Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Thursday, April 16, 2015
Katika moja
ya kipindi cha luninga niliona mabishano
baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati
wa kwanza ni ‘utajiri’ na msamiati wa pili ni ‘tajiri’. Mmoja alisisitiza ''utajiri ni
kuwa na chakula kingi,nguo nyingi na nyumba nyingi'' Wapili alikanusha usemi wa
mtu wa kwanza na kaka wa tatu akadakia kwa mbwembwe zote akisema''tajiri au
utajiri ni kuwa na kile unachotaka''. Mimi kama mtazamaji nilivutiwa sana na hayo mazungumzo kiasi cha kuweza
kutofautisha hiyo nomino (tajiri) na kivumishi (utajiri) kwa upana. Na kabla
msomaji hujafika mbali naomba kwanza
tuelewane katika haya mambo mawili; utajiri na tajiri. Nikisema utajiri namaanisha
ni kiasi ama hali ya kuwa na uhuru wa fedha unaoambatana na kumiliki mali na raslimali
kwa kiwango ambacho ni tofauti na watu
wengi wanaokuzunguka. Na tajiri ni yule mtu ambaye kafikia hiyo hali ya
kumiliki ukwasi (pesa,mali,raslimali) zaidi , kufuatia mipango, jitihada, malengo
na bidii katika uwekezaji alioanza muda
mrefu . Huu mchakato wa muda mrefu unaeleza wazi kuwa, miongoni mwa matajiri wengi mafanikio sio lelemama bali ni jasho itokanayo na
kudhibiti matumizi zidi ya
mapato. Kitendo kinachowapelekea mabilionea wengi wabakiwe na akiba ambayo hutumika mara
mbili. Kwanza katika kununua ‘asset’ na pili kulinda biashara zao.Matumizi ya fedha ya ziada katika kununua assets kama viwanja, mashamba, nyumba za kupangisha hutoa
faida nyingine . Hivyo kunakuwa na utajiri mpya unaoletwa na hizo ‘assets’ . Mchezo ambao ni mwendelezo kama vile kuku awezavyo kutotoa
mayai na mayai yakaleta kuku wengi zaidi.Na tumizi la pili ni jinsi akiba inavoweza kulinda
hazina ya mtu mwenye pesa, kwani akiba inayotokana
na miradi ya tajiri huifadhiwa kwa minajili ya kuokoa jahazi pale tu mambo yanapokwenda
mrama.Endapo ikitokea ujasiliamali wa bilionea unakumbwa na dhoruba ya madeni na hasara, hadi kuyumbisha mradi. Akiba ya tajiri
huyo huja kama nanga inayoweza kulinda mradi wake zidi ya dhoruba (madeni, hasara). Na
hivyo kuendelea salama akiwa kifua mbele daima. Mpaka hatua hii bado hatujaona
siri kubwa za matajiri, ungependa kuzijua ??,Basi msikilize Bill Gate, Michael Jordan, Steve Jobs, Oprah Winfrey na wengine wakidadavua siri nane za matajiri.
1. ''Kuzaliwa
masikini sio kosa lako,kufa masikini ni kosa''Anatoa siri hiyo Bill Gate ambaye aliacha chuo na kuonekana
hafai hadi pale alipopigana na kujipatia
mafanikio ya utajiri mkubwa ulioletwa na
jitihada ya kuanzisha kampuni yake maarufu duniani kama Microsoft.
2.''Nakubali
kuna kushindwa , kila mmoja hushwindwa ila sikubali
kutojaribu tena' Ni siri ya pili anayotoa Michael Jordan, ambaye amewahi
kukataliwa na timu yake ya shule ikisemekana hakuwa na kiwango cha kuridhisha
katika mchezo wa kikapu simanzi iliyomfanya kumwaga kilio cha uchungu kama mtoto
mchanga . Na leo hii baada ya kutoghairi na'kujaribu tena ' Jordan anaitwa
mchezaji bora duniani wa ‘basket’ na mwanamichezo tajiri ulimwenguni.
3.''Kila
mmoja ni balozi wa maisha yake , hakuna mwingine atawakilisha au kuishi kwa
ajili yako''Ni siri ya tatu anayosema Oprah Winfey aliyewahi kutimuliwa kazi katika kituo kimoja cha television kwa
madai kuwa hakufiti katika hiyo tasinia ya habari. Jambo lililomfanya ajisimamie
na kuwa vyote ‘balozi’na ‘mtendaji’ wa
maisha yake akanzisha kipindi cha
televisheni (oprah show) ambacho kilijichukulia umaarufu mkubwa hata kumfanya
afungue kituo binafsi cha tv, Oprah tv network. Uwekezaji uliofungua daraja la
ujasiliamali na Oprah kuwa miongoni mwa wanawake matajiri duniani.
4.''Maranyingine
unapofanya ubunifu ni rahisi kutenda makosa, ni vyema kuyabaini mapema (makosa) na kusahihisha'' Hii ni siri ya
nne iliyobeba mafanikio ya Steve Jobs, muasisi aliyewahi kusimamishwa kwenye
kampuni aliyoianzisha mwenyewe kwa madai ya kutofanya vizuri katika kampuni. Kitendo kilichomfanya aionyeshe dunia yeye ni nani hasa
pale linapokuja swala la ubunifu wa teknolojia'innovation'. Kwani
hasira za bwana Steve zimesababisha Ipod na iphone kuheshimika sokoni na yeye
kurudi kwenye kampuni yake ya Apple kama kinara wa ubunifi aliyeingia kwenye
chati ya matajiri wakubwa duniani.
5''Usiogope
kufa,ogopa kutojaribu'' Ni maneno ya bwana Shawn Corey Carter maarufu kama Jay Z. Ambaye alitemwa na kampuni kadhaa zinazojihusisha na usambazaji wa ‘albam’.Kisa kilichomchochea mwanamziku huyo wa miondoko ya kufoka foka kuuza na kusambaza kazi
zake mwenyewe . Huku akiwa ni mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja (mama). Jay z
hakusita kujaribu .kwa kuuza nakala za kazi yake ndani ya gari dogo, na kwa miguu hadi akajulikana
na kupata kianzio. Hatua iliyomfanya awe na njozi njema ya kutengeneza Recording Rebel, mavazi na
uwekezaji kibao hadi kuwa miongoni mwa wasanii tajiri duniani
.
6.''Siri
yangu kuwa na biashara iliyofanikiwa ni matokeo ya kujituma kwa bidii'' Anasema Aliko Dangote ambaye alitoka
nyumbani na kwenda kuchapa kazi kwa mjomba wake , mtu muhimu aliyemsaidia Dangote kupata mtaji na
kufanya biashara za sukari, cement ,.Akawa sio tu muuzaji bali
mzalishaji wa hizo bidhaa. Baraka hiyo ni jambo lililofungua njia ya mwafrika huyu kuitwa
tajiri wa kwanza Nigeria, Tajiri mkubwa Afrika na tajiri wa kwanza duniani kwa
watu weusi. (kwa muujibu wa gazeti la
uchumi, Forbes 2014)
7.''Nafasi
ya kuishi ni moja lakini hiyo moja ukiitumia vizuri inatosha'' Ni siri ya saba
inayosemwa na kundi la the Beatles ambalo linaundwa na waingereza wanne waliofukuzwa
studio kwa kile kinachosemakana' wana sauti mbaya na wasingekuwa na manufaa
yeyote katika soko la muziki'. Maneno hayo yaliwafanya The beatles watafute studio
zaidi na kupiga kazi kama vichaa hadi kuvunja rekodi ya mauzo hapo Uingereza na
Marekani. Baadae album yao ikaitwa ya
kwanza na bora duniani . Hivyo ikawa ni fursa ya kupata pesa na kuwekeza . Nafasi iliyopelekea kupata heshima ya ulimwengu kama kundi bora la muda wote katika
miondoko ya ‘rock’ na watu waliokamata fedha chafu zaidi miongoni mwa makundi ya
miaka ya 1960.
8.''Mafanikio
ni asilimia 1 inayotokana na asilimia 99 ya kushindwa'' ni siri
ya mwisho inayoletwa kwenu na bwn Soichiro
Honda ambaye ni enjinia wa kijapani aliepigwa chini na kampuni ya Toyota baada ya kutomzania kama injinia bora.Soichiro hakuwa na vigezo
ikiwemo elimu ya juu.Na hili hakukubali liwe ndio tatizo, kwani kama wenzake
tuliowaona,Soichiro Honda aliendelea kutengeneza mashine za magari na pikipiki huku hatua hiyo
ikitafsiriwa na baadhi ya watu kama ni ukanjanja na kushindwa.Mazingira
yaliomjengea kiu ya kutaka kufanikiwa haraka.Kabla ya kupata tuzo kutoka
ujerumani na kuwa raisi wa kampuni yake mwenyewe inayojulikana kama Honda Motor Company.Inayofanya vizuri dunia
nzima ,kwa kuzarishi sio tu piki piki bali pia jenereta,magari,mashine
za kufyeka nyasi n,k.
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...