Thursday, April 13, 2017
Kuishi ni sayansi inayotegemea majaribio mengi.Kinachoshindikana leo kirudiwe tena kesho.Huko ndo kuishi.Usifanya kosa na kukata tama .Kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe.Ukikosa tone la maji sasa jipe moyo kuna bahari inakusubiri mbele.Rudia hicho kitu,hizo hatua hiyo shughuri naamini utaifikia bahari yako.Ukiteleza leo kamwe usifunge kichwa nakuamini unabahati mbaya.Una mkosi una ‘’gundu’’.Lah hasha huna hizo bahati mbaya isipokuwa Kuna kitu maisha yanakufunza.Yanasema jiandae muda wako unawadia,rekebisha kasoro hizi chache uwe mkomavu baadae.Tunawatu wengi kama mifano ambao walikata tama katika umri kama wako na leo wanavilio vya kudumu.Hawana namna nyingine ila isipokuwa wanaomba muda urudi nyuma wasahihishe makosa.Makosa yaliyozaliwa na chaguzi za kukata tamaa.Walipokutana na  punje moja ya mchanga waliogopa kusonga mbele.Wakizani ni lazima mbele ya safari  kuna jangwa kubwa likiwasubiri.Lah hasha.Kuishi hakuko hivyo.Kuishi ni sayansi,kuishi ni majaribio, kabla ya hitimisho fanya upembuzi wa kutosha.Mimi na wewe tungali tuna muda,tungali tuna afya,tungali tuna akili,tungali tuna pumzi.Tukiunganisha vyote hivi hakika safari yetu haitavunjika na zaidi sana tutakutana ana kwa ana na bahari iliyosheheni lulu.Lulu Isiyo ndogo kwa vipimo,wala ndogo kwa kimo.Hii itakuwa sawa sawa na mapenzi yetu.Italingana na ndoto zetu,itafanana na juhudi zetu.Lulu hii haitakuwa na upendeleo.Itatii kiu kadri ya kila mmoja alivyothubutu ,kadri ya kila mmoja alivyoitafta.

Punje ya  mchanga anaweza kuwa rafiki yako,ndugu yako,maamuzi yako au jambo lolote linalokufanya usisogee mbele.

Jangwa ni wazo pingamizi uoga ,wasiwasi,hisia lemavu kuwa siku za usoni hutofanikiwa na hicho kitu unachokifanya

Kuchimba kaburi lako ni kudidimiza uwezo binafsi uliojaaliwa na mwenyezi,ni kuweka kikomo cha kila elimu ulioipata hapa duniani.

Tone la maji ni pamoja na  fursa,bahati,nafasi,kazi au chochote ambacho kinamuinua mutu toka katika dhiki aliyonayo mpaka fahari na anasa anazozingoja

Bahari yako ni fahari,anasa,furaha,matarajio Yaani Kikomo kikubwa cha Starehe(K.K.S)na kila kitu ambacho ni kinyume na shida unazopitia.


 Gundu ni hali na hisia ya kutokuwa na bahati ni bayana ya nadharia zinazohusishwa na mikosi kutokubalika,kutoendelea daima. 

Popular Posts