Monday, December 12, 2016
Haya ni mazungumzo ya babu wa kisasa  na mjukuu .Mjukuu aliuliza swali kwa babu.''Babu kuishi ni nini?'' Babu akamjibu ''Kuishi ni  safari  baina ya  pande kuu mbili, upande wa kuzaliwa na upande wa kifo''.Mjukuu kwa mshangao akauliza tena''kuzaliwa na kifo?.Babu kwa hali ya utulivu akajibu,ndio mjukuu wangu.Kila mmoja imemlazimu kuzaliwa na kufa.Kuja na kuondoka.Mjukuu akadakia''kwa hiyo babu,nani anajua nitakufa lini?''Babu akasogeza kiti vyema na kumueleza mjukuu.'' Tofauti na mungu ni wachache wanaoweza kusema utakufa lini.Nao ni watabiri au watu waliopewa nguvu ya kuona hatima ya maisha yako''.''Kwani wewe huwezi?'' Mjukuu akang'ang'aniza huku akimukazia macho babu yake.Babu kwa kutambua tabia ya ung'ang'anizi wa mjukuu,alianza kwa kusema.''Chozi ni kimiminika cha matukio mawili.furaha na huzuni.Mtu analia machozi, huzuni ikimshika. Anaomboleza  kwa sababu uwepo wako ulimpa mengi ya kujifunza .Mfululizo wa uhai wako ni somo linalojiandika kila siku vichwani mwa watu….Wachache watasahau habari ya kifo chako ndani ya muda mfupi.Lakini wengi watasherekea na wewe muda wa uhai wako. Ukizaliwa wanadamu wanasherekea. Mama ,kaka na ''washikaji''  watakuenzi wakiweka siku maalumu kwa ajili yako , ‘’birthday’’. Kila mwaka ifikapo tarehe ya siku uliozaliwa ‘maswaiba’ watakuambia ‘’Happy birthday’’ ’’Happy born day’’ na maneno mengi ya lugha maridhawa.Ili wakonge mtima wako na chozi la furaha likutoke.Kana kwamba hiyo haitoshi.Wataenda mbali zaidi  wakiandika’’Uishi miaka buku( 1000.). Kuna jambo hawatalitambua ,nalo ni mwisho wa maisha yako. Nawe mjukuu wangu  utakufa baada tu ya kupita duara nne za kuishi.

DUARA LA KWANZA UTAKUWA NA  NGUVU UNA MUDA UNA IDEA HUNA PESA.
Wewe kama inge ukiingia duniani utakuwa na nguvu mikononi  na miguuni.Kwa nguvu ulizonazo. Itakuja siku utazunguka huku na huko.Muda  mwingi ukijaribu sehemu kubwa ya  mawazo yako.Ufanye nini uache nini.Mambo mengi yanakusibu.Karibu yote yanawezekana.Ila mchawi atakuwa mtaji.Tatizo litakuwa ni pesa. Kwa mazingira yako hiki kitakuwa kipindi  kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 29
Image result for no money

DUARA LA PILI UTAKUWA NA NGUVU  UNA PESA UNA IDEA HUNA MUDA
Kama vile simba jike, nguvu zako zitakuwa maradufu mwilini. Ukifanya shughuri ngumu kushinda hapo mwanzo.Kwa kila kazi ujira utaingia. Akaunti ya idea itasoma vizuri, utakuwa na utulivu kwenye jambo moja. Kwani muda wa majaribio ulishapita.Itafika kipindi utaitwa aidha Boss, mwalimu, dokta, mfanyabiashara n,k.Uwapo njiani kuelekea ofisini au kurudi nyumbani. Utaelewa maana halisi ya bango lililonyuma ya lori, daladala, hiace, bus au boda boda linalosomeka’’Tatizo ni muda’’Kwa sababu kipindi hiki utakuwa na wingi wa majukumu.Muda wako utakakuwa mfinyu.Utafanya kazi, zaidi ya kupumzika.Hapo utakuwa una umri wa miaka 30-39
Image result for no time
.
DUARA LA TATU UTAKUWA NA KIKOMO CHA NGUVU UNA MUDA UNA PESA HUNA IDEA.
Kuna nyakati zinakuja nguvu ya mwili itafika kikomo.Haitaongezeka kabisa.Utastafishwa kazi au utafikiria kustaafu mwenyewe.Utendaji wako utakuwa ule wa ‘’one step at a time’’Kazi nyingi hazitafanyinyika mara moja.Hakuna namna, utakabidhi vijana. Wenye nguvu zaidi yako.Muda mwingi utazunguka huku na kule.Kuanzia Milima mirefu ( Kilimanjaro, Evaristi) mbuga za wanyama (Serengeti ,Amazoni ) ,   majangwani  (Dubai,Cairo) hadi fukwe za bahari (Mombasa, Brazil).Wakati unakula jasho na meema ya ulimwengu.Fedha itakuwa inaongezeka kila kukicha.Na utabaini kuwa una kosa kitu.Nacho  ni kimoja tu.idea. una wingi wa pesa ,una  uchache wa idea.Utaanzisha mashindano ya kutafuta idea.Watu kadhaa wataulizwa ''kwa kiwango cha pesa flani unaweza kufanya nini?''.Hapa mjukuu utakuwa una umri kati ya miaka 40-70.

Image result for no idea

DUARA LA NNE UTAKUWA NA IDEA UNA PESA UNA MUDA HUNA NGUVU.

Baada ya mashindano na  matembezi ya huku na kule na kumuona huyu na yule..Jua litazama.Utakuwa ni mchovu.Kwani kichwa kitakuwa na mengi.Utapumzika na kisha kuchuuja idea ulizopata.Utaitwa mshauri wakampuni mwenye busara.   Atoae mawazo madogo, yanayotengeneza faida kubwa ya pesa.Watumishi wako wataamini wewe si wa kawaida  .Kwa namna unavyotatua shida ngumu na kuleta maslahi  kirahisi. .Jina lako litabebwa na heshima uliojenga.Nafasi yako italeta marafiki wapya.Makanisa, Misikiti ,Shule ,Vyama na taasisi nyingi zitakupenda. Hautosita kuzisaidia pale unapoweza.Wajukuu na watu watakupenda. Shida ni moja  tu,nguvu..Nguvu itapungua kila mwaka, utakuwa taratibu sana.Hautokuwa mtu wa safari za mara kwa mara.Siku za usoni utashindwa kufanya vidogo ulivyoweza mwanzoni. Hutofunga tai, viatu, vishikizo wala kuvaa mkanda..Hautoweza kujinywesha maji wala kujilisha chakula.Ukiona hizi dalili mjukuu wangu zinakupata,tambua mwisho wa uhai wako umefika.Hapa utakuwa na umri wa miaka 71 na kuendelea

Image result for tired black old man

0 comments:

Popular Posts