Thursday, April 13, 2017
Kuishi ni sayansi inayotegemea majaribio mengi.Kinachoshindikana leo kirudiwe tena kesho.Huko ndo kuishi.Usifanya kosa na kukata tama .Kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe.Ukikosa tone la maji sasa jipe moyo kuna bahari inakusubiri mbele.Rudia hicho kitu,hizo hatua hiyo shughuri naamini utaifikia bahari yako.Ukiteleza leo kamwe usifunge kichwa nakuamini unabahati mbaya.Una mkosi una ‘’gundu’’.Lah hasha huna hizo bahati mbaya isipokuwa Kuna kitu maisha yanakufunza.Yanasema jiandae muda wako unawadia,rekebisha kasoro hizi chache uwe mkomavu baadae.Tunawatu wengi kama mifano ambao walikata tama katika umri kama wako na leo wanavilio vya kudumu.Hawana namna nyingine ila isipokuwa wanaomba muda urudi nyuma wasahihishe makosa.Makosa yaliyozaliwa na chaguzi za kukata tamaa.Walipokutana na  punje moja ya mchanga waliogopa kusonga mbele.Wakizani ni lazima mbele ya safari  kuna jangwa kubwa likiwasubiri.Lah hasha.Kuishi hakuko hivyo.Kuishi ni sayansi,kuishi ni majaribio, kabla ya hitimisho fanya upembuzi wa kutosha.Mimi na wewe tungali tuna muda,tungali tuna afya,tungali tuna akili,tungali tuna pumzi.Tukiunganisha vyote hivi hakika safari yetu haitavunjika na zaidi sana tutakutana ana kwa ana na bahari iliyosheheni lulu.Lulu Isiyo ndogo kwa vipimo,wala ndogo kwa kimo.Hii itakuwa sawa sawa na mapenzi yetu.Italingana na ndoto zetu,itafanana na juhudi zetu.Lulu hii haitakuwa na upendeleo.Itatii kiu kadri ya kila mmoja alivyothubutu ,kadri ya kila mmoja alivyoitafta.

Punje ya  mchanga anaweza kuwa rafiki yako,ndugu yako,maamuzi yako au jambo lolote linalokufanya usisogee mbele.

Jangwa ni wazo pingamizi uoga ,wasiwasi,hisia lemavu kuwa siku za usoni hutofanikiwa na hicho kitu unachokifanya

Kuchimba kaburi lako ni kudidimiza uwezo binafsi uliojaaliwa na mwenyezi,ni kuweka kikomo cha kila elimu ulioipata hapa duniani.

Tone la maji ni pamoja na  fursa,bahati,nafasi,kazi au chochote ambacho kinamuinua mutu toka katika dhiki aliyonayo mpaka fahari na anasa anazozingoja

Bahari yako ni fahari,anasa,furaha,matarajio Yaani Kikomo kikubwa cha Starehe(K.K.S)na kila kitu ambacho ni kinyume na shida unazopitia.


 Gundu ni hali na hisia ya kutokuwa na bahati ni bayana ya nadharia zinazohusishwa na mikosi kutokubalika,kutoendelea daima. 
Wednesday, March 8, 2017
Mama ni mwanamke anayejali,anayejinyima ili mwanae apate.Anachukia kushiba wakati mwanaye ananjaa.Anachukia kupendeza wakati mwanaye hana nguo ,anachukia kulala wakati mwanaye analia.Anapenda mtoto apate mara mbili ya apatavyo yeye.Anapenda mwanaye anawili mara mbili ya yeye.Haweki chuki ya kudumu moyoni hata kama mwanaye anaitwa msaliti wa jamii au adui wa watu.Mara nyingi hupambana kurudisha  utii  na heshima ya mwanae .Asiwe seheme na  upande chachu wa maisha.Hutoa msaada kutoka kila idara ya uwezo wake.Amwone huyo mwanae juu.Hususani katika kutimiza ndoto na malengo. Tuliobahatika kusaidiwa na huyu mwanamke wa nguvu sio mimi na wewe tu.bali pia tunao wafuatao.
1.AMBWENE YESAYA(A.Y)
Image result for ambwene yesaya
Msanii mkubwa na nguzo kongwe katika sanaa.Ana platform thabiti inayosaidia hata wasanii wenzake kupata nafasi za kushirikiana na wasanii wa nje.Kama alivyomnganisha Diamond na Davido.Lakini ukarimu na mapenzi haya ni kitu kilichofunguliwa baraka na mama yake.Anasema mama ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumpatia fedha kwa ajili ya kurekodi nyimbo ya kwanza.

2.JUMA (JUX) 
Image result for juma jux
Hakuna msanii anayevaa vizuri juu ya jux .Utasema koti, tshirt, jeans ,cheni vilidizainiwa maalumu kwa umbile lake.Akiwa masomoni Uchina wanafunzi aliokuwanao walihisi ni  mmarekani mweusi.Kitendo kilichomuamsha hisia  na kuanzisha bland ya African boy.Kando na mziki,utanashati na ujasiliamali.Jux anaheshimu mchango wa mama yake baada ya kufungua pazia la neema,akimpatia pesa kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo yake ya kwanza.

3.MICHAEL(BELLE 9)
Image result for belle 9 tanzania
Anathibitisha kuimba ni kipaji anaweza kuandika chochote kikawa wimbo mzuri.Hata kama  ni kudai deni,kubembeleza mwenza au habari za kutendwa,Ni mbunifu wa sauti na mteuzi fasaha wa maneno.Huchezea lugha na kutufikia kirahisi masikioni.Akitamka masogange utapenda ilihali huelewi anachomaanisha.Akisema ''nilipe nisepe'' utamlipa deni lake faster.Akitamka sumu ya penzi,utakuwa radhi kuilamba hata kama huna maziwa.Lakini naye kama A.Y naJUX,mama yake ndiye  mzazi wa mwanzoni na msaidizi wa karibu  kumpatia sapoti ya hali na mali kwenye mziki 

4.LIL SAMIL(MR BLUE)
Image result for MR BLUE TANZAnia
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 watoto wengi Tanzania walishawishika kurap.Na walihisi pengine ni kazi rahisi kama sindano kupenyeza nyuzi za koti.Ushawishi huo ulitokana na umaaru wa kazi nzuri za hip hop zilizovuma enzi hizo.Miongoni mwa hao watoto waliofanikiwa kupenyeza na kumantain hadi leo ni Mr blue.Wengi walifanya lakini sio kama blue.Mimi pia nilitaka kuwa kama blue halikadhalika rafiki zangu hakuna aliyemuweza Anastyle yake ya kuflow akibana maneno kwa mikogo si ya nchi hii.Hasa pale anapotamka kwenye baadhi ya nyimbo''unacheza raga'' na ''basi mororo''.Lakini kiini cha safari hii ndefu ni matokeo ya mama mzazi wa msanii huyu(wenyezi amlaze mahala pema peponi) kwa kumsapoti mwanae toka alipofaulu mtihani wa darasa la saba.

5.NASIB ABDUL (DIAMOND PLUTNUMS)
Image result for diamond platnumz
Mwisho katika list yetu ni Diamond.Ambaye namwona kama balozi wa mziki wa Tanzania kwa namna flani.Kutoka tandale, kutumia jina la Z Anto kariakoo na kufanya official video ya nje na ogopa dj ya kenya.Kutoka kwa Wema Tanzania!,kufika kwa Zari uganda! hadi kwa Coldstar Nigeria.!.Kutoka kwa Mzee Ngurumo Bongo,Papaa Wemba Congo hadi kwaNelson Mandela South Afrika(their soul should rest in peace)Kutoka nchi ya Magufuli,nchi ya Mugabe mpaka nchi ya Trump na Neyo .Lakini kitu ambachohawezi kusahau ni muumba wake na namna ya kipekee kabisa mama  mzazi alivyouza kito cha thamani ili yeye afanikiwe kuingia studio.
Tuesday, January 17, 2017
Waswahili husema ‘siku hazilingani’ ni kweli. Leo ukifurahi, kesho utaduwaa. Na richa ya juhudi kubwa inayopimwa na jasho zito , majanga hayaishi kutuandama. Wakati mwingine chozi la uchungu linapita  . Jicho linazibwa  usione  fursa hata moja mbele yako. Na ghafra ukishtuka umeshajikwaa kwenye kisiki cha umaskini. Hapo utajiuliza maisha yana maana kweli?Na hakutakuwa na jibu.Maana matatizo yanakuwasha  kuliko upupu.Shida zinashamili kama magugu.Sikio halisikii habari njema tena.Ukifungulia redio  ikutie moyo ,majonzi ndo kwanza yanakithiri.  Matangazo  ni ya nafasi za shule zaidi ya nafasi za ajira, ni ya vyuo zaidi ya mahala pa kazi. Katika juhudi za kuepuka huo mfadhaiko unageuza jicho mpaka kulia kwako ambako kuna ‘tv’.Ni kipindi cha habari , bila kuamini mboni zako unajionea viongozi wakitumbuliwa Ili hali mifumo ikiachwa.Hasa elimu. Kabla hujaongeza sauti ya luninga , simu yako inayokaribia kukata ‘charge’sababu ya shida za umeme ,inaita.Ni ndugu analalamika maisha magumu pesa hakuna..Mkopeshe japo "jero" . Bila mafanikio ya kumweleza jinsi ulivyopigika,simu yake inakata hana voucher.Kufumba na kufumbua,,umeme umekata na simu inazima kumbe hata bila ya voucher kuisha bado mawasiliano yangekata tu.Ukiwa kwenye joto kali baada ya umeme kukata unabakia kutazama sura yako kwenye  televisheni iliyozima. Punde mwenyekiti wa wapangaji anakumbusha ni zamu yako kulipa LUKU,mzunguko ushakufikia. Ungali bado katika hali hii ya sintofahamu baada ya simu kumaliza moto, redio kupoteza matumaini  tv kuzima na sasa kulipa LUKU.Anakuja baba mwenye nyumba kudai chake. Utatamani kusikia maneno ya wasanii hawa.
1.’’Acha kulia ni shida za dunia ebu tulia’’Jose chamillioni
2.’’Haya yote ni maisha ipo siku yatakwisha leo mmoja anangaika mambo yamebadilika’’P funk
3. ’’Kama unapata moja kwa nini usipate na mia,hiyo inawezekana kwa wote waliona nia’’Prof jay
4.’’usikubali wakakushinda,Kwani wao waweze wananini na sisi tushindwe tuna nini’’Juma nature
5. ’’Wakati wako ndio leo kutimiza malengo yako nakusihi anza sasa jishughurishe utapata’’Ben Paul.
6.’’Na ugumu wote wa maisha shida zote za  kutaabisha usikate tama usivunije moyo’’Kara Jeremiah

Monday, January 16, 2017

Kuna milango mitano ya watu kuwa matajiri wakubwa ambayo mabilionea duniani wanatokea:


1. WATAALAMU WANAOLIPWA VIZURI
Kundi la kwanza ni wanataaluma wanaolipwa vizuri (well paid professionals) kama wanasheria wazuri, madaktari bingwa na wahandisi. Wengi waliofanikiwa katika kundi hili wanajua jinsi ya kuweka akiba na kuwekeza akiba zao kwenye maeneo yenye marejesho mazuri. Mabilionea wanaotokea kundi hili ni asilimi 10 tu ya mabilionea wote.


Image result for stephen hawking
2. WAKURUGENZI WA MAKAMPUNI MAKUBWA
Kundi lingine la mabilionea ni wakurugenzi wanaolipwa vizuri na makampuni makubwa (well paid executives). Hawa ni asilimia 10 ya mabilionea wote pia. Mara nyingi hawa huwa wametoka na kampuni mbali na wamekua nayo wakipandishwa cheo baada ya cheo mpaka kufikia hatua ya juu. Mara nyingi, watu wachache katika kundi hili huwa na uwezo mkubwa wa kuzishikilia fedha zao na kutozifuja na hiyo huwafikisha kwenye ubilionea.

Image result for executives who are billionaires
3. MAAFISA MAUZO
Kundi la tatu ni maafisa mauzo au mameneja wa idara za mauzo. Hawa huwa ni takriban asilimia 5 ya mabilionea wote na kinachowafanya wawe mabilionea ni kwa sababu ya nafasi ya kupata kamisheni kutokana na mauzo wanayoyafanya. Wengi wao huwa ni waajiriwa wa makampuni ambayo wamekuwa wakifanya nayo kazi kwa muda mrefu na kuzifahamu vizuri na baadaye kuja kuwa na milango mingi ya mafanikio.
Image result for top salesman

4. WATU WENYE VIPAJI MAALUM
Kundi la nne ni watu wenye vipaji maalumu kama wanamichezo, wanamuziki, watunzi wa filamu na vitabu na kadhalika. Hawa ni wachache sana 1%, lakini huonekana wengi sana kwa sababu ya kelele zinazoendana na umaarufu wao. 

Image result
5. WAJASIRIAMALI
Hili ndiyo kundi kubwa kuliko mengine yote, asilimia 74% ya mabilionea wote ni wajasiriamali. Hii inamaanisha kuwa nafasi ya mtu yeyote kuwa bilionea ni kubwa zaidi kupitia ujasiriamali kuliko kitu kingine chochote. 
Image result for reginald mengi biography
Sunday, January 1, 2017
     Mwaka mpya n kitu kizuri kutokea,hatuna budi kusherekea.Ila lazima tujue tunasherekea nini?.Taasisi za dini zinatufundisha kushukuru kwa kila jambo,ni sawa.Ila tushukuru tukisherekea kwa kiasi.By the way kuna sababu nyingi za kusherekea.Ikiwemo kuwa mzima,kutimiza malengo n.k.Hapa sitaongelea kwa kina habari ya sherehe na kusherekea .Nipo kwa ajili ya kushare mawazo ya watu wengine juu ya mwaka mpya.Na hapa chini wanasema

1.     Mwaka mpya ni kama kitabu cha kurasa tupu kinachosubiri kuandikwa.Tunaweza kukiandika kwa kuanza leo kujiwekea malengo.
Image result for book with empty pages
2.     Mwaka huu maombi yako yasikike  ndoto zote zitimie,jasho lote lizae .
Image result for christian muslim prayer
3.     Mwaka huu jiamini tena na upate kila unachostahili
Related image
4.     Ingawa hakuna anayeweza kurudi nyuma atengeneze mwanzo mzuri,sote tuna nafasi ya kuanza sasa na kufanya mwisho mzuri.

5.     Mwanzo wa mwaka ni mwanzo wa kufanya kila unachokusudia.

6.     Mwanzo wa mwaka ni kama karatasi nzuri isiyo na kitu.inayosubiri wewe kuiambia dunia hadithi yako
Image result for empty page
7.     Tukubali,tukatae mwaka mpya utaleta changamoto mpya,lakini tupende ,tusipende utakuja na fursa nyingi pia.
Image result for opportunity
8.     Ishi chini ya mwenye ndoto na mtendaji,anayeamini na kutafakari, lakini zaidi ya yote ishi na yule anayeona uweza ndani yako hata kama wewe  hujioni.
Image result for best company to hang with

9.     Haimanishi unatoka wapi cha msingi ni unaelekea wapi
1o.     .Kunywa kiasi,pangilia,tafta marafiki,punguza unene,kuwa chanya na tumia pesa kwa uangalifu.
Image result for no drinking

Popular Posts