Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Monday, July 18, 2016
Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini mara saba katika kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?. Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.
1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain

2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki
3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr
4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''

5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya
tatizo na utatuzi

6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama
katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.


7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo
safi zaidi ya ulivyokuwa hapo mwanzo

8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo
utalisogelea.

9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi
gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.

Friday, July 15, 2016
Tazama hapa.>>>>>>matokeo
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza

4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani

6.Tabora Boys,-Tabora

7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro

9.Ilboru,-Arusha

10.Tandahimba-Mtwara
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza

4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani

6.Tabora Boys,-Tabora

7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro

9.Ilboru,-Arusha

10.Tandahimba-Mtwara
Sunday, July 10, 2016
Mambo!. Kila kukicha kinazaliwa kipaji kipya Tanzania.Na kila ,mwaka kunazaliwa studio mpya mtaani.Tangu sanaa ya mziki igeuke ajira.Vijana wa kibongo wameikimbilia fursa.Hakuna anayetaka kubakia shabiki kama mimi au wewe.Vijana wanataka kuwa wasanii na maproduza. Wanatamani kulingana au kumzidi Diamond na Alikiba,Nahreel na Lamar.Ni kitu kizuri kuwa na mtazamo wa mafanikio.Lakini ni kitu kibaya kutoweka daraja thabiti la kufikia hiyo ndoto au hayo mafanikio..Sitaki uchoke ndg ila nakumbusha tu kuwa,huwezi kuitwa msanii au kufanya sanaa ,Kama hauna mbinu na akili ya ziada. Bilashaka unatambua kuwa hata mvuvi hawezi kuvua samaki iwe sangara au pweza, bila ujuzi. Mfano Mvua sangara anaamini hawezi kupata sangara kwa kutumia chakula asichokipenda sangara .Halikadhalika mvuvi wa pweza anatambua hatoweza kumpata pweza bila kuiingia kwenye maji yanayopendwa na pweza. Wembe ni ule ule mmoja hata kwa wewe unaetaka kufanya mziki hapa nchini, bila kujali ni Hiphop, taarabu, kwaito zuku, bolingo, segere, singeli, baikoko n.k. Huwezi kujizolea wafuasi bila kujua wanachopendelea .Bila kujua tabia ya mziki.Na kuonekana mjuzi kama yule mvuvi anayejua samaki anahitaji nini ,inachukua mbinu na akili ya ziada kama nilivyotangulia kusema,Gharama na nguvu pia .Kati ya mbinu nyingi ambazo unazijua,umezisikia .Kuna chache nakukumbushia ambazo kwa namna moja ama nyingine naamini zitakusogeza mahala katika jitihada na harakari za kuwa msanii nyota wa mziki Tanzania.
1.Uandishi .Joh Makin anasema''Uandishi wa nyimbo ni feeling na feeling ni kama mtu anavyopata mtoto yaani kuna uumbaji''Lady Jay Dee anaelezea zaidi kwa kusema''mara nyingi nyimbo mimi ninazoandika huwa ni vitu vya ukweli ambavyo aidha ni kwangu au kwa jamii''
.

2.Collabo(kushirikiana). Msanii Alikiba anasema''Unaweza kufanya nyimbo na mastaa isiwe nzuri,Staa kwa staa.Unaweza kufanya na underground(chipukizi) na ikawa nzuri.Sometimes feeling zina kuwa tofauti tunaamka tofauti''

3,Manager: A.Y anaelezea kuwa''Kuna vigezo vya kunimeneji mimi cha kwanza ufanye kazi atleast mara tatu ya mimi ninavyofanya kazi, kingine ni lazima huyo manager aje na networking(mtandao)wake''.Na kuhusu wasanii chipukizi anaongezea'' mtu hana single au anayo moja hajapata nafasi ya kutengeneza atleat hit song(nyimbo nzuri pendwa) nne kujipima na wasanii wengine,hapo hapo anataka manager,huwezi kuwa na manager wakati hujaijua biashara yako hata kwa kiasi fulani''


4.Promo(utanbulisho na matangazo ya wimbo):Ommy Dimpozi anashauri''Kwenye huu mziki kuna aina ya promo inaweza kufanya mziki usikae sana,inakuwa kama unavumisha kitu vuu kweli kina kuja na ule upepo alafu ukipotea upepo na nyimbo inapotea na watu wanataka tena nyimbo mpya.Kwa hiyo kuna zile aina za promo za vurugu zinaweza sababisha nyimbo zisikae''


5.Kujiamini.Jaji maarufu wa kipindi cha kusaka vipaji vipya,Bongo star search bwana master Jay anasema''.Msanii anatakiwa kuwa mtu ambaye anajiamini kupita kiasi,hutaki kuwekeza hela yako kwa mtu ambaye ana kipaji lakini hajiamini.Mtu mwenye kipaji nusu na kujiamini mia anaweza kufanya vizuri kuliko mwenye kipaji mia na kujiamini nusu''


,
6.Fanya research(tafiti) Profesa jay anasema''Ukitaka kufanya mziki mzuri lazima ufanye mziki wa watu,sio ufanye mziki wangu(mtu binafsi),so lazima ufanye research watu wanahitaji nini na kwa muda gani,lazima uangalie jamii yako inayokuzunguka,ambayo unataka kuiimbia ipo katika situation(hali) gani ,kama wanataka bata(anasa,furaha) waimbie nyimbo za bata,kama wapo kwenye stuation ngumu waimbie nyimbo za kuwapa moyo''

7.Mafanikio: Mambo makubwa yote wanayomiliki wanamziki hayatokani na mziki pekee.Mwana Fa anasema''Nilichogundua ni kwamba wasanii wote matajiri,hawafanyanyi mziki pekee hawawi matajiri kwa sababu yamziki.Mifano yote hai tunayo''
8.Hitimisho;Msanii Chemical anasema''Sanaa ni kuchukua kile ulichonacho ukijumlisha na vya watu wengine vingi''


Saturday, June 25, 2016
Wakati wengine wakisema ujuzi ni aina ya kazi au shughuri yenye kufanyika vizuri baada ya elimu au mafunzo maalumu.Wahenga wanasema ujuzi hauzeeki.Kwa maana ni uwezo unaopatikana kwa mtu hasa akiwa amepita hatua ya kupokea maelekezo, na kufanya matendo mengi.Dhana ya ujuzi imekuwa ya kikazi au ki uwezo kulingana na mfumo anaoaksi mtu..Ukiwa ni mtumishi wa ofisi rasmi ujuzi wako itakuwa ni utoaji wa huduma inayokubalika hapo kazini kwako.Na endapo umejiajiri au kuajiriwa sekta zisizo rasmi ,ujuzi ni ule uwezo wa kutoa matokeo mazuri ya chochote chema unachofanya.Kwa muda mwingi njozi kubwa na fikira pana zimekuwa kama baba na mama wa ujuzi katika mazingira yetu.Kujua zaidi kuhusu hilo fuatilia haya maneno 10
1.Kama mmea ustawivyo kwa mbolea na sio jua kali ndivyo Ujuzi umtajirishavyo mtu na sio maneno matupu
2.Ni vyema kila mmoja akawa na kila ujuzi na asiutumie,kuliko kutokuwa na huo ujuzi na ukataka uutumie

3.Kuna sheria za kufuata ili ubahatike,na kila jambo haliundi bahati,kwa waelevu wanatambua ujuzi ni njia mathubuti ya kuwa mtu mwenye bahati
4.Kumpatia mwanao ujuzi ni bora kuliko kumpatia vipande elfumoja vya madini ya dhahabu
5.Elimu huja kwa kujifunza ila ujuzi huja kwa uzoefu.
6.Elimu pekee sio ujuzi, bali ikizidishwa mara elfukumi ndio itakuwa ujuzi
7.Marudio ni mama wa ujuzi
8.Ujuzi ni mshikamano wa uzoefu,akili na upenzi wa jambo vikiwa pamoja

9.Ujuzi na kujiamini ni jeshi lisilopigwa wala kushindwa
10.Kama huna ujuzi ipo siku inakuja kipaji chako kitakwama,kwani ujuzi ni dhana ya matendo,bidii na shauku ya kutaka uwe bora kila kukicha,
Friday, June 17, 2016
Vitu vingine vinashangaza aisee! Jana unakula visheti vya mama HasaniTandale gengeni.Leo unapata dina ya chief cooker wa hotel ya nyota tano ufaransa!.Kweli mchawi wa giza ni mwanga na adhabu ya umasikini ni utajiri.Kumbe kila mtu ni mwandishi wa sheria za maisha yake!!.Ni uchaguzi binafsi aidha katiba yako itambulike kwa rasmu za umaskini au za utajiri.Nikiangalia mbali naona kijana anayeomba nafasi majukwaani.Namuona anasimama stejini akiwa na uwoga,hawezi kushika mic.Ni kwa sababu ni mara ya kwanza kufanya jambo hili.Na sasa nikivuta pumzi na kupepesa macho kwa suprise!!.Namwona kijana yule yule akiwa na nguvu mikononi.Hata mic haitetemeki ni vile inajua imekamatwa na gwiji.Gwiji anasimama na mic akiihamisha kutoka mkono mmoja hadi mwingine,Akikituna nayo jukwa la mkoa mmoja hadi mwingine.Na baada ya kukodoa macho vizuri namwona gwiji yule akiwa na magwiji wa kimataifa.Wanaotoka mashariki na maghribi mwa Afrika.Magharibi na mashariki mwa dunia.Gwiji anatokea kupendwa .Anapata wapenzi ambao miongoni mwao wanamzalia mtoto.Vyombo vya habari na mitandao inamfuatilia kila hatua anayopitia.Kila kazi anayofanya.Kila safari anayokwenda. Hadi ile ya ufaransa kwa chief cooker wa hotel ya nyota tano.Mhhhhh .Kwa vile kila mmoja amegeuzia mjadala kwa gwiji huyu inanilazimu nimjue jina lake.Kumbe anaitwa Diamond Plutnums.ha ha haa.Nimechoka kbs,Wakati nikidhani namtambua vya kutosha nashangazwa na kelele za sentensi 8 nyingine ambazo hata wewe pengine huzijui kuhusu huyu Diamond Plutnnums.

2.KUJITOLEA:Anapenda kutenda wema kwa watu .Yupo tayari yeye
akose madensa wake wapate.Katika kipindi
cha EFM Radio,kinachoitwa uhondo dancer wa Diamondi Mose Iyobo alisikika akisema
haya.’’Kuna vitu vingine (Diamond platinum)anafanya kwa kujitolea lakini kwetu
sisi inabidi atulipe’’

3.MAHUSIANO:Hana tabia ya kuchunguza simu ya mpenzi wake.Katika kipindi na Millard Ayo TV Diamond alifunguka’’Nakumbuka nilishashikaga simu ya demu wangu zamani ikanicost tangia hapo nikakoma kushika simu za mwanamke na mpaka leo siwezi kushika hata kama inaita.’’

4.CHAKULA:Hapendelei vyakula vya kwenye ndege.Akiwa
nchini ni mdau wa wali maini ndizi
mbivu.Uingereza ugali nyama ya kukaanga.Nigeria egusi ,fufu,South
Africa chicken tikker ,pizza
5.IMANI:Upande wa kuamini Platnums anamtanguliza Mungu mbele‘’Katika
maisha ukimwomba mwenyezi mungu na
ukaweka nia thabiti na ukijutuma vinawezekana’’anasema

6.MAFANIKIO:Yeye katika swala la kupata, anaheshimu vilivyo kuwekeza katika muda,. Diamond anasema‘’Kwenye mafanikio unapata muda mfupi sana wa
kupumzika’’

7.MITANDAO:Anakubali jinsi unavyotumia social networks vyema ndivyo unavyonufaika . .Na hapa anasema ''Ukitumia mitandao
kwa njia nzuri unaweza kufika mbali.
8.KAZI:Katika ufanyaji wa shughuri mbalimbali daimondi anadira
kuu moja,kazi inapaswa iwe na kiwango ama ubora wa kutosha kwani hii ni sababu ya wewe kutambulika.Katka sentence ya maneno nane amesema ''Ubora wa kazi yako ndio unakufanya uwe staa’’

Friday, June 10, 2016
Kati ya movie za kuvutia na zilizonibadilisha fikra, ni hii movie maarufu ya JUMONG.
Movie hii maarufu wengi waliiangalia na kufurahia mapigano ila mimi nilifanikiwa kujifunza yafuatayo na yakanibadili:
1. 👨🏻Baba yake na Jumong, Haemosu, alikuwa na Kusudi la kutimiza lakini hakufanikiwa kulitimiza.
Funzo: Wazazi wetu wengi hawajatimiza malengo na kusudi zao maishani, hivyo tusiogope, tuamue tu kutimiza kusudi zetu.
Funzo: Wazazi wetu wengi hawajatimiza malengo na kusudi zao maishani, hivyo tusiogope, tuamue tu kutimiza kusudi zetu.
2. 👨🏻Jumong hakulifahamu kusudi lake hadi pale alipokutana na misukosuko kutoka katika familia yake.
Funzo: Misukosuko ina nafasi kubwa kutubadili chanya.

3. 👨🏻Kipaji cha Jumong cha kupiga mishale na kuongoza kilimsaidia kufikia kusudi lake kubwa la kuanzisha taifa kubwa.
Funzo: Kipaji ulichonacho kina nafasi kubwa kukufanikisha maishani ukikijua na kukitumia.
Funzo: Kipaji ulichonacho kina nafasi kubwa kukufanikisha maishani ukikijua na kukitumia.

4. 👨🏻Jumong alifanikiwa kwa kujenga timu ya marafiki 👫👬wachache na kuwafanya wawe hodari na waaminifu kwake na kutambua kusudi kubwa alilonalo.
FUNZO: Chagua vizuri aina ya marafiki wa kuwa nao na kutokuwa nao. Hawa wana nafasi kubwa ya kukufanya ufanikiwe au usifanikiwe maishani.

5. 👨🏻Jumong alikuwa ana mtazamo chanya katika kila jambo.
Funzo: Hata jambo liwe gumu vipi, bado kuna tumaini na unaweza kufanikiwa.
6. 👨🏻Jumong alijifunza wapi wazazi wake walikosea na akaamua kupatia
Funzo: Jifunze kwa waliokutangulia kwani huwezi kuishi miaka ya kutosha na hadi kugundua makosa yote duniani.
7. 🤔Pamoja na misukosuko mbalimbali aliyoipata Jumong, bado aliweza kufikia Kusudi lake kwa kuwa tu alikuwa na udhubutu na uamuzi sahihi kufuata ndoto yake.
Funzo: Fuata ndoto yako, jiamini na utafanikiwa sana.
Funzo: Fuata ndoto yako, jiamini na utafanikiwa sana.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...




