Wednesday, January 27, 2016
2.Millard Afrael Ayo.
 Mwandishi wa habari  , aliowahi kupewa tuzo ya mtangazaji bora wa kiume anayependwa(2014), mwaka mmoja mbele, 2015, taaluma ya habari inamfanya atabasamu kwa kufanikisha ufunguzi  wa Kituo binafsi cha redio alichokiita TZA.Ndani ya mwaka huo tabasamu inaendelea kushamiri baada ya Millard Ayo. Com Kutunukiwa tuzo ya Website/blog inayopendwa Tanzania. Katika tuzo za watu zilizofanyika Hyatt Legency, Dar es salaam. Ushindi huo unakuja kwa kuziacha tovuti nyingine  kama; issamichuzi.blogspot.com,  jamii forum. Com,  dj chokamusic. Com. 2015 pia ilistawisha mbegu za tabasamu jingine pale huyu mtu wa nguvu anayesihi watu wakae karibu na speaker za redio,  kuanzisha Application(Millard Ayo app) inayopatikana Google play na play store.App Inayosaidia wapenzi wa Habari anazotoa wasipitwe na chochote kile.  Lakini tujiulize, Millard Afrael Ayo ni mtu wa namna gani?...Huyu ni miongoni mwa Watanzania wabunifu,  anaejua kutumia muda,  wazo, pesa,  na watu  kwa dhamira ya kutimiza ndoto zake. Ndani ya muda wa miaka 11 (toka 2004 alipoanza kazi ya utangazaji had 2015 mwaka wa neema) Millard katoka ngazi ya ufukara mpaka Ile ya maisha bora. Wakati miaka 11 sio muda kidogo kwa hayo mabadiliko makubwa aliofanya. Huo muda umezaa mawazo na mipango yakinifu ikiwemo; kufanya kazi na vituo bora vya matangazo Tanzania (redio one /itv, clouds fm ) .Muda umezaa fikra za kuboresha production, show na matangazo ya hewani yatakayofanyika chini ya Radio yake.TZA. Mpango ambao ni moja ya malengo  matano ya siri, anayosema" muda ukiwa tayari nitaweka wazi "  Kuhusu pesa je?, Ujue sio rahisi kila mtu kutunza sh. mia na hatimae siku moja utimize kiasi cha million moja. Uwezo wa namna hii unapatikana ndani ya kingo za nafsi chache zilizokusudia kweli  . Millard Ayo  anasemaje "kwa malimbikizo ya mshahara amepata nguvu ya kununua vifaa vyote vya TZA. "kununua camera na mic za kisasa zinazotumika na Millard Ayo TV. Matumizi ambayo sio tu yanaimarisha anachokipenda (kazi) bali pia humsogeza karibu na watu. Mpaka mwaka 2015 Millard Ayo ni kipenzi cha watu. Anayeshika namba Tatu (3)Kwa kuwa mtanzania maarufu aliyefikisha idadi  ya followers million moja na zaidi  huko mitandaoni(instagram) . Huku namba moja ikishikwa na Mwanamuziki Abdul Nasib maarufu "Diamond Plutnumz" Namba mbili inakamatwa na aliyekuwa mwandani wake Diamond na miss Tanzania 2007, Wema Abraham Sepetu. Watu ni kiungo kikuu cha mafanikio ya Millard. Bila pongezi, maoni, chuki, upendo na ushirikiano wao, zile ndoto, fedha, muda, na bidii pekee visingemfikisha hapo alipo leo. Kila lakheri millard 
Tuesday, January 12, 2016
5.Samia Suluhu Hassani.
 Mwana mama aliyegawanya miaka  55 katika familia, elimu na siasa. Akiwa anazaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1960, Bi Samia anapata bahati  ya mtende.Kuwa makamu Wa rais na mwanamke wa kwanza kushika wazifa huo. Baada ya miaka 54 ya uhuru wa Tanzania .Hata hivyo nafasi kama hiyo pamoja na vyeo vikubwa anavyovipata mwaka 2015 sio jambo geni kwa Samia. Kwani baada ya kufanya kazi na N.g.os, Shirika la Chakula duniani na ubunge , marais wawili kwa awamu tofauti waliwahi kumteua mara tatu  mwanaharakati huyo kuwa waziri. Mwaka 2000  Rais wa Zanzibar,Amani Karume alimteua Suluhu kuwa waziri wa Leba, jinsia na watoto ikifuatiwa na mwaka 2005 waziri wa utalii. Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete pia alimteua awe waziri wa mambo ya muungano. Ukiwa unataka kujua nini kipo nyuma ya pazia, Bi Suluhu hasiti kwa hilo, anatoa siri kwa maneno yasiozidi manne (4),kwamba amefika hapo kutokana na’’ ueledi na umakini katika kila jambo analolifanya’’.Ni kweli asemacho kwa sababu katikati ya miaka ya 80 (1986)Samia Hasani Suluhu alihitimu elimu ya mambo ya utawala chuoni Mzumbe. Mwishoni mwa hiyo miaka ya 80 (1989) Aliongeza elimu yake katika moja ya chuo huko Pakistan na mwanzoni mwa miaka ya 90(1991)Bi Suluhu alihitimu elimu nyingine ya uongozi Hyderabad, India, na mapema mwaka 1994 alihitimu elimu ya mambo ya uchumi  huko Uingereza katika chuo cha Manchester na katika mwaka Wa neema, 2015, Samia alipata ujuzi mpya wa uchumi na maendeleo ya jamii katika chuo cha kimarekani kinachoitwa Southern New Hampshire. Lakini pamoja na yote hayo Bi Samia ni mke, na mama Wa watoto wanne. Tena anayelea na kupenda familia yake vizuri.Kwa historia hii bi Samia ni miongoni mwa wanawake maarufu na wenye ushawishi nchini.Kama  Asha Rose Migiro, Janeth Magufuli, Anna Mwighwira, Salima Kikwete nikitaja kwa uchache .

4.Mbwana Ally Samatta.
 Wazungu wana msemo usemao "umri ni namba" . Kwa maana idadi ya Miaka tuliyonayo sio kikwazo cha kutokuwa watu tunaojikusudia kuwa. Hakika unaweza fanya chochote katika umri wowote. Haya ndio maelezo yanayomvisha kilemba  bwana Samata. Mchezaji aliyezliwa 1992 na mwaka 2015 kugeuka dhahabu  pale alipo pewa tuzo ya ufungaji bora wa ligi za mabingwa afrika. Ikifuatiwa na kuwania tuzo ya mchezaji bora Wa afrika anayecheza ligi za ndani. Ni mswahili wa kwanza kuleta mchango kwa timu akiiwezesha  timu yake kutwaa kombe la mabingwa wa afrika 2015 . Pengine unajiuliza Samata ni nani?. Huyu ni mtanzania mwenye umri wa miaka 23 anayechezea timu ya mpira Wa miguu nchini Kongo inayoitwaTP Mazembe . Mnamo mwaka 2011 Samata aliuzwa kwa dau nono la dola za kimarekani mil 100(shilingi  mil 150 za kipind kile )na  Simba Sport Club.Huku yeye akipewa sh. Mil 50. Mpk mwaka wa neema, 2015, Mbwana Samatta tayari anamiliki pesa, mali, majumba matano na magari ya kifahali  manee;Range Rover yenye thamani ya mil 80 na Chrysler crossfire ya mil 50. Tukisahau habari ya utajiri , Samata anamudu vyema nafasi ya ushambuliaji akiwa uwanjani . Kwa mwaka 2015 tu ameifungia tp mazembe goli saba, kitu kilichomfanya awindwe na ligi za ulaya kw tiketi ya timu za ubelgiji .Kwa nafasi hiyo Samata ataingia kwenye orodha ya watanzania wachache waliowahi kuchezea ligi za nje ya bara la Afrika.Tukikumbuka kuwa wachezaji wengine waliofikia hiyo hatua ni pamoja na Haruna Moshi "Bobani", Athuman Machupa waliokuwa Sweden, Renatus .Njohole, Uswizi, Mwinyi Kazimoto, Qatar .Henry Joseph, Norway na Danny Mrwanda aliyekuwa Vietnam.Tunakutakia mafanikio mema Samata.

 3..Amri Athuman 'King majuto'.
 
Kama sio kipofu utakubali mwaka 2015 ulikuwa mzuri kwa gwiji wa vimbwanga nchini, mzee king majuto. Kwani tumeshuhudia siku moja baada ya kuachia filamu mpya ya Shikamoo Mzee . Tenda za pesa zilimfuata mzee wa watu. Akifanya matangazo ya bidhaa tofauti tofauti zaid ya muigizaji mwingine.  Hivyo kutawala sura za magazeti, vipindi vya TV na redio . Ni miaka miwili imepita (2013-2015) tangu Majuto atangazwe kama muigizaji aliyelipwa vizuri na kampun ya steps production. Akipokea kiasi cha sh. Mil 20 kwa mwezi, kwenye mahojiano aliofanya na kipindi cha Amplifya kinachorushwa na Miradi Ayo.  Habari inayoashiria kuwa, huenda na mwaka 2015, Majuto akawa mbele kwa kupiga mpunga mnono. Kwa sababu muigizaji huyo wa comedy kanyakua tuzo ya mchekeshaji bora Wa mwaka , pale viwanja vya Nyerere Dar es salaam.Akiwabwaga akina Jangala,  Salma Jabu"Nisha" ambao  ni wachekeshaji wazuri nchini. Ni zaidi ya miaka 50  tangu Majuto aanze kufanya kazi za uchekeshaji . Anasema "Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 tokanimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu"Miongoni mwa filamu zilizomuweka sokoni ni Daladala, Mtu mzima ovyo, Naenda kwa Mwanangu, Back from New York na Shikamoo Mzee. Mbali na yote mvunja mbavu huyu ni baba Wa familia ya watoto tisa na  amefanikiwa kujenga nyumba tatu, kuanzisha shamba kubwa la kilimo .kusomesha wanae, kwenda Makka na kununua magari matano. Kwa maendeleo haya ,mzee ni changamoto kubwa kwa wachekeshaji wanao chipukia na wale wakongwe kama Onyango, Mzee Jangala, Senga , Pembe, Brother K, Nisha na wengine. 
Monday, January 4, 2016

Huku mwaka 2015 unamalizika.Shangwe za kukaribisha mwaka mwingine zinamiminika.Wengi  tukiwa ni washangiliaji ,tunasahau kuuliza swali alililojiuliza,rais wetu katika sherehe za uhuru,kwa nini tunasherekea?.Kutoka kwenye swali tutanweza kupata jibu kwa kutumia watu wachache kwa namna moja ama nyingine wanastahili kusherekea .Wale ambao neema iliwangukia ,walichosema kilitimia,walichofanya kilifanikiwa hata mengi waliokusudia yalionekana.Kitu kibaya kuhusu idada ya watu hawa ni kuwa japo wengi walifanikiwa tutatazama  wachache tu wasiopungua 10.Lakini Jambo zuri ,hawa sio wageni ni wale tuliozoea kuwaona kwenye michezo, dini, burudani, siasa, biashara, elimu, filamu na  sekta nyinginezo. Athari za hawa wachachehazi kuvuma kwenye tv, redio, magazeti, internet tu. Bali hata wewe walikuhusu kiganjani mwako pale ulipounga bundle ili usipitwe na habari zao.Maisha yao,mafanikio yao  na harakati zao.Unataka kuwafahamukwa undani ?, tazama mfululizo ujao.

10.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.
Ni mmoja wa watu waliopewa majina mengi mwaka 2015.Tingatinga,mzee wa msimamo,mchapa kazi,jembe n.k. Majina yote yalifutia ubora wake katika wizara  alizokwisha shika ikiwemo ya ujenzi,uvuvi,ardhi. kisha kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Jasho likamvuja kwani hakuwa peke ake katika kinyang’anyiro ni watu makumi walichuana.Hatimaye katika chama chake akatoka yeye .Hali iliomkutanisha na wapinzani wapya toka vyama vingine.Hapakuwa na njia fupi ya maisha kwa Bwana Magufuli.Zaidi ya kutia mafuta kwenye gari,weka funguo na kuzunguka nchi nzima kuwakumbusha watanzania kwa nini  yeye anafaa kuchukua ridhaa ya kuwaongoza.Mnamo Octoba 25,2015 alipaki gari na kungoja wananchi wafanye yao. Tahere 5 November 2015 mizunguko na hapa kazi tu zikazaa matunda akahapishwa kama rais wa awamu ya tano ya jumhuri wa mungano wa Tanzania.

9.Edward Lowassa.
Mwaka umekuwa wa neema kwa kile kinachosemekana kama kavunja record ya ushawishi kwa umma.Dhidi yamtazamo wao juu ya vyama pinzani, awali vyama pinzani havikuwa na nguvu kubwa kama alioleta  bwana huyu.Kwa mara ya kwanza kanda ya ziwa walipiga deki rami .Kaskazini walichora ngozi rangi ya chama chake,magharibi walipunga mikono hewani kama feni,kusini walifurika viwanjani haijawahi tokea.Vitendo hivi vilifuatia ishara ya mabadiliko na  kutokata tamaa.Alioioonyesha mgombea huyu.Kwani baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kusaka wagaombea katika chama tawala.Alisimama wima katika chama pinzani na hivyo akafanikiwa kuimarisha ngombe ya upinzani  kuliko ilivyowahi kuwa hapo mwanzo.Kwa kuongezaa idadi ya wabunge kutoka upinzani na kufungua pazia jipya la ushindani wa kisiasa.Jina lake halitosahaulika katika historia za  hili taifa.

8.Diamond Platnums
Kama mafanikio yangekuwa yanapimwa na wingi wa majina.Diamond Plutnums  angekuwa trionea.Ukiachilia mbali jina la Naseeb  Abdul anajiita Chibwa, Dangote,rais wa wasafi,Mr ngololo,baba tifa,na sasa anajifananisha na mfalme wa chi kavu katika wanyama kwa kujiita ‘simba’.Yote tisa kumi huyu kijana kagusa mafanikio ya maana 2015.Baada ya kuingia  mgogoro wa  mashabiki (  team diamond vs team  kiba )Kijana wa majina mengi alipata muda mgumu kama sio uchungu wa mafanikiao.hali iliyomfanya atuache tumeshika vichwa kwa mshangao alipofanya kazi na wasanii wakubwa akiwemo,Neyo,Usher,A.K.A,Mafikizolo,Mr fleva.Wengi wao wakiwa ni wa afrika magharibi  afrika ya kusini na Marekani. Mwaka ukapendeza zaidi alivyotwaa tuzo ya Best Africa Act, BestWorld wide act,Best collaboration,Video bora ya mwaka n.k.Huku hizi tuzo zikiwa ni za ndani ya Tanzania,ndani ya afrika na Nje ya afrika.Dangote ama simba kama anavyojiita kakunja mkeka kwa kufungua studio inayosimamia kazi za wasanii wengine .Akiwemo Hermonize anaetamba na kibao cha Aiyola.Kama haitoshi ndani ya mwaka huo huo alipata binti yake wa kwanza waliomuita TIFA.

7.Alikiba
Huku akiwa ni baba wa watoto watatu; wa kike wawili na wa kiume mmoja.Alikiba amevuna zaidi ya alichokipanda mwaka 2015.Kufuatia kibao kimoja kuleta tuzo tano .Ambazo ni za ubora  katika uimbaji,utumbuizaji na utungaji. Sio jambo la kitoto eti.Baada ya kuachia single ya Mwana.Kiba alizimisha kelele zote redioni na ile iliyobaki ni mwana dar es salaam.Kumaanisha ilistahili kuwa nyimbo bora ya mwaka  graduation za vijijini hadi mijini,zilitumia ‘mwana’ kama nyimbo kuu katika sherehe zao.Ni kazi hii ilipelekea kuzuka  kwa ugomvi wa team mtandaoni .Baadhi ya watu waliamini king kiba yupo juu zaidi ya Diamond na wengine hawakuamini hiyvo.Unajua nini kilichofuata?Hii nyimbo bora ya afro pop ilimfanya Ali kiba aachie kibao kingine matata alichokiita ‘cheketua’ ndani ya masaa 10 tu kilipata zaidi  ya viewers 42,000 youtube.Jambo ambalo halijawahi kutokea.Mbali na hayo bidii yake imemuweka mjini kwa kupata show nyingi akizipiga kwa mfumo wa live band na kawaida  kisha  akanehemeka tena alivyoungana  na nguli wenzake wa muziki(NEYO) kwenye kipindi cha coke studio.

6.MOHAMMED  DEWJI

Sio mgeni  kwa wapenzi wa kandanda na wafanyabiashara ,kufanya ujasiliamali kumemleta mlangoni mwa familia zetu.Mwaka  2015 Ulikuwa wa fanaka, baada ya kuwa tajiri wa 1500 duniani.akaingia  miongoni mwa matajiri 30 Africa  na wa kwanza  Tanzania .Akimtangulia milionea Rostam Aziz,Said Salim Bakheresa, Murji na Mengi.Mo ni kijana kwa muonekano lakini mzee kwa busara .Anauza, anazalisha na kusambaza bidhaa na huduma zake.Huduma na bidhaa kama vile unga,mafuta,pembejeo na usafirishaji ni mwanya unaomfanya kijana huyu awe bilionea namba moja nchini anayefuatiwa na Rostam.Kujihusisha na kilimo,fedha,mawasiliano pamoja na usimamizi mzuri wa kampuni yao inayoitwa METL.Ilikuwa juhudi nzuri baada ya jarida la masuala ya biashara na ujasiliamali,Forbes.kumtunuku mtanzania huyu heshima ya mtu wa mwaka’’person of the year’’

Nikiwa mwanza mwaka 2004 nilikuwa mwanafunzi aliyependa somo la historia. Moja ya mada niliyopenda ni colonialism. Mada ilinifunza , miongoni mwa athari walioleta wakoloni ni kurudisha nyuma maendeleo ya  Tanzania. Huku maeneo ya kusini mwa nchi yakitajwa kuwa duni  zaidi ya kwingine. Nikasoma pia Mtwara na lindi ni mfano wa maeneo hayo. Lakini cha ajabu mwaka 2011 nikiwa mwaka wa kwanza katika chuo kimoja cha hapa mtwara niliona mambo ni tofauti  .Mtwara ya kipindi hiki inapiga hatua kuliko picha niliojengewa na ile mada. Kuna ulinzi wa mali na usalama wa afya. Kuna shule, vyuo na taasisi za elimu. Kuna viwanja vya michezo, vikundi vya sanaa na mahala pa burudani.Kuna viwanja vya ndege,bandari na stand za bus. Kufikia mwaka 2014, niliona Viwanda vya cement, vyombo vya habari, na rasli mali za mafuta na gesi,  huku fukwe za mtwara mjini zikiwa na hotel nzuri na maandhari safi. Nakumbuka katika kufurahia  mazingira haya nilikuwa napiga zoezi kila alfajiri. Kisa kilichopelekea nipoteze simu.Pale uchovu uliponifanya nisahau hicho chombo cha mawasiliano juu ya canteen ya chuo. Mungu ni mkubwa simu ilipatikana  siku kumi baadae.(Niliipata vipi hiyo ni stori ya siku nyingine) na mwishoni mwa mwaka 2015 nikirudi chuoni  kwa ajili ya kumsapoti mdogo wangu aliehitimu chuo .Nilipata bahati  kutembelea fukwe tofauti tofauti. Msanga mkuu, Veta, makonde, bandari ya zamani . Ambapo sikusita kuogelea baharini ,  wakati nafanya hivyo mwenzangu ambaye ni mgeni hapa aliniuliza, ’’ni mambo gani ya kuzingatia katika fukwe za mtwara?’’ Nikiwa majini nilianza kwa kumwambia . ’’Yapo mengi ya kuzingatia ila nitaanza na haya’
1.URUMBA (wadudu). Ukiwa unaogelea kuwa makini na wadudu walio na miiba iliyowazunguka mwili mzima. Wakiwa katika rangi nyeusi na sura ya duara mara nyingi wadudu hawa hujisogeza karibu na miamba . Na kwa kuwa miiba yake ni nchi moja na zaidi na upana wa sindano ya mkono , ukimkanyaga mmoja mwiba unavunjikia mwilini mwako. Idadi ya miiba iliyokuingia inasababisha  mwasho mkali, maumivu na baadae homa. Wenyeji wa pwani wanashauri ukipatwa na tatizo hili(urumba) , mapema chukua  mafuta ya taa tia mahala miiba imeikuingia. Baada ya siku mbili mpaka tatu utapona
.

2.ASKARI. Uwapo katika fukwe za shangani, kama makonde na veta askari wa dolia ni wengi. Hivi vikosi haviruhusu raia abaki maeneo haya muda wote. Ikifika saa 12 :30 jioni , watu hufukuzwa.  Saa 1 giza likiwa kubwa  askari polisi hukamata watu . Raia hufikishwa kituoni. Wakipewa adhabu ya kutotii sheria za fukwe.

3.MV MAFANIKIO. Ni feli inayobeba magari ,mizigo na  watu wanaotoka na kuelekea msanga mkuu.Baada ya fukwe za veta na makonde kuwa na mashabiki wengi. Fukwe za kivuko cha Msanga mkuu ndio imekuwa habari ya mjini miongoni mwa watu. Hakuna namna ya kuenjoy pwani hii kama hujui utaratibu wa Mv mafanikio. Huanza asubu sana kukamilisha safari yake. Muda wa mwisho ni jioni  saa 12. Kabla ya kuondoka hupiga honii. Ukifika chomboni mkononi uwe na ticket . Kuna nauli ya mtu, gari na mizigo mikubwa. Mpaka mwaka 2014 disemba nauli ya mtu mzima ilikuwa ni sh. 300.
4.KUPWAA NA KUJAA. Raha ya fukwe ipo machoni mwa mtazamaji. Hivyo ni msingi kutambua wewe unapenda msimu wa bahari ikiwa ina maji  au ikiwa haina. Kuna nyakati bahari hupwaa, hapa ni muda maji yapo mbali sana na fukwe. Ukitazama utaona maadhari kama ya jangwa, miamba vigumu kupata maji ya shingo wala ugoko. Na wakati imejaa huwa ni wiki  nzuri kwa waogeleaji. Ukitokea pwani utaona fukwe zinatenganishwa na mawimbi ya amaji. Ukiyafuata yatakuanzia kweye ugoko ,kiuno , shingo mpaka mwili mzima utabebwa .
5.SIKU KUU. Ni siku njema kwa mambo mengi zikiwemo fukwe. Wakati wa chrismas, mwaka  mpya, Idd n.k Fukwe za mtwara hufurika watu zaidi ya mchanga. Siku kuu wanavyuo, watoto wa mjini, raia wa kawaida kutoka kona zote za mtwara hujumuika hapa. Hizi siku mhimu huambatana na matukio mhimu kama upigaji picha , biashara za vyakula na vinywaji. Huku mziki , nyama choma na burudani  zikiwa pale fukwe ya makonde.
6.USAFIRI. Ni mhimu kujua utatokaje eneo moja hadi jingine. Kama ilivyo lazima kujua utafikaje ufukweni endapo upo nyumbani. sio vigumu , kama wewe unaishi mtwara au ni mgeni nabado haumiliki chombo cha usafiri. Kwanza kuna usafiri wa aina nne. Taxi,Bajaj,Bodaboda na baiskel. Pili kila usafiri una gharama yake. Wakati taxi au gari za kukodi zikiongoza kwa gharama, bajaji na boda boda(pikipiki) huwa ni nafuu ikitegemea na idadi yenu. Ukiwa ni mtu wa mzoezi baiskel zipo unachotakiwa ni kukodi na kueleza unachukua kwa masaa mangapi. Mwisho kabisa kwa wewe unaeishi mbali na hizi fukwe ni mhimu kutambua kuwa usafiri unapatikana.



Popular Posts