Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Thursday, April 16, 2015
Katika moja
ya kipindi cha luninga niliona mabishano
baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati
wa kwanza ni ‘utajiri’ na msamiati wa pili ni ‘tajiri’. Mmoja alisisitiza ''utajiri ni
kuwa na chakula kingi,nguo nyingi na nyumba nyingi'' Wapili alikanusha usemi wa
mtu wa kwanza na kaka wa tatu akadakia kwa mbwembwe zote akisema''tajiri au
utajiri ni kuwa na kile unachotaka''. Mimi kama mtazamaji nilivutiwa sana na hayo mazungumzo kiasi cha kuweza
kutofautisha hiyo nomino (tajiri) na kivumishi (utajiri) kwa upana. Na kabla
msomaji hujafika mbali naomba kwanza
tuelewane katika haya mambo mawili; utajiri na tajiri. Nikisema utajiri namaanisha
ni kiasi ama hali ya kuwa na uhuru wa fedha unaoambatana na kumiliki mali na raslimali
kwa kiwango ambacho ni tofauti na watu
wengi wanaokuzunguka. Na tajiri ni yule mtu ambaye kafikia hiyo hali ya
kumiliki ukwasi (pesa,mali,raslimali) zaidi , kufuatia mipango, jitihada, malengo
na bidii katika uwekezaji alioanza muda
mrefu . Huu mchakato wa muda mrefu unaeleza wazi kuwa, miongoni mwa matajiri wengi mafanikio sio lelemama bali ni jasho itokanayo na
kudhibiti matumizi zidi ya
mapato. Kitendo kinachowapelekea mabilionea wengi wabakiwe na akiba ambayo hutumika mara
mbili. Kwanza katika kununua ‘asset’ na pili kulinda biashara zao.Matumizi ya fedha ya ziada katika kununua assets kama viwanja, mashamba, nyumba za kupangisha hutoa
faida nyingine . Hivyo kunakuwa na utajiri mpya unaoletwa na hizo ‘assets’ . Mchezo ambao ni mwendelezo kama vile kuku awezavyo kutotoa
mayai na mayai yakaleta kuku wengi zaidi.Na tumizi la pili ni jinsi akiba inavoweza kulinda
hazina ya mtu mwenye pesa, kwani akiba inayotokana
na miradi ya tajiri huifadhiwa kwa minajili ya kuokoa jahazi pale tu mambo yanapokwenda
mrama.Endapo ikitokea ujasiliamali wa bilionea unakumbwa na dhoruba ya madeni na hasara, hadi kuyumbisha mradi. Akiba ya tajiri
huyo huja kama nanga inayoweza kulinda mradi wake zidi ya dhoruba (madeni, hasara). Na
hivyo kuendelea salama akiwa kifua mbele daima. Mpaka hatua hii bado hatujaona
siri kubwa za matajiri, ungependa kuzijua ??,Basi msikilize Bill Gate, Michael Jordan, Steve Jobs, Oprah Winfrey na wengine wakidadavua siri nane za matajiri.
1. ''Kuzaliwa
masikini sio kosa lako,kufa masikini ni kosa''Anatoa siri hiyo Bill Gate ambaye aliacha chuo na kuonekana
hafai hadi pale alipopigana na kujipatia
mafanikio ya utajiri mkubwa ulioletwa na
jitihada ya kuanzisha kampuni yake maarufu duniani kama Microsoft.
2.''Nakubali
kuna kushindwa , kila mmoja hushwindwa ila sikubali
kutojaribu tena' Ni siri ya pili anayotoa Michael Jordan, ambaye amewahi
kukataliwa na timu yake ya shule ikisemekana hakuwa na kiwango cha kuridhisha
katika mchezo wa kikapu simanzi iliyomfanya kumwaga kilio cha uchungu kama mtoto
mchanga . Na leo hii baada ya kutoghairi na'kujaribu tena ' Jordan anaitwa
mchezaji bora duniani wa ‘basket’ na mwanamichezo tajiri ulimwenguni.
3.''Kila
mmoja ni balozi wa maisha yake , hakuna mwingine atawakilisha au kuishi kwa
ajili yako''Ni siri ya tatu anayosema Oprah Winfey aliyewahi kutimuliwa kazi katika kituo kimoja cha television kwa
madai kuwa hakufiti katika hiyo tasinia ya habari. Jambo lililomfanya ajisimamie
na kuwa vyote ‘balozi’na ‘mtendaji’ wa
maisha yake akanzisha kipindi cha
televisheni (oprah show) ambacho kilijichukulia umaarufu mkubwa hata kumfanya
afungue kituo binafsi cha tv, Oprah tv network. Uwekezaji uliofungua daraja la
ujasiliamali na Oprah kuwa miongoni mwa wanawake matajiri duniani.
4.''Maranyingine
unapofanya ubunifu ni rahisi kutenda makosa, ni vyema kuyabaini mapema (makosa) na kusahihisha'' Hii ni siri ya
nne iliyobeba mafanikio ya Steve Jobs, muasisi aliyewahi kusimamishwa kwenye
kampuni aliyoianzisha mwenyewe kwa madai ya kutofanya vizuri katika kampuni. Kitendo kilichomfanya aionyeshe dunia yeye ni nani hasa
pale linapokuja swala la ubunifu wa teknolojia'innovation'. Kwani
hasira za bwana Steve zimesababisha Ipod na iphone kuheshimika sokoni na yeye
kurudi kwenye kampuni yake ya Apple kama kinara wa ubunifi aliyeingia kwenye
chati ya matajiri wakubwa duniani.
5''Usiogope
kufa,ogopa kutojaribu'' Ni maneno ya bwana Shawn Corey Carter maarufu kama Jay Z. Ambaye alitemwa na kampuni kadhaa zinazojihusisha na usambazaji wa ‘albam’.Kisa kilichomchochea mwanamziku huyo wa miondoko ya kufoka foka kuuza na kusambaza kazi
zake mwenyewe . Huku akiwa ni mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja (mama). Jay z
hakusita kujaribu .kwa kuuza nakala za kazi yake ndani ya gari dogo, na kwa miguu hadi akajulikana
na kupata kianzio. Hatua iliyomfanya awe na njozi njema ya kutengeneza Recording Rebel, mavazi na
uwekezaji kibao hadi kuwa miongoni mwa wasanii tajiri duniani
.
6.''Siri
yangu kuwa na biashara iliyofanikiwa ni matokeo ya kujituma kwa bidii'' Anasema Aliko Dangote ambaye alitoka
nyumbani na kwenda kuchapa kazi kwa mjomba wake , mtu muhimu aliyemsaidia Dangote kupata mtaji na
kufanya biashara za sukari, cement ,.Akawa sio tu muuzaji bali
mzalishaji wa hizo bidhaa. Baraka hiyo ni jambo lililofungua njia ya mwafrika huyu kuitwa
tajiri wa kwanza Nigeria, Tajiri mkubwa Afrika na tajiri wa kwanza duniani kwa
watu weusi. (kwa muujibu wa gazeti la
uchumi, Forbes 2014)
7.''Nafasi
ya kuishi ni moja lakini hiyo moja ukiitumia vizuri inatosha'' Ni siri ya saba
inayosemwa na kundi la the Beatles ambalo linaundwa na waingereza wanne waliofukuzwa
studio kwa kile kinachosemakana' wana sauti mbaya na wasingekuwa na manufaa
yeyote katika soko la muziki'. Maneno hayo yaliwafanya The beatles watafute studio
zaidi na kupiga kazi kama vichaa hadi kuvunja rekodi ya mauzo hapo Uingereza na
Marekani. Baadae album yao ikaitwa ya
kwanza na bora duniani . Hivyo ikawa ni fursa ya kupata pesa na kuwekeza . Nafasi iliyopelekea kupata heshima ya ulimwengu kama kundi bora la muda wote katika
miondoko ya ‘rock’ na watu waliokamata fedha chafu zaidi miongoni mwa makundi ya
miaka ya 1960.
8.''Mafanikio
ni asilimia 1 inayotokana na asilimia 99 ya kushindwa'' ni siri
ya mwisho inayoletwa kwenu na bwn Soichiro
Honda ambaye ni enjinia wa kijapani aliepigwa chini na kampuni ya Toyota baada ya kutomzania kama injinia bora.Soichiro hakuwa na vigezo
ikiwemo elimu ya juu.Na hili hakukubali liwe ndio tatizo, kwani kama wenzake
tuliowaona,Soichiro Honda aliendelea kutengeneza mashine za magari na pikipiki huku hatua hiyo
ikitafsiriwa na baadhi ya watu kama ni ukanjanja na kushindwa.Mazingira
yaliomjengea kiu ya kutaka kufanikiwa haraka.Kabla ya kupata tuzo kutoka
ujerumani na kuwa raisi wa kampuni yake mwenyewe inayojulikana kama Honda Motor Company.Inayofanya vizuri dunia
nzima ,kwa kuzarishi sio tu piki piki bali pia jenereta,magari,mashine
za kufyeka nyasi n,k.
Friday, March 20, 2015
Binafsi
nimezoe miradi ya familia ni maduka ya bidhaa kama simu, nguo, mifugo, daladala, n.k. Ambayo huanza
na kasi ,baadae kudorora na baadhi ya miradi kupotea kabisa.Tafiti zinaonyesha kuwa kati
ya miradi mitatu ya familia ni mradi mmoja
tu hudumu.Na kwa huo mradi unaodumu hakika uongozi ni sindano kubwa katika kufuma timu ya
usimamizi wake.Wakati biashara hii inayomilikiwa kiasi kikubwa na wanafamilia
inategemea sana menegementi bora. Mataifa ya Izrael , Canada ambayo uchumi wake
umestawishwa kwa zaidi ya asilimia 65 na miradi ya familia.Wanatambua siri
nyingine za kufanikiwa kwa biashara zao. Moja, ni mgawanyo wa majaukumu baina ya
wanafamilia. Baba, mama ,kaka na dada anahusika na jukumu moja moja kati ya
uhasibu, matangazo, utafiti, soko na maboresho. Korea na India ambao pia ni
majabari wa miradi ya familia. Wanatambua fika kuwa,ukuu wao katika hizo biashara
ni matokeo mazuri ya kuweka mipango ya kudumu ambayo hufuatwa na kila kizazi
kinachorisishwa mradi. Palestine taifa lenye miradi mingi ya famillia kama
kitovu cha uchumi wake, pia wanang’oa mizizi ya maendeleo yao. Wakibainisha kuwa
kutoweka hisia za ndani katika hizi biashara ni nyota njema inayoangaza mafanikio
ya miradi ya familia.Katika suala la hisia mtama zaidi unamwagwa
kuwa,sio kila ndugu ajiriwe au kupata huduma ya bure, ila vigezo na
masharti vizingatiwe. Na Italy ambao ni watengenezaji suti wazuri wameachia
mikono ya familia inue haya mavazi ya thamani katika kila jicho la ulimwengu. Zaidi
ya asilimia 90 ya miradi ya kifamilia
nchini humo huepuka matumizi mabaya ya faida inayozalishwa na mradi , jambo
linalozuia mparaganyiko na kusambaratika kwa biashara zao.Ikumbukwe tu kuwa
miradi hii ni ya aina nyingi kama vidonge.Kuna miradi mikubwa kuna miradi midogo.Barafu,karanga,na
nyanya za magengeni ni miradi ya familia yenye sura ndogo.Makampuni ya
gari,simu,vitabu , ni miradi ya familia yenye sura
kubwa.Unafahamu biashara kubwa za kifamilia ambazo zitakuacha mdomo wazi ?,Basi
usichoke, tazama namba moja hadi kumi hapa chini.
1.Toyota
2.Ford Motor
3.Tata group
4.Volkswagen
5.Samsung
6.LG
7.Motorola
8.Siemens
9.Kodak
10.World
Wrestling Entertainment(WWE)
Friday, February 27, 2015
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unaoletwa na uteuzi wa nguo ambazo huwa na rangi mbalimbali.Mfano katika shule sio jambo geni mwanafunzi kumtambua mwalimu aliye na hasira , kwa kutumia aina ya nguo alizovaa. Hata katika usafiri ni rihasi kubaini hadhi ya mtu kwa kutumia nguo tu .Kwa maana mavazi ni lugha ya ishara inayojisimamia bila sauti. Nakumbuka siku moja nikiwa jijini mwanza ,katika moja ya kituo cha magari madogo maarufu kama daladala.Nilishuudia kijana akikosa msaada ilihali alikuwa na shida kubwa. Kijana alielekea kwa mzee kuomba msaada wa nauli.Mzee ni baba wa makamo kwa sauti na jicho alivyomkazia muomba msaada.Kinyume na fikira zangu ,yule mzee hakutoa hata shilingi .Baaadala yake akadai asingeweza kumpatia kijana fedha.kwani kijana alikuwa na maisha mazuri. Dhana iliyoletwa na kijana kuvaa kofia nyekundi, shati jeusi , kaptula jekundu , soksi nyeusi viatu vyekundu na kitambaa cheusi. Mwisho jitihada zilivyogonga mwamba, kijana akatoweka' kilaini' kama wasemavyo waswahili wa kisasa.Tukio hili halipo mbali na wasemavyo wanasaikolojia, wataalamu wa tabia,akili na mienendo ya binadamu.Ambao wamethibitisha kuwa tamaduni na mazingira mbalimbali ni sababu kuu zinzopelekea mavazi kupewa maana tofauti tofauti katika jamii.Wakielezea kwa undani zaidi,wataalam hao wanadai mavazi ya rangi ,nyekundu, blue, nyeupe, nyeusi, njano na kijani yana maana zifuatazo.
1.Nguo za rangi nyekundu.ni mavazi yanaofananishwa na taswira ya damu au moto.Kwa baadhi ya watu huwa ni vazi linalomaanisha nguvu,mabavu na utawala ,jambo linalopelekea mtu huyu kupewa umakini katika kundi la watu.Pia vazi jekundu ni ishara ya upendo wa dhati kama linavyopewa umuhimu katika harusi za kihindi,kijapani na vipindi vya valentine day pamoja na Christmas.Lakini pia kwa baadhi ya tamaduni, vazi jekundu hutafsiriwa kama kiashiria cha hatari au vita
2.Nguo za rangi ya Blue mara nyingi huwakilisha bahari na anga.Hii ranga kupendwa na wanaume zaidi.Mtu mwenye sharti, t shirt au vazi lolote la blu,hutafsriwa na jamii kama tu muaminifu,mkweli,mpole ,mwenye kujiamini na mtulivu.Lakini pia kuna mazingira mengine ambayo huashiria vazi la blue kama huzuni
3.Nguo za rangi ya kijani.Wakati hii rangi husadifu uoto wa asili,kijani kibichi na mazingira.Vazi la kijani hutambulisha mtu kama anayekuaa,anayebadilika na kujitegemea .Kwa miaka mingi kijani imekuwa ni rangi inayohusishwa na maswala ya uchumi pamoja na fedha.
4.Nguo za rangi Nyeupe.Hii rangi huchukuliwa kama taswira ya nuru au mwanga hivyo hata kufanya mavazi meupe kuonyesha watu wanaoweza kuleta matumaini,kama madaktari. Pia huashiria usafi, utimilifu uungwana na mtu asiye na hatia.Kama walivyo baadhi ya mabibi harusi ndani ya shela,na viongozi wa dini ndani ya kanzu na majoho meupe
5.Nguo za rangi ya Manjano(njano).Hii ni rangi inayojumuisha mchanganyiko wa nyekundu na nyeupe kama wakati wa mawio au jua la asubuhi.Njano ikiwa ni miongoni mwa rangi ing'aayo sana,Vazi lake humaniisha mvaaji ana furaha, ni tegemezi, mshindi, mtaka uhuru.Nchini Japani na china manjano ni rangi ya watu wenye hadhi ya juu na kueshimika.
6.Nguo za rangi nyeusi ni kielelezo cha upotevu wa rangi nyingine na mtu aliye vaa shati ,suruali au gauni nyeusi inaatafsiriwa ana huzuni au majonzi(utamaduni wa kimagharibi),,Pia kwa baadhi ya mazingira vazi jeusi huwa ni ishara ya usiriasi,mamlaka,na ukuu.Kama zilivyo maarufu suti nyeusi,na viongozi wa serikali. kadharika joho jeusi na mahakimu
Monday, December 8, 2014
Kwa muda mwingi wasanii wamekuwa wazungumzaji wakuu , wakisema visa na mikasa ya kila siku.Sauti zao hujadili makosa ya jamii, mafanikio ya jamii n.k. Wakati wakiongelea makosa ambayo huambatanishwa na shughuri za kibinadamu zisizofanikiwa au kutekelezwa kwa kiwango stahiki. Pia wasanii huangaza mafanikio ya watu katika jamii kwa kutazama jitihada za mwanaume au mwanamke zilizotoa matunda katika utaftaji wa maisha bora.Msaani mmoja anapofanikisha kuongea juu ya kushindwa na kufaulu kwa kugusia shida na raha lazima kazi yake ipendwe na jamii.Vile vile msanii anapoweza kutia moyo watu au mtu aliyepoteza matumaini ya kuishi halikadhalika kazi yake hupendwa. Na pale huyu msanii akifumbua fumbo gumu kwa wananchi, mchango wake daima hausahauliki mapema. Katika jopo la la watu ambao ni kioo cha jamii ,hatuwezi kuwasahau wanamuziki. Kwa kuwa ni miongoni mwa wasanii muhimu katika jamii, ambao hugeuka waalimu na kutoa maarifa ya mambo yatukabiliyo kila mara. Hivyo nakusihi ufuatilie kile wasnii wa Afrika mashariki wanachosema kuhusu maisha.
1.''maisha ni kama safari ni safari hakuna ajuaye kesho itakuaje''Jaquar
2.''Maisha ni sawa na kupiga mbizi,leo juu kesho chini,usinicheke kukosa.''Twanga pepeta.
3''Maisha ya mtaani ninanayo yaona sio sawa na ya shule niliyoyasoma''FID Q,na witness
4.'' Maisha ni fumbo fumbua,maisha ni bahati ,ifumbate maisha ni mapigano,pigana'' Mwijuma Muumin
5.''Maisha ni kitendawili kigumu sana leo umepata kesho umekosa'' kimobitel
6.''maisha ni tendo lifanikishe,maisha ni huzuni ishinde,maisha ni mtihani faulu'' Mwijuma Muumin
7 .''Maisha ni safari nitafika msafiri kwa imani ya kuamnika sitofichwa kama siri''One the Incredible
8. ''maisha ni karata unaweza ukalamba dume,ukalamba garasha, ukalamba mzungu wa nne''Geez Mabovu
Tuesday, December 2, 2014
Mwezi novemba mwaka 2014 nilifika mkoa fulani hapa Tanzania kwa ajili ya mahafali . Na kwa kuwa matumizi ya simu za kisasa''smartphone'' ni makubwa kwa kila mmoja ili nibidi ninunue simu ya dizaini hiyo ilahisishe mambao yangu. Hii ilikuwa ni simu ya tecno H6 iliyoweza kupiga picha za ubora mzuri kama zile za kamera ya kawaida. Ila mungu si Athumani asubuhi ya keshokutwa, siku mbili baadae, niliamkia mazoezini kama ada yangu . Nikikimbia kando ya bahari ya hindi kwa muda wa nusu saa hali iliopelekea kuchoka sana kwani ni muda sijafanya joging. Hata jioni nikiwa katika mgahawa mmoja ,najivinjari kwa smartphone mkono wa kushoto na maji mkono wa kulia nikinywa taratibu kwa fundo la kizembe bado nilihisi uchovu wa mwili na akili uliotokana na zoezi la asubuhi. Baadae kidogo niliondoka eneo hilo la chuo kulipokuwa na mgahawa nakuelekea nje. Nikiwa nje nilitaka kuwajuza marafiki zangu kuwa nipo tayari mkoani hapo, ndio ghafla nashishituka sina simu mfukoni wala mkononi. Japo akili ilikuwa imechoka , niliweza kumbuka kuwa , kabla ya kulipia maji kwa muhudumu niliacha simu mezani na sikuichukua wakati naondokka eneo hilo. Nikafanya jitihada za kumdadisi mhudumu hakuweza kufahamu lolote. Nikauliza watu waliokuwa karibu yangu wakitazama mechi ya West Brom na Arsenal Betting iliyochezwa siku hiyo ya jumamosi tarehe 29 novemba , nao pia walikana kuiona smartphone yangu mpya iliyokuwa na siku tatu tu toka ninunue. Hatimaye nimeuliza mtandaoni na majibu yao yameshauri matumizi ya programm zifuatazo.
1. LOOKOUT. Hii ni moja ya programm inayomwezesha mmliki wa simu aina ya android kubaini mienendo ya simu iliyopotea. Huku ikitoa taarifa mahala simu ilipo , Pia hii programu inapiga picha za siri bila mwizi au aliyechukua kutambua na kutuma moja kwa moja kwa anuani yako uliojisajilia katika hiyo programm.Ina uwezo wa kufunga ama kufuta habari binafsi zilizondani ya simu na endappo upo karibu na mtu mwenye simu yako programm inakuwezesha kuruhusu simu itoe alarm na kumkamata mwizi.
2. LOOKOUT PLAN B. Tofauti ya programm hii na ya kwanza ni kuwa Lookout plan B hutumika na baadhi ya simu tu zinazotumia mifumo ya android. Na wakati programm zote katika hii list zinahitaji kuwekwa katika simu kabla haijaibiwa, Lookout plan b inaweza kuingizwa katika kifaa kilichopotea ama kuibiwa hata baada ya mwizi kutokomea Ni kwa njia ya mtandao Lookout Plan B huweza kufikia simu iliyopokonywa.
3. PREY. Kama zilivyo programm nyingine hii pia inapatikana Google play , yaani katika simu zitumiazo android . Au kwa urahisi sana zinajulikana kwa jina la '' simu za tachi' '(touch). Prey ni programm ambayo inauwezo wa kuonyesha mitandoo yote inayotumiwa na simu yako iliyopotea. Lakini hata kama kulikuwa na picha za muhimu hii ni prograam iayoweza kuzihifadhi katika account au anuani yako ya google.Zaid Prey huweza kutumika hata kutafta laptop na tablets zilizopotea.
4. FIND MY PHONE. Hii programm inatofautiana na nyingine kwa kuwa inawafaa watumiaji wa Iphone na vifaa vingine vinavyotengenezwa na kampuni ya Mac.Ambao ni wazalishaji wa ipod, ipad na simu zaIphone. Habari nyeti za mtu alizoacha katika simu hupelekwa na progrmm hii hadi uwanja wa icloud. ambako mmliki wa simu hufika kwa kufanya usajili mdogo. Hapa utajua simu yako iko wapi, nani anaitumia kwa kutazama picha zilizopigwa kwa usiri wakati mwizi akiitumia.

5. ANDROID DEVICE MANAGER, Ni aina nzuri ya programm katika kurudisha simu kwa kuwa ina sifa kama programm nyingine ikiwemo ile ya kuwafaa watumiaji wa android, Pia ina mambo muhimu ya kuzingatia kama ; kupata simu iliyopotea .kwanza. inatakiwa iwe imeunganishwa na mtandao, pili, iunganishwe na na programm hii kabla haijaibiwa, tatu, simu itaonekana baada ya kuwa karibu na minara ya simu, huduma za wireless, bloothooth na mifumo mingine yenye kutuma mawasiliano katika satellite za google , nne, kuifikia simu iliyopotea unatakiwa kutumia simu tofauti, computer au kifaa kingine. Mwisho hii programm kama hizo zilizotajwa juu hupata simu ikiwa imewashwa na sio kuzimwa
.Kumbuka ni vyema kutoa taarifaya upotevu wa mali yako katika uongozi wa serikali kama polisi au ofisi ya kijiji kabla ya kufanya ufuatiliaji kwa kutumia programm hizi.
Saturday, November 8, 2014
Safari ya miguu 100 huanza na hatua moja. Ni kanuni iliyodarizi safari nyingi za mafanikio. Kutana
na safari ya aina hii inayomhusu mwanafunzi Ben, anayetokea familia ya chini yenye mzazi mmoja, anayemudu milo
mitatu kwa taabu. Ili watoto wa familia hii washibe mama anapaswa kujinyima, akihangaika na kazi mbili , tatu au zaidi. Wakati wazazi wengine wameketi na kazi moja inayowalipa vyema , mama Ben hukatisha usingizi
mnono ili kuanza mapema kazi za kupiga deki, pasi, kufua nguo, kuosha vyombo n.k . Mama
huyu huzunguka nyumba za madokta, maprofesa na watu wengine wenye
kipato cha juu ambako hufanya kazi hizo za ndani . Hali inayomfanya kukimu familia tu na asifikirie kuponda raha ama kula bata
wasemavyo vijana wa sasa. Hivyo hiyo fedha kidogo anyoipata hugharamia
mlo, mavazi na elimu ya wanaye . Kwa hii nafasi mzazi huyu katimiza malengo
mawili ; kumkabidhi elimu mtoto wake, na
yeye mwenyewe kumkabidhi mungu naisha yake. Kama kipepeo afuatavyo ua , mmea
ufuatavyo jua .Mwanae Ben anafuatilia elimu kwa
umakini mkubwa.Lakini jitihada zinagonga mwamba baada ya kushika nafasi za
mwisho darasani. Kitu kinachoibua chachu ya kujaribu tena kwanI Ben anajua fika hana urithi mwingine zaidi ya elimu. Na huo ndio unakua mwanzao wa Ben kukamata nafasi
za kwanza darasani, anafaulu kuingia chuo,na
kuchukua masomo ya kitabibu. Hadi leo Ben ni Miongoni mwa madaktari bingwa
anayefanya upasuaji wa ubongo, ikulu ya ufahamu wa binadamu. Dr Ben
Carson kafungua taasis ya kusaidia watu wasiojiweza maalufu kama Dr Ben Carson
Foundation, kafanya upasuaji mgumu wa
kutenganisha mapacha walioungana vichwa , Dr Ben kapokea tunzo nyingi za heshima
na ni muamerika muafrika wa kwanza
kufanya kazi katika kitengo nyeti cha afya kilichipo nchini Marekani akiwa na umri mdogo zaidi. Ben sasa ni
baba na anafamilia anayoitunza na kuipenda na sasa ana kula mlo bora wa chakula cha aina yeyote anachotaka..Mpaka
kufika hapo Ben anaorodhesha mambo sita yaliomfanya avune pakacha kubwa la
mafanikio kiasi hicho.
1.Kutambua Kipaji. Kila mmoja ana uwezo wa asili katika kazi,wajibu ama jambo fulani linalohitaji nguvu na akili. Mmoja huweza kuimba,mwinginekuongea, kuongoza,kufundisha n.k ,mmoja kufikiri,mwingine kutenda,kuhamasisha, kushawishi n.k. Huu uwezo binafsi(Kipaji) ukitambulika na kuendelezwa katika nyanja sahihi . Maisha ya kila mmoja wetu yatakuwa bora zaidi.katika Ualimu,uongozi,biashara,sheria,udaktari na kazi nyingine aipendayo.
2.Kuwa muaminifu.Ben,anaona uaminifu kama rangi inayo mtambulisha kila mmoja wetu zidi ya watu wamzungukao.Ukienda kinyume na kuwa raghai watu watakufahamu kwa tabia hiyo ambayo madhara yake ni kujifungia milango mingi ya fursa zilizo mbele yako.Ila kwa kubakia muaminifu upendo wa jamii,familia na marafiki utaongezeka hata upatikanaji wa nafasi mbalimbali utaongezeka pia, kwa maana uaminifu hujenga imani na matumaini mioyoni mwa watu wakuzungukao.
3.Jifunze kwa waliofanikiwa.Karibu kila ndoto tulizonazo kuna watu walizitimiza, hivyo ni vyema kujifunza kutokana na hao waliotutangulia kwa kuangalia walianza lini, waliweza vipi, kwa nini walishindwa na kutokata tamaa hata baada ya matatizo kuwa kabili..Kama una ndoto ya uongozi kuna viongozi bora duniani,nchini na mikoani.Kama ni ujasiliamali wapo wa kimataifa,kitaifa,wilaya hadi mtaani.Ukitaka kuwa hodari jifunze kwa mahodari ,na ukitaka kuwa mzuri jifunze toka kwa wazuri.
4.Kuongeza Elimu na maarifa. Unapokuwa na ujuzi, uelewa, na uzoefu lazima uhitajike na kuthaminika Elimu hiyo uliojifunza toka kizazi fulani, shule fulani, darasa fulani, mtaa fulani ina stahili kuongezwa mara kwa mara ili kupata ufanisi mkubwa.Hata kisu kitumikapo bila kunolewa hupoteza makali. . Kadri unavyokuwa na elimu zaidi ndo utakavyokuwa muhimu na wa thamani zaidi.
5.Kutumia Vitabu. Siri za maarifa makubwa zimefichwa katika vitabu vidogo.Utulivu wa fikra za wasomi zipo vitabuni. Mawazo endelevu ya wajuzi walio na busara yapo vitabuni. Hekima ya maelekezo rahisi juu ya mambo magumu huhifadhiwa katika kurasa za vitabu.Kwa muujibu wa Carson, usomaji wa maandishi kama vitabu ni maradufu kwa kujenga akili, maarifa na elimu katika kichwa zaidi ya kutazama tv au kusikiliza sauti.
6.Kuwa na hofu ya mungu. Ben,anaamini kuwa hakuna kipaji,uaminifu, elimu, kujifunza, wala vitabu kama hukumtanguliza mungu mbele. Kwani kila kitu alichoumbiwa mwanadamu kililetwa mbele yake na mungu. Hivyo ni vyema kumuomba mungu akutangulie katika kila jambo unalofanya,na unalotarajia kufanya kwa maana yeye ndio mwenye utaratibu na ratiba ya hatma zetu.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...



















































