Sunday, March 16, 2014
Kukua kwa nyanja ya teknolojia duniani imeendana bega kwa bega na kukua kwa matumizi yake  barani afrika. Kwa mapinduzi hayo matatizo makuu ya hili bara sasa yanaelezeka kirahisi kuliko hapo awali. Hapa siongelei tu vita, umaskini,  vifoo na magonjwa kama matatizo  yanayokumba bara hili,  bali pia ukabila, rushwa na mengineyo, kama vizuizi vinavyofunga milango ya kuelekea katika uwanja wa maendeleo. Teknolojia inayojaribu kwa ukaribu kuondoa vizuizi hivyo, imetoa fursa kwa mitandao ya kijamii, blog,  muziki, picha, na filamu kufikisha habari kwa uharaka zaidi. Filamu ndio teknolojia ambayo ni kiini cha maada yangu kwa leo. Hivi sasa makampuni makubwa yanayojihusisha na masuala ya filamu ulimwenguni, Hollywood pictures,  HBO films, Lion Gate Entertainment n.k,  yanawekeza Afrika. Uwekezaji huo unafuatia fursa ya uchumi iliyopo katika bara hili. Mtandao wa Wikipedia unasema '' Afrika ni bara lenye utajiri wa rasili mali lakini wakazi wake ni maskini '' Huu ukweli wa tatizo hili na mengine yaliotajwa hapo juu unadhihirishwa na filamu kumi zifuatazo.
1.SOMETIMES IN APRIL
2.THE DEADLY VOYAGE
3.SARAFINA
4.HOTEL RWANDA
5.ROOTS
6.NERIA
7.THE GODS MUST BE CRAZY
8.THE WHITE MAASAI

9.JERUSALEM
                                      
10.BLOOD DIAMOND
Tuesday, March 4, 2014
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo tayari kusikiliza sauti mhimu  toka moyoni mwako.Miongoni mwa sauti hizi ni pamoja na ile nia  ya kutafuta ukweli wa jambo,  kutafta maamuzi sahihi na  kupata mawazo endelevu , na yakinifu. Endapo mmoja ana kiu katika kuona matunda  ya sauti hizi, huyu mtu ni wazi kuwa ana chemichemi za hekima ndani yake. Kama ilivyo kwa ufahamu, hekima halikadharika hupatikana kwa mtu yeyote aliye na nia kama zilizotajwa hapo juu. Huyu mtu wa hekima na busara hutoka katika tabaka la aina yeyote.Kuanzia kwa wazee, vijana, wanaume, wanawake, mabwana, watumwa, tajiri, masikini, wasomi hadi wasiosoma .Matabaka haya ya watu katika jamii hayahukumu mgawanyo wa hekima na busara ndani ya vichwa vya wanajamii.Hugawanya tu mitazamo yao. Kutokana na hali hii tunapata misemo, maneno, nahau na methati juu ya maisha, kazi, dini , tamaduni na vitu chungumzima vinavyosukuma gurudumu la jitihada katika maendeleo ndani na nje ya jamii zetu . Misemo, maneno na aina nyingi za fasihi simulizi mara nyingi zimekuwa haziathiriwi na vipindi, nyakati hata muda. Ni kwa kuwa fikira pevu,chanya na yakinifu zilitumika kuchimbua mizizi ya hekima iliyokuwa imejificha chini sana. Na hizi fikira ni matokeo ya ugumu na urahisi wa mapambano ya kila siku zidi ya maisha , yanaoibua uzoefu wa kukabiliana na changamoto za mara kwa mara au zile zinazofanana. Hapa ni maneno na misemo ya maisha toka kwa watu kumi mashuhuri duniani.
1.''Maisha ni kile kinachokutatiza wakati unapangilia mikakati yako ''John Lennon(mwanamziki)

2.''Maisha ni asilimia 10 ya kile kinachonipata  na asilimia 90 ni kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali'' Charles Swindolls(mchungaji)

3.''Muda wako unakikomo, kamwe usipote kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu mwingine''Steve Job(mhasisi wa Kampuni ya  Apple )


4.''Maisha  huchanua na kusinyaa kutokana  na ujarisi wa mtu husika''Anais Nin(mwandishi wa kihispania)


5.''Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotaraji''Henry David Thoreau(mwandishi wa kimarekani)


6.''Maisha hayapimwi kwa idadi ya pumzi tuivutayo ,hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu''Maya Angelou(mshairi)


7.''Changamoto hupendezesha maisha,na kukabiliana nazo ndio  maana  halisi ya maisha''Joshua J Marine(mtoa nukuu)

8.''Mtu hata badili maisha yake kama hakuanza na kubadiri fikira zake''William James(mwanasaikolojia)

9.''Kwa kutazama tu ulichonacho maishani ,kila siku utahisi unazaidi,ila kwa kutazama unachokosa maishani  kamwe hutokuwa na zaidi''Oprah Winfrey(muongozaji wa maonyesho ya televisheni)


10.''Maisha ni kile ukitendacho,ipo hivyo.itakuwa hivyo''Grandma moses(msanii wa vitu asili katika umri mkubwa)

Popular Posts