Wednesday, April 11, 2012
             Kitabu kwanza kinabaki kumuenzi na kumutambua gwiji na nguli wa sanaa ya filamuSteve Charles Kanumba maarufu kama ''The great'',kwa mchango wake mkuu kwa taifa,hadi ngazi ya familia.
               Hakuna atakaye bisha kuwa Kanumba alikuwa ni mwalimu pengine kuzidi hata walimu wengine wenye shahada na stashahada za elimu.Kwani kwa filamu zake sio tu kafundisha jamii nyingi bali pia kaelimisha familia chungu mzima.

              Kana kwamba haitoshi amepunguza hata tatizo la ajira kwa kutoa nafasi nyingi kwa wadau wa filamu.Tukianza kutaja makampuni ya usambazaji,maduka,kumbi za sinema hadi machinga mmoja mmoja aliyejipatia kipato kwa kazi ya kuuza filamu za kanumba tutakesha.

              Kaletea taifa fedha za kigeni toka nchi tofauti za ukanda wa maziwa makuu hadi magharibi mwa afrika .

             Utalii wa nchi hasa hukua baada ya nchi husika kujitangaza,kaka etu Kanumba katutanganza Tanzania sio chini ya nchi takribani 20 duniani.

             Upande wa lugha ya kiswahili bila shaka hakuna mtu atanong'ona nikisema kuwa Kanumba alikuwa ni balozi mzuri wa kunadi na kueneza lugha hii maridhawa ya kiswahili.

                  Lakini pia tusisahau kuwa ni vijana wangapi leo nchini wanaendeleza mapambano zidi ya maisha kwa kuhamasishwa na mfano bora wa Stevene Charles Kanumba ama "the great''.Kweli wahenga walisema ''vyema havidumu'' na ''heshima ya mwanadamu hudhihirika siku ya kifo chake'' 
                Kaondoka Akionyesha Njia Ubunifu na Mfano Bongomovie star Afuate(K.A.N.U.M.BA)
Wednesday, April 4, 2012
NI UKWELI ULIO DHAHIRI KUWA HAKUNA KUJIKWAA KUSIKOKUWA NA SABABU.SABABU HALISI NI KITU AU HALI ILIYOPELEKEA UKWAZIKE,HII HUUSISHA MTAZAMO NA UPEO UPANDE WA FIKIRA, LAKINI PIA STAMINA NA NGUVU UPANDE WA MWILI.SIRAHA HIZI KUU MBILI HUTAFASISIRI KWA MAREFU NA MAPANA, KWA NINI HASA MWANADAMU HUKWAZIKA MAISHANI KATIKA MISINGI YOTE YA MAISHA ,SI TUU KIJAMII,SIASA,UCHUMI,BALI PIA KI ELIMU

Popular Posts