Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Monday, July 18, 2016
Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini mara saba katika kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?. Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.
1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain
2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki
3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr
4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''
5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya
tatizo na utatuzi
6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama
katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.
7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo
safi zaidi ya ulivyokuwa hapo mwanzo
8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo
utalisogelea.
9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi
gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.
Friday, July 15, 2016
Tazama hapa.>>>>>>matokeo
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza
4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani
6.Tabora Boys,-Tabora
7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro
9.Ilboru,-Arusha
10.Tandahimba-Mtwara
Na hizi ni top ten ya shule zilizofanya vizuri
1..Kisimiri,-Arusha
.
2.Feza Boys,-Dar es Salaam
3.Alliance Girls,-Mwanza
4.Feza Girls,-Dar es Salaam
5.Marian Boys,-Pwani
6.Tabora Boys,-Tabora
7.Kibaha,-Pwani
8.Mzumbe-Morogoro
9.Ilboru,-Arusha
10.Tandahimba-Mtwara
Sunday, July 10, 2016
Mambo!. Kila kukicha kinazaliwa kipaji kipya Tanzania.Na kila ,mwaka kunazaliwa studio mpya mtaani.Tangu sanaa ya mziki igeuke ajira.Vijana wa kibongo wameikimbilia fursa.Hakuna anayetaka kubakia shabiki kama mimi au wewe.Vijana wanataka kuwa wasanii na maproduza. Wanatamani kulingana au kumzidi Diamond na Alikiba,Nahreel na Lamar.Ni kitu kizuri kuwa na mtazamo wa mafanikio.Lakini ni kitu kibaya kutoweka daraja thabiti la kufikia hiyo ndoto au hayo mafanikio..Sitaki uchoke ndg ila nakumbusha tu kuwa,huwezi kuitwa msanii au kufanya sanaa ,Kama hauna mbinu na akili ya ziada. Bilashaka unatambua kuwa hata mvuvi hawezi kuvua samaki iwe sangara au pweza, bila ujuzi. Mfano Mvua sangara anaamini hawezi kupata sangara kwa kutumia chakula asichokipenda sangara .Halikadhalika mvuvi wa pweza anatambua hatoweza kumpata pweza bila kuiingia kwenye maji yanayopendwa na pweza. Wembe ni ule ule mmoja hata kwa wewe unaetaka kufanya mziki hapa nchini, bila kujali ni Hiphop, taarabu, kwaito zuku, bolingo, segere, singeli, baikoko n.k. Huwezi kujizolea wafuasi bila kujua wanachopendelea .Bila kujua tabia ya mziki.Na kuonekana mjuzi kama yule mvuvi anayejua samaki anahitaji nini ,inachukua mbinu na akili ya ziada kama nilivyotangulia kusema,Gharama na nguvu pia .Kati ya mbinu nyingi ambazo unazijua,umezisikia .Kuna chache nakukumbushia ambazo kwa namna moja ama nyingine naamini zitakusogeza mahala katika jitihada na harakari za kuwa msanii nyota wa mziki Tanzania.
1.Uandishi .Joh Makin anasema''Uandishi wa nyimbo ni feeling na feeling ni kama mtu anavyopata mtoto yaani kuna uumbaji''Lady Jay Dee anaelezea zaidi kwa kusema''mara nyingi nyimbo mimi ninazoandika huwa ni vitu vya ukweli ambavyo aidha ni kwangu au kwa jamii''
.
2.Collabo(kushirikiana). Msanii Alikiba anasema''Unaweza kufanya nyimbo na mastaa isiwe nzuri,Staa kwa staa.Unaweza kufanya na underground(chipukizi) na ikawa nzuri.Sometimes feeling zina kuwa tofauti tunaamka tofauti''
3,Manager: A.Y anaelezea kuwa''Kuna vigezo vya kunimeneji mimi cha kwanza ufanye kazi atleast mara tatu ya mimi ninavyofanya kazi, kingine ni lazima huyo manager aje na networking(mtandao)wake''.Na kuhusu wasanii chipukizi anaongezea'' mtu hana single au anayo moja hajapata nafasi ya kutengeneza atleat hit song(nyimbo nzuri pendwa) nne kujipima na wasanii wengine,hapo hapo anataka manager,huwezi kuwa na manager wakati hujaijua biashara yako hata kwa kiasi fulani''
4.Promo(utanbulisho na matangazo ya wimbo):Ommy Dimpozi anashauri''Kwenye huu mziki kuna aina ya promo inaweza kufanya mziki usikae sana,inakuwa kama unavumisha kitu vuu kweli kina kuja na ule upepo alafu ukipotea upepo na nyimbo inapotea na watu wanataka tena nyimbo mpya.Kwa hiyo kuna zile aina za promo za vurugu zinaweza sababisha nyimbo zisikae''
5.Kujiamini.Jaji maarufu wa kipindi cha kusaka vipaji vipya,Bongo star search bwana master Jay anasema''.Msanii anatakiwa kuwa mtu ambaye anajiamini kupita kiasi,hutaki kuwekeza hela yako kwa mtu ambaye ana kipaji lakini hajiamini.Mtu mwenye kipaji nusu na kujiamini mia anaweza kufanya vizuri kuliko mwenye kipaji mia na kujiamini nusu''
,
6.Fanya research(tafiti) Profesa jay anasema''Ukitaka kufanya mziki mzuri lazima ufanye mziki wa watu,sio ufanye mziki wangu(mtu binafsi),so lazima ufanye research watu wanahitaji nini na kwa muda gani,lazima uangalie jamii yako inayokuzunguka,ambayo unataka kuiimbia ipo katika situation(hali) gani ,kama wanataka bata(anasa,furaha) waimbie nyimbo za bata,kama wapo kwenye stuation ngumu waimbie nyimbo za kuwapa moyo''
7.Mafanikio: Mambo makubwa yote wanayomiliki wanamziki hayatokani na mziki pekee.Mwana Fa anasema''Nilichogundua ni kwamba wasanii wote matajiri,hawafanyanyi mziki pekee hawawi matajiri kwa sababu yamziki.Mifano yote hai tunayo''
8.Hitimisho;Msanii Chemical anasema''Sanaa ni kuchukua kile ulichonacho ukijumlisha na vya watu wengine vingi''
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...