Wednesday, November 6, 2013
Ni jumamosi, wiki ya tatu ya mwezi oktoba,mashindano makubwa yanayoshirikisha michezo na burudani mbalimbali katika chuo kishiriki cha SAUTI,Stella Maris Mtwara, yakiarudi  kwa kishindo kikuu. Haya mashindano ni maarufu sana kama BIG SCORE. Huku mwaka huu, 2013 yakichukua sura nyingine kabisa. Mashabiki, wachezaji na viongozi hawarudi nyuma pia kufanya kila liwezekanalo katika kuboresha sura hii mpya. Msimu huu washiriki wanaongezeka. Wakitoka ngazi tofauti za elimu kama ngazi ya cheti,stashahada na shahada. Mbali na wimbi la ushiriki, michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na mpira wa mikono unatiwa hamasa na radha kwa ingizo jipya la wachezaji hodari na mashabiki machachari. BIG SCORE kama mashindano mengine, inaundwa na uongozi wenye  malengo mengi. Moja ya malengo hayo ni  kukuza na kuendeleza mahusiano mema baina ya washiriki. Kwa maana ya wanafunzi, , viongozi,  watawala, wafanyakazi na watu wengine ambao ni sehemu ya jamii ya hiki chuo,Stella Maris Mtwara.Hapa chini  ni baadhi tu ya matukio yaliopata kujiri katika uzinduzi wa mashindano haya ya wanataaluma.
1
































Popular Posts