Sunday, June 14, 2015
Wahenga husema ukitaka kuruka juu sharti uagane na nyonga na mgaa gaa na upwa hali wali mkavu.Ivi ni nani anayeamini mwalimu anaweza kufika mbali awe raisi au kiongozi wa nchi? Wakati  ukweli unasadiki kuwa, nafasi hizo za juu huheshimika kwa sababu ni kitovu cha mamlaka makubwa na hukaliwa na  wachache .Kuna asilimia kubwa ya viongozi katika ikulu  chimbuko lao linatokana na kazi ya kufundisha watu darasani.Kitendo kinachowapa  msingi wa kusimama mbele ya halaiki wakizungumza na kuongoza  .Haya matunda ya ualimu ni kiiza machoni pa  watu wanaobeza taaluma hiyo kila kukicha.Kwa madai kuwa   ’ualimu ni kitanzi cha ajira ‘ na(walimu) hawaishiwi vitimbwi dhidi ya serikali .Ukizingatia katika moja ya sherehe za wafanyakazi hapa nchini, waalimu  wamewahi kutuma ujumbe kwa raisi uliovuta umakini wa mamilioni ya watanzania.Ujumbe ulibeba maneno mawili tu ,  yaliosomeka ’’shemeji unatuchaje’’lakini ‘message’ ilikuwa ‘sent and delivered’.hahahaha lazima ucheke.Ukiweka kando mzaha  huo na ubezaji, bilashaka tutakubaliana kuwa viongozi na waalimu wana mambo kadhaa yanayoendana,moja ikiwa ni  watu wanaofanya kazi  karibu na jamii , lakini pia wana fursa inayowaka  kama mwenge wa taifa unaosubiliwa kwa hamu ulete maendeleo ya nchi.Basi sikuchoshi tena na wafuatao ni   maraisi waliofikia hicho cheo ilihali wanajua dustor,chaki na rula zinakazi gani ubaoni  
 1.Baraka Obama.

2.Yoweri Museveni.

3.Robert  Gabriel Mugabe

4.bill Clinton

5.Kwame Nkrumah


6.John Evans Atta Mills

7.kenneth Kaunda


8.Benito Mussolin


9.julius Nyerere




0 comments:

Popular Posts