Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Wednesday, March 8, 2017
Mama ni mwanamke anayejali,anayejinyima ili mwanae apate.Anachukia kushiba wakati mwanaye ananjaa.Anachukia kupendeza wakati mwanaye hana nguo ,anachukia kulala wakati mwanaye analia.Anapenda mtoto apate mara mbili ya apatavyo yeye.Anapenda mwanaye anawili mara mbili ya yeye.Haweki chuki ya kudumu moyoni hata kama mwanaye anaitwa msaliti wa jamii au adui wa watu.Mara nyingi hupambana kurudisha utii na heshima ya mwanae .Asiwe seheme na upande chachu wa maisha.Hutoa msaada kutoka kila idara ya uwezo wake.Amwone huyo mwanae juu.Hususani katika kutimiza ndoto na malengo. Tuliobahatika kusaidiwa na huyu mwanamke wa nguvu sio mimi na wewe tu.bali pia tunao wafuatao.
1.AMBWENE YESAYA(A.Y)
Msanii mkubwa na nguzo kongwe katika sanaa.Ana platform thabiti inayosaidia hata wasanii wenzake kupata nafasi za kushirikiana na wasanii wa nje.Kama alivyomnganisha Diamond na Davido.Lakini ukarimu na mapenzi haya ni kitu kilichofunguliwa baraka na mama yake.Anasema mama ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumpatia fedha kwa ajili ya kurekodi nyimbo ya kwanza.
2.JUMA (JUX)
Hakuna msanii anayevaa vizuri juu ya jux .Utasema koti, tshirt, jeans ,cheni vilidizainiwa maalumu kwa umbile lake.Akiwa masomoni Uchina wanafunzi aliokuwanao walihisi ni mmarekani mweusi.Kitendo kilichomuamsha hisia na kuanzisha bland ya African boy.Kando na mziki,utanashati na ujasiliamali.Jux anaheshimu mchango wa mama yake baada ya kufungua pazia la neema,akimpatia pesa kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo yake ya kwanza.
3.MICHAEL(BELLE 9)
Anathibitisha kuimba ni kipaji anaweza kuandika chochote kikawa wimbo mzuri.Hata kama ni kudai deni,kubembeleza mwenza au habari za kutendwa,Ni mbunifu wa sauti na mteuzi fasaha wa maneno.Huchezea lugha na kutufikia kirahisi masikioni.Akitamka masogange utapenda ilihali huelewi anachomaanisha.Akisema ''nilipe nisepe'' utamlipa deni lake faster.Akitamka sumu ya penzi,utakuwa radhi kuilamba hata kama huna maziwa.Lakini naye kama A.Y naJUX,mama yake ndiye mzazi wa mwanzoni na msaidizi wa karibu kumpatia sapoti ya hali na mali kwenye mziki
4.LIL SAMIL(MR BLUE)
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 watoto wengi Tanzania walishawishika kurap.Na walihisi pengine ni kazi rahisi kama sindano kupenyeza nyuzi za koti.Ushawishi huo ulitokana na umaaru wa kazi nzuri za hip hop zilizovuma enzi hizo.Miongoni mwa hao watoto waliofanikiwa kupenyeza na kumantain hadi leo ni Mr blue.Wengi walifanya lakini sio kama blue.Mimi pia nilitaka kuwa kama blue halikadhalika rafiki zangu hakuna aliyemuweza Anastyle yake ya kuflow akibana maneno kwa mikogo si ya nchi hii.Hasa pale anapotamka kwenye baadhi ya nyimbo''unacheza raga'' na ''basi mororo''.Lakini kiini cha safari hii ndefu ni matokeo ya mama mzazi wa msanii huyu(wenyezi amlaze mahala pema peponi) kwa kumsapoti mwanae toka alipofaulu mtihani wa darasa la saba.
5.NASIB ABDUL (DIAMOND PLUTNUMS)
Mwisho katika list yetu ni Diamond.Ambaye namwona kama balozi wa mziki wa Tanzania kwa namna flani.Kutoka tandale, kutumia jina la Z Anto kariakoo na kufanya official video ya nje na ogopa dj ya kenya.Kutoka kwa Wema Tanzania!,kufika kwa Zari uganda! hadi kwa Coldstar Nigeria.!.Kutoka kwa Mzee Ngurumo Bongo,Papaa Wemba Congo hadi kwaNelson Mandela South Afrika(their soul should rest in peace)Kutoka nchi ya Magufuli,nchi ya Mugabe mpaka nchi ya Trump na Neyo .Lakini kitu ambachohawezi kusahau ni muumba wake na namna ya kipekee kabisa mama mzazi alivyouza kito cha thamani ili yeye afanikiwe kuingia studio.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...