Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Sunday, August 24, 2014
Katika ukuaji wa mtu ndani ya jamii fulani, unashabihiwa na mambo zaidi ya manee , na ukuaji huo hautofautiani na ule wa mmea ndani ya msitu.Mmea hauchipui hadi kuwa hatua ya mti bila kuathiriwa na joto, mwanga, maji na udongo. Usawa wa hivi viumbe hai ki makuzi unapatikana baada ya mimea na watu kuzongwa na athari za mazingira yanayozunguka viumbe vyote viwili . Haya mazingira mwisho wa siku ni sababu za unyoofu, uzuri, afya, stamina na maisha marefu ya viumbe hao. Wakati mimea inakumbwa na athari zitokanazo na mazingira kama hali ya hewa, rutuba, ardhi n.k .Binadamu anakabiliwa na vipengele vitano vinavyoathiri maisha yake ambayo ni ;familia, makundi, shule, dini na vyombo vya habari. Vipera hivi ni mizizi ya uelewa kwa binadamu , na huwa havifuatani kwa mtiririko na mpangilio maalum isipokuwa hutokea kulingana na muda pamoja na mahali mtoto anapoishi.
.1.Familia ni kitovu awali cha maarifa kwa binti ama kijana. Kupitia familia, watu hawa hujua dunia kwa mara ya kwanza katika hali mbili; ya kuishi na watu na jinsi ya mapokezi . Ueredi unaosababishwa na vitendo vya kunakiri na kurudia wafanyavyo wazazi na ndugu wengine wanaowazunguka vijana .Marudio ni njia pekee kwa wanajamii wachanga kujaribu mienendo na maisha ya utu uzima. Kupitia mikono ya mama, baba,kaka ,dada , shangazi ,mjomba n.k , mtoto hukomaa kiakili na kimwili mpaka kujibu maswali mengi juu ya dunia.
..3.Makundi ni idadi ya wasichana ,wavulana na watu wengine wanaovutiwa kuendesha jambo katika hali ya ushirikiano ,wingi na umoja . Kama msemo usemao'' onyesha rafiki zako nikueleze tabia yako''.Ndivyo makundi huathiri ukuaji wa mtu mmoja. Katika makundi, marafiki wakikutana, watu wa rika moja wakionana, na wenye umri unaoendana wakijumuika, huathiriana mmoja baada ya mwingine hatimaye wote. Athari yake hujipambanua katika mazungumzo, hisia, ufahamu na mtazamo wao.Hali inayotokea aidha wakiwa wanafahamu ama kutotambua mabadiriko hayo .Kama uzi wa mafuta unavyoshika moto kwa kasi, halikadhalika tabia ya mtoto mmoja hushika na kuenea kwa wenzake.Japo mara nyingi huwa ni jumla ya tabia za watoto ndani ya makundi zinazoathiri akili ya mvula ama msichana mmoja.Endapo kundi sio jema mtoto hubomoka kwa kuwa na maadili mabaya na kundi likiwa bora kijana hujengeka kwa kuwa na tabia sitahiki .
4.Dini ni kisima cha imani, chenye utamaduni na taratibu maalum kinachotoa mafunzo ya kiroho kuhusu mwenendo wa mtu na namna ya kukabiliana na ulimwengu .Elimu ya kina hutolewa na watu maalum walioteuliwa kwa misingi na kanuni za dini na madhehebu tofauti tofauti.Huu ni utaratibu ambao unashabaha ya kuwezesha binadamu kupata mafunzo ya mambo yasionekana na yale ya kimwili.Wakati utaratibu wa kupata haya mafunzo hupitia kuabdu, kusali, ama kuswali ukiendelea. Dini huwa kama shule kwa kuwa na watu wa aina mbili, watu wanaofika ili kupata elimu ambao huitwa waumini.Na wengine ni watu ambao hutoa hayo mafunzo, ambao pia hupewa majina kulingana na aina ya dini.Ndani ya dini mambo yasionekana ama kujificha huitwa mambo ya kiroho. Huku yale ya onekanayo au ya kimwili yakibakia kuwa ni kuvaa, kula, kunywa , kulala n.k. Hivyo waumini huenda katika madhehebu yao ili kupokea maarifa juu ya mambo ya kawaida na yale ya kiroho.Muumini aendae kinyume na utaratibu uliopangwa huwa amefanya makosa ambayo hutambuliwa kama dhambi,ama maovu na kutakiwa kutofanya hayo makosa tena.Mwisho vijana waliokulia ndani ya dini huwa ni toauti na wale ambao hawakulelewa katika misingi hiyo.
2.Shule ni uwanja wa elimu unaofafanua mazingira, hali, historia,na maarifa kuhusu mtoto anapotoka, alipo na atakapo kwenda. Mambo haya huwa katika masomo na sehemu ndogo ndogo ambazo huitwa mada au topic .Kisha huandaliwa waelimishaji maalum ambao husimama baadala ya wazazi ili kufundisha watoto hawa, ambacho ni kizazi kisichokuwa na maono pevu juu ya ulimwengu.Waelimishaji huitwa waalimu na na watoto huitwa wanafunzi. Wakiwa shuleni huendelea kubadiri utafakali wa matukio, maada, watu na vitu kutokana na masomo mbalimbali wanayopata ndani ya taasisi hiyo.Hata wakiwa vijana, ambayo ni hatua kiasi ya ukomavu wa binadamu.Shule na taasisi nyingine za elimu hupanuka kwa kujali umri na uhitaji ya huyu mwanajamii komavu.Kwa kumuelekeza afuate nini,aache nini,anapaswa kuifanyia nini jamii yake na kuafanua kwa kina taifa na dunia ni dhana zenye mantiki gani mbele ya uso wake.
..3.Makundi ni idadi ya wasichana ,wavulana na watu wengine wanaovutiwa kuendesha jambo katika hali ya ushirikiano ,wingi na umoja . Kama msemo usemao'' onyesha rafiki zako nikueleze tabia yako''.Ndivyo makundi huathiri ukuaji wa mtu mmoja. Katika makundi, marafiki wakikutana, watu wa rika moja wakionana, na wenye umri unaoendana wakijumuika, huathiriana mmoja baada ya mwingine hatimaye wote. Athari yake hujipambanua katika mazungumzo, hisia, ufahamu na mtazamo wao.Hali inayotokea aidha wakiwa wanafahamu ama kutotambua mabadiriko hayo .Kama uzi wa mafuta unavyoshika moto kwa kasi, halikadhalika tabia ya mtoto mmoja hushika na kuenea kwa wenzake.Japo mara nyingi huwa ni jumla ya tabia za watoto ndani ya makundi zinazoathiri akili ya mvula ama msichana mmoja.Endapo kundi sio jema mtoto hubomoka kwa kuwa na maadili mabaya na kundi likiwa bora kijana hujengeka kwa kuwa na tabia sitahiki .
4.Dini ni kisima cha imani, chenye utamaduni na taratibu maalum kinachotoa mafunzo ya kiroho kuhusu mwenendo wa mtu na namna ya kukabiliana na ulimwengu .Elimu ya kina hutolewa na watu maalum walioteuliwa kwa misingi na kanuni za dini na madhehebu tofauti tofauti.Huu ni utaratibu ambao unashabaha ya kuwezesha binadamu kupata mafunzo ya mambo yasionekana na yale ya kimwili.Wakati utaratibu wa kupata haya mafunzo hupitia kuabdu, kusali, ama kuswali ukiendelea. Dini huwa kama shule kwa kuwa na watu wa aina mbili, watu wanaofika ili kupata elimu ambao huitwa waumini.Na wengine ni watu ambao hutoa hayo mafunzo, ambao pia hupewa majina kulingana na aina ya dini.Ndani ya dini mambo yasionekana ama kujificha huitwa mambo ya kiroho. Huku yale ya onekanayo au ya kimwili yakibakia kuwa ni kuvaa, kula, kunywa , kulala n.k. Hivyo waumini huenda katika madhehebu yao ili kupokea maarifa juu ya mambo ya kawaida na yale ya kiroho.Muumini aendae kinyume na utaratibu uliopangwa huwa amefanya makosa ambayo hutambuliwa kama dhambi,ama maovu na kutakiwa kutofanya hayo makosa tena.Mwisho vijana waliokulia ndani ya dini huwa ni toauti na wale ambao hawakulelewa katika misingi hiyo.
5.Kipengele cha tano ni vyombo vya habari , ambavyo huwa ni hatari na baraka kutegemea na kijana na huduma za hivyo vyombo.Kijana atakuwa katika hatari inayotokana na vyombo kama redio, televisheni, magazeti, na mitandao (internet) pale atakapokosa misingi endelevu ya kujisimamia.Ambayo inatokana na familia, ushauri mzuri wa makundi, elimu bora ya shule na mafunzo ya dini. Kwa maana vifaa hivi vya mawasiliano huchukua tamaduni, imani, lugha, sanaa, michezo na tanzu zote za maisha toka sehemu tofauti za dunia.Kama vile jamii za kisasa ,taifa lililoendelea, na mabara yenye hatua nzuri za kimaisha.Na kupereka katika jamii zinazoishi maisha ya kale na zama za nyuma.Vyomba vya habari hutoa picha za maendeleo toka ughaibuni kitu ambacho huwavutia vijana wengi katika mataifa yanaendelea na kutaka kuwa kama hao wawaona katika sinema, magazeti,internet na mitandao mingine ya kijamii.Usishangea mavazi ya kileo,misemo ya kisasa,nyimbo ,mahusiano na miondoko ya vijana wa karne ya 21 .Hii ni sehemu yamapinduzi na athari zitokanazo na vyombo vya habari tulivyonavyo chumbani,sebureni,mtaani na kwingine kote.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...