye mwingine  isipokuwa ni Izacka chaula(Chella), ambaye ni mmoja ya watu waliobahatika kuliona jua takribani miongo miwili na nusu iliyopita. Kwa maana ya kutimiza  miaka    24 sasa toka azaliwe mwaka 1990 , huko  wilayani Njombe (hivi sasa ni mkoa) ndani ya mji wa Iringa. Akiwa huko mwanzoni mwa miaka ya 2000, ana umri usiozidi  miaka 10 , kipaji chake  kama  vipaji vingine kinastawishwa na kuchavushwa na baba yake mdogo anayeitwa Zakayo L Mwalongo (Mtoza Mc)  ,ambaye ukaribu wake na Chella  unajenga kundi linaloitwa MICHANO LUKUKI, kama ngao ya ujuzi  katika uandishi wa tungo maridhawa. Hatimaye mtoto huyu  wa pili kati ya watoto watano anagundulika na karama ya kupenyeza mawazo pevu, endelevu na shawishi  kwa uwezo wake katika uandishi wa beti na mizani mahiri ,jambo ambalo linamfanya awe mjuzi wa matatizo , changamoto na matukio  mbalimbali ya jamii na jumuiya anayoishi. Baadae sifa ya uandishi wa  mashahiri yenye kuonya, kukanya na kufungua mboni na ngome za masikio mengi, inajenga taswira pevu , komavu , pale anapokuwa   shule ya msingi Kibena  mkoani Njombe. Hapo shuleni marafiki wanaelewa na kutambua harakati na Sanaa anayoifanya Chella . Ndipo sasa  anatilia maanani tunu yake aliobarikiwa kuwa nayo na kuboresha zaidi hicho kipaji , anapoingia  sekondari ya Mpechi na Philip Mangula   na kupata  nafasi ya kushiriki shindano linaloitwa Philip Mangula Star Search (PMSS).Tukio linaloandaliwa na uongozi wa shule, mahususi   kutafuta vipaji vya wanafunzi shuleni hapo. Mnamo mwaka 2008 akiwa kidato cha nne shuleni Mangula , Izacka Chaula maarufu sasa kama Chella anakuwa mshindi namba moja  zidi ya washiriki wengine wapatao 30, walioshindana katika tukio hilo la kumtafta bingwa mmoja.  Safari ya matumaini, iliyojaa utashi na wingi wa ueledi inapata mafanikio, pale mshindi huyu    anapobahatika kujiunga na elimu ya kidato cha sita, Kwiro Boys high school, huko wilayani Mahenge Ulanga, mkoani Morogoro. Ni ndani ya mji huo usio na bahari, hisia za kutaka kurejea studio zinamshamiri  mwanafunzi huyu  . Hivyo anashawishika  kuandaa tungo ya nyimbo yake ya kwanza anayoipa jina la “Rudi mkoa”. Kibao kinachoelezea tabia ya vijana wengi kulowea katika miji mikubwa kama Dar es salaam huku wakisahua kurudi mikoani mwao.Ila utunzi na Sanaa hii haibadiri dira na imani yake katika elimu, kwani yeye huamini  kuwa, elimu ndio taa inayoweza kufukuza giza la ujinga na kurejesha nuru ya maarifa. Mwaka 2011 mwanaharakati huyu anafaulu kidato cha sita, hivyo  anajiunga na masomo ya juu katika chuo cha SAUT Mtwara (STEMMUCO ). Akiwa chuoni hapo anapata fursa ya kuwa mmoja kati ya  wanachuo wanaounda kundi  linalojihusisha na maswala ya muziki na sanaa,kundi hilo linajulikana kama Stemmuco All Stars  .Vitu vitatu anavyovipenda chella ndani ya kundi ni umoja na ushirikiano wa wanazuoni,vipaji vikubwa walivyonanvyo wasomi wenzake na michango mizuri itokanayo na mitazamo chanya. Mbali na shughuli za kikundi , thamani na mchango  wa wanakikundi ,Chella amekutanisha mawazo yake na watu wengine  wenye tunu ya kuandaa mashahiri yenye shabaha katika  kuelimisha na kufunza. Hawa mahodari wa fasihi andishi ni pamoja na Mtoza mc, Domokaya, BeckaTittle, Jebby Mubarak, Joseph Haule’’ prof jay’’, P-the MC, Juma Kassim Kiroboto ‘‘juma nature’’ Juma Jazz , Nicolazo n.k.Wanaomsaidia Kutoa kwa ufasaha kila aina ya uwezo na kitu alichanacho msomi na mtanzania huyu. Anafanikiwa kuandika mashairi mazuri na hatimaye kutia sauti yake inayoibua chachu , mapinduzi, na mabadiliko ya sanaa yake.Hali hii ni kielelezo tosha  jinsi mwanaharakati, mwanamapinduzi na mwajibikaji huyu  anavyopigana kwa hali na mali  hata kuingia mikoa zaidi ya mitano ,mitaa zaidi ya tisa,katika studio zaidi ya 10 ,akifanya kazi na waandaji wa midundo(music producer) wasiopungua 7 na kushirikiana na wasanii wanaonzia 10 hadi 20.Chella amefanikiwa kuingia baadhi ya miji kama  Dodoma, Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Njombe Mbeya, Ruvuma na Mtwara . Akifikia mitaa mbalimbali  ya mikoa hiyo kama Railway, Masaki, Kinondoni, Kigogo, Mbezi, na kuingia studio za Tongwe Rec, Mkubwa na Wanawe, Koma studio, Robbies Rec , Kp Rec, Shine Rec, Natal Rec, Baridi Touch, E-Lab,Kimya Rec , Mama Land Rec, George Rec,Goka rec,AB Rec  na nyingine  nyingi, chini ya waandaji mahiri wa muziki  nchini wakiwemo akina Geof Master(manuva), Kona Beats,Main, Jero,Pezo,Tonny(Efficiency man), Necka Beats, Jose Braiz Beats,Kagusa Andrew. Uchaguzi wa  wadau hawa wa   muziki , umezingatia  vitu vikuu viwili ambavyo ni, uchipukizi na ukongwe wao katika tasinia ya mziki, unaochangia   kazi kuwa  na uzuri. Upekee na ubunifu tofauti wa kazi zao. Mantiki inayopelekea kuonekana kwa vionjo vya kiasili na radha iliyojificha ndani ya sanaa na kazi za mwana hip hop na msomi huyu. Baadhi ya kazi ambazo Chella kafanya ni pamoja na Rudi mkoa (Dar imekupa kiburi), tatizo nini (ft Geof Master), nitafika ft becka Title, mimi na Yule ft Juma jazz, ningezaliwa Dar, naongea na wallet, Bado napambana,jiulize , usiniache , Azimio la kijiji n.k, . Kazi hizi na ushirikiano  alioufanya  msanii huyu na wajuzi wengine toka nje na ndani ya tasnia ya muziki imesaidia katika kumjengea mtazamo  wa ziada  Ukiachilia kando kimkoa, kikanda na kitaifa Chela ana mtazamo na ndoto za kufikia ngazi ya kimataifa kwa kufanya kazi bora zaidi kama zile za kina Marshall Bruce Mathers ''eminem''na wana hip hop  wengine wanaofanya vizuri duniani kote. 
                                                      






















Saturday, July 27, 2013
Ni miongoni mwa  maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha  ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanadamu bila kubagua kama  ni mwalimu au mwanafunzi,amesoma ama hakusoma .Tutangalia aina mbili za elimu.Elimu rasmi na elimu isiyorasmi( formal and non-formal education).Hapa kuna tumaini jema katika kufahamu ukweli na pengine maana juu ya maisha.Kwani kuna misemo na maana nyingi sana za maisha katika aina hizi mbili za elimu .  Kama ilivyo katika misamiati mingine mingi , msamiati wa maisha umeibuka gumzo hata kupelekea wanafalsafa ,wasanii  na waelimishaji  wengi kujaribu kuongelea  maisha.Mawazo yao katika maana ya maisha ,inatofautiana sana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.Tofauti kubwa ni katika mtazamo, uwezo wa kutafakari na kufikiri .Kutoka Tanzania tutangalia misemo na maana mbalimbali za maisha zitokanazo na wasanii watano(5)sambamba na sanaa zao za muziki.

1. "Maisha ni kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka"Fid q



2."Maisha ni kama gwaride kuna mwisho na wa kwanza ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza"Stamina

3.''Maisha siyo  komborela ukasubiri kubutua jipange jitume ipo siku utafunua"Nay wa Mitego


4."Maisha ni kutenda na siyo majaribio"Mrisho Mpoto


5."Amini wewe ndiye steringi na maisha ndio sinema"Prof jay

Popular Posts