Saturday, September 21, 2013
Baada ya kuona sababu kuu nne(4)za usahaurifu katika kujisomea.Hapa tutatazama njia mbadala za kuepuka tatizo la usahaurifu.Lakini mbali na kuzungumzia njia hizi mbadala.Inampasa msomaji kujenga kumbukumbu wakati wa kusoma. Kwa kuachana na sababu zipelekeazo usahaurifu,na kuanza kusoma vitu vichache,kuweka umakini wa kutosha,kuelewa anachosoma na kuwa katika hali njema ya afya.Na hizi zifuatazo ni njia mbadala sita(6) za kuepuka usahaurifu.

1.Zingatia mlo bora kwa afya

2.Fanya mazoezi ya mwili

3.Pata masaa takribani 8 usinziapo

4.Weka kanuni binafsi zitakazo kukumbusha


5.kazia kumbukumbu  kwa kufundisha wenzako

6. Zingatia,tunza na tumia vyema muda

Monday, September 16, 2013
Kama ilivyo kwa maeneo mengine ya dunia,mikoa ya Tanzania hufanana na kutofautiana.Usawa na tofauti huchangiwa na hali ya hewa,ardhi,sura ya nchi,tamaduni na shughuri zinazofanyika katika mikoa husika.Shughuri hizi ni kilimo,uvuvi.biashara.usafirishaji,utalii,uchimbaji madini n.k.Zifuatazo ni picha za mikoa kumi (10)ya Tanzania

1.MTWARA

2.RUVUMA

3.MBEYA

4.IRINGA

5.MOROGORO

6.TANGA

7.KAGERA

8.ARUSHA

9.MWANZA

10.DAR ES SALAAM
  .

Usahaurifu katika usomaji ni hali ya ubongo kushindwa kurejea,kukumbuka au kuwaza baadhi ya vitu vilivyosomwa muda uliopita.Hivi vitu ni pamoja na maada mbalimbali(topics),  masomo na majibu ya maswali kadhaa ambayo huwa ni muhimu katika kusoma. Bila kuzingatia mtu alisoma kwa muda gani,mfupi au mrefu ,masaa mengi au machache,usahaurifu umekuwa kikwazo kwa watu wengi sana hasa wanafunzi,hata kupelekea kutofanya vyema katika mitihani  na masomo yao kwa ujumla.Uchunguzi  wa hivi karibuni unaonyesha kuna sababu nyingi zipelekeazo mtu mmoja kusahau.Katika kurasa hii tutangalia sababu hizi katika makundi makuu manee(4).

1.Usomaji wa vitu vingi bila mpangilio na ratiba maalum

2.Kutoweka umakini wa kutosha katika kile kinachosomwa
 
3.  Mwanafunzi kutoelewa anachokisoma


 
4. Hali ya kiafya kama mawazo,msongo ,magonjwa n.k


Tuesday, September 10, 2013
Karibu katika kila hatua tuchukuazo,maneno tusemayo,kazi tufanyazo na mipango tuwekayo,huwa ni matokeo mazuri ya maamuzi fulani.Haya maamuzi bila kujali ni mazuri au mabaya,magumu au rahisi,huchukua nafasi kubwa ya muelekeo wa maisha yetu.Tafiti nyingi za kisaikolojia(psychology) zinaonyesha kuwa moja ya changamoto kubwa inayomsibu mwanadamu ni kuchua maamuzi sahihi, kwa muda sahihi na mahali sahihi.Kutoa mwanga zaidi juu ya kufikia maamuzi sahihi.Zifuatazo ni hatua saba(7) zinazopendekezwa na wasomi katika nyanja ya saikolojia(psychology)

1.Tambua tatizo au utata

2.Changanua tatizo/utata

3.Orodhesha njia kadhaa za kukabili tatizo


4.Kwa kila njia pima uzuri na ubaya wake


5.Baada ya kupima weka hisia zako katika njia bora zaidi

6.Fanya uamuzi

7.Mwisho tathimini uamuzi wako,kama ulikuwa sahihi..na hautosita kuchua siku nyingine.
 

Popular Posts