Tuesday, March 6, 2018
Baada ya kuangalia mafanikio ya watu.Ilifika  kipindi nikasema''Martin huu ni wasaa wako''.Nikapumzika Kusoma vitabu vya ujasiliamali ,kutazama movie za insparation na kuzungumzia ndoto za kupata mali.Nikajisemea''kwa nini nisiache maneno na kuweka kila ninachokijua katika vitendo?''Ukiachilia mbali swala la kuomba baraka na kudra za mwenyezi mungu,Mtoa ridhiki.Nilianza na vitendo katika hatua mbili tatu.Hatua ya kwanza nilitafta mtaji,pili nikatafta mradi,tatu nikatafuta sehemu ya kuweka  na mwisho msimamizi .Ndani ya miezi sita ya uendeshaji nimefanikiwa kujifunza vitu vya msingi vitano.

1.KUWA MAKINI NA MKOPO
Image result for LOAN
Pesa ya kukopa ni hatari ,kabla ya kuchukua kiasi tasilimu kutoka kwa mtu au taasisi.Andaa sehemu uliyoifanyia utafti wa kina .Kisha wekeza pesa ya mkopo.Niliongozana na rafiki zangu  wanne, sote tukachukua kiwango sawa cha pesa ila baada ya hii miezi sita.Ni mmoja tu kati ya wanee aliyefanikiwa na mkopo.

2.WEKA KANDO MATUMIZI YAKO NA PESA YA BIASHARA
Image result for business and family
Pili nimejifunza kuwa mradi wa biashara ,kama ununuzi na uzaaji wa bidhaa za rejareja unahitaji uvumilivu sana.Biashara hii inapenda uwekezaji wa muda mrefu .Kila pesa ya mauzo iandikwe na kuachwa hapo ofisini.Kitendo cha kuamisha faida ,kitendo cha kuchanganya mapato na matumizi binafsi au ya familia ni sumu kwa ukuaji wa mradi wako.Miezi itaenda ,mwaka utakata biashara yako ingali vilenvile.

3.USIMWAMINI MTU KATIKA PESA AU BIASHARA 
Image result for never trust anyone
Karibu kila mwenye pesa nyingi aidha  aliwahi kudhurumiwa,kutapeliwa ama kuibiwa.Kwa wasiofahamu huwaona wenye miradi kama mabahiri,wachoyo wasiosaidia.Ila toka niingizwe mkenge na vijana tuliokuwapamoja.Imani kwa kila ninayeshirikiana naye kwenye biashara imetoweka.Kila anayetaka mkopo, kuazima kiasi kikubwa cha pesa namuona ni wale wale tu.

4.BIASHARA NI MAISHA NA TABIA YAKO
Image result for creating yourself
Biashara siyo kazi au ajira.Biashara ni tabia ya mtu ni  mfumo wako wa maisha.Wengi wanaofeli kwenye hatua ndogo kama hii yangu.Walifanya kosa ambalo nimekumbana nalo mara nyingi.Binafsi nilikuwa na tabia ya huruma halikadhalika kuamini watu.Nikawa mkopeshaji mzuri tena asiyeweka hata rekodi saaa nyingine.Nilipendenda kupunguza bei kupia hata ile niliyomumulia.Baada ya mambo kuanza ugumu hasara kukithiri,Mwenyewe nilibadili mfumo wa maisha na hii tabia  mpaka biashara nayo ikaanza kubadilika,

5,KUWA MBUNIFU NA JITUME KULIKO ULIVYOWAHI KUJITUMA
Image result for work hard and smart
Kila unachotaka kukiona kesho ndani ya biashara yako,kianzishe sasa.Usikubali kulala kabla hujafanya jukumu ulilojiwekea.Mimi nilikuwa na ndoto kubwa  katika biashara,Sikuwahi fikiri kama nitachukua muda mwingi kukuza biashara kwanza kabla ya kunufaika.Ndani ya miezi sita nahangaika na kuweka muonekano wa ofisi usadifu dira yangu,Najifunza mbinun kadhaa za kuleta wateja wapya kila mwezi.Pia najifunza uwezo walionao wapinzani wangu dhidiya udhaifu wangu.Mwisho nikitaza vizuri najiona nasogea nilipokusudia jana.


Popular Posts