Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Tuesday, January 17, 2017
Waswahili
husema ‘siku hazilingani’ ni kweli. Leo ukifurahi, kesho utaduwaa. Na richa ya
juhudi kubwa inayopimwa na jasho zito , majanga hayaishi kutuandama. Wakati
mwingine chozi la uchungu linapita . Jicho linazibwa usione fursa hata moja mbele yako. Na ghafra ukishtuka umeshajikwaa kwenye kisiki cha
umaskini. Hapo utajiuliza maisha yana maana kweli?Na hakutakuwa na jibu.Maana matatizo yanakuwasha kuliko upupu.Shida zinashamili kama magugu.Sikio halisikii habari njema tena.Ukifungulia redio ikutie moyo ,majonzi ndo kwanza
yanakithiri. Matangazo ni ya nafasi za shule
zaidi ya nafasi za ajira, ni ya vyuo zaidi ya mahala pa kazi. Katika juhudi za kuepuka huo mfadhaiko
unageuza jicho mpaka kulia kwako ambako kuna ‘tv’.Ni kipindi cha habari , bila
kuamini mboni zako unajionea viongozi wakitumbuliwa Ili hali mifumo ikiachwa.Hasa elimu. Kabla hujaongeza sauti ya
luninga , simu yako inayokaribia kukata ‘charge’sababu ya shida za umeme ,inaita.Ni ndugu analalamika maisha magumu pesa hakuna..Mkopeshe japo "jero" . Bila mafanikio ya kumweleza jinsi ulivyopigika,simu yake inakata hana voucher.Kufumba na kufumbua,,umeme umekata na simu inazima kumbe hata bila ya voucher kuisha bado mawasiliano yangekata tu.Ukiwa kwenye joto kali baada ya umeme kukata unabakia kutazama sura yako kwenye televisheni iliyozima. Punde mwenyekiti wa wapangaji anakumbusha ni zamu yako kulipa LUKU,mzunguko ushakufikia. Ungali bado katika hali hii ya
sintofahamu baada ya simu kumaliza moto, redio kupoteza matumaini tv
kuzima na sasa kulipa LUKU.Anakuja baba mwenye nyumba kudai chake. Utatamani kusikia maneno ya wasanii hawa.
1.’’Acha
kulia ni shida za dunia ebu tulia’’Jose chamillioni
2.’’Haya
yote ni maisha ipo siku yatakwisha leo mmoja anangaika mambo yamebadilika’’P
funk
3. ’’Kama unapata moja kwa nini
usipate na mia,hiyo inawezekana kwa wote waliona nia’’Prof jay
4.’’usikubali
wakakushinda,Kwani wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini’’Juma nature
5. ’’Wakati wako ndio leo kutimiza
malengo yako nakusihi anza sasa jishughurishe utapata’’Ben Paul.
6.’’Na ugumu
wote wa maisha shida zote za kutaabisha
usikate tama usivunije moyo’’Kara Jeremiah
Subscribe to:
Post Comments
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...
0 comments:
Post a Comment