Monday, June 23, 2014

Kwa rika ni kijana , kijana wa futi 5, mtazamo ni  chanya, chanya inayo aksi elimu  ya juu, idadi ni wa pili kati ya watoto watano wa familia ya mh Abraham.L.Chaula.Ni mwajibikaji, ni mwanamapinduzi na   mwanaharakati asimamapo kati ya ndugu, jamaa na rafiki zake  . Utendaji ni mwana fasihi anayefanya sanaa inayoshabiana na vitu vitatu muhimu ambavyo ni, maisha, mazingira halikadhalika tamaduni inayomzunguka.  Kwake uthubutu ni kujituma, kujaribu na kufikia malengo. Kitu ambacho ni cha thamani na kinahitaji  juhudi zaidi  . Huyu siye mwingine  isipokuwa ni Izacka chaula(Chella), ambaye ni mmoja ya watu waliobahatika kuliona jua takribani miongo miwili na nusu iliyopita. Kwa maana ya kutimiza  miaka    24 sasa toka azaliwe mwaka 1990 , huko  wilayani Njombe (hivi sasa ni mkoa) ndani ya mji wa Iringa. Akiwa huko mwanzoni mwa miaka ya 2000, ana umri usiozidi  miaka 10 , kipaji chake  kama  vipaji vingine kinastawishwa na kuchavushwa na baba yake mdogo anayeitwa Zakayo L Mwalongo (Mtoza Mc)  ,ambaye ukaribu wake na Chella  unajenga kundi linaloitwa MICHANO LUKUKI, kama ngao ya ujuzi  katika uandishi wa tungo maridhawa. Hatimaye mtoto huyu  wa pili kati ya watoto watano anagundulika na karama ya kupenyeza mawazo pevu, endelevu na shawishi  kwa uwezo wake katika uandishi wa beti na mizani mahiri ,jambo ambalo linamfanya awe mjuzi wa matatizo , changamoto na matukio  mbalimbali ya jamii na jumuiya anayoishi. Baadae sifa ya uandishi wa  mashahiri yenye kuonya, kukanya na kufungua mboni na ngome za masikio mengi, inajenga taswira pevu , komavu , pale anapokuwa   shule ya msingi Kibena  mkoani Njombe. Hapo shuleni marafiki wanaelewa na kutambua harakati na Sanaa anayoifanya Chella . Ndipo sasa  anatilia maanani tunu yake aliobarikiwa kuwa nayo na kuboresha zaidi hicho kipaji , anapoingia  sekondari ya Mpechi na Philip Mangula   na kupata  nafasi ya kushiriki shindano linaloitwa Philip Mangula Star Search (PMSS).Tukio linaloandaliwa na uongozi wa shule, mahususi   kutafuta vipaji vya wanafunzi shuleni hapo. Mnamo mwaka 2008 akiwa kidato cha nne shuleni Mangula , Izacka Chaula maarufu sasa kama Chella anakuwa mshindi namba moja  zidi ya washiriki wengine wapatao 30, walioshindana katika tukio hilo la kumtafta bingwa mmoja.  Safari ya matumaini, iliyojaa utashi na wingi wa ueledi inapata mafanikio, pale mshindi huyu    anapobahatika kujiunga na elimu ya kidato cha sita, Kwiro Boys high school, huko wilayani Mahenge Ulanga, mkoani Morogoro. Ni ndani ya mji huo usio na bahari, hisia za kutaka kurejea studio zinamshamiri  mwanafunzi huyu  . Hivyo anashawishika  kuandaa tungo ya nyimbo yake ya kwanza anayoipa jina la “Rudi mkoa”. Kibao kinachoelezea tabia ya vijana wengi kulowea katika miji mikubwa kama Dar es salaam huku wakisahua kurudi mikoani mwao.Ila utunzi na Sanaa hii haibadiri dira na imani yake katika elimu, kwani yeye huamini  kuwa, elimu ndio taa inayoweza kufukuza giza la ujinga na kurejesha nuru ya maarifa. Mwaka 2011 mwanaharakati huyu anafaulu kidato cha sita, hivyo  anajiunga na masomo ya juu katika chuo cha SAUT Mtwara (STEMMUCO ). Akiwa chuoni hapo anapata fursa ya kuwa mmoja kati ya  wanachuo wanaounda kundi  linalojihusisha na maswala ya muziki na sanaa,kundi hilo linajulikana kama Stemmuco All Stars  .Vitu vitatu anavyovipenda chella ndani ya kundi ni umoja na ushirikiano wa wanazuoni,vipaji vikubwa walivyonanvyo wasomi wenzake na michango mizuri itokanayo na mitazamo chanya. Mbali na shughuli za kikundi , thamani na mchango  wa wanakikundi ,Chella amekutanisha mawazo yake na watu wengine  wenye tunu ya kuandaa mashahiri yenye shabaha katika  kuelimisha na kufunza. Hawa mahodari wa fasihi andishi ni pamoja na Mtoza mc, Domokaya, BeckaTittle, Jebby Mubarak, Joseph Haule’’ prof jay’’, P-the MC, Juma Kassim Kiroboto ‘‘juma nature’’ Juma Jazz , Nicolazo n.k.Wanaomsaidia Kutoa kwa ufasaha kila aina ya uwezo na kitu alichanacho msomi na mtanzania huyu. Anafanikiwa kuandika mashairi mazuri na hatimaye kutia sauti yake inayoibua chachu , mapinduzi, na mabadiliko ya sanaa yake.Hali hii ni kielelezo tosha  jinsi mwanaharakati, mwanamapinduzi na mwajibikaji huyu  anavyopigana kwa hali na mali  hata kuingia mikoa zaidi ya mitano ,mitaa zaidi ya tisa,katika studio zaidi ya 10 ,akifanya kazi na waandaji wa midundo(music producer) wasiopungua 7 na kushirikiana na wasanii wanaonzia 10 hadi 20.Chella amefanikiwa kuingia baadhi ya miji kama  Dodoma, Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Njombe Mbeya, Ruvuma na Mtwara . Akifikia mitaa mbalimbali  ya mikoa hiyo kama Railway, Masaki, Kinondoni, Kigogo, Mbezi, na kuingia studio za Tongwe Rec, Mkubwa na Wanawe, Koma studio, Robbies Rec , Kp Rec, Shine Rec, Natal Rec, Baridi Touch, E-Lab,Kimya Rec , Mama Land Rec, George Rec,Goka rec,AB Rec  na nyingine  nyingi, chini ya waandaji mahiri wa muziki  nchini wakiwemo akina Geof Master(manuva), Kona Beats,Main, Jero,Pezo,Tonny(Efficiency man), Necka Beats, Jose Braiz Beats,Kagusa Andrew. Uchaguzi wa  wadau hawa wa   muziki , umezingatia  vitu vikuu viwili ambavyo ni, uchipukizi na ukongwe wao katika tasinia ya mziki, unaochangia   kazi kuwa  na uzuri. Upekee na ubunifu tofauti wa kazi zao. Mantiki inayopelekea kuonekana kwa vionjo vya kiasili na radha iliyojificha ndani ya sanaa na kazi za mwana hip hop na msomi huyu. Baadhi ya kazi ambazo Chella kafanya ni pamoja na Rudi mkoa (Dar imekupa kiburi), tatizo nini (ft Geof Master), nitafika ft becka Title, mimi na Yule ft Juma jazz, ningezaliwa Dar, naongea na wallet, Bado napambana,jiulize , usiniache , Azimio la kijiji n.k, . Kazi hizi na ushirikiano  alioufanya  msanii huyu na wajuzi wengine toka nje na ndani ya tasnia ya muziki imesaidia katika kumjengea mtazamo  wa ziada  Ukiachilia kando kimkoa, kikanda na kitaifa Chela ana mtazamo na ndoto za kufikia ngazi ya kimataifa kwa kufanya kazi bora zaidi kama zile za kina Marshall Bruce Mathers ''eminem''na wana hip hop  wengine wanaofanya vizuri duniani kote. 
                                                      






















Monday, June 16, 2014
Kwa muda sasa radio, magazeti, tv , na mitandao imekuwa ni milango mikubwa  inayofungua njia kwa  tasinia  ya michezo kupenyeza  hadi  kufikia wasikilizaji na watazamaji wengi  .Hali  inayosababishwa  na upepo  wa michezo unaovumishwa na wadau wa sekta hiyo. Wachezaji, wawekezaji na wadau wengine  wa kandanda, kikapu, gofu, tenesi , mpira wa pete n.k, kwa asilimia zaidi ya 70 wameweza kufanya michezo ikawa moja ya kivutio kikubwa cha wageni halikadharika wenyeji katika nchi mbalimbali .Huku Siri ya kuwa kivutio cha aina hiyo ikibakia kuwa ni miundombinu bora na ya kisasa.Kwa kutazama kandanda, ambao ni mchezo unaoongoza kwa kupendwa na mashabiki wengi duniani, muundo wa viwanja vyake lazima ukufurahishe.Hasa ukiangalia   michuano mikubwa ya mpira wa miguu  kama vile   kombe la dunia ,ligi kuu za mabara  na mashindano mengi maarufu ya mchezo huo . Hivyo kitabu kwanza  Blogspot ikapata muda wa kuandaa picha zinazoelezea hali halisi ya viwanja kadhaa nchini Tanzania. Huku swali la kujiuliza likiwa ni, je iwapo tutakuwa waandaji wa kombe la dunia, viwanja vyetu vinaweza kukidhi hadhi na viwango vinavyohitajika?.Tazama picha za viwanja vitano vya Tanzania
Kiwanja cha ccm kirumba,mwanza kwa juu
.
Uwanja wa kirumba kwa pembeni
ndani ya uwanja wa kirumba

Kiwanja cha Maji maji Songea kwa juu

Maji maji Songea
uwanja wa maji maji kwa pembeni
Ndani ya uwanja wamajimaji, songea

Ndani ya uwanja wa maji maji songea


Uwanja wa Nangwanda Mtwara kwa juu

Uwanja wa Nyamagana, Mwanza

Uwanja mpya Dar es salaam kwa juu

Uwanja mpya na wa zamani ,Dar es salaam kwa juu
uwanja mpya kwa pembeni
uwanja mpya kwa pembeni








Ndani ya uwanja mpya  wa Dar es salaam




Popular Posts