Monday, June 15, 2015
Ni kwa muda sasa katika jamii nyingi kumwona kijana kavaa headphone akisikiliza mziki. Swali tunalojiuliza. Ni je hawa vijana wanavutiwa na asali ipi katika hiyo burudani? Tena sio jambo la kushangaza kusikia mdundo mkubwa ndani ya vyumba vya wanachuo na makazi ya vijana hasa wale walio wapya katika ajira.Wakati mikito ya muziki haitenganishwi na masikio ya vijana wengi.Siku hizi kuna magari,kumbi za starehe,ambazo ni mahususi kwa kuweka wadau wa mziki pamoja.Kama wewe ni mpezi wa fukwe lazima utakua unazijua hiace na gari binafsi ambazo huja na mziki 'mnene'.Na kama umeingia night club au kupita mahala penye disco ni rahisi sana kubaini kundi la masharobalo wakiegeza mfano wa wasanii wa magharibi wanaofanya miondoko ya kufoka foka. Remmy Ongala kutoka Afrika aliwahi kuuliza mziki ni nini?Kujua zaidi mziki ni nini na kwa sababu gani  vijana wanapenda sana mziki soma tafiti hapa chini.

1.Kufanya kazi wakati kuna mziki inapelekea hali chanya na kuongeza uzarishaji


2.Mdundo na mkito hufanya akili ijiamini na kuwa na nguvu

3.Kusikiliza mziki mara kwa mara ni tiba ya ubongo dhidi ya uvimbe wa hilo eneo(brain tumor)

5.Sauti kubwa kwa baadhi ya wapenda mziki huwapa furaha 




6.Maneno na mapigo katika baadhi ya miziki hupunguza msongo wa mawazo


7.Mziki hukomaza hisia changa na ni dawa ya kujiamini

9.kiafya inasemekana mziki huchangia kuzalishwa kwa chembe hai , kinga ya mwili na hupunguza matatizo ya moyo



0 comments:

Popular Posts