Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Showing posts with label kujifunza. Show all posts
Showing posts with label kujifunza. Show all posts
Tuesday, June 7, 2016
Bahati ni ndoa ya vitu viwili: maandalizi na fursa.Fursa ni msingi wajambo moja,nafasi .Nafasi ni mahusiano ya mambo matatu;nia uwezo na utekelezaji..Palikuepo na mtu mmoja alie amini katika bahati,fursa,nafasi, na utekelezaji .Huyo mmoja alikuwa kiongozi.Uongozi wake ulijaa utani.Hata moja ya kauli yake pendwa akiwa na raia wake ilikuwa ni hii.''Ndugu wana nchi msidharau vitu vidodo,vitu vidogo vinaumiza,kama mnabisha jaribuni kukalia sindano'' .Halaiki ilikufa kwa mbavu baada ya huu utani.Ukitaka kuamini vitu vidogo ni muhimu vinaendesha dunia,na ukivithamini utafurahia ,hautaumia ungana nami kwenye hizi stori zifuatazo
Hakuwahi kujiona kama mpiga ngumi,au bingwa wa makonde kimataifa.Mpaka pale alikumbwa na mkasa mdogo sana.Mohamedi Ali akiwa kijana mdogo miaka kama kumi na kitu ivi.Aliibiwa baiskel anayoipenda .Na akaripoti kwa askari kuwa akimpata mwizi atampiga.Askari alimwambia atamwajibishaje mwizi yule wakati hana uwezo wa kupigana.Basi ikabidi askari amfundishe Mohamedi Ali kuchapa masungwi.Baada ya kuiva hakumtafta mwizi ila akaingia kwenye mashindano ya ngumi
.
2.MOHAMMED DEWIJ
Safari yake ki siasa ilianza baada ya kuona tukio dogo mkoani mwake Singida.Anasimulia''Nimetoka(Singida mjini) km 6 nakutana na mzee mmoja,kulikuwa kuna maji ya njano chini ,alikuwa na ndoo na sinia,amechuchumaa akiteka maji nakutia ndani ya chombo.Nikamsalimia mzee Shikamoo,unafanya nini hayo maji,akasema haya maji ndio tunakunywa sisi.Sikumwamini hadi pale nimefika kwake na kuona watoto wakinywa maji yale yale ,mzee akanisihi MO,kwa nini usigombee ubunge?''Sauti ikamgusa Bwana MO.MO akagombea ubunge.MO akachimba visima .Wananchi wa Singida wakanufaika kwa huduma ya maji.

3.JUX
Licha ya kupenda kun'gaa na mziki ,Juma jux hakuwahi kufikiri kama ni mwimbaji.Jux alikuwa anafanya hip hop kama vijana wengi wa mtaani. Nini kilimbadilisha? Baada ya Jux kumsindikiza msanii mkubwa studio.anatokewa na jambo dogo linaloleta hamu ya uimbaji..Na hapa jux mwenyewe anasimulia .''Tulienda studio na Cyril,Cyril alitakiwa kufanya collabo na Makamua .Makamua alikuwa msanii mkubwa.Basi(Cyril) akampigia Makamua,Makamua akadai atakuja, tulichoma sana mahindi pale(tulikaa sana).Kuanzia kama saa moja mpaka saa tano tano.Maneke( producer wa muziki) akawa kaweka ile Beat.Ile beat imewekwa mie nikawa kama naimba tu unajua mzuka wa studio.Maneke akasikia naimba,akasema ebu imba tena,nikaimba.Akanambia mbona unaweza kuimba kwa nini unachana(kurap).Saa izo naogopa kinoma naogopa ile mic sana,sio nilikuwa naogopa kuimba,nilikuwa naogopa kusikiliza nyimbo yangu mwenyewe kwenye redio,nilikuwa naona aibu sana.Akasema(Maneke) unaweza kuimba jaribu.Nakumbuka ndo mara ya kwanza naingia booth kurekodi''
Friday, March 20, 2015
Binafsi
nimezoe miradi ya familia ni maduka ya bidhaa kama simu, nguo, mifugo, daladala, n.k. Ambayo huanza
na kasi ,baadae kudorora na baadhi ya miradi kupotea kabisa.Tafiti zinaonyesha kuwa kati
ya miradi mitatu ya familia ni mradi mmoja
tu hudumu.Na kwa huo mradi unaodumu hakika uongozi ni sindano kubwa katika kufuma timu ya
usimamizi wake.Wakati biashara hii inayomilikiwa kiasi kikubwa na wanafamilia
inategemea sana menegementi bora. Mataifa ya Izrael , Canada ambayo uchumi wake
umestawishwa kwa zaidi ya asilimia 65 na miradi ya familia.Wanatambua siri
nyingine za kufanikiwa kwa biashara zao. Moja, ni mgawanyo wa majaukumu baina ya
wanafamilia. Baba, mama ,kaka na dada anahusika na jukumu moja moja kati ya
uhasibu, matangazo, utafiti, soko na maboresho. Korea na India ambao pia ni
majabari wa miradi ya familia. Wanatambua fika kuwa,ukuu wao katika hizo biashara
ni matokeo mazuri ya kuweka mipango ya kudumu ambayo hufuatwa na kila kizazi
kinachorisishwa mradi. Palestine taifa lenye miradi mingi ya famillia kama
kitovu cha uchumi wake, pia wanang’oa mizizi ya maendeleo yao. Wakibainisha kuwa
kutoweka hisia za ndani katika hizi biashara ni nyota njema inayoangaza mafanikio
ya miradi ya familia.Katika suala la hisia mtama zaidi unamwagwa
kuwa,sio kila ndugu ajiriwe au kupata huduma ya bure, ila vigezo na
masharti vizingatiwe. Na Italy ambao ni watengenezaji suti wazuri wameachia
mikono ya familia inue haya mavazi ya thamani katika kila jicho la ulimwengu. Zaidi
ya asilimia 90 ya miradi ya kifamilia
nchini humo huepuka matumizi mabaya ya faida inayozalishwa na mradi , jambo
linalozuia mparaganyiko na kusambaratika kwa biashara zao.Ikumbukwe tu kuwa
miradi hii ni ya aina nyingi kama vidonge.Kuna miradi mikubwa kuna miradi midogo.Barafu,karanga,na
nyanya za magengeni ni miradi ya familia yenye sura ndogo.Makampuni ya
gari,simu,vitabu , ni miradi ya familia yenye sura
kubwa.Unafahamu biashara kubwa za kifamilia ambazo zitakuacha mdomo wazi ?,Basi
usichoke, tazama namba moja hadi kumi hapa chini.
1.Toyota
2.Ford Motor
3.Tata group
4.Volkswagen
5.Samsung
6.LG
7.Motorola
8.Siemens
9.Kodak
10.World
Wrestling Entertainment(WWE)
Friday, February 27, 2015
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unaoletwa na uteuzi wa nguo ambazo huwa na rangi mbalimbali.Mfano katika shule sio jambo geni mwanafunzi kumtambua mwalimu aliye na hasira , kwa kutumia aina ya nguo alizovaa. Hata katika usafiri ni rihasi kubaini hadhi ya mtu kwa kutumia nguo tu .Kwa maana mavazi ni lugha ya ishara inayojisimamia bila sauti. Nakumbuka siku moja nikiwa jijini mwanza ,katika moja ya kituo cha magari madogo maarufu kama daladala.Nilishuudia kijana akikosa msaada ilihali alikuwa na shida kubwa. Kijana alielekea kwa mzee kuomba msaada wa nauli.Mzee ni baba wa makamo kwa sauti na jicho alivyomkazia muomba msaada.Kinyume na fikira zangu ,yule mzee hakutoa hata shilingi .Baaadala yake akadai asingeweza kumpatia kijana fedha.kwani kijana alikuwa na maisha mazuri. Dhana iliyoletwa na kijana kuvaa kofia nyekundi, shati jeusi , kaptula jekundu , soksi nyeusi viatu vyekundu na kitambaa cheusi. Mwisho jitihada zilivyogonga mwamba, kijana akatoweka' kilaini' kama wasemavyo waswahili wa kisasa.Tukio hili halipo mbali na wasemavyo wanasaikolojia, wataalamu wa tabia,akili na mienendo ya binadamu.Ambao wamethibitisha kuwa tamaduni na mazingira mbalimbali ni sababu kuu zinzopelekea mavazi kupewa maana tofauti tofauti katika jamii.Wakielezea kwa undani zaidi,wataalam hao wanadai mavazi ya rangi ,nyekundu, blue, nyeupe, nyeusi, njano na kijani yana maana zifuatazo.
1.Nguo za rangi nyekundu.ni mavazi yanaofananishwa na taswira ya damu au moto.Kwa baadhi ya watu huwa ni vazi linalomaanisha nguvu,mabavu na utawala ,jambo linalopelekea mtu huyu kupewa umakini katika kundi la watu.Pia vazi jekundu ni ishara ya upendo wa dhati kama linavyopewa umuhimu katika harusi za kihindi,kijapani na vipindi vya valentine day pamoja na Christmas.Lakini pia kwa baadhi ya tamaduni, vazi jekundu hutafsiriwa kama kiashiria cha hatari au vita
2.Nguo za rangi ya Blue mara nyingi huwakilisha bahari na anga.Hii ranga kupendwa na wanaume zaidi.Mtu mwenye sharti, t shirt au vazi lolote la blu,hutafsriwa na jamii kama tu muaminifu,mkweli,mpole ,mwenye kujiamini na mtulivu.Lakini pia kuna mazingira mengine ambayo huashiria vazi la blue kama huzuni
3.Nguo za rangi ya kijani.Wakati hii rangi husadifu uoto wa asili,kijani kibichi na mazingira.Vazi la kijani hutambulisha mtu kama anayekuaa,anayebadilika na kujitegemea .Kwa miaka mingi kijani imekuwa ni rangi inayohusishwa na maswala ya uchumi pamoja na fedha.
4.Nguo za rangi Nyeupe.Hii rangi huchukuliwa kama taswira ya nuru au mwanga hivyo hata kufanya mavazi meupe kuonyesha watu wanaoweza kuleta matumaini,kama madaktari. Pia huashiria usafi, utimilifu uungwana na mtu asiye na hatia.Kama walivyo baadhi ya mabibi harusi ndani ya shela,na viongozi wa dini ndani ya kanzu na majoho meupe
5.Nguo za rangi ya Manjano(njano).Hii ni rangi inayojumuisha mchanganyiko wa nyekundu na nyeupe kama wakati wa mawio au jua la asubuhi.Njano ikiwa ni miongoni mwa rangi ing'aayo sana,Vazi lake humaniisha mvaaji ana furaha, ni tegemezi, mshindi, mtaka uhuru.Nchini Japani na china manjano ni rangi ya watu wenye hadhi ya juu na kueshimika.
6.Nguo za rangi nyeusi ni kielelezo cha upotevu wa rangi nyingine na mtu aliye vaa shati ,suruali au gauni nyeusi inaatafsiriwa ana huzuni au majonzi(utamaduni wa kimagharibi),,Pia kwa baadhi ya mazingira vazi jeusi huwa ni ishara ya usiriasi,mamlaka,na ukuu.Kama zilivyo maarufu suti nyeusi,na viongozi wa serikali. kadharika joho jeusi na mahakimu
Monday, December 8, 2014
Kwa muda mwingi wasanii wamekuwa wazungumzaji wakuu , wakisema visa na mikasa ya kila siku.Sauti zao hujadili makosa ya jamii, mafanikio ya jamii n.k. Wakati wakiongelea makosa ambayo huambatanishwa na shughuri za kibinadamu zisizofanikiwa au kutekelezwa kwa kiwango stahiki. Pia wasanii huangaza mafanikio ya watu katika jamii kwa kutazama jitihada za mwanaume au mwanamke zilizotoa matunda katika utaftaji wa maisha bora.Msaani mmoja anapofanikisha kuongea juu ya kushindwa na kufaulu kwa kugusia shida na raha lazima kazi yake ipendwe na jamii.Vile vile msanii anapoweza kutia moyo watu au mtu aliyepoteza matumaini ya kuishi halikadhalika kazi yake hupendwa. Na pale huyu msanii akifumbua fumbo gumu kwa wananchi, mchango wake daima hausahauliki mapema. Katika jopo la la watu ambao ni kioo cha jamii ,hatuwezi kuwasahau wanamuziki. Kwa kuwa ni miongoni mwa wasanii muhimu katika jamii, ambao hugeuka waalimu na kutoa maarifa ya mambo yatukabiliyo kila mara. Hivyo nakusihi ufuatilie kile wasnii wa Afrika mashariki wanachosema kuhusu maisha.
1.''maisha ni kama safari ni safari hakuna ajuaye kesho itakuaje''Jaquar
2.''Maisha ni sawa na kupiga mbizi,leo juu kesho chini,usinicheke kukosa.''Twanga pepeta.
3''Maisha ya mtaani ninanayo yaona sio sawa na ya shule niliyoyasoma''FID Q,na witness
4.'' Maisha ni fumbo fumbua,maisha ni bahati ,ifumbate maisha ni mapigano,pigana'' Mwijuma Muumin
5.''Maisha ni kitendawili kigumu sana leo umepata kesho umekosa'' kimobitel
6.''maisha ni tendo lifanikishe,maisha ni huzuni ishinde,maisha ni mtihani faulu'' Mwijuma Muumin
7 .''Maisha ni safari nitafika msafiri kwa imani ya kuamnika sitofichwa kama siri''One the Incredible
8. ''maisha ni karata unaweza ukalamba dume,ukalamba garasha, ukalamba mzungu wa nne''Geez Mabovu
Tuesday, December 2, 2014
Mwezi novemba mwaka 2014 nilifika mkoa fulani hapa Tanzania kwa ajili ya mahafali . Na kwa kuwa matumizi ya simu za kisasa''smartphone'' ni makubwa kwa kila mmoja ili nibidi ninunue simu ya dizaini hiyo ilahisishe mambao yangu. Hii ilikuwa ni simu ya tecno H6 iliyoweza kupiga picha za ubora mzuri kama zile za kamera ya kawaida. Ila mungu si Athumani asubuhi ya keshokutwa, siku mbili baadae, niliamkia mazoezini kama ada yangu . Nikikimbia kando ya bahari ya hindi kwa muda wa nusu saa hali iliopelekea kuchoka sana kwani ni muda sijafanya joging. Hata jioni nikiwa katika mgahawa mmoja ,najivinjari kwa smartphone mkono wa kushoto na maji mkono wa kulia nikinywa taratibu kwa fundo la kizembe bado nilihisi uchovu wa mwili na akili uliotokana na zoezi la asubuhi. Baadae kidogo niliondoka eneo hilo la chuo kulipokuwa na mgahawa nakuelekea nje. Nikiwa nje nilitaka kuwajuza marafiki zangu kuwa nipo tayari mkoani hapo, ndio ghafla nashishituka sina simu mfukoni wala mkononi. Japo akili ilikuwa imechoka , niliweza kumbuka kuwa , kabla ya kulipia maji kwa muhudumu niliacha simu mezani na sikuichukua wakati naondokka eneo hilo. Nikafanya jitihada za kumdadisi mhudumu hakuweza kufahamu lolote. Nikauliza watu waliokuwa karibu yangu wakitazama mechi ya West Brom na Arsenal Betting iliyochezwa siku hiyo ya jumamosi tarehe 29 novemba , nao pia walikana kuiona smartphone yangu mpya iliyokuwa na siku tatu tu toka ninunue. Hatimaye nimeuliza mtandaoni na majibu yao yameshauri matumizi ya programm zifuatazo.
1. LOOKOUT. Hii ni moja ya programm inayomwezesha mmliki wa simu aina ya android kubaini mienendo ya simu iliyopotea. Huku ikitoa taarifa mahala simu ilipo , Pia hii programu inapiga picha za siri bila mwizi au aliyechukua kutambua na kutuma moja kwa moja kwa anuani yako uliojisajilia katika hiyo programm.Ina uwezo wa kufunga ama kufuta habari binafsi zilizondani ya simu na endappo upo karibu na mtu mwenye simu yako programm inakuwezesha kuruhusu simu itoe alarm na kumkamata mwizi.
2. LOOKOUT PLAN B. Tofauti ya programm hii na ya kwanza ni kuwa Lookout plan B hutumika na baadhi ya simu tu zinazotumia mifumo ya android. Na wakati programm zote katika hii list zinahitaji kuwekwa katika simu kabla haijaibiwa, Lookout plan b inaweza kuingizwa katika kifaa kilichopotea ama kuibiwa hata baada ya mwizi kutokomea Ni kwa njia ya mtandao Lookout Plan B huweza kufikia simu iliyopokonywa.
3. PREY. Kama zilivyo programm nyingine hii pia inapatikana Google play , yaani katika simu zitumiazo android . Au kwa urahisi sana zinajulikana kwa jina la '' simu za tachi' '(touch). Prey ni programm ambayo inauwezo wa kuonyesha mitandoo yote inayotumiwa na simu yako iliyopotea. Lakini hata kama kulikuwa na picha za muhimu hii ni prograam iayoweza kuzihifadhi katika account au anuani yako ya google.Zaid Prey huweza kutumika hata kutafta laptop na tablets zilizopotea.
4. FIND MY PHONE. Hii programm inatofautiana na nyingine kwa kuwa inawafaa watumiaji wa Iphone na vifaa vingine vinavyotengenezwa na kampuni ya Mac.Ambao ni wazalishaji wa ipod, ipad na simu zaIphone. Habari nyeti za mtu alizoacha katika simu hupelekwa na progrmm hii hadi uwanja wa icloud. ambako mmliki wa simu hufika kwa kufanya usajili mdogo. Hapa utajua simu yako iko wapi, nani anaitumia kwa kutazama picha zilizopigwa kwa usiri wakati mwizi akiitumia.

5. ANDROID DEVICE MANAGER, Ni aina nzuri ya programm katika kurudisha simu kwa kuwa ina sifa kama programm nyingine ikiwemo ile ya kuwafaa watumiaji wa android, Pia ina mambo muhimu ya kuzingatia kama ; kupata simu iliyopotea .kwanza. inatakiwa iwe imeunganishwa na mtandao, pili, iunganishwe na na programm hii kabla haijaibiwa, tatu, simu itaonekana baada ya kuwa karibu na minara ya simu, huduma za wireless, bloothooth na mifumo mingine yenye kutuma mawasiliano katika satellite za google , nne, kuifikia simu iliyopotea unatakiwa kutumia simu tofauti, computer au kifaa kingine. Mwisho hii programm kama hizo zilizotajwa juu hupata simu ikiwa imewashwa na sio kuzimwa
.Kumbuka ni vyema kutoa taarifaya upotevu wa mali yako katika uongozi wa serikali kama polisi au ofisi ya kijiji kabla ya kufanya ufuatiliaji kwa kutumia programm hizi.
Monday, September 15, 2014
1
.
2.Usalama
wa maisha
3. upendo na mahusiano
.4.Uwezo na heshima.
.5. Uhuru
katika
Thursday, September 11, 2014
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na ajira hawakuweza kutafta mvuto kwa namna inayohusisha gharama kubwa.Hawakuweza kuingia gym, hawakuwrza kumudu vifaa maluum vya bei mbaya. Hali iliyopelea mmoja kati yao kutafta mwalimu wa mazoezi ya mwili kwa njia ya mkopo. Na mwingine kujisimamia katika mazoezi ya aina hiyo bila mwalimu kabisa. Neema alipata msaada mkubwa toka kwa huyu mwalimu wa mazoezi. Ibrahim halikadhalika alifanikiwa kutokana na bidii aliyojiwekea katika mazoezi. Wawili hawa katu hawakukata tamaa ya mazoezi hata siku moja kwa kuwa walipenda michezo kuliko kitu kingine.Walipenda kuwa wanamitindo kuliko kazi nyingine. Walivutiwa na uzuri kuliko sifa nyingine. Baada ya miezi mitatu kupita huku zoezi ni kama dini na kitu cha muhimu kwao, mmoja wa vijana hawa anatokea kuwa kisura aliyevutia sana na mwingine ni mtanashati aliyependeza sana. Huku siri yao kubwa kufika hapo walipo ndani ya muda kidogo, ikitokana na juhudi katika mazoezi yafuatayo..
1,KURUKA KAMBA. Ni zoezi rahisi lisilochukua gharama kubwa.Zoezi hili linafanyika sehemu nyingi kwa sababu vifaa vyake ni rahisi kubeba na hupatikana kwa uepesi.Kwa kuwa linahusisha mikono,miguu,mgongo na viungo vingine vya mwili,huongeza stamina,nguvu na kukaza misuri ya mrukaji. Ni moja ya zoezi zuri katika kupunguza uzito wa mwili.
2.KUKIMBIA.Ni zoezi linalofanyika uwanjani,barabarani,mbugani na sehemu nyingi za uwazi mkubwa.Zoezi hili hupendeza pasipokuwa na jua kali hasa majira ya asubuhi na majira ya jioni..Ni moja ya zoezi zuri kwa mapafu na moyo.Kwani viungo hivi hurejesha msukumo wa damu na hewa kuwa vyema,kiasi cha mkimbiaji kupata nguvu na pumzi ya kutosha katika mwili wake.
3.PUSH UP. Ni zoezi rahisi, linalochukua gharama ndogo sana na gharama hii ni muda pekee . Mbali na muda, push up hazihitaji uwanja mpana zaidi ya chunba chako. Kwa kupiga push up ndani ya nyumba itakusaidia kukaza mwili sehemu ya juu. Ukianza na kupanuka kifua, ikifuatiwa na kuimarisha mabega, mikono mgongo na tumbo. Ni zoezi zuri kwa ukakamavu
4.KUOGELEA . Ni mchezo ambao huvutia watu wengi, watoto kwa wakubwa wenye kipato na wasionacho. Lakini wakati karibu kila mmoja anafurahai mchezo huo, kuna faida nyingi mwili hupata Kwanza ni mara mbili ya zoezi la kukimbia, na huimarisha misuli ya mwili kutokana na ukinzani wa maji. Pili huondoa mfadhaiko na msongo wa mawazo, tatu ni zoezi linalohusisha
miguu, mikono, mabega na viungo vya mwili karibu vyote na baadae mwili hujengeka na kukaa fiti.
5.KUENDESHA BAISKEL. Kwa kuendesha tu usafiri wa baiskel ni sehemu ya zoezi muhimu sana kwa afya . Miguu inapokazana kupita mpando na ama tambarare. Mwili unashitua misuli inayosukuma nguvu zaidi . Zoezi hili linasaidia ubongo kwa kuwa makini na kunakiri chochote kinachoendelea. Unapofikia hatua ya kutoa jasho wakati wa zoezi hili , inasaidia kupunguza taka mwili na mafuta yasiotakiwa mwilini. Hatimaye mwendeshaji mwenye uzito mkubwa atakuwa anapunguza uzito endapo tu ataendesha baiskel mara kwa mara.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...







































