Friday, June 17, 2016
Vitu vingine vinashangaza aisee! Jana unakula visheti vya mama HasaniTandale gengeni.Leo unapata dina ya chief cooker wa hotel ya nyota tano ufaransa!.Kweli mchawi wa giza ni mwanga na adhabu ya umasikini ni utajiri.Kumbe kila mtu ni mwandishi wa sheria za maisha yake!!.Ni uchaguzi binafsi aidha katiba yako itambulike kwa rasmu za umaskini au za utajiri.Nikiangalia mbali naona kijana anayeomba nafasi majukwaani.Namuona anasimama stejini akiwa na uwoga,hawezi kushika  mic.Ni kwa sababu ni mara ya kwanza kufanya  jambo hili.Na sasa nikivuta pumzi na kupepesa macho kwa suprise!!.Namwona kijana yule yule akiwa na nguvu mikononi.Hata mic haitetemeki ni vile inajua imekamatwa na gwiji.Gwiji anasimama na mic akiihamisha kutoka mkono mmoja hadi mwingine,Akikituna nayo jukwa la mkoa mmoja hadi mwingine.Na baada ya kukodoa macho vizuri namwona gwiji yule  akiwa na magwiji wa kimataifa.Wanaotoka mashariki na maghribi mwa Afrika.Magharibi na mashariki mwa dunia.Gwiji anatokea kupendwa .Anapata wapenzi ambao miongoni mwao wanamzalia mtoto.Vyombo vya habari na mitandao inamfuatilia kila hatua anayopitia.Kila kazi anayofanya.Kila safari anayokwenda. Hadi ile ya ufaransa kwa chief cooker wa hotel ya nyota tano.Mhhhhh .Kwa vile kila mmoja amegeuzia mjadala kwa gwiji huyu inanilazimu nimjue jina lake.Kumbe anaitwa Diamond Plutnums.ha ha haa.Nimechoka kbs,Wakati nikidhani namtambua vya kutosha nashangazwa na kelele za sentensi 8 nyingine ambazo hata wewe pengine huzijui kuhusu huyu Diamond Plutnnums.

1.NIDHAMU:Diamondi anatabia ya ukweli,haweki maigizo na uongo ili aonekane ni bora.Meneja wakeBabu Tale anathibitisha hili kwa kusema kuwa''Sitaki kumsifia Dioamond ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa wengine(wasnii kutoka wcb) lazima wafuate tabia za kaka yao,



2.KUJITOLEA:Anapenda kutenda wema kwa watu .Yupo tayari yeye akose  madensa wake wapate.Katika kipindi cha EFM Radio,kinachoitwa uhondo dancer wa Diamondi Mose Iyobo alisikika akisema haya.’’Kuna vitu vingine (Diamond platinum)anafanya kwa kujitolea lakini kwetu sisi inabidi atulipe’’


3.MAHUSIANO:Hana tabia ya kuchunguza simu ya mpenzi wake.Katika kipindi na Millard Ayo TV Diamond alifunguka’’Nakumbuka nilishashikaga simu ya demu wangu zamani ikanicost tangia hapo nikakoma kushika simu za mwanamke na mpaka leo siwezi kushika hata kama inaita.’’

4.CHAKULA:Hapendelei vyakula vya kwenye ndege.Akiwa nchini  ni mdau wa wali maini ndizi mbivu.Uingereza ugali nyama ya kukaanga.Nigeria egusi ,fufu,South Africa chicken tikker ,pizza
5.IMANI:Upande wa kuamini Platnums anamtanguliza Mungu mbele‘’Katika maisha ukimwomba mwenyezi  mungu na ukaweka nia thabiti na ukijutuma vinawezekana’’anasema

6.MAFANIKIO:Yeye katika swala la kupata, anaheshimu vilivyo kuwekeza katika muda,. Diamond anasema‘’Kwenye mafanikio unapata muda mfupi sana wa kupumzika’’

7.MITANDAO:Anakubali jinsi unavyotumia social networks  vyema ndivyo  unavyonufaika . .Na hapa anasema ''Ukitumia mitandao kwa njia nzuri unaweza kufika mbali.



8.KAZI:Katika ufanyaji wa shughuri mbalimbali daimondi anadira kuu moja,kazi inapaswa iwe na kiwango ama ubora wa kutosha kwani hii ni sababu ya wewe kutambulika.Katka sentence ya maneno nane amesema ''Ubora wa kazi yako ndio unakufanya uwe staa’’

0 comments:

Popular Posts