Friday, February 27, 2015
Wakati sauti  hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi   hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana  na muonekano  unaoletwa na uteuzi wa nguo ambazo huwa na rangi mbalimbali.Mfano katika shule sio jambo geni mwanafunzi kumtambua mwalimu aliye na hasira , kwa kutumia aina ya nguo  alizovaa. Hata katika usafiri ni rihasi kubaini hadhi ya mtu kwa kutumia nguo tu .Kwa maana mavazi ni lugha ya ishara inayojisimamia bila sauti. Nakumbuka siku moja nikiwa jijini mwanza ,katika moja ya kituo  cha magari madogo maarufu kama daladala.Nilishuudia kijana  akikosa msaada ilihali alikuwa na shida kubwa. Kijana alielekea kwa mzee kuomba msaada wa nauli.Mzee  ni baba wa makamo kwa sauti na jicho alivyomkazia muomba msaada.Kinyume  na fikira zangu ,yule mzee hakutoa hata shilingi .Baaadala yake  akadai asingeweza kumpatia kijana fedha.kwani kijana alikuwa na maisha mazuri. Dhana iliyoletwa na  kijana kuvaa kofia nyekundi, shati jeusi , kaptula jekundu , soksi nyeusi viatu vyekundu na kitambaa cheusi. Mwisho jitihada zilivyogonga mwamba, kijana akatoweka' kilaini' kama wasemavyo waswahili wa kisasa.Tukio hili  halipo mbali na wasemavyo wanasaikolojia, wataalamu wa tabia,akili na mienendo  ya binadamu.Ambao wamethibitisha kuwa  tamaduni na mazingira mbalimbali ni sababu kuu zinzopelekea mavazi kupewa maana tofauti tofauti katika jamii.Wakielezea kwa undani zaidi,wataalam hao wanadai mavazi ya rangi ,nyekundu, blue, nyeupe, nyeusi, njano na kijani yana maana zifuatazo.

1.Nguo za rangi nyekundu.ni mavazi yanaofananishwa na taswira ya damu au moto.Kwa baadhi ya watu huwa ni vazi linalomaanisha nguvu,mabavu na utawala ,jambo linalopelekea mtu huyu kupewa umakini katika kundi la watu.Pia vazi jekundu ni ishara ya upendo wa dhati kama linavyopewa umuhimu katika harusi za kihindi,kijapani na vipindi vya valentine day pamoja na Christmas.Lakini pia kwa baadhi ya tamaduni, vazi jekundu hutafsiriwa kama kiashiria cha hatari au vita


2.Nguo za rangi ya Blue mara nyingi huwakilisha bahari na anga.Hii  ranga kupendwa na wanaume zaidi.Mtu mwenye sharti, t shirt au vazi lolote la blu,hutafsriwa na jamii kama tu  muaminifu,mkweli,mpole ,mwenye kujiamini na mtulivu.Lakini pia kuna mazingira mengine ambayo huashiria vazi la blue kama huzuni


3.Nguo za rangi ya kijani.Wakati hii rangi husadifu uoto wa asili,kijani kibichi na mazingira.Vazi la kijani hutambulisha mtu kama anayekuaa,anayebadilika na kujitegemea .Kwa miaka mingi  kijani imekuwa ni rangi inayohusishwa na maswala ya uchumi pamoja na fedha.


4.Nguo za rangi Nyeupe.Hii rangi huchukuliwa kama taswira ya nuru au mwanga hivyo hata kufanya mavazi meupe kuonyesha watu wanaoweza kuleta matumaini,kama madaktari. Pia huashiria usafi, utimilifu uungwana na mtu asiye na hatia.Kama walivyo baadhi ya mabibi harusi ndani ya shela,na  viongozi wa dini ndani ya kanzu na majoho meupe

5.Nguo za rangi ya Manjano(njano).Hii ni rangi inayojumuisha mchanganyiko wa nyekundu na nyeupe kama wakati wa mawio au jua la asubuhi.Njano ikiwa ni miongoni mwa rangi ing'aayo sana,Vazi lake  humaniisha mvaaji ana furaha, ni tegemezi, mshindi, mtaka uhuru.Nchini Japani na china manjano ni rangi ya watu wenye hadhi ya juu na kueshimika.

6.Nguo za rangi nyeusi ni kielelezo cha upotevu wa rangi nyingine na mtu aliye vaa shati ,suruali au gauni nyeusi inaatafsiriwa ana huzuni au majonzi(utamaduni wa kimagharibi),,Pia kwa baadhi ya mazingira vazi jeusi huwa ni ishara ya usiriasi,mamlaka,na ukuu.Kama zilivyo maarufu suti nyeusi,na viongozi wa serikali. kadharika joho jeusi na mahakimu

0 comments:

Popular Posts