Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Tuesday, March 6, 2018
Baada ya kuangalia mafanikio ya watu.Ilifika kipindi nikasema''Martin huu ni wasaa wako''.Nikapumzika Kusoma vitabu vya ujasiliamali ,kutazama movie za insparation na kuzungumzia ndoto za kupata mali.Nikajisemea''kwa nini nisiache maneno na kuweka kila ninachokijua katika vitendo?''Ukiachilia mbali swala la kuomba baraka na kudra za mwenyezi mungu,Mtoa ridhiki.Nilianza na vitendo katika hatua mbili tatu.Hatua ya kwanza nilitafta mtaji,pili nikatafta mradi,tatu nikatafuta sehemu ya kuweka na mwisho msimamizi .Ndani ya miezi sita ya uendeshaji nimefanikiwa kujifunza vitu vya msingi vitano.
1.KUWA MAKINI NA MKOPO

Pesa ya kukopa ni hatari ,kabla ya kuchukua kiasi tasilimu kutoka kwa mtu au taasisi.Andaa sehemu uliyoifanyia utafti wa kina .Kisha wekeza pesa ya mkopo.Niliongozana na rafiki zangu wanne, sote tukachukua kiwango sawa cha pesa ila baada ya hii miezi sita.Ni mmoja tu kati ya wanee aliyefanikiwa na mkopo.
2.WEKA KANDO MATUMIZI YAKO NA PESA YA BIASHARA

Pili nimejifunza kuwa mradi wa biashara ,kama ununuzi na uzaaji wa bidhaa za rejareja unahitaji uvumilivu sana.Biashara hii inapenda uwekezaji wa muda mrefu .Kila pesa ya mauzo iandikwe na kuachwa hapo ofisini.Kitendo cha kuamisha faida ,kitendo cha kuchanganya mapato na matumizi binafsi au ya familia ni sumu kwa ukuaji wa mradi wako.Miezi itaenda ,mwaka utakata biashara yako ingali vilenvile.
3.USIMWAMINI MTU KATIKA PESA AU BIASHARA

Karibu kila mwenye pesa nyingi aidha aliwahi kudhurumiwa,kutapeliwa ama kuibiwa.Kwa wasiofahamu huwaona wenye miradi kama mabahiri,wachoyo wasiosaidia.Ila toka niingizwe mkenge na vijana tuliokuwapamoja.Imani kwa kila ninayeshirikiana naye kwenye biashara imetoweka.Kila anayetaka mkopo, kuazima kiasi kikubwa cha pesa namuona ni wale wale tu.
4.BIASHARA NI MAISHA NA TABIA YAKO

Biashara siyo kazi au ajira.Biashara ni tabia ya mtu ni mfumo wako wa maisha.Wengi wanaofeli kwenye hatua ndogo kama hii yangu.Walifanya kosa ambalo nimekumbana nalo mara nyingi.Binafsi nilikuwa na tabia ya huruma halikadhalika kuamini watu.Nikawa mkopeshaji mzuri tena asiyeweka hata rekodi saaa nyingine.Nilipendenda kupunguza bei kupia hata ile niliyomumulia.Baada ya mambo kuanza ugumu hasara kukithiri,Mwenyewe nilibadili mfumo wa maisha na hii tabia mpaka biashara nayo ikaanza kubadilika,
5,KUWA MBUNIFU NA JITUME KULIKO ULIVYOWAHI KUJITUMA

Kila unachotaka kukiona kesho ndani ya biashara yako,kianzishe sasa.Usikubali kulala kabla hujafanya jukumu ulilojiwekea.Mimi nilikuwa na ndoto kubwa katika biashara,Sikuwahi fikiri kama nitachukua muda mwingi kukuza biashara kwanza kabla ya kunufaika.Ndani ya miezi sita nahangaika na kuweka muonekano wa ofisi usadifu dira yangu,Najifunza mbinun kadhaa za kuleta wateja wapya kila mwezi.Pia najifunza uwezo walionao wapinzani wangu dhidiya udhaifu wangu.Mwisho nikitaza vizuri najiona nasogea nilipokusudia jana.
1.KUWA MAKINI NA MKOPO

Pesa ya kukopa ni hatari ,kabla ya kuchukua kiasi tasilimu kutoka kwa mtu au taasisi.Andaa sehemu uliyoifanyia utafti wa kina .Kisha wekeza pesa ya mkopo.Niliongozana na rafiki zangu wanne, sote tukachukua kiwango sawa cha pesa ila baada ya hii miezi sita.Ni mmoja tu kati ya wanee aliyefanikiwa na mkopo.
2.WEKA KANDO MATUMIZI YAKO NA PESA YA BIASHARA
Pili nimejifunza kuwa mradi wa biashara ,kama ununuzi na uzaaji wa bidhaa za rejareja unahitaji uvumilivu sana.Biashara hii inapenda uwekezaji wa muda mrefu .Kila pesa ya mauzo iandikwe na kuachwa hapo ofisini.Kitendo cha kuamisha faida ,kitendo cha kuchanganya mapato na matumizi binafsi au ya familia ni sumu kwa ukuaji wa mradi wako.Miezi itaenda ,mwaka utakata biashara yako ingali vilenvile.
3.USIMWAMINI MTU KATIKA PESA AU BIASHARA

Karibu kila mwenye pesa nyingi aidha aliwahi kudhurumiwa,kutapeliwa ama kuibiwa.Kwa wasiofahamu huwaona wenye miradi kama mabahiri,wachoyo wasiosaidia.Ila toka niingizwe mkenge na vijana tuliokuwapamoja.Imani kwa kila ninayeshirikiana naye kwenye biashara imetoweka.Kila anayetaka mkopo, kuazima kiasi kikubwa cha pesa namuona ni wale wale tu.
4.BIASHARA NI MAISHA NA TABIA YAKO

Biashara siyo kazi au ajira.Biashara ni tabia ya mtu ni mfumo wako wa maisha.Wengi wanaofeli kwenye hatua ndogo kama hii yangu.Walifanya kosa ambalo nimekumbana nalo mara nyingi.Binafsi nilikuwa na tabia ya huruma halikadhalika kuamini watu.Nikawa mkopeshaji mzuri tena asiyeweka hata rekodi saaa nyingine.Nilipendenda kupunguza bei kupia hata ile niliyomumulia.Baada ya mambo kuanza ugumu hasara kukithiri,Mwenyewe nilibadili mfumo wa maisha na hii tabia mpaka biashara nayo ikaanza kubadilika,
5,KUWA MBUNIFU NA JITUME KULIKO ULIVYOWAHI KUJITUMA

Kila unachotaka kukiona kesho ndani ya biashara yako,kianzishe sasa.Usikubali kulala kabla hujafanya jukumu ulilojiwekea.Mimi nilikuwa na ndoto kubwa katika biashara,Sikuwahi fikiri kama nitachukua muda mwingi kukuza biashara kwanza kabla ya kunufaika.Ndani ya miezi sita nahangaika na kuweka muonekano wa ofisi usadifu dira yangu,Najifunza mbinun kadhaa za kuleta wateja wapya kila mwezi.Pia najifunza uwezo walionao wapinzani wangu dhidiya udhaifu wangu.Mwisho nikitaza vizuri najiona nasogea nilipokusudia jana.
Thursday, April 13, 2017
Kuishi ni sayansi inayotegemea
majaribio mengi.Kinachoshindikana leo kirudiwe tena kesho.Huko ndo
kuishi.Usifanya kosa na kukata tama .Kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi lako
mwenyewe.Ukikosa tone la maji sasa jipe moyo kuna bahari inakusubiri mbele.Rudia
hicho kitu,hizo hatua hiyo shughuri naamini utaifikia bahari yako.Ukiteleza leo
kamwe usifunge kichwa nakuamini unabahati mbaya.Una mkosi una ‘’gundu’’.Lah
hasha huna hizo bahati mbaya isipokuwa Kuna kitu maisha yanakufunza.Yanasema
jiandae muda wako unawadia,rekebisha kasoro hizi chache uwe mkomavu baadae.Tunawatu
wengi kama mifano ambao walikata tama katika umri kama wako na leo wanavilio
vya kudumu.Hawana namna nyingine ila isipokuwa wanaomba muda urudi nyuma
wasahihishe makosa.Makosa yaliyozaliwa na chaguzi za kukata tamaa.Walipokutana
na punje moja ya mchanga waliogopa
kusonga mbele.Wakizani ni lazima mbele ya safari kuna jangwa kubwa likiwasubiri.Lah
hasha.Kuishi hakuko hivyo.Kuishi ni sayansi,kuishi ni majaribio, kabla ya
hitimisho fanya upembuzi wa kutosha.Mimi na wewe tungali tuna muda,tungali tuna
afya,tungali tuna akili,tungali tuna pumzi.Tukiunganisha vyote hivi hakika
safari yetu haitavunjika na zaidi sana tutakutana ana kwa ana na bahari
iliyosheheni lulu.Lulu Isiyo ndogo kwa vipimo,wala ndogo kwa kimo.Hii itakuwa
sawa sawa na mapenzi yetu.Italingana na ndoto zetu,itafanana na juhudi zetu.Lulu
hii haitakuwa na upendeleo.Itatii kiu kadri ya kila mmoja alivyothubutu ,kadri
ya kila mmoja alivyoitafta.
Punje ya mchanga anaweza kuwa rafiki yako,ndugu
yako,maamuzi yako au jambo lolote linalokufanya usisogee mbele.
Jangwa ni wazo pingamizi uoga
,wasiwasi,hisia lemavu kuwa siku za usoni hutofanikiwa na hicho kitu
unachokifanya
Kuchimba kaburi lako ni
kudidimiza uwezo binafsi uliojaaliwa na mwenyezi,ni kuweka kikomo cha kila elimu
ulioipata hapa duniani.
Tone la maji ni pamoja na fursa,bahati,nafasi,kazi au chochote ambacho
kinamuinua mutu toka katika dhiki aliyonayo mpaka fahari na anasa anazozingoja
Bahari yako ni
fahari,anasa,furaha,matarajio Yaani Kikomo kikubwa cha Starehe(K.K.S)na kila
kitu ambacho ni kinyume na shida unazopitia.
Gundu ni hali na hisia ya kutokuwa na bahati
ni bayana ya nadharia zinazohusishwa na mikosi kutokubalika,kutoendelea daima.
Wednesday, March 8, 2017
Mama ni mwanamke anayejali,anayejinyima ili mwanae apate.Anachukia kushiba wakati mwanaye ananjaa.Anachukia kupendeza wakati mwanaye hana nguo ,anachukia kulala wakati mwanaye analia.Anapenda mtoto apate mara mbili ya apatavyo yeye.Anapenda mwanaye anawili mara mbili ya yeye.Haweki chuki ya kudumu moyoni hata kama mwanaye anaitwa msaliti wa jamii au adui wa watu.Mara nyingi hupambana kurudisha utii na heshima ya mwanae .Asiwe seheme na upande chachu wa maisha.Hutoa msaada kutoka kila idara ya uwezo wake.Amwone huyo mwanae juu.Hususani katika kutimiza ndoto na malengo. Tuliobahatika kusaidiwa na huyu mwanamke wa nguvu sio mimi na wewe tu.bali pia tunao wafuatao.
1.AMBWENE YESAYA(A.Y)

Msanii mkubwa na nguzo kongwe katika sanaa.Ana platform thabiti inayosaidia hata wasanii wenzake kupata nafasi za kushirikiana na wasanii wa nje.Kama alivyomnganisha Diamond na Davido.Lakini ukarimu na mapenzi haya ni kitu kilichofunguliwa baraka na mama yake.Anasema mama ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumpatia fedha kwa ajili ya kurekodi nyimbo ya kwanza.
2.JUMA (JUX)

Hakuna msanii anayevaa vizuri juu ya jux .Utasema koti, tshirt, jeans ,cheni vilidizainiwa maalumu kwa umbile lake.Akiwa masomoni Uchina wanafunzi aliokuwanao walihisi ni mmarekani mweusi.Kitendo kilichomuamsha hisia na kuanzisha bland ya African boy.Kando na mziki,utanashati na ujasiliamali.Jux anaheshimu mchango wa mama yake baada ya kufungua pazia la neema,akimpatia pesa kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo yake ya kwanza.
3.MICHAEL(BELLE 9)

Anathibitisha kuimba ni kipaji anaweza kuandika chochote kikawa wimbo mzuri.Hata kama ni kudai deni,kubembeleza mwenza au habari za kutendwa,Ni mbunifu wa sauti na mteuzi fasaha wa maneno.Huchezea lugha na kutufikia kirahisi masikioni.Akitamka masogange utapenda ilihali huelewi anachomaanisha.Akisema ''nilipe nisepe'' utamlipa deni lake faster.Akitamka sumu ya penzi,utakuwa radhi kuilamba hata kama huna maziwa.Lakini naye kama A.Y naJUX,mama yake ndiye mzazi wa mwanzoni na msaidizi wa karibu kumpatia sapoti ya hali na mali kwenye mziki
4.LIL SAMIL(MR BLUE)
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 watoto wengi Tanzania walishawishika kurap.Na walihisi pengine ni kazi rahisi kama sindano kupenyeza nyuzi za koti.Ushawishi huo ulitokana na umaaru wa kazi nzuri za hip hop zilizovuma enzi hizo.Miongoni mwa hao watoto waliofanikiwa kupenyeza na kumantain hadi leo ni Mr blue.Wengi walifanya lakini sio kama blue.Mimi pia nilitaka kuwa kama blue halikadhalika rafiki zangu hakuna aliyemuweza Anastyle yake ya kuflow akibana maneno kwa mikogo si ya nchi hii.Hasa pale anapotamka kwenye baadhi ya nyimbo''unacheza raga'' na ''basi mororo''.Lakini kiini cha safari hii ndefu ni matokeo ya mama mzazi wa msanii huyu(wenyezi amlaze mahala pema peponi) kwa kumsapoti mwanae toka alipofaulu mtihani wa darasa la saba.
5.NASIB ABDUL (DIAMOND PLUTNUMS)
Mwisho katika list yetu ni Diamond.Ambaye namwona kama balozi wa mziki wa Tanzania kwa namna flani.Kutoka tandale, kutumia jina la Z Anto kariakoo na kufanya official video ya nje na ogopa dj ya kenya.Kutoka kwa Wema Tanzania!,kufika kwa Zari uganda! hadi kwa Coldstar Nigeria.!.Kutoka kwa Mzee Ngurumo Bongo,Papaa Wemba Congo hadi kwaNelson Mandela South Afrika(their soul should rest in peace)Kutoka nchi ya Magufuli,nchi ya Mugabe mpaka nchi ya Trump na Neyo .Lakini kitu ambachohawezi kusahau ni muumba wake na namna ya kipekee kabisa mama mzazi alivyouza kito cha thamani ili yeye afanikiwe kuingia studio.
Tuesday, January 31, 2017
NECTA yatangaza. Wanafunzi 277,283 (asilimia 70.09) waliofanya mtihani 2016 wafaulu,Wavulana wafaulu kwa asilimia 73.26, wasichana 67.06

Shule za Dar zaongoza washika mkia matokeo ya kidato cha Nne.

Shule za Dar zaongoza washika mkia matokeo ya kidato cha Nne.
Tuesday, January 17, 2017
Waswahili
husema ‘siku hazilingani’ ni kweli. Leo ukifurahi, kesho utaduwaa. Na richa ya
juhudi kubwa inayopimwa na jasho zito , majanga hayaishi kutuandama. Wakati
mwingine chozi la uchungu linapita . Jicho linazibwa usione fursa hata moja mbele yako. Na ghafra ukishtuka umeshajikwaa kwenye kisiki cha
umaskini. Hapo utajiuliza maisha yana maana kweli?Na hakutakuwa na jibu.Maana matatizo yanakuwasha kuliko upupu.Shida zinashamili kama magugu.Sikio halisikii habari njema tena.Ukifungulia redio ikutie moyo ,majonzi ndo kwanza
yanakithiri. Matangazo ni ya nafasi za shule
zaidi ya nafasi za ajira, ni ya vyuo zaidi ya mahala pa kazi. Katika juhudi za kuepuka huo mfadhaiko
unageuza jicho mpaka kulia kwako ambako kuna ‘tv’.Ni kipindi cha habari , bila
kuamini mboni zako unajionea viongozi wakitumbuliwa Ili hali mifumo ikiachwa.Hasa elimu. Kabla hujaongeza sauti ya
luninga , simu yako inayokaribia kukata ‘charge’sababu ya shida za umeme ,inaita.Ni ndugu analalamika maisha magumu pesa hakuna..Mkopeshe japo "jero" . Bila mafanikio ya kumweleza jinsi ulivyopigika,simu yake inakata hana voucher.Kufumba na kufumbua,,umeme umekata na simu inazima kumbe hata bila ya voucher kuisha bado mawasiliano yangekata tu.Ukiwa kwenye joto kali baada ya umeme kukata unabakia kutazama sura yako kwenye televisheni iliyozima. Punde mwenyekiti wa wapangaji anakumbusha ni zamu yako kulipa LUKU,mzunguko ushakufikia. Ungali bado katika hali hii ya
sintofahamu baada ya simu kumaliza moto, redio kupoteza matumaini tv
kuzima na sasa kulipa LUKU.Anakuja baba mwenye nyumba kudai chake. Utatamani kusikia maneno ya wasanii hawa.
1.’’Acha
kulia ni shida za dunia ebu tulia’’Jose chamillioni
2.’’Haya
yote ni maisha ipo siku yatakwisha leo mmoja anangaika mambo yamebadilika’’P
funk
3. ’’Kama unapata moja kwa nini
usipate na mia,hiyo inawezekana kwa wote waliona nia’’Prof jay
4.’’usikubali
wakakushinda,Kwani wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini’’Juma nature
5. ’’Wakati wako ndio leo kutimiza
malengo yako nakusihi anza sasa jishughurishe utapata’’Ben Paul.
6.’’Na ugumu
wote wa maisha shida zote za kutaabisha
usikate tama usivunije moyo’’Kara Jeremiah
Monday, January 16, 2017
Kuna milango mitano ya watu kuwa matajiri wakubwa ambayo mabilionea duniani wanatokea:
1. WATAALAMU WANAOLIPWA VIZURI
Kundi la kwanza ni wanataaluma wanaolipwa vizuri (well paid professionals) kama wanasheria wazuri, madaktari bingwa na wahandisi. Wengi waliofanikiwa katika kundi hili wanajua jinsi ya kuweka akiba na kuwekeza akiba zao kwenye maeneo yenye marejesho mazuri. Mabilionea wanaotokea kundi hili ni asilimi 10 tu ya mabilionea wote.

Kundi lingine la mabilionea ni wakurugenzi wanaolipwa vizuri na makampuni makubwa (well paid executives). Hawa ni asilimia 10 ya mabilionea wote pia. Mara nyingi hawa huwa wametoka na kampuni mbali na wamekua nayo wakipandishwa cheo baada ya cheo mpaka kufikia hatua ya juu. Mara nyingi, watu wachache katika kundi hili huwa na uwezo mkubwa wa kuzishikilia fedha zao na kutozifuja na hiyo huwafikisha kwenye ubilionea.
Kundi la tatu ni maafisa mauzo au mameneja wa idara za mauzo. Hawa huwa ni takriban asilimia 5 ya mabilionea wote na kinachowafanya wawe mabilionea ni kwa sababu ya nafasi ya kupata kamisheni kutokana na mauzo wanayoyafanya. Wengi wao huwa ni waajiriwa wa makampuni ambayo wamekuwa wakifanya nayo kazi kwa muda mrefu na kuzifahamu vizuri na baadaye kuja kuwa na milango mingi ya mafanikio.
4. WATU WENYE VIPAJI MAALUM
Kundi la nne ni watu wenye vipaji maalumu kama wanamichezo, wanamuziki, watunzi wa filamu na vitabu na kadhalika. Hawa ni wachache sana 1%, lakini huonekana wengi sana kwa sababu ya kelele zinazoendana na umaarufu wao.

Hili ndiyo kundi kubwa kuliko mengine yote, asilimia 74% ya mabilionea wote ni wajasiriamali. Hii inamaanisha kuwa nafasi ya mtu yeyote kuwa bilionea ni kubwa zaidi kupitia ujasiriamali kuliko kitu kingine chochote.
Sunday, January 1, 2017
Mwaka mpya n kitu kizuri kutokea,hatuna budi kusherekea.Ila lazima tujue tunasherekea nini?.Taasisi za dini zinatufundisha kushukuru kwa kila jambo,ni sawa.Ila tushukuru tukisherekea kwa kiasi.By the way kuna sababu nyingi za kusherekea.Ikiwemo kuwa mzima,kutimiza malengo n.k.Hapa sitaongelea kwa kina habari ya sherehe na kusherekea .Nipo kwa ajili ya kushare mawazo ya watu wengine juu ya mwaka mpya.Na hapa chini wanasema
2. Mwaka huu maombi yako yasikike ndoto zote zitimie,jasho
lote lizae .

3. Mwaka huu jiamini tena na upate kila unachostahili
4. Ingawa hakuna anayeweza kurudi nyuma atengeneze mwanzo
mzuri,sote tuna nafasi ya kuanza sasa na kufanya mwisho mzuri.
5. Mwanzo wa mwaka ni mwanzo wa kufanya kila unachokusudia.
7. Tukubali,tukatae mwaka mpya utaleta changamoto mpya,lakini tupende
,tusipende utakuja na fursa nyingi pia.

8. Ishi chini ya mwenye ndoto na mtendaji,anayeamini na
kutafakari, lakini zaidi ya yote ishi na yule anayeona uweza ndani yako hata
kama wewe hujioni.
9. Haimanishi unatoka wapi cha msingi ni unaelekea wapi
1o. .Kunywa
kiasi,pangilia,tafta marafiki,punguza unene,kuwa chanya na tumia pesa kwa
uangalifu.
Wednesday, December 21, 2016
Toka ulimwengu ugeuke kijiji.Habari husambaa haraka
kuliko moto wa petrol.Hauhitaji nguvu
kufuatilia mitindo,teknolojia,siasa na michezo. Siku izi kila mmoja ni
model,IT,photographer ,kiongozi,na mchambuzi.Kwa sababu taarifa zinapatikana kila mahali.Kuanzia facebook
,Whats apps.Instagram na kwingineko.Ukaribu wa dunia na mitandao ya kijamii ni chachu ya uelevu..Utitiri wa vyanzo vya habari kupitia simu za mikononi laptop na tablets zilizounganishwa na internet ni shina la wasomi na kundi la waelevu tulionao.Kuendena na kasi ya mabadiliko yanayotokea ughaibuni kote inategemea unamiliki kifaa gani? Ukinunua tecno,huwawei,Samsung,iphone au ipad yenye 3G hakika wewe umeukata.Kwani internet ni mama wa habari ,aliyezaa mitandao ya kijamii .Inayokupatia kile unachotaka .Familia hii inakuwa kila siku kwa maana kunazaliwa
mitandao mipya na followers wapya. Je unajua list ya social networks bora 2016?.
1.Facebook2.Youtube
3.Reddit
4.Tweeter

5.Pinterest
6.Instagram
7.Tumblr
8.Linked In

9.Yahoo Answers
10.Yelp
Monday, December 12, 2016
Haya ni mazungumzo ya babu wa kisasa na mjukuu .Mjukuu aliuliza swali kwa babu.''Babu kuishi ni nini?'' Babu akamjibu ''Kuishi ni safari baina ya
pande kuu mbili, upande wa kuzaliwa na upande wa kifo''.Mjukuu kwa mshangao akauliza tena''kuzaliwa na kifo?.Babu kwa hali ya utulivu akajibu,ndio mjukuu wangu.Kila mmoja imemlazimu kuzaliwa na kufa.Kuja na kuondoka.Mjukuu akadakia''kwa hiyo babu,nani anajua nitakufa lini?''Babu akasogeza kiti vyema na kumueleza mjukuu.'' Tofauti na mungu ni wachache wanaoweza kusema utakufa lini.Nao ni watabiri au watu waliopewa nguvu ya kuona hatima ya maisha yako''.''Kwani wewe huwezi?'' Mjukuu akang'ang'aniza huku akimukazia macho babu yake.Babu kwa kutambua tabia ya ung'ang'anizi wa mjukuu,alianza kwa kusema.''Chozi ni kimiminika cha matukio mawili.furaha na huzuni.Mtu analia machozi, huzuni ikimshika. Anaomboleza kwa sababu uwepo wako ulimpa mengi ya
kujifunza .Mfululizo wa uhai wako ni somo linalojiandika kila siku vichwani mwa
watu….Wachache watasahau habari ya kifo chako ndani ya muda mfupi.Lakini wengi watasherekea na wewe muda wa uhai wako. Ukizaliwa wanadamu wanasherekea. Mama ,kaka na ''washikaji'' watakuenzi wakiweka siku maalumu kwa ajili
yako , ‘’birthday’’. Kila mwaka ifikapo tarehe ya siku uliozaliwa ‘maswaiba’
watakuambia ‘’Happy birthday’’ ’’Happy born day’’ na maneno mengi ya lugha
maridhawa.Ili wakonge mtima wako na chozi la furaha likutoke.Kana kwamba hiyo haitoshi.Wataenda mbali
zaidi wakiandika’’Uishi miaka buku( 1000.). Kuna jambo hawatalitambua ,nalo ni mwisho wa maisha yako. Nawe mjukuu wangu utakufa baada tu ya kupita duara nne za kuishi.
DUARA LA KWANZA UTAKUWA NA NGUVU UNA MUDA UNA IDEA HUNA PESA.
Wewe kama inge ukiingia duniani utakuwa na nguvu mikononi na miguuni.Kwa nguvu ulizonazo. Itakuja siku utazunguka huku na huko.Muda mwingi ukijaribu sehemu kubwa ya mawazo yako.Ufanye nini uache nini.Mambo mengi
yanakusibu.Karibu yote yanawezekana.Ila mchawi atakuwa mtaji.Tatizo litakuwa ni
pesa. Kwa mazingira yako hiki kitakuwa kipindi kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 29

DUARA LA PILI UTAKUWA NA NGUVU
UNA PESA UNA IDEA HUNA MUDA
Kama vile simba jike, nguvu zako zitakuwa maradufu mwilini. Ukifanya
shughuri ngumu kushinda hapo mwanzo.Kwa kila kazi ujira utaingia. Akaunti ya
idea itasoma vizuri, utakuwa na utulivu kwenye jambo moja. Kwani muda wa
majaribio ulishapita.Itafika kipindi utaitwa aidha Boss, mwalimu, dokta, mfanyabiashara
n,k.Uwapo njiani kuelekea ofisini au kurudi nyumbani. Utaelewa maana halisi ya bango lililonyuma ya
lori, daladala, hiace, bus au boda boda linalosomeka’’Tatizo ni muda’’Kwa sababu kipindi hiki utakuwa na wingi wa majukumu.Muda wako utakakuwa mfinyu.Utafanya kazi, zaidi ya
kupumzika.Hapo utakuwa una umri wa miaka 30-39

.
DUARA LA TATU UTAKUWA NA KIKOMO CHA NGUVU UNA MUDA UNA PESA HUNA IDEA.
Kuna nyakati zinakuja nguvu ya mwili itafika kikomo.Haitaongezeka
kabisa.Utastafishwa kazi au utafikiria kustaafu mwenyewe.Utendaji wako utakuwa ule wa ‘’one
step at a time’’Kazi nyingi hazitafanyinyika mara moja.Hakuna namna, utakabidhi
vijana. Wenye nguvu zaidi yako.Muda mwingi utazunguka huku na kule.Kuanzia Milima
mirefu ( Kilimanjaro, Evaristi) mbuga za wanyama (Serengeti ,Amazoni ) , majangwani (Dubai,Cairo) hadi fukwe za bahari (Mombasa, Brazil).Wakati unakula jasho na meema ya
ulimwengu.Fedha itakuwa inaongezeka kila kukicha.Na utabaini kuwa una kosa kitu.Nacho ni kimoja tu.idea. una wingi
wa pesa ,una uchache wa idea.Utaanzisha mashindano ya kutafuta idea.Watu kadhaa wataulizwa ''kwa kiwango cha pesa flani unaweza kufanya nini?''.Hapa mjukuu utakuwa una umri kati ya miaka 40-70.


DUARA LA NNE UTAKUWA NA IDEA UNA PESA UNA MUDA HUNA NGUVU.
Baada ya mashindano na matembezi ya huku na kule na kumuona huyu na yule..Jua litazama.Utakuwa ni mchovu.Kwani kichwa kitakuwa na mengi.Utapumzika na kisha kuchuuja idea ulizopata.Utaitwa mshauri wakampuni mwenye busara. Atoae mawazo madogo, yanayotengeneza faida kubwa ya pesa.Watumishi wako wataamini wewe si wa kawaida .Kwa namna unavyotatua shida ngumu na kuleta maslahi kirahisi. .Jina lako litabebwa na heshima uliojenga.Nafasi
yako italeta marafiki wapya.Makanisa, Misikiti ,Shule ,Vyama na taasisi nyingi
zitakupenda. Hautosita kuzisaidia pale unapoweza.Wajukuu na watu watakupenda. Shida ni moja tu,nguvu..Nguvu
itapungua kila mwaka, utakuwa taratibu sana.Hautokuwa mtu wa safari za mara kwa mara.Siku za usoni utashindwa kufanya vidogo ulivyoweza mwanzoni. Hutofunga
tai, viatu, vishikizo wala kuvaa mkanda..Hautoweza kujinywesha maji wala kujilisha chakula.Ukiona hizi dalili mjukuu wangu zinakupata,tambua mwisho wa uhai wako umefika.Hapa utakuwa na umri wa miaka 71 na kuendelea


Monday, July 18, 2016
Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini mara saba katika kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?. Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.
1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain

2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki
3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr
4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''

5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya
tatizo na utatuzi

6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama
katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.


7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo
safi zaidi ya ulivyokuwa hapo mwanzo

8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo
utalisogelea.

9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi
gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.

Friday, July 15, 2016
Tazama hapa.>>>>>>matokeo
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza

4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani

6.Tabora Boys,-Tabora

7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro

9.Ilboru,-Arusha

10.Tandahimba-Mtwara
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza

4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani

6.Tabora Boys,-Tabora

7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro

9.Ilboru,-Arusha

10.Tandahimba-Mtwara
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...





