Thursday, January 23, 2014
Bila shaka umewahi kufika dukani kutazama kompyuta  ukashindwa uchague ipi?. Pengine umewahi kuchagua mashine kadhaa na ukashindwa ununue ipi? . Na hata baada ya  kununua kifaa hiki umekutwa na hisia za kutaka kuuza?. Kama haitoshi , baada ya kuuza umebaki njia panda kwa maswali mengi,  utachukua tena kompyuta ya sifa gani?.Usiumize kichwa .Haya maswali na mengine mengi ni jambo la kawaida  hasa kwa watumiaji wengi wa kompyuta, huu ni wakati  wa changamoto kama ilivyo katika kuchagua bidhaa ya aina yeyote ile . Linapokuja swala  la sifa zipi ni bora na  zipi sio bora, unapohitaji kuchukua, kuchagua , kupendekeza ama kununua kompyuta . Mtumiaji anapaswa kuwa na mwanga halikadharika elimu kiasi ,kuhusu tabia na uimara wa hiki chombo cha umeme . Hivyo kabla ya uamuzi wa kuchukua, kuchagua ,kupendekeza ama kununua kompyuta husika, inakupasa uwe na ujuzi na uelewa wa kutosha juu ya hiki chombo. Katika kukujuza zaidi juu ya sifa, tabia na uimara wa kifaa hiki cha digitali, Kitabukwanza inakuletea mambo 10 muhimu ya kuzingatia unapohitaji kompyuta .

1.Unapaswa kujua jina la kompyuta


2.Unapaswa kubainisha aina ya matumizi (elimu/mchanganyiko/mengineyo)

3.Unataka mashine ya ukubwa wa kiasi gani(Local disk)


4.Unahitaji kompyuta yenye kuchakata kwa uwezo gani(Processor)

5.Uwezo wa kompyuta kurejea kumbukumbu  ulizo tia ndani(RAM)



6.Ukubwa wa kioo(screen resolution) ni muhimu kwa watazamaji wa filamu''movies''



7.Unataka aina gani ya mfumo wa kuendeshea kompyuta  (window xp,vista,7,8,mac)

8.Inaandika/inachoma mfumo gani wa santuri(cd/vcd/dvd writer)


9.kamera(web cam)ni muhimu kwa mitandao ya kijamii,skype,facebook n.k

10.Ukubwa/umbo(size) 







0 comments:

Popular Posts