Saturday, December 28, 2013


Kompyuta ni nini?, iligunduliwa wapi?, muda gani na nani?. Ni maswali rahisi kuuliza na magumu kujibu.Ugumu unatokana na ukweli kwamba,kompyuta ni chombo cha umeme chenye kufikia, kuchakata, kuonyesha na kutunza habari (data) mbalimbali, kinachoundwa na sehemu nyingi, huku karibu kila sehemu ikiwa na mgunduzi wake anayejitegemea.Bill Gate ,Zuse na Steve Job ni mifano tu ya majina machache yajulikanayo kati ya mengi yalioleta mapinduzi juu ya chombo hiki cha digitali . Urahisi wa kuuliza maswali pia, unasukumwa sana na mchango mkubwa wa hiki kifaa cha umeme, ambacho kiligundulika Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1930,ambapo mpaka sasa kimesaidia katika maeneo kadha wa kadha. Sio tu majumbani, mashuleni, maofisini, viwandani lakini pia hata maeneo muhimu ya huduma za kiafya kama  zahanati. Mpaka kufikia maendeleo yanayoonekana leo; kuchapa kazi, kusikiliza muziki, kutazama filamu, kufuatilia habari , kutuma na kupokea maombi ya kazi, elimu kwa njia ya mtanadao (internet) nk , chombo hiki kimepitia kizazi zaidi ya kimoja. Na vifuatavyo ni vizazi vikuu vinee  vya kompyuta.
1.kizazi cha kwanza(1946-1958)





2.kizazi cha pili(1959-1964)




3.kizazi cha tatu(1965-1970)



4.kizazi cha nne(1971mpaka sasa)


Wednesday, November 6, 2013
Ni jumamosi, wiki ya tatu ya mwezi oktoba,mashindano makubwa yanayoshirikisha michezo na burudani mbalimbali katika chuo kishiriki cha SAUTI,Stella Maris Mtwara, yakiarudi  kwa kishindo kikuu. Haya mashindano ni maarufu sana kama BIG SCORE. Huku mwaka huu, 2013 yakichukua sura nyingine kabisa. Mashabiki, wachezaji na viongozi hawarudi nyuma pia kufanya kila liwezekanalo katika kuboresha sura hii mpya. Msimu huu washiriki wanaongezeka. Wakitoka ngazi tofauti za elimu kama ngazi ya cheti,stashahada na shahada. Mbali na wimbi la ushiriki, michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu na mpira wa mikono unatiwa hamasa na radha kwa ingizo jipya la wachezaji hodari na mashabiki machachari. BIG SCORE kama mashindano mengine, inaundwa na uongozi wenye  malengo mengi. Moja ya malengo hayo ni  kukuza na kuendeleza mahusiano mema baina ya washiriki. Kwa maana ya wanafunzi, , viongozi,  watawala, wafanyakazi na watu wengine ambao ni sehemu ya jamii ya hiki chuo,Stella Maris Mtwara.Hapa chini  ni baadhi tu ya matukio yaliopata kujiri katika uzinduzi wa mashindano haya ya wanataaluma.
1
































Sunday, October 27, 2013
Kuna vitu vingi  binadamu ni vigumu kuviepuka. Moja ya vitu hivi ni kitendo cha kusinzia, kulala au vingenevyo utavyopenda kuita. Usingizi unamahusiano ya karibu sana na maisha yetu ya kila siku. Furaha, wasiwasi  na aina nyingine za hisia huathiriwa kwa kiasi kikubwa na usingizi. Mbali na kuathiri, usingizi hutawala hali nzima ya kila siku. Kwa    kutekeleza vyema , kawaida au vibaya katika  majukumu. Majukumu haya ni pamoja na kusoma, kutibu, kufundisha n.k. Sababu ipelekeayo  aina fulani ya utekelezaji  leo, ni matokeo ya muda na masaa ya usingizi mtu aliopata kusinzia jana  . Baadhi ya tafiti na chunguzi za kisayansi zinaonyesha binadamu kwa wastani hupaswa kulala kwa masaa yasiopungua manane(8). Mafanikio haya ya kisayansi katika tafiti na uchunguzi hayakutinananga hapo tu, bali yalijikita ndani zaidi na kupata mwanya wa kutoa faida kadhaa zitokanazo na usingizi. Na hivyo zifuatazo ni faida tisa zitokanazo na usingizi.

1.Kujenga kinga ya mwili


2.Huboresha kumbukumbu

3.Huwezesha kutafakari vyema

4.Kuharakisha umetaboli''metabolism''

5.Huleta hali nzuri''good mood''

6.Hupunguza mfadhaiko''stress''

7.Hupelekea kujifunza vyema

8.Huchochea umakini''concentration''

9. Hupunguza uzito  wa mwili

Saturday, September 21, 2013
Baada ya kuona sababu kuu nne(4)za usahaurifu katika kujisomea.Hapa tutatazama njia mbadala za kuepuka tatizo la usahaurifu.Lakini mbali na kuzungumzia njia hizi mbadala.Inampasa msomaji kujenga kumbukumbu wakati wa kusoma. Kwa kuachana na sababu zipelekeazo usahaurifu,na kuanza kusoma vitu vichache,kuweka umakini wa kutosha,kuelewa anachosoma na kuwa katika hali njema ya afya.Na hizi zifuatazo ni njia mbadala sita(6) za kuepuka usahaurifu.

1.Zingatia mlo bora kwa afya

2.Fanya mazoezi ya mwili

3.Pata masaa takribani 8 usinziapo

4.Weka kanuni binafsi zitakazo kukumbusha


5.kazia kumbukumbu  kwa kufundisha wenzako

6. Zingatia,tunza na tumia vyema muda

Monday, September 16, 2013
Kama ilivyo kwa maeneo mengine ya dunia,mikoa ya Tanzania hufanana na kutofautiana.Usawa na tofauti huchangiwa na hali ya hewa,ardhi,sura ya nchi,tamaduni na shughuri zinazofanyika katika mikoa husika.Shughuri hizi ni kilimo,uvuvi.biashara.usafirishaji,utalii,uchimbaji madini n.k.Zifuatazo ni picha za mikoa kumi (10)ya Tanzania

1.MTWARA

2.RUVUMA

3.MBEYA

4.IRINGA

5.MOROGORO

6.TANGA

7.KAGERA

8.ARUSHA

9.MWANZA

10.DAR ES SALAAM
  .

Popular Posts