Monday, September 16, 2013

Usahaurifu katika usomaji ni hali ya ubongo kushindwa kurejea,kukumbuka au kuwaza baadhi ya vitu vilivyosomwa muda uliopita.Hivi vitu ni pamoja na maada mbalimbali(topics),  masomo na majibu ya maswali kadhaa ambayo huwa ni muhimu katika kusoma. Bila kuzingatia mtu alisoma kwa muda gani,mfupi au mrefu ,masaa mengi au machache,usahaurifu umekuwa kikwazo kwa watu wengi sana hasa wanafunzi,hata kupelekea kutofanya vyema katika mitihani  na masomo yao kwa ujumla.Uchunguzi  wa hivi karibuni unaonyesha kuna sababu nyingi zipelekeazo mtu mmoja kusahau.Katika kurasa hii tutangalia sababu hizi katika makundi makuu manee(4).

1.Usomaji wa vitu vingi bila mpangilio na ratiba maalum

2.Kutoweka umakini wa kutosha katika kile kinachosomwa
 
3.  Mwanafunzi kutoelewa anachokisoma


 
4. Hali ya kiafya kama mawazo,msongo ,magonjwa n.k


Tuesday, September 10, 2013
Karibu katika kila hatua tuchukuazo,maneno tusemayo,kazi tufanyazo na mipango tuwekayo,huwa ni matokeo mazuri ya maamuzi fulani.Haya maamuzi bila kujali ni mazuri au mabaya,magumu au rahisi,huchukua nafasi kubwa ya muelekeo wa maisha yetu.Tafiti nyingi za kisaikolojia(psychology) zinaonyesha kuwa moja ya changamoto kubwa inayomsibu mwanadamu ni kuchua maamuzi sahihi, kwa muda sahihi na mahali sahihi.Kutoa mwanga zaidi juu ya kufikia maamuzi sahihi.Zifuatazo ni hatua saba(7) zinazopendekezwa na wasomi katika nyanja ya saikolojia(psychology)

1.Tambua tatizo au utata

2.Changanua tatizo/utata

3.Orodhesha njia kadhaa za kukabili tatizo


4.Kwa kila njia pima uzuri na ubaya wake


5.Baada ya kupima weka hisia zako katika njia bora zaidi

6.Fanya uamuzi

7.Mwisho tathimini uamuzi wako,kama ulikuwa sahihi..na hautosita kuchua siku nyingine.
 
Sunday, July 28, 2013
Kama gari linavyohitaji magurudumu na vitu muhimu katika kusafiri, harikadharika elimu inapaswa kuwa na kila kitu muhimu kumudu  madhumuni ya kutoa uelewa kwa jamii.Mbali na sera ya elimu,walimu na mtaala.Elimu hukosa vitu vya msingi kwa maana ya kujenga nguzo imara na thabiti yenye kutoa mwanya wa mafunzo bora. Uhakika wa mafunzo bora unategemea pia,uwepo wa madarasa,mbao za kuandikia ,viti na miundombinu nyingine.Miundombinu ni kitu cha msingi ,ni moja ya daraja kubwa liletalo matokeo mazuri ya ufaulu .Ni bayana ya ngome kuu inayolinda na kuwezesha maarifa na elimu ya mtoto.Kama miundombinu ikiboreshwa hasa katika shule za misingi(primary schools),ni wazi kuwa kutakuwa na mapinduzi makubwa hata ngazi ya sekondari na vyuo. .Zifuatazo ni picha 10 zikionyesha matatizo yatokanayo na ukosefu wa miundombinu bora katika shule za misingi
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.
 
10.

 
Saturday, July 27, 2013
Ni miongoni mwa  maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha  ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanadamu bila kubagua kama  ni mwalimu au mwanafunzi,amesoma ama hakusoma .Tutangalia aina mbili za elimu.Elimu rasmi na elimu isiyorasmi( formal and non-formal education).Hapa kuna tumaini jema katika kufahamu ukweli na pengine maana juu ya maisha.Kwani kuna misemo na maana nyingi sana za maisha katika aina hizi mbili za elimu .  Kama ilivyo katika misamiati mingine mingi , msamiati wa maisha umeibuka gumzo hata kupelekea wanafalsafa ,wasanii  na waelimishaji  wengi kujaribu kuongelea  maisha.Mawazo yao katika maana ya maisha ,inatofautiana sana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.Tofauti kubwa ni katika mtazamo, uwezo wa kutafakari na kufikiri .Kutoka Tanzania tutangalia misemo na maana mbalimbali za maisha zitokanazo na wasanii watano(5)sambamba na sanaa zao za muziki.

1. "Maisha ni kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka"Fid q



2."Maisha ni kama gwaride kuna mwisho na wa kwanza ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza"Stamina

3.''Maisha siyo  komborela ukasubiri kubutua jipange jitume ipo siku utafunua"Nay wa Mitego


4."Maisha ni kutenda na siyo majaribio"Mrisho Mpoto


5."Amini wewe ndiye steringi na maisha ndio sinema"Prof jay

Wednesday, May 15, 2013
Ni baada ya chuo cha Stemmuco kufuatiwa na mfululizo wa matukio makubwa ya kimichezo,kama yale ya THE BIG SCORE ,INTER YEAR(CLASS)COMPETITION na mengine mengi,juma pili hii ya tarehe 11 mei 2013 inapambwa na tukio kubwa zaidi katika historia ya michezo Mtwara.Hili ni tukio pekee linalobeba uhusishaji wa vyuo na taasisi zaidi ya sita.Bandari,Utumishi,TCC,STEMMUCO,Jeshi nk.Tukio hili  limepewa jina maarufu kama  PRO LIFE.Katika fainali za Pro life Stemmuco na Utumishi wanafanikiwa kumenyana katika viwanja maarufu vya Mtwara,Nangwanda Stadium .Mpaka kipenga cha mwisho katika dakika ya 90 Utumishi wanaibuka kidedea zidi ya mahasimu wao  kwa gori 2-1.Na hizi ni picha  kumi na nne(14)za matukio mbalimbali yaliopata kujili katika viwanja hivyo.
1.
2.
3.
4.
Muamuzi akimzawadia kadi ya njano moja ya wachezaji kutoka Utumishi





5.
Hapa ni mashabiki  wa Stemmuco wakishangilia kwa shamlashamla zote na vuvuzela

6.

7.
Benchi la mashabiki timu ya  Utumishi

8.

9.

10.
 
moja ya wachezaji wa Utmishi akitoka njee ya uwanja baada ya maumivu ya mguu

11.

12.
Mashabiki wa Stemmuco kwa sauti na nguvu zote hawakuchoka kushangilia
13.
Utumishi pia hawakukaa kimya hata sekunde moja
14.
Dr Msafiri, mlezi na mwanzilishi wa mashindano haya akiwa pamoja na watangazaji



Monday, April 1, 2013


Wakati kosa ni moja yakifika mawili ni makosato.Hivyo kitendo cha kutotenda au kutofanya jambo kwa usahihi huku ukienda kinyume na utaratibu unaoendesha jambo hilo,kitazalisha dhana iitwayo kosa.Upande wa pili wa kosa huleta dhana nyingine iitwayo adhabu.Adhabu ni hatua ya kumwajibisha mtu kwa dhumuni la kujirudi na kufuata utaratibu unaoendesha jambo fulani alilokeuka mwanzo.Zifuatazo ni picha tisa(9) zikionyesha makosa na adhabu katika mashule
1.KOSA:Kulewa


2.KOSA:Kutazamia



3.KOSA:Kutazamia

4.KOSA:Kutazamia

5.ADHABU

6.ADHABU

7.ADHABU

8.ADHABU


 9.ADHABU




Popular Posts