Friday, June 10, 2016

Kati ya movie za kuvutia na zilizonibadilisha fikra, ni hii movie maarufu ya JUMONG.
Movie hii maarufu wengi waliiangalia na kufurahia mapigano ila mimi nilifanikiwa kujifunza yafuatayo na yakanibadili:
1. 👨🏻Baba yake na Jumong, Haemosu, alikuwa na Kusudi la kutimiza lakini hakufanikiwa kulitimiza.
Funzo: Wazazi wetu wengi hawajatimiza malengo na kusudi zao maishani, hivyo tusiogope, tuamue tu kutimiza kusudi zetu. 

2. 👨🏻Jumong hakulifahamu kusudi lake hadi pale alipokutana na misukosuko kutoka katika familia yake.
Funzo: Misukosuko ina nafasi kubwa kutubadili chanya.

3. 👨🏻Kipaji cha Jumong cha kupiga mishale na kuongoza kilimsaidia kufikia kusudi lake kubwa la kuanzisha taifa kubwa.
Funzo: Kipaji ulichonacho kina nafasi kubwa kukufanikisha maishani ukikijua na kukitumia. 

4. 👨🏻Jumong alifanikiwa kwa kujenga timu ya marafiki 👫👬wachache na kuwafanya wawe hodari na waaminifu kwake na kutambua kusudi kubwa alilonalo.
FUNZO: Chagua vizuri aina ya marafiki wa kuwa nao na kutokuwa nao. Hawa wana nafasi kubwa ya kukufanya ufanikiwe au usifanikiwe maishani. 

5. 👨🏻Jumong alikuwa ana mtazamo chanya katika kila jambo.
Funzo: Hata jambo liwe gumu vipi, bado kuna tumaini na unaweza kufanikiwa.
 
6. 👨🏻Jumong alijifunza wapi wazazi wake walikosea na akaamua kupatia 
Funzo: Jifunze kwa waliokutangulia kwani huwezi kuishi miaka ya kutosha na hadi kugundua makosa yote duniani. 
7. 🤔Pamoja na misukosuko mbalimbali aliyoipata Jumong, bado aliweza kufikia Kusudi lake kwa kuwa tu alikuwa na udhubutu na uamuzi sahihi kufuata ndoto yake.
Funzo: Fuata ndoto yako, jiamini na utafanikiwa sana.

0 comments:

Popular Posts