Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Saturday, December 12, 2015
Furaha
huanza juu na kumalizikia chini kama
moto wa mshumaa, na ikiwa chini hurejeshwa
tena juu ili iangaze nafsi kama jua linavyoangaza dunia. Unakumbuka sio mara
moja tumesikia furaha ikipotea.Baada ya muda inarudi?.Basi wakati ikipotea
hujificha, ili simanzi itutawale , na huzuni
itufike. Tuwapo ndani ya hizi hali hujiona wapweke na hatufai kama tone la
chozi mbele ya mvua . Ni upweke na uchungu huu ambao nafsi hupitia , hatimaye mtu mmoja anadhamiria
kuitafta furaha kwa gharama yeyote.Wakati mmoja akifanya haya, furaha huwa inarejeshwa juu taratibu ili uzito wa amani ukae mioyoni mwetu .Faraja na neema zije juu ya amani. Pale furaha yote inaporudi
huyo mtu atakuwa na sababu kubwa ya kuishi na kupendeza. Kwani sakafu ya moyo
wake imepata kile ilichokosa kwa muda mwingi. Tabasamu la huyu mtu sasa lazima ling’ae Kuliko hata
nyota iwakayo saa nane za usiku.Ikiwa unataka usitengane na furaha unashauriwa kufuata njia zifuatazo
1.TUMIA FURSA.Ukitaka kuwa mtu wa furaha kila mara, usishindane na hali,usigombane na watu hata kubishana sana kwa sababu ya tukio fulani.Kwani siri ya furaha ni kuruhusu kila hali ije kama ilivyo na sio wewe unavyofikiria ni lazima iwe.Na kisha thubutu kuitumia kwa style na mbinu zako zote.
2.KUBALI UWEZO WAKO.Kwa maana ya kawaida uwezo ni ile nguvu ulionayo,kiasi cha fedha unachopata ,au idadi ya mali unayomiliki, Mitaji hii na mingine mingi ni nyenzo kuu ya kukutoa sehemu moja hadi nyingine.Kwani sisi husahau kuwa furaha haipatikani kwa kumiliki kila kikubwa unachotamani, bali furaha huja kwa kuthamini kile kidogo ulichonacho toka mwanzo.
3.PENDA CHANGAMOTO.Kuna misemo ya kihindi isemayo kuwa ''hata nyota isingeweza kun'gaa kama kusingekuwapo na giza'',''Hata mvua isingeweza kunyesha kama kusingekuwapo na joto''Ikiashiria kupata kitu kimoja ni lazima kutambua mchango wa kitu kingine ambacho ni kibaya ama kizuri.Kwa maana huwezi kuthamini ukimya kama hujawahi kusikia kelele na huwezi kuthamini furaha kama hujapata uchungu.Furaha ya kweli ni mbegu inayoota baada ya shina la uzuni kuanguka.mizizi ya chuki kung'auka.
4.TAFTA MAFANIKIO.Hapa usichanganye haya maneno mawili; mafanikio na ushindi.Ushindi ni dhana inayoambatana na mapambano ama mashindano baina ya mtu mmoja na mwingine.Lakini mafanikio ni ile funguo ya furaha baada nguvu , fedha, mipango kufikia malengo ya juu.Haya malengo chanya ndio hatua kubwa unazopaswa kuzifikia ndani ya siku,wiki,mwezi n.k Kulingana na ulivyojiwekea.Mafanikio ni chakula muhimu kwa kila moyo wa furaha.
5.CHAGUA MTAZAMO SAHIHI.Hii ni namna tunavyoangalia mambo.Ni jinsi tunavyofanana au kutofautiana na wengine.Chunguzi za masulara ya furaha zinasema.Mtu anayetizama kazi za mwenzake kwa mtazamo chanya .Huambukiza furaha mara dufu zaidi ya mwingine atazamaye shughuri hizo kwa mtazamo hasi.Na tafiti ikaongezea kuwa kadri unavyotoa furaha kwa wingi ndivyo unavyopokea kwa wingi .
1.TUMIA FURSA.Ukitaka kuwa mtu wa furaha kila mara, usishindane na hali,usigombane na watu hata kubishana sana kwa sababu ya tukio fulani.Kwani siri ya furaha ni kuruhusu kila hali ije kama ilivyo na sio wewe unavyofikiria ni lazima iwe.Na kisha thubutu kuitumia kwa style na mbinu zako zote.
2.KUBALI UWEZO WAKO.Kwa maana ya kawaida uwezo ni ile nguvu ulionayo,kiasi cha fedha unachopata ,au idadi ya mali unayomiliki, Mitaji hii na mingine mingi ni nyenzo kuu ya kukutoa sehemu moja hadi nyingine.Kwani sisi husahau kuwa furaha haipatikani kwa kumiliki kila kikubwa unachotamani, bali furaha huja kwa kuthamini kile kidogo ulichonacho toka mwanzo.
3.PENDA CHANGAMOTO.Kuna misemo ya kihindi isemayo kuwa ''hata nyota isingeweza kun'gaa kama kusingekuwapo na giza'',''Hata mvua isingeweza kunyesha kama kusingekuwapo na joto''Ikiashiria kupata kitu kimoja ni lazima kutambua mchango wa kitu kingine ambacho ni kibaya ama kizuri.Kwa maana huwezi kuthamini ukimya kama hujawahi kusikia kelele na huwezi kuthamini furaha kama hujapata uchungu.Furaha ya kweli ni mbegu inayoota baada ya shina la uzuni kuanguka.mizizi ya chuki kung'auka.
4.TAFTA MAFANIKIO.Hapa usichanganye haya maneno mawili; mafanikio na ushindi.Ushindi ni dhana inayoambatana na mapambano ama mashindano baina ya mtu mmoja na mwingine.Lakini mafanikio ni ile funguo ya furaha baada nguvu , fedha, mipango kufikia malengo ya juu.Haya malengo chanya ndio hatua kubwa unazopaswa kuzifikia ndani ya siku,wiki,mwezi n.k Kulingana na ulivyojiwekea.Mafanikio ni chakula muhimu kwa kila moyo wa furaha.
5.CHAGUA MTAZAMO SAHIHI.Hii ni namna tunavyoangalia mambo.Ni jinsi tunavyofanana au kutofautiana na wengine.Chunguzi za masulara ya furaha zinasema.Mtu anayetizama kazi za mwenzake kwa mtazamo chanya .Huambukiza furaha mara dufu zaidi ya mwingine atazamaye shughuri hizo kwa mtazamo hasi.Na tafiti ikaongezea kuwa kadri unavyotoa furaha kwa wingi ndivyo unavyopokea kwa wingi .
Thursday, November 12, 2015
Japokuwa kuna giza,mwanga,mwezi , jua , bado siku hazifanani.Kama hivyo ndivyo ni kitu gani hasa hufanana?.Siku zote wewe na mimi tumeumbiwa uhitaji.Kwa maana nyingine kila siku tunaongeza idadi ya vitu tunavyopenda,tunavyotaka. Vitu hivi vinaweza kutengwa katika mipango na katika uchumi. Katika uchumi,mimi napenda mshahara mkubwa.Bila shaka hupendi kuingiza pato dogo ,unapenda? .Haya mahitaji ya kifedha ni sehemu ndogo kati ya ile kubwa iundayo mahitaji yetu ya msingi.Yaani malazi,makazi,chakula na mavazi. Katika upande mmoja ukubwa wa mahitaji ya msingi umepanuka kiasi cha kuziba macho yasione mipango rahisi ya kujikwamua.Kwani tuzibwapo na kipindi cha njaa,usingizi,baridi n.k .Huwa ni ngumu kufikiria mipingo ya muda mrefu au ya kudumu itakayotuepusha na taabu hizo.Na upande wa pili ni wakati unapokuwa huru husurutishwi na chakula, malazi, makazi, mavazi.Katika hii saa ambapo hatujazibwa na mahitaji tunaweza kuweka malengo, kuoata ndoto, kufanya mipango na kupendekeza mbinu. Hizi harakati na mipangalio zinavuma tokea ndani ya mioyo yetu zikipita vichwani na kutua akilini. Akili ndio makao makuu ya kila ndoto,mipango na mbinu tulizojiwekea.Kwa kuwa hii sehemu ya ubongo ni mhimu kwetu kama nahodha ndani ya meli.Basi tunapaswa kuitunza, kuiboresha na kuitumia kwa uangalifu. Ahsanteh kwa watu waliotufunza kusoma na kuandika, kwani kwa kitendo chao tumetambua akili hutiwa mwanga. Akili hutolewa gizani. Akili hubadirika. Akili hupokea maarifa kulingana na mambo yanayoizunguka.Na ili tufikie mahitaji ya kifedha na ya msingi tunapaswa kuwa waalimu wa akili zetu, tukizifundisha kulingana na somo zuri linalojiandika katika kuta za familia , mitaa, jamii na maeneo mengine tunayoishi. Zikiwemo kata, wilaya , mikoa ,nchi ,bara n.k.Bila kuchukua mazuri ya sehemu uliopo akili hizi tunazilisha sumu .Itakayoua 'future' zetu .
Thursday, November 5, 2015
Kuna msemo wa miaka mingi usemao apandaye haba atavuna haba. Maana yake inaendana sambamba na maisha ya vijana wawili waliotoka familia tofauti. Mmoja ni Paul mwenye miaka 20 aliyetoka familia duni , na mwingine ni Michael mwenye miaka 21 aliyetoka familia bora. Hawa vijana kulikuwa na kitu kilichoondoa tofauti zao. Hiki kitu ilikuwa ni kiu ya mafanikio. Kila mmoja alitamani maisha mazuri. Kulikuwa hakuna njia ya kupata hayo maisha bila kuhusisha wazazi wao. Paul alimwendea baba ake aliyekuwa mfugaji na mkulima akiomba maelekezo namna gani ataweza kufanikiwa. Baba ake alimwambia mwanaye jambo asiloweza kutegemea. Hili jambo halikufanana na lile Michael aliloambiwa na mzazi wake. Michael alipomsihi baba ake,ampatie siri ya kupata mali na fedha kama zilizopo nyumbani. Mzazi wake alimcheka sana kabla hajasema yafuatayo. ''mwanangu mimi sikupata chochote toka kwa baba angu, babu yangu alisema kitu kimoja ambacho nataka usikisahau maishani mwako, sisi tumebarikiwa katika lolote tutakaloanzisha, likiwa sahihi utakuwa tajiri kama mimi ama marehemu babu yako'' Baada ya mazungumzo hayo Michael alianza safari ya kutafta maisha . Tukirudi kwa Paul tunamuona akianza safari ya maisha huku neno la mzazi wake likiwa kichwani na kumrudia mara kwa mara . Mzazi wake alimwambia kuwa ''mifugo na mashamba alionayo alipewa na baba ake,'' akasisitiza kuwa baba ake alisema ''wao hawakuumbiwa mafanikio mengine wataendeleza mashamba na mifugo kwa kizazi hadi kizazi ''Lakini Paul hakuwa mtu wa kukata tamaa. Aliondoka kwao akaanza maisha katika biashara. Biashara ya kwanza ikafeli, akafanya ya pili ikafeli, ya tatu ikafeli, ya nne ika feli, Kabla hajaanza biashara ya tano .Paul mwenye miaka 26 sasa .alikumbuka kauli ya mzazi wake ''wao hawakuumbiwa mafanikio mengine wataendeleza mashamba na mifugo kwa kizazi hadi kizazi'' ndipo akafanya hiyo biashara ambayo nayo kwa bahati mbaya ilishindikana. Paul aliketi chini na kutafakari kisha akarudi kwao kuwa mkulima na mfugaji kama babu yake ,Huku kijana mwenzake( Michael) anatoka kwao na mtaji aliotafta mwenyewe anaanza na biashara ya kwanza inampa hasara, ya pili inamtia hasara , ya tatu inamtia hasara , ya nne inamtia hasara, ya tano inamtia hasara ya sita inamtia hasara ya saba inafeli , ya nane inakwama ya tisa ina inajifunga, Katika Biashara ya kumi , Michael akiwa na umri wa miaka 30 anakumbuka maneno ya mzazi wake ''sisi tumebarikiwa, katika lolote tutakaloanzisha likiwa sahihi umekuwa tajiri kama mimi ama marehemu babu yako'' na alipojaribu hii biashara ya kumi ikamfilisi. Lakini Michael hakati tamaa na mwisho anakuja kufanikiwa katika biashara ya 20 akiwa na umri wa mika 40 .Na kuwa tajiri kushinda hata baba na babu yake.Kwani;
1. Ule muda wote wa makosa ulimjengea uzoefu na ujuzi mkubwa katika nidhamu ya fedha, uchumi na biashara.
2.Imani yake haikutetereka kwa maana hakuamini kwenye kushindwa
3.Alijua hata kama huna kitu una nafasi ya kupata kitu kama tu bidii ni shina la utaftaji wa hicho kitu
4.Alibaini kuwa bahati sio kuzaliwa katika familia bora ama duni bali ni mwenyewe kuandaa mazingira yatakayopokea fursa na kuigeuza iwe ajira au mradi
5.Alipata ufahamu kuwa kuendelea sio lazima uwezeshwe, ukopeshwe, utaftiwe bali maendeleo yanaanza kwa chochote ulichonacho ikiwemo wazo, elimu, nguvu , juhudi, akili,imani na bidii
6.Paul alishindwa kwa kuwa dira yake ilizimwa na maneno ya mzazi
7.Alikomea maisha ya kawaida kwa kuwa kauli ya mzazi ilitawala uwezo na mipango yake.
9.Kosa kubwa kuliko yote alilofanya Paul ni kitendo cha kukata taamaa.
Wednesday, July 22, 2015
Nilipokuwa mtoto kuna kundi kubwa la marafiki walinizunguka.
Mmoja wao alijulikana kwa jina la Pola. Mie na rafiki yangu pola tulishirikiana kwa ukaribu juu ya mambo mawili. Pola alipenda sinema za Anord Shwarzenegger , mimi za Jack Chan. Rafiki angu asipokwenda kutazama sinema, alipenda kucheza mpira. Ambalo ni jambo la pili lililotunganisha
. Pola akikusanya makaratasi, mimi nilifuma mpira . Ujamaa wetu uliwakasirisha
watoto wengine. Wangefurahi kutuona tukitengana, huku Sinema na kandanda vikiwa
kando na maisha yetu kuliko mbingu
na ardhi.
Baada ya kuandaa mipira . Ukitukosa uwanjani tupo juu ya
miti tukifanya kile tulichoamini ni mazungumzo. Na watoto wengine walikiita
kuwa ni mabishano. Mada kuu ya maneno yetu ilikuwa
ni sinema. Pola alikuwa nimwingi wa
furaha tukianza hizi mada. Bilashaka
sikuleta kilio mbele ya macho yake. Kama yeye ambavyo hakuleta kero usoni mwangu. Mazungumzo ghafla yalikata tuliposikia filimbi (priiii). Kwa sababu ilikuwa ni saa ya kandanda, tuliteremka
viwanjani tukiungana na watoto wengine wakiwemo maadui. Kama marafiki wengi wa utotoni , hatukucheza kandanda katika timu
pinzani hata siku moja. Daima tulikuwa
wa timu moja. Kwa kipindi kile mechi hazikufika mwisho bila mtoto mmoja kuwa Mohamed ali, akipiga ngumi na mwingine Van damme akipiga mateke. Waliopewa kipondo ni
wachezaji waliokuwa hawana kosa. Katikati
ya tifutifu sikupendezwa kuona rafiki angu akipigwa , licha ya umri wa miaka 6
niliokuwa nao, niliamini ningelimtetea Pola (niliyemzidi mwaka mmoja) , kama
kuku mdogo anavyolinda kifaranga wake baada
ya mwewe kukaribia. Sijui nini humwingia
pola , kwani wakati wa vurugu jamaa alitumia siraha kama Anord Shwarzenegger (kipenzi chake).
Akianza kuwatupia mawe watoto waonevu . Na kuchapa fimbo zisizo na mpangilio . Vita ikifikia hapa Sikukimbia, niliwakimbiza,
sikuogopa niliwaogopesha kwa mbio na
ujasiri kama Jackie Chan (kipenzi changu).
Miaka ikaenda sote
tukahitimu elimu ya msingi. Nikabahatika kuingia sekondari. Akafanikiwa kufanya biashara . Miaka ikapita
nikachaguliwa form six. Akabahatika kuwa
wakala wa vinywaji vya kokakola. Miaka
ikazidi kusonga. Nikajiunga na Chuo, Yeye akajiunga na miradi mikubwa . Nikasikia
Pola kaoa na kufungua biashara za Tv, DVD
, CD na ving’amuzi. Muda ukapita , nikapata ajira ya ualimu, kitengo cha michezo. Sijasikia chochote toka kwa rafiki
yangu . Mtu tuliolindana wakati wa vita , leo muda wa amani tunatengana. Mtu
aliyenifundisha umoja, ananiacha katika utengano. Hua sikomei hapo kuwaza. Siku za
likizo, nikifuatilia tamthilia za
kikorea ,kimarekani na Uingereza. Hujiuliza mswali yasiyo na majibu. Tungekuwa na mawasiliano na Pola angempenda
mastar kama jumong?, Angemfurahia Will Smith au Harry Potter? Hakuna wa kujibu haya maswali miongoni mwetu
.Sio mimi,wala wewe isipokuwa ni Pola tu. Kabla na wewe hujampoteza rafiki ako kipenzi ,uliepitia
nae hatua nyingi za ukuaji,mateso na raha,njaa na shibe,furaha na huzuni.Napenda
ujifunze jinsi urafiki wetu ulivyovunjika.
1.sote tulikuwa busy
2.Mawasiliano yalikuwa magumu tukiamini itakuwa usumbufu
mmoja kuwasiliana na mwingine
3.Kisha tulidhani mmoja kati yetu atakuwa wa kwanza kumtamtafta mwenzake
4.Baada ya kipindi najiuliza kwa nini mimi tu ndo nianzishe
mawasailiaano?
5.Hatukuonyeshana upendo tuliounyeshana thamani zetu
6.Bila mawasiliano ni wazi kuwa kumbukumbu baina yetu
ilizaliwa,ikakuwa na mwisho ikafa
7.Hatimaye
tukasauliana hadi leo
Wednesday, July 15, 2015
Miaka ya nyuma ilikuwa ni miongoni mwa nyumba nzuri hiyo
sehemu. Mmliki wake ni bwana tajiri ambaye kila mmoja alimtazama kwa msaada. Gari
ilikuwa ni kivutio cha kila jicho. Ilikuwa ni kama ndoto iliyotimia pale mmliki
alivyoongeza gari na nyumba katika idadi ya miliki zake
Lakini leo mali zote ni chakavu na kwa mujibu wa asili ya
vitu, kimoja lazima kichoke ili kingine kije. Nyumba izeeke ili nyingine ijengwe, gari lichoke ili jipya linunuliwe. Je unadhani ni vyema kwa mtu
wa namna hii , anayeishi na kumiliki hili gari la kale kuitwa mwenda wa zimu
hivi sasa, na apelekwe mirembe au sehemu nyingine ya vichaa?
Sidhani, kwa sababu hakuna
jipya chini ya jua. Nguo yako ya thamani ni dekio kwa mwingine, Salio lako la bank
ni kiasi ambacho mwingine anatoa msaada
bure. Mrembo au mtanashati ulinaye leo kaachwa na mwenzako jana. Hata dada anayeitwa
kahaba pale mtaani au kule hotelini siku moja alikuwa bikira. Sasa ya nini
majivuno? Maisha ni mafupi kujisikia, kujiona dhidi ya mwenzako. ’’Tungali
wakosefu, hakuna mkamilifu’’ . Anasema
steve job. Hakuna kitakachotusaidia wala sipendi kuona watu wakijikweza nakujivunia
mali, uzuri, akili, kiwango cha elimu, umaarufu na miliki za dunia. Mungu anasema ’’Pendaneni na muongeze marafiki’’
Siku zote kumbuka yule unayemdharau wakati unaelekea juu ndo yule utakaye mkuta wakati unashuka
chini. Hivyo usiwe ni kisababishi cha matatizo kwa mwingine. Kama utakuwa
kisababishi , utakuwa umejipalia kaa la
matatizo mwenyewe, na hakika , hao uliowaletea shida watakuwa sehemu ya matatizo yako siku moja.
Mwisho usisahau kuwa hata matawi ya mgomba kuna siku huitwa majani makavu. Hivyo hupaswi kupumbazwa na
mali za duniani. Kwani siku moja zitachakaa na kufa.
Endapo muda utafika ukahisi kulia, basi niite, siahidi kukufanya ucheke siku
hiyo, lakini tutalia sote. Siku moja
ukitaka kukimbilia mbali, usiogope, niite. Nakuahidi nitakimbia pembeni yako. Lakini
ikitokea ukaniita na usisikie jibu, huenda
nakuhitaji. Kwa maana siku itakuja mmoja wetu hatokuepo tena. Na itakuwa
umeshachelewa kusema ‘I care’. Machozi yatakuto lakini haisaidii, nimeshatangulia mbele za haki.
Tuesday, July 7, 2015
Mabadiliko
ni kama maji huweza kuchukua umbo la sura yeyote. Na huweza kufuata uelekeo
mmoja au zaidi. Ukitazama sura ya teknolojia
iliopo leo utabaini hii sio taswira iliokuepo jana, yaani miaka 20 iliyopita. Mageuzi
haya yanatokea huku wagunduzi kuntu wakiwa ni miongoni mwa watu adimu katika hiki
kipindi. Richa ya kukosekana kwa wagunduzi nguri wakiwemo; Isack Newton, Pythogrus,
Edson Thomas, kati ya miaka 1995 hadi 2015 . Kuna upepo wa mabadiliko
unaoletwa na waboreshaji wanaofuata misingi ya hao wagunduzi kuntu. Wagunduzi
dhahiri, wangunduzi halisi , wagunduzi waliovuma miaka yote. Ndani ya hiki kipindi cha miongo miwili ( miaka
20 ). Kuna wabunifu wanaochipukia na kumiminika
kama utitiri. Hawa ndio shina
linaloshikilia urahisi wa maisha na urahisi wa mawasiliano katika dunia ya leo.
Hali inayopelekea mambo yaliokuwa hayawezekani miaka 20 iliyopita kufanikiwa. Na
hapa ni baadhi ya hayo mambo
1.IMO,SKYPE
Kitendo cha kuonana ana kwa ana baina ya watu wawili walio katika sehemu tofauti za mchi , ilikuwa ni kitendawili katika niaka ya 90. Ahsanteh kwa teknolojia ya imo na skype kwa kuleta nyuso na sauti za watu karibu. Wapendanao waliokuwa wametenganishwa na umbali, masomo, kazi na majukumu ,sasa wanafursa ya kusalimiana na kutazamana kwa ukaribu kama pua na mdomo.
2.WHATSAPP
Ilikuwa ni
rahisi kwa mganga wa kienyeji wakati
ule. Kuendesha majadiliano na watu anaowaona yeye tu , kama hiyo haitoshi
aliweza kusema kitakachojiri duniani
kabla ya mimi na wewe kutambua lolote.Baada ya simu kuingia kila mtu kapatiwa
uwezo huo. Tena kama ina whats app ndio mtajadiliana hadithi zote kuanzia; siasa
, katiba, tamaduni , uongozi, ajira, michezo, burudani ,utabiri wa hali ya
hewa,kubet n.k .Vyanzo vya hizi habari kwa mwaka 2015 sio tena ‘mafundi’ au waganga
wa kienyeji pekee bali ni rafiki zako,wanafunzi
wenzako,wafanyakazi na jamaa uliohifadhi namba zao katika simu ya kiganjani
mwako. Kwa kutumiana jumbe za sauti,picha na video Whats app hukupa maarifa pamoja na taarifa za hayo matukio mbalimbali
3.YOUTUBE
1995,Televisheni ilikuwa ni kila kitu juu ya
masuala ya video. Kuona ‘kichupa’ au video mpya ya msanii unayempenda ilikupasa
utege jicho kwa luninga. Ukikosa tukio kubwa katika taarifa ya habari ulitakiwa
kuwa mvumilivu hadi taarifa irudiwe, vinginevyo ungoje kipindi maalumu au mwisho wa wiki. Hali sio
hiyo tena miaka ya kuanzia 2005, na Shukrani za kipekee ziendee youtube kwa kutupa uhondo wa video tulizokosa,
tuzitakazo katika muda wowote, mahali popote na kwa mtu yeyote. matukio makubwayaliokupita au uliyoyakosa
katika tv utayapa hapa.
4.SHAZAM
Unakumbuka
enzi hizo ukisikia mziki mzuri redioni, unatamani mtangazaji ataje jina la huo
wimbo?. Ama unapita mahala kuna mdundo wa nyibo za ughaibuni,zinakugusa moyoni lakini
hujui msanii wala jina la wimbo? Hii shida sasa imefika mwisho.Mwaka 2015 Kazi
imerahisishwa sana . Ni vyepesi zaidi ya
kumsukuma mlevi. Kwa kutumia shazam unaelekeza tu simu au komputa karibu na
mdundo wa nyimbo, na ndani ya sekunde
umeshapata jina la msanii na nyimbo
.
5.GOOGLE
EARTH
Zamani
ilikuwa ni ngumu kufika pointi moja bila
kuwa na mwenyeji, bila kuuliza ama kupanda chombo cha usafiri. 2015 unaweza
kutembea dunia nzima bila kukwea pipa, kuchukuwa treni, kupita na meli wala
kupanda basi. Ikiwa una google earth na mji una ramani mtandaoni , utaelekezwa njia za kupita kwa mguu, kwa gari hadi sehemu
za kuvinjari, hotel, supermarket, beach na
kona za afya ; hospitali, zahanati, na
maduka ya madawa baridi. Google hawatoi tu ramani bali pia vituo mhimu
unavyotaka kujua
.
6.FACEBOOK
Karibu kila
mmoja ana damu ya uandishi. kubali!, kataa!. Kwa maana anafurahi kushirikisha
jamii dhidi ya mafanikio ,mipango, ndoto,
huku akitia moyo marafiki na kuomba
msaada wa maombi kwa ndugu hata pongezi kuto kwa jamaa . Mmoja yupo huru kutoa
mawazo na hisia zake mbele ya wengine. Hii sehemu ya maisha ya mtu mmoja dhidi
ya wengine hufanyika kwa maandishi yanayoambatanishwa na picha nzuri ya
mhusika. Kama ishara ya kujuza jamii nini kinachoendelea upande wake. Endapo hujui
ninachojaribu kuelezea hapa, nakusihi
jiunge na facebook, ukashuhudie jinsi uhuru wa kujieleza ‘freedom of expression’
inavyotendewa haki. Ikiwa una kumbukumbu nzuri, pengine umebahatika kuishi na
wezee katika miaka ya 90. Utaona bibi na
babu zetu hawakufaidi dhana nzima ya uhuru wa mawasiliano.Ukilinganisha na
FACEBOOK
7.TWITTER
Nakumbuka
nilisoma kitabu kimoja zamani kidogo, ambacho kilielezea namna wafalme
walivyokuwa wakituma jumbe ulimenguni.Kitendo kilifanya na mtu mwenye mbio sana
aliagizwa kupeleka nyaraka katika himaya nyingine , na hiyo himaya iliteua mjumbe wao mwenye kasi sana mpaka
falme ya tatu .Ambayo pia ilieneza habari katika falme ya nne. Mtindo uliendelea mpaka falme ya sita ,saba hadi ya mwisho.Na baada ya miaka habari ilienea
ulimenguni kote. Stori ya hiki kitabu chenye maisha ya zamani, kinafunua muongozo
wa teknolojia ya twitter . Kitu ambacho twitter hufanya japo ni ni ndani ya sekunde,au
dakika tu. Ni kueneza habari kwa haraka, Hivyo miomgoni mwa matumizi mengi ya
tweeter, dunia nzima hujua nini
kimejiri. Kwa kuendeleza habari husika iwe ni Alshabab, Sunami, mapinduzi, ongezeko
la joto n.k .Ndani ya masaa taarifa
itakuwa imefika uchina, Marekani, uingereza, Brazil, Australia na Tanzania .
Dunia nzima hupelekewa taarifa kwa kufanya swala endeleve linaloitwa ‘retweete’
8.INSTAGRAM
Wakati sote
tunaamini bank ni nyumba ya pesa, ghala ni nyumba ya mazao na msitu ni sehemu
ya miti. Basi instagram ni nyumba au
sehemu ya picha. Zamani kuona picha ya msanii, mtu maarufu au kiongozi mkubwa
ilikuwa nadra, mpaka utafte gazeti au kutembelea maneo ya kazi zao. Ahsanteh
Instagram kutuletea pozi, dizaini, mbwembwe na matukio mengi ya watu hawa
katika mfumo wa picha.
9.EBAY, AMAZON,
KUPATANA
Unakumbuka
wakati unauza bidhaa na hakuna mteja? .Unataka kununua mali hakuna hakuna muuzaji?.
Ilikuwa ni zama ya miaka ya 90. Kuanzia mwaka 2015 Ebay, Amazoni, Kupatana.com (
Tanzania ) inatoa uhuru wa kuuza na
kununua bidhaa yoyote mtandaoni. Hapa utapata nyumba, mavazi, usafiri, vitabu, mashamba n.k
10.HULKSHARE,
SOUND CLOUD
Sauti ina
thamani yake na ili hii haiba idhihirike haina budi kukusanywa pamoja katika
mfumo flani. Miaka ya 90, miziki ilitunzwa
vyema katika santuri, kanda , cd na baadae miaka ya 2000 , zikaingia flash. Lakini
ukisahau mbinu hizi . Hulkshare na sound clound ni mapinduzi makubwa miongoni
mwa mengi katika kutunza, kusikiliza na kupakuwa au ku ’download’ sauti, nyimbo,
midundo, mziki unayoipenda.
Monday, June 15, 2015
A.Y au Ambwene Yessaya ni mwanamziki mkongwe anayetetemesha bongo fleva likija swala la mafanikio.Msanii huyu kajiwekea mizizi mirefu hadi nje ya mipaka ya Tanzania.Akianzia na kundi la East Coast Army ,A.Y anapata umarufu kwa uwezo wake wa kurap vizuri,na baadae anajitegemea huku akifanyakazi na wasanii wakubwa kama Sean Kingstone,Romeo,n,k. Na hapa anakuuliza ''Ni kitu gani huwafanya watu wawe na
mafanikio?'' kisha anasema ''Leo namalizia kukupa siri 10 ambazo ukizizingatia utabadilika na
kuwa mtu ambaye kila mmoja atakuwa akikuangalia kama mfano.''Ambwene Yessaya(2015).
1. siri ya kwanza:UNAVYOFIKIRIA NDIO
KILA KITU
Siku zote kuwa na mawazo
chanya. Fikiria mafanikio na sio kushindwa. Kuwa makini na mazingira hasi. Siri
hii inafaa kuwa ya muhimu zaidi kwenye orodha ya mambo ntakayokuambia.Imani kuwa unaweza kuyafikia malengo
yako inapaswa kuwa imara. Pindi unapojiambia mwenyewe kuwa ‘siwezi..’, basi
hautaweza. Mambo chanya huwatokea watu chanya.
2. siri ya pili:KUWA MSTAHIMILIVE NA
JITUME
Mafanikio ni kama marathon
na sio mbio fupi. Kamwe usikate tamaa. Ukimuuliza kila mtu aliyefanikiwa leo au
ukisoma historia za watu wenye uwezo mkubwa kifedha na maisha kwa jumla,
utagundua kuwa walijituma sana hadi kufika hapo
walipo.
Hakuna njia ya mkato katika kufikia
kilele cha mafanikio. Lakini kama unafanya kitu ambacho unakipenda – basi sioni
hata kama unaweza kukiita ni kazi!
3. siri ya tatu: KUWA TOFAUTI
Kama utafanya kitu kile
kile kama wengine wanavyofanya, ni ngumu sana kuwa na mafanikio. Ni muhimu sana
kupata kitu tofauti na kukomaa nacho.Hivi ndivyo itakuwa rahisi
watu kukuona na wewe kupata unachotaka. Iwe ni fedha, uhusiano wenye maana, mtu
tofauti huvutia wote.
4. siri ya nne: ANZA SASA
Watu wengi hushindwa
kuufikia uwezo wao wa juu kabisa kwasababu huwa hawaanzi kufanya kitu. Siku
zote wamekuwa ni watu wa kujiandaa, kujipanga na kusubiri muda mzuri wa kuanza.Kama ningeendelea kusubiri
hadi leo pengine nisingekuwa na mafanikio haya niliyonayo. Kama nisingechukua
hatua za kusafiri na kwenda Kenya, Uganda na kwingineko, nisingekuwa msanii
ninayejulikana kama hivi sasa.Kama nisingekuwa mjasiri na
kuamua mwenyewe kubadilisha video zangu na kuzigharamikia, naamini nisingewapa
moyo wasanii wenzangu wanaowekeza sasa kwenye kazi zao. Kujiongeza ni neno
sahihi hapa! Kama unataka kujenga
nyumba, ni ngumu kupata kwa mfano shilingi milioni 50 za hapo hapo ili uanze.
Anza kwa hicho ulichonacho mkononi na utashangaa kuwa una nyumba tayari! Si
unaujua ule usemi kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha?
Je
unasubiri kitu fulani kabla ya kuanza? Ni kitu gani kibaya sana kinaweza
kutokea kama ukianza sasa? Kama wewe ni mtu ambaye umekuwa ukisubiri muda
muafaka ufike, acha kusoma post hii na anza kufanya kile umekuwa ukitaka
kufanya. Post hii itaendelea kuwepo hapa hapa ukirejea tena. Ha ha ha ha!
Tukutane kwenye siri ya tano!
5. siri ya tano:ISHI KWA
KILE ULICHONACHO/UNACHOINGIZA
Watu wenye uwezo huepuka
sana kutumia hovyo fedha zao. Lakini cha ajabu, miongoni mwa wengi wenye kipato
cha chini huishi maisha yaliyo juu ya uwezo wao. Hutumia zaidi kuliko kile
wanachoingiza na hivyo kujikuta na madeni mengi. Kama wewe ni mtu wa aina hii,
punguza sasa ili kujiwekea akiba kwaajili yako na familia yako.
6. siri ya sita:KUJIWEKEA TABIA NJEMA ZA KILA
SIKU
Tabia njema ni msingi wa
kutengeneza utajiri. Tofauti kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao
hawajafanikiwa ipo kwenye tabia zao za kila siku. Watu waliofanikiwa wana tabia
njema ama ili kueleweka zaidi niyaite mazoea mengi mazuri kuliko yale mabaya.
Kama unaelewa kuwa tabia
zako mbaya zinakukwamisha kuwa tajiri, utambuzi huo utakuwa ni hatua ya kwanza
katika kuboresha mienendo yako.
Kwenye kitabu chake
kiitwacho ‘Rich Habits - The Daily Success Habits of Wealthy Individuals’, Tom
Corley anakupa ushauri wa kuchukua karatasi na kuorodhesha tabia zako mbaya
kwenye column moja na kisha zibadilishe kila moja kwenye column nyingi kwaajili
ya tabia njema. Mfano ni kama huu:
Tabia mbaya
Ninaangalia mno TV
Sikumbuki majina ya watu
Ninajizuia mwenyewe hadi kuwa na saa moja tu ya kuangalia TV
Ninaandika majina ya watu na kuyakumbuka
Watu wengi waliofanikiwa huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Ninajizuia mwenyewe hadi kuwa na saa moja tu ya kuangalia TV
Ninaandika majina ya watu na kuyakumbuka
Watu wengi waliofanikiwa huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Tabia njema
Kisha kwa siku 30, fuata
maelekezo ya kwenye orodha ya tabia zako njema. Utashangaa namna
utakavyofanikiwa.
7. siri ya saba:USIOGOPE
KUOMBA MSAADA
Watu waliofanikiwa hawana
kasumba ya kufa na tai shingoni kama mjerumani. Walipokumbana na vikwazo
walitafuta msaada wa hali na mali kwa wale waliokuwa na nafasi kuwazidi.
Kila mmoja na ule uthubutu
wa kufanya mambo yake mwenyewe, ni nzuri katika upande mmoja lakini pia mbaya
katika upande mwingine.
Kama kuna mtu unamfahamu ni
mjuzi kwenye sekta fulani na unahisi anaweza kukusaidia katika mradi wako sio
mbaya ukimshirikisha katika ushauri.
8. siri ya nane:NI MARUFUKU
KUKATA TAMAA
Safari ya kuyafikia
mafanikio sio rahisi hata kidogo. Kama unataka kuwa na maisha mazuri kwa njia
halali, ni lazima utakutana na vikwazo vingi ambavyo kama hutokuwa jasiri, ni
rahisi sana kuanguka.Usikate tamaa pale mambo
yanapokuwa magumu. Watu waliofanikiwa huvumilia. Hubadilisha njia. Hujaribu
kitu kipya. Husonga mbele. Wanaweza kubadilisha muelekeo lakini huendelea
mbele.
9. siri ya tisa:TAFUTA
USHAURI KWA WATU WALIOFANIKIWA
Watu wengi waliofanikiwa
huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia
kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika
nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama
ukienda mwenyewe.Kama unataka kuwa na afya njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana
afya. Kama unataka kuwa tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe
baadhi ya siri zake.
10.siri ya kumi:JIWEKEE AKIBA
Wahenga walisema akiba
haiozi na haba na haba hujaza kibaba. Watu wengi hudhani kuwa ili uweze kuweka
akiba ni lazima uwe na kipato cha juu. Nakubali kabisa kuwa wakati mwingine
watu hujikuta tukishindwa kutunza chochote kwasababu majukumu ni mengi kuzidi kipato
chetu, lakini hebu chukua mfano huu:
Wakati ulipokuwa ukiingiza
50,000 kwa wiki, kwanini uliweza kuishi kwa hicho unachokipata na maisha
yalienda? Kisha ulipokuja kupata 100,000 kwa wiki maisha yalibadilika kwa muda
lakini baadaye ukaja kuona tena kuwa hiyo nayo haitoshi! Fundisho hapo ni kuwa
binadamu hatuwezi kuridhika kwa kile tunachokipata na kwamba tunaishi kwa kile
kinachopatikana.
Kwahiyo kama unaingiza
50,000 kwa wiki, ukifanikiwa tu kuweka 5,000 kwa wiki, kwa mwaka mzima utakuwa
umeweka akiba ya 260,000! Lakini pia utaweza kujibana na kuishi kwa 45,000
iliyobakia.
Wengi wenu hapa mnapata
zaidi ya hapa hivyo kama mkiwa na desturi ya kujiwekea akiba, hutaamini kiasi
cha fedha ambacho utakuwa umefikisha baada ya mwaka mmoja au miaka mitano kwa malengo
marefu zaidi. Anza sasa kujiwekea akiba.
Watu wengi waliofanikiwa
huyazungumzia mafanikio yao kwa kuwaongelea watu fulani waliowasaidia
kuwaongoza kufika hapo walipo. Washauri (mentor) wamepitia njia unayohangaika
nayo sasa na wanaweza kukuongoza kufika uendako wa haraka zaidi kuliko kama
ukienda mwenyewe.
Kama unataka kuwa na afya
njema, utahitaji kwenda kwa mshauri ambaye tayari ana afya. Kama unataka kuwa
tajiri, basi pia mtafute mtu ambaye ni tajiri akupe baadhi ya siri zake.
Je! Siri hizi 10 nilizokupa
zimekufundisha au kukuwekea kitu kichwani?
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...