Waliotembelea
Tafuta
Labels
- afya (10)
- akili (1)
- filamu (4)
- filamu.video (1)
- kipaji (6)
- kompyuta (2)
- kujifunza (17)
- kuona (1)
- maneno (6)
- matokeo (1)
- mazoezi (2)
- mbinu (1)
- michezo (5)
- mitandao ya kijamii (1)
- mwaka (1)
- mziki (1)
- ndoto (2)
- njia (1)
- nukuu (6)
- picha (12)
- picture (10)
- sikiliza (1)
- social ntworks (1)
- tafiti (5)
- teknolojia (5)
- tukio (7)
- usahaulifu (1)
- usingizi (1)
- video (4)
- wasanii (4)
Tuesday, May 20, 2014
Mashindano yanayohusisha vyuo vingi vya hapa Mtwara, maarufu kama pro life, yalifikia kilele hapo jana jumapili ya tarehe 18 april,2014.Huku mshindi wa mpira wa pete akiwa ni mwenyeji wa mashindano hayo,chuo cha Sauti Mtwara(stemmuco),akifatiwa na mshindi wa mpira wa kikapu ambaye ni Bandari .Hatimaye kinara katika mchezo wa mpira wa miguu ama kandanda uliokuwa na vuta nikuvute nyingi, hadi kufikia matuta, mshindi aliibuka tena timu ya Bandari.Hii ni sehemu ya matukio mbalimbali yaliyojili uwanjani hapo Nangwanda.
Monday, May 12, 2014
Kila kukicha bendera ya Afrika inazidi kupepea.Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa kimataifa , 2013. Kati ya mabara saba duniani, Africa ni sehemu ya pili kwa kuwa na wakazi wengi ulimwenguni wanaofikia idadi ya watu billioni moja . Kwa namba hiyo eneo hili lenye jumla kubwa ya waafrika linakuwa nyuma ya Asia, bara lenye wanaume na wanawake wengi wanaokadiriwa kufikia bilioni nne . Afrika tofauti na mabara mengine ni mahali panapotoa fursa ya wanadamu kuishi kwa upendo , kuishi kwa mshikamano na kusaidiana kama ndugu wa familia moja. Ukaribu unaojengwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya utu . Tabia hii nzuri ni zao la utamaduni usiohoji maswali kama wewe ni nani, unatoka wapi, unamiliki nini n.k. Wanasema ukitaka kuona shina la ukarimu, mizizi ya uungwana chonde chonde usisite kukanyaga ardhi ya Afrika. Ukitaka kuona ngozi ya kipekee iliyobeba mvuto na mwonekano asilia kama ''chocolate'' hima hima rejea barani Afrika.Pia ukipatwa na shauku ya wanyama wazuri, madini ya kipekee, misitu na mbuga kubwa zenyekustaajabisha moyo na macho kamwe usisite kufika Afrika. Kwa kuwa ni mahali sahihi kwa hadhina hiyo. Kama haitoshi, sura nchi ya eneo hili lenye watu wenye nguvu nyingi , linazungukwa na bahari takribani nne, ikiwemo ile ya Hindi, Atlantik, Meditreniani na bahari Nyekundu ''Red sea''. Toka usawa wa bahari Afrika imemejaariwa miinuko mikubwa, milima mirefu hata kufikia zaidi ya mita 58OO . Mfano mwepesi kabisa ni mlima maarufu ulimwenguni, kilimanjaro. Kando na vilima, mipando na aina nyingine za miinuko yenye kupendezesha macho sana. Bara hili lenye kabila nyingi za asili ya kibantu lina mabonde, miteremko na nyufa ambazo ni njia na nyumba ya maziwa , mito na chemchemi. Sehemu hizi za maji zina majina makubwa yavumayo Ulaya, Amerika, Australia na kwingineko ulimwenguni .Ukiachilia mbali ziwa Tanganyika na mto Naija kuna ziwa Victoria na mto nile kama vivutuo maarufu . Lakini ikumbukwe ni ndani ya mabonde ya bara la Afrika tu ambapo historia inasema, fuvu la binadamu wa kwanza duniani lilivumbuliwa. Baadae teknolojia ikathibitisha masalia ya mafuvu hayo na ya viumbe hai wengine walioishi miaka mingi barani hapa, imechangia wingi wa nishati ya gesi na mafuta katika ardhi ya Afrika. Nishati hii inaweza kuzalisha umeme mkubwa sana.Gesi ya Mtwara ,Tanzania na Oil ya Naija Dellta, Naijeria ni mfano kidogo tu wa nishati hiyo iliyojificha mabondeni humo. Mwisho ni vyema kujifahamisha kuwa kama binadamu anavyopitia vipindi kadhaa hadi kukua. Halikadhalika ardhi hii ya watu weusi imepiti vipindi vikuu takribani sita. Vikiwemo vile vya ; ukuaji wa miji ''state formation'' , kukutana na wageni ''the early contcact'' , biashara ya utumwa, biashara harali '' legitimate trade'' , ukoloni, uhuru na hatimaye ukoloni mambo leo '' neo colonialism''
Mbuga ya Serengeti ni miongoni mwa vivutio vikubwa barani Afrika na hapa ni wakati wa mawio |
Dhahabu |
Almasi |
Madini ya Tanzanite |
Twiga wa Afrika |
msitu wa Kongo |
mto Nile |
Wageni toka mabara mengine wakikaribishwa Afrika ,hapo juu ni msanii Shaggy |
umoja na ushirikiano ni jadi isiyofichika barani Afrika |
Visura wenye rangi ya chocolate ni chimbuko la Afrika |
Subscribe to:
Posts
(Atom)
Popular Posts
-
Hekima huja sio tu kwa kuona matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo ...
-
Ibrahim na Neema huvutiwa sana na mitindo.Ndoto yao juu ya tasinia hii ilianza kwa kupenda haiba na unadhifu.Wakiwa ni vijana wasio na aj...
-
Katika moja ya kipindi cha luninga niliona mabishano baina ya watu watatu, hawa jamaa walitofautiana katika misamiati miwili. Msamiati wa...
-
Kwa mujibu wa mtandao mashuhuri duniani unaoeleza maada na mambo mbalimbali , Wikipedia the free encyclopedia . Kusoma ni mchakato wa ku...
-
Wakati mwili wa binadamu ni kama jumba ,akili huwa kama funguo ikusababishayo kufik ia kila chumba cha maamuzi. Maamuzi hufikiwa baada ya ...
-
Ni miongoni mwa maswali ya msingi sana hapa duniani ,mtu kuhoji,kudadisi na kujiuliza maisha ni nini?Kwa kuwa maisha yanagusa kila mwanad...
-
Wakati sauti hujaribu kudokeza baadhi ya tabia za ndani, mavazi hodokeza mawazo, fikra na hisia za mtu .Hii hutokana na muonekano unao...
-
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2013 yanatoka tar 21 februari 2014 , huku mabadiliko kadhaa yakijitokeza. Mabadiliko haya ni pamoja na...
-
Kupokea maarifa na elimu kutoka chanzo kimoja,mtu mmoja hadi hatua ya kutafasiriwa na akili ya mtu mwingine,haina budi kuja kwa njia ya kuji...
-
Kombe la dunia(2014) ilikua ni michuano ya kabumbu,ambayo ilianza tar 12 mwezi june na kuisha 13 july, huku ilikonga mioyo ya wanamichezo ...